Jipangeni aisee ili msiishie kudanganywa na utamu wa pilau mkashindwa kuhoji mengi yaliyojificha nyuma ya pazia.
Mbowe ni fundi wa kuongea na kujenga hoja, lakini vipi kuhusu chama chake kuwapa nafasi vijana wakaleta mawazo na mchango mpya?. Tangu 2004 mpaka leo ni miaka 14, jamaa bado kashikilia nafasi yake huku akiwadanganya kwa eloquence taaamu kama sukari!!.
Badilikeni, vinginevyo mtabakia mkikosa muelekeo mpya wa uongozi, mtabakia mkikosa busara mpya za kiuongozi.
Miaka 14 madarakani ndio yale yale kina Kagame, Mugabe na Museveni, ni kudumaa kwa demokrasia katika chama chenye neno demokrasia kama utambulisho wake.