Haki za wastaafu wa EAC..........zitapatikanaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki za wastaafu wa EAC..........zitapatikanaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 2, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Mahakama Kuu kupitia wanahaki J. Nyerere na J. Utamwa kwa pamoja wametia dosari za kisheria hati ya makubaliano kati ya wastaafu tajwa na serikali kuwa hayatekelezeki kutokana na hoja zifuatazo:-

  a) Aya namba mbili na tatu za makubaliano zilikuwa zinaonyesha ya kuwa walikubaliana wastaafu kulipwa kutoka na kumbukumbu za mafaili yao lakini katika aya ya tatu ikawekwa takwimu ya Tshs 177 Bilioni ambayo haina maelezo ya jinsi ilivyopatikana na sasa ndipo mgogoro wa kuyatekeleza makubaliano waanzia....................

  Wastaafu waona hiyo bilioni 117 qwamepounjwa na serikali ikishikilia ndiyo walichokubaliana..................

  Ufumbuzi ni kuwa wastaafu wakayapinge hayo makubaliano kuwa hayatekelezeki na hivyo yanadhalalisha mahakama..........haiwezekani makubaliano yafanyike bila ya kuwepo kwa viambatanisho vya kuonyesha kila mstaafu alistahili nini na hivyo kutegemea huruma ya mdaiwa ambaye ni serikali kulipa atakavyo............

  Aya namba 7 ya makubaliano ya kuwa serikali ambayo ni mdaiwa kuwalipa wanasheria wa wastaafu ni makosa makubwa ya kisheria kwa sababu hao wanasheria wasingeweza kuwatendea haki wateja wao kwa kukubali kuwatumikia mabwana au wateja wawili................huo ulikuwa ni mgongano wa kimasilahi kabisa na pekee yake watosha kuifuta hati ya makubaliano na wadau wakaendelea na kesi kama vile hawajawahi kukubaliana lolote vile...........
   
Loading...