Hakikisha seals zote za kwenye bodi la gari zipo sawa ili panya wasiingie ndani

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,328
Kama huyu alifungiwa redio waya wakachukulia kwenye battery, wakapush kile kiraba kinachozuia maji na takataka zingine kuingia ndani ya gari kutokea kwenye engine ili wapitishe waya. 👇👇

LMC_20220511_113918030_8.4.300.NIGHT.jpg

Bahati mbaya ule waya ulikuwa mnene hivyo raba haikuweza kurudi kukaa mahali pake kama ilivyokuwa mwanzo.

Matokeo yake panya wameingia and hii ndio outcome.

LMC_20220511_112434531_8.4.300.NIGHT.jpg

LMC_20220511_110420299_8.4.300.NIGHT.jpg

LMC_20220511_112426767_8.4.300.NIGHT.jpg

Panya wametafuna wires na kuzikata.

Na ubaya matatizo kama haya kwenye diagnosis sensor fulani ina shida. Usipojiongeza kucheki kama wire zipo sawa utabadili sensors na tatizo halitaisha.

Sometimes pia inakuwa ni ngumu kutrace wires na kujua wapi zimekatika hasa kama sehemu hiyo imejificha.
 
Panya ni waharibifu...kwangu waliingia kwenye injin kwa kupitia chini ya uvungu wa gari, wakakatakata kile kitambaa fulani hivi kinawekwe kwenye bonnet kuzuia joto la injini.....sijui walipenya wapi hivyo vitambaa wakavipeleka ndani ya gari, wakavijaza ndani ya matundu ya AC na kwenye blower motor...

Nilikereka ila sikuwa na lakufanya zaidi ya kubomoa bomoa dashboard na swhemu zingine..nikaondoa hayo matakataka..
 
Aiseeeee.... Lakini sijui ndani waliingiaje maana body la gari matundu yote huwa wanakuwa wameziba.
 
Back
Top Bottom