Uchaguzi 2020 Hakika Tundu Lissu ni "living miracle"

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,700
2,000
Mengi yalisemwa kuhusu YEYE pale aliposhambuliwa kwa jaribio la kioga ili kuweza kupoteza maisha yake. Zilijengwa hoja hafifu ili kuhalalisha udhalimu ule, kumbe wabaya wake hawakutambua ili mbegu iote ni lazima ichimbiwe ardhini na kisha imee na hatimaye iweze kugeuka kuwa mche na baadaye mti wenye matunda mema.

Kila kitu kimekwisha kugeuka! Zilianza kampeni kwa watu kuwa na woga wa kumlaki na hata kuhudhiria mikutano yake. Watu walitishiwa pale endapo wangeonekana ktk mikutano yake hasa watumishi wa umma. Viongozi wenye mashaka mengi wa kidini walijikwepa naye. Waburudishaji wa Bongo fleva na hata wana habari na vyombo maarufu vya habari vilijngiwa na hofu kuonekana vikijihusisha naye.

Kule mkoa wa Mbeya walisema ni ngome yake. Sumbawanga ikaongea, Katavi nayo ikaongea. Kagera ikapaza sauti. Sasa! Sasa! Sasa! Hata Geita! Ngome ya Mkulu nayo inashikwa na midadi na kuongea!

Kweli huyu ni "Victor" aliyeandaliwa kupitia mpango wa Mungu ili apate kuwaongoza Watanzania, ili haki ya Mungu ikapate kutawala. Sauti ya mbaali sana ya mtumishi wa Mungu Bagonza ilinong'oneza, Mzee wa upako naye hayupo nyuma, mtumishi mwingine Mwingira naye ameanza kupaza sauti.

Sasa imekuwa ni kubana tu na kiachia. Huwezi kuyazuia mafuriko ya maji ama gharika kwa mikono. Hakika Tundu Lissu ni chaguo la Mungu, na kwa hakika ni "real living miracle"

It is honour to be part of winning team, and it not honour to be part of few violent criminals. Tundu Lissu huyu hapa kila mwenye kuguswa na kesho ya Tanzania yetu ni lazima ampe kura yake. Tarehe 28-10-2020 siyo mbali kutoka siku hii ya leo, mimi ana kura yangu, vipi wewe?
 

Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,640
2,000
Ukijiroga ukaenda kwenye mkutano wa Lisu, ukitoka unawaza kupigia CCM, nahisi utakuwa na upungufu wa akili mbili.

Kwa nondo zile nilizosikia leo Geita, nimejuwa kwa nini hata taarifa zinatolewa zikiwa hazihusu mikutano ya Lisu(hasa TBC)
 

Wervemarcel

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
2,372
2,000
Mengi yalisemwa kuhusu YEYE pale aliposhambuliwa kwa jaribio la kioga ili kuweza kupoteza maisha yake. Zilijengwa hoja hafifu ili kuhalalisha udhalimu ule, kumbe wabaya wake hawakutambua ili mbegu iote ni lazima ichimbiwe ardhini na kisha imee na hatimaye iweze kugeuka kuwa mche na baadaye mti wenye matunda mema..
Naomba kuuliza MZEE WA UPAKO KASEMAJE KUHUSU LISSU?

Labda na mimi napitwa.
 

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
10,076
2,000
Risasi 16 siyo mchezo. Umpende usimpende TL, huo ndio ukweli. Ni muujiza. Hata Jiwe akimwona, anaona ni mzimu tu anaopambana nao.
Kati ya watu ambao Magufuli anaogopa kukutana nao ana kwa ana ni Tundu Antipas Lissu.

Fikiria kama lowassa mwanaccm mwenzake alikuwa anamkwepa kwepa sijui kwa Lissu itakuwaje.

Na kingine kinachomshinda Magufuli kumbana Lissu ni kwamba Lissu hakuwahi kuwa fisadi kama Lowassa so hata kwa kumkamatia anashindwa zaidi ya kuwatumia vijana wa Ak47 wamshughulikie.
 

fordrick2012

Member
Sep 3, 2020
54
125
We don't care kama ni wa miujuzi au wa shetani sisi leti ni moja tu
1600971821667.png
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
12,314
2,000
Sawa! Kupigwa kwake risasi ni kitendo cha kupingwa na kila mtu!

Lakini hiyo haiwezi kuwa tiketi ya kufikiri atapewa urais kwa kuhurumiwa.
.
Ingekuwa hivyo hata Ulimboka angepewa hata ubunge tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom