Haki ni sheria au sheria ni haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki ni sheria au sheria ni haki

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Chifu kamaliza, Nov 26, 2011.

 1. C

  Chifu kamaliza Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napata shida katika hili kwa sababu gani nasema hivi Watanzania tulio wengi atuzifahamu sheria ya nchi yetu yaani(katiba) sasa kumekuwa na tabia ya watu wengi mno kusema wanadai haki kwenye mambo ambayo hata hawajui sasa hii haki wanayoidai pasipo kuijua sheria ni sahihi naomba mnisaidie kwa hili
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Zote mbili zinaleta maana kutegemea na situation.
  Ila mpaka "haki iwe sheria" lazima jamii husika iwe inaamini kwamba "sheria ni haki".

  Kuhusu waTanzania kudai haki wasizojua zinachukuliwaje kisheria ni sawa na kipofu kuanza kujenga daraja kwenye mto asiojua unaanzia na kuishia wapi. Wengi wetu hatujui haki zetu kikatiba ni zipi. . . hivyo hata tukipewa nafasi ya kuzitaja na kuzitetea itakua kazi bure.Sema wakubwa hii ndio hali wanayopenda maana hata kuikosoa nako kunakua kazi maana huwezi kukosoa/pinga kitu usichojua.

  Labda kuwe na kipengele cha kujifunza mashuleni.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama masheria yenyewe yameandikwa kwa lugha ya kizungu sisi akina Ngabu tutaelewa nini?
   
 4. m

  moshingi JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haki ni jambo ambalo jamii husika imekubaliana kuwa haliwezi kutenganishwa na uwepo wa mwanadamu, kwamba pindi
  unapozaliwa kuwa mwanadamu hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kukutenga nacho akawa hakutenda kosa,
  mfano haki ya kuishi, mara unapozaliwa mwanadamu kuishi ni jambo ambalo haipaswi kutenganishwa nalo, vivyo hivyo kwa haki nyinginezo kama vile, haki ya kupata habari, kujumuika, kutobaguliwa nakadhalika. Haki hizi hata ukienda vijijini ambako hakuna wataalam na wasomi mbalimbali watakueleza kuwa kuua mtu ni jambo baya na siyo haki, HAKI ni jambo la asili ya uhuru wa mwanadamu.
  HATAHIVYO jamii imejiwekea utaratibu maalumu wa kuhakikishia watu wake ASILI YA UHURU WAO. Ikumbukwe kwamba siku zote mwanadamu amekuwa katika mapambano ya kuhakikisha kuwa anazidi kuwa huru, ndiyo maana pamekuwepo maendeleo mengi ya sayansi na teknolojia ili kumfanya binadamu kuwa huru zaidi, kuishi muda mrefu zaidi kwa mfano kupata matibabu, kuwa huru kutoa maoni yake mfano jukwaa kama hili na mengineyo, nakadhalika.
  Utaratibu maalumu wa kuwahakikishia watu uhuru wao ndiyo unaitwa SHERIA. Hivyo basi sheria ni chombo kinachotumika kuratibu uhuru wa watu. Ndiyo maana sheria hutungwa na watu kupitia wawakilishi wao(BUNGE). Hata hivyo wakati mwingine bunge laweza kutunga sheria inayokinzana na haki, yaani inayopunguza uhuru wa binadamu, hapo sheria hiyo itakuwa siyo ya haki. Endapo akajitokeza mtu kuipinga MAHAKAMANI sheria anayohisi kuwa siyo ya haki mahakama yaweza kuipiga marufuku isitumike hata kama imepitishwa na bunge na kusainiwa na Rais.(rejea kesi ya Mch. Mtikila kuhusu mgombea binafsi).
  kUTOKANA NA MAELEZO HAYO HAPO JUU UTAONA JIBU LA SWALI LAKO KUWA NI SHERIA SIYO HAKI WALA HAKI SIYO SHERIA BALI NI VITU VINAVYOTEGEMEANA ILI KIMOJA KIWEPO LAZIMA KINGINE KIONEKANE MFANO WA KUKU NA YAI.
   
Loading...