Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 16,372
- 37,938
Wakuu haya maisha unaweza pata kila (material things) na bado furaha usiipate. Mara nyingi huwa nacheka sana watu wanapopewa ushauri wa tafuta pesa baada ya kutendwa.
Nikirudi nyuma katika wakati kipindi hicho nikiwa hoehae na kwanza ndo niko shule, nikatokea kumpenda sana binti mmoja, nilihangaika sana kumshawishi na nikakutana na vitimbwi vya kila aina, sikukata tamaa nikiamini ndio fungu langu..
Toka 2006 akaja kunikubali 2008 ila bad enough baada ya miezi kadhaa akaja kunibwaga kwa madai kwamba siko moyoni mwake na hata akiniita mpenzi nafsi inamsuta. Niliyapokea haya katika muda ambao sikuutaraji tena nikiwa nimefunga safari ndefu kumfata yeye.
Niliondoka kishingo upande huku sumu ya penzi nikiwa nimeshailamba, hakika aliuvunja moyo wangu vipande vipande, tokea hapo sikuwa tena na imani na hawa viumbe. Na kila aliyekatiza anga zangu alionja joto ya jiwe, hata sikuona thaman ya penzi..
Baada ya miaka kadhaa yule yule aliyeuvunja moyo vipande vipande akarudi na kudai ananipenda sana, anataka nimuoe na ndani ya wiki akadai anitambulishe kwa baba ake. Nilimkubalia lakini lengo lilikuwa kumuumiza tu, alifunga safari na kunifata, nilikaa naye kama wiki na alipoondoka ndo ukawa mwisho wa mapenzi..
Nikajifanya kauzu ihali nampenda, sasa tangu aondoke bado nauguza moyo wangu na siamini kama utapoa. Mbaya zaidi huyu mwanamke kashaolewa na ana watoto wawili sasa.
Kila nilikojaribu kwenda najikuta sifiki kokote, kwa kifupi hakijaeleweka bado, kuna muda nafikiri pengine wengine hatupo duniani kwa ajiri ya kuoa. Kifupi ni kwamba ni miaka 10 sasa ila bado hakijaeleweka.