Hakika wazungu watatuchunga kama wanyama wa serengeti.

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Baba wa taifa alisema maneno haya (wazungu watatuchunga kama wanyama wa serengeti) ni baada ya kutoa maelezo marefu kuhusu umuhimu wa mfanyakazi anayeitwa mwalimu akatoa maneno makali sana ili yadumu kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. maneno ya mwalimu aliyosema ni haya "nguvu ya mwalimu mtu mpumbavu hawezi kuiona nguvu ya mwalimu sio sawa na mtu anayeua kwa kutumia bunduki nguvu ya mwalimu ni ya kuamua je tujenge TAIFA hili au tuibomoe. Kama wakiamua tuibomoe basi wazungu watatuchunga kama wanyama wa serengeti".Hiyo nukuu ni muhtasari.

Basi serikali hii ilimdharau sana mwalimu, akadharaulika, akadhalilika sana na watu wakaaminishwa kwamba ualimu ni kazi isiyo na heshima, isiyo na staha, isiyostahili malipo mazuri, ni kazi ya shida, ni kazi ya wachovu. Sasa nadhani kwa matokeo ya mwaka huu ambapo asilimia TANO tu! (5%) ndio waliopata div 1,2 na 3 na (95%) ni wale waliopata div 4 na 0 watu wenye akili wameelewa maana yake ni nini matokeo haya. Mwaka 2008 walimu walitaka kugoma serikali ikatishia walimu na kuwalazimisha kurudi kazini mara moja kwa lugha ya gadhabu kutoka kwa mkuu wa kaya huku wakionyenyewa nguvu ya dola na akaenda mbali kwamba akasema hata kura zao kama wafanyazi hahitaji. Walim wakatii amri wakarudi kazini ila HAKUNA KAZI BALI UHARIBIFU (mgomo baridi). Walimu hawakupenda malumbano sana safari hii kwa kuwa matatizo yao sio ya jana wala juzi ni miaka mingi na walikuwa wamevumilia kwa kuipenda nchi yao ladba siku moja mambo yakiwa mazuri tutaboreshewa maslahi yetu. Kumbe ni danganya toto wanajineemesha wenyewe na kumsahau mwalimu ambaye kwa kifupi ndiye aliye kazini tangu UHURU kujenga taifa la TANZANIA kwa bei ya jasho lake kwa kuwafundisha watanzania wa fani mbalimbali madaktari, marubani, maprofesa, mashee, mapandri, wataalamu wa kilimo na aina kila aina ili kujenga taifa kubwa lenye nguvu lenye utajiri mwingi wa mali na tamaduni na lenye kujitemea siku za usoni lakini imani ya kukumbukwa walimu ikafutwa wakapewa zawadi ya kudharauliwa.Bila shaka yoyote mwalimu katufikisha pabaya mno tupende tusipede ingawa matatizo mengine sio kwamba hayapo.
Ushauri wangu serikali iwaombe radhi walimu na iboreshe maslahi yao. Watu wengine hawapendi kuambiwa ukweli ila hamna jinsi. kila siku ooh! vitabu, vyumba vya madasa ohh! maabara nani kawaloga nyiye viongozi wa taifa hili? huu si muda wa kutafuta mahali pa kujificha.
Ushuhuda kutoka kwangu nwenyewe nilisoma chini ya mti mpaka darasa la tano lakini tukafanya vizuri sana tu nikajiunga shule ya kata ambayo haikuwa na maabara ya sayansi lakini walimu kwa moyo walionao kwa kutengeneza vifaa kwa vitu asilia lakini kwa principal ileile tulifaulu vizuri leo niko chuo nasoma sayansi. Alafu mnadharau mwalimu hamna akili kabisa. Nawaslisha wanajamvi.
 
Back
Top Bottom