Haki ni jambo ambalo jamii husika imekubaliana kuwa haliwezi kutenganishwa na uwepo wa mwanadamu, kwamba pindi
unapozaliwa kuwa mwanadamu hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kukutenga nacho akawa hakutenda kosa,
mfano haki ya kuishi, mara unapozaliwa mwanadamu kuishi ni jambo ambalo haipaswi kutenganishwa nalo, vivyo hivyo kwa haki nyinginezo kama vile, haki ya kupata habari, kujumuika, kutobaguliwa nakadhalika. Haki hizi hata ukienda vijijini ambako hakuna wataalam na wasomi mbalimbali watakueleza kuwa kuua mtu ni jambo baya na siyo haki, HAKI ni jambo la asili ya uhuru wa mwanadamu.
HATAHIVYO jamii imejiwekea utaratibu maalumu wa kuhakikishia watu wake ASILI YA UHURU WAO. Ikumbukwe kwamba siku zote mwanadamu amekuwa katika mapambano ya kuhakikisha kuwa anazidi kuwa huru, ndiyo maana pamekuwepo maendeleo mengi ya sayansi na teknolojia ili kumfanya binadamu kuwa huru zaidi, kuishi muda mrefu zaidi kwa mfano kupata matibabu, kuwa huru kutoa maoni yake mfano jukwaa kama hili na mengineyo, nakadhalika.
Utaratibu maalumu wa kuwahakikishia watu uhuru wao ndiyo unaitwa SHERIA. Hivyo basi sheria ni chombo kinachotumika kuratibu uhuru wa watu. Ndiyo maana sheria hutungwa na watu kupitia wawakilishi wao(BUNGE). Hata hivyo wakati mwingine bunge laweza kutunga sheria inayokinzana na haki, yaani inayopunguza uhuru wa binadamu, hapo sheria hiyo itakuwa siyo ya haki. Endapo akajitokeza mtu kuipinga MAHAKAMANI sheria anayohisi kuwa siyo ya haki mahakama yaweza kuipiga marufuku isitumike hata kama imepitishwa na bunge na kusainiwa na Rais.(rejea kesi ya Mch. Mtikila kuhusu mgombea binafsi).
kUTOKANA NA MAELEZO HAYO HAPO JUU UTAONA JIBU LA SWALI LAKO KUWA NI SHERIA SIYO HAKI WALA HAKI SIYO SHERIA BALI NI VITU VINAVYOTEGEMEANA ILI KIMOJA KIWEPO LAZIMA KINGINE KIONEKANE MFANO WA KUKU NA YAI.