Haki na Wajibu

believer

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
633
213
Kuna hili suala la Bandari linaloendelea Nchini, limekuwa lichukua sura tofauti tofauti kila kukicha, na kadri siku zinavyozidi kwenda, mambo mbalimbali yamekuwa yakijitokeza hasa mara baada ya Bunge la Bajeti kutenga muda wakati fulani siku ya Jumamosi kwa ajili ya kujadili jambo la Bandari, kutolea ufafanuzi vipengele mbalimbali ndani ya kinachoitwa Mkataba.

Kwakuwa mambo yenyewe ni ya kisheria nk imeonekana dhahiri kuwa kunahitajika umakini wa hali ya juu katika kulielekea jambo hili, Tumeshuhudia muendelezo wa hili jambo kama vile kufunguliwa Kesi katika Mahakama Kuu Mkoani Mbeya, Wasomi kadhaa wanaoheshimika katika Taifa letu kujitokeza na kutoa maoni yao kama vile Prof. Anna Tibaijuka, Prof Issa Shivji, Balozi Dkt. Wilbrod Slaa, Wanasiasa kama vile Mh. Catherine Magige, Mh. Jerry SIlaa, watu maarufu kama vile Steven Nyerere, watangazaji kama Maulid Kitenge, Gerald Hando, Maafisa mbalimbali kutoka Serikalini, Serikali kwa ujumla na Viongozi waandamizi pia.

Kilichotokea ni kama vile wasomi kama baadhi niliowataja na watanzania wengine walitoa maoni na kuchambua maeneo ambayo kimsingi wanaona yana ukakasi, mapungufu au yanapaswa kuangaliwa kwa kina, kilichofuata ni kama tena makundi mengine yamekuwa yakijitokeza na kuuelezea huo unaitwa Mkataba wa Bandari ya kwamba ni mzuri na jamii inayoonesha wasiwasi wa suala zima la Bandari ni kwasababu tu hawajaelewa, hivyo lazima waelewe.

Ukiangalia kwa kina ni kama vile kila anayeelewesha juu ya hili suala anaeleza faida ambazo kimsingi ni kama HAKI ndani Mkataba, ya kwamba Bandari ikichukuliwa/ zikichukuliwa kutakuwa na faida kubwa, uwezo wa kutoa huduma utaongezeka, Ajira zitaongezeka, Teknolojia itapanuka, uwekezaji utaimarika, mapato yaongezeka nk nk. Mkataba wowote unakuwa na HAKI na WAJIBU.

Nakubaliana kabisa na faida hizo na ni kweli tunahitaji uwekezaji Nchini, Ila upande wa WAJIBU ndio hasa unaogombewa na walio wengi, ya kwamba katika uwekezaji huo wale wawekezaji wanaokuja Nchini kutoka huko Dubai kutuletea mafaida mazuri kabisa yaliyoelezwa na yanayoeleweka siku zote, JE WAO WATAPATA NINI, WAO WATANUFAIKA NA NINI, JE VIPENGELE VYA MKATABA KAMA VILE WANAPOSEMA BANDARI (Je wanamaanisha Bandari zote Nchini? au Bandari ya Dar es salaam? na vipi kuhusu muda wa Mkataba, Je ni miaka 20? 40? 50? au mingapi), TUTAKAPOCHOKANA KWA SABABU YOYOTE ILE TUNAACHANA VIPI KIMKATABA?

Huu hapo juu ni sehemu ndogo tu ya WAJIBU ambao kimsingi watanzania wanataka kujua,
na yapo mengi katika mioyo ya watanzania wanataka kujua, kwasababu wana kumbukumbu ya mikataba mingi iliyoumiza Taifa, Aidha watanzania wanaona suala la Bandari ni nyeti sana kwa Usalama wa Nchi, Ustawi wa Taifa na kwa Urithi wa vizazi vyao. Hata ukiangalia wasomi waandamizi waliojitokeza mapema kuhoji mambo ambayo mimi nimeyaweka kwenye kundi la WAJIBU, wengi wao ni wazee kwa maana wamefanyakazi muda wa kutosha, wameona mengi na wanajua wanayoyasema. Kwanza hata maisha yao sio kwamba wana njaa wao, watoto wao au hata wajukuu wao, wala hawatafuti teuzi ila wanatafuta namna ya kuliponya Taifa ili wajukuu wetu sisi wataokuwepo Nchini mwaka 2095 waendelee kuwa watanzania ndani ya Tanzania yao ikiwa na mali, utajiri na baraka tulizopewa na Mungu.

Hata kwa mtanzania wa kawaida kabisa kwa mara ya kwanza unaiona hofu moyoni mwake juu ya jambo hili, watanzania wasipuuzwe na kuonekana ya kwamba wanaihitaji tu kuendelea kuelezwa kuhusu faida zilizopo kwenye hicho kinachoitwa Mkataba. Watanzania wameonyesha Hofu ya wazi kuhusu jambo hili, kama lina nia njema ni vyema walio wengi wakasilizwa hata kama uelewa wao ni mdogo, lakini kiukweli haiwezi kuwa eti kundi dogo likawa na Akili kuliko kundi kubwa, kinachotofautisha hapa ni Mamlaka na Wadhifa wa kundi dogo kwa niaba ya kundi kubwa. Kwa mara ya kwanza kundi kubwa limeonyesha Hofu ya wazi lisipuuzwe. HAKI tunakiri tumeielewa ila WAJIBU haujaeleweka, kama jambo hili lina nia njema, taulo limedondoka tuchutame tu.
 
Back
Top Bottom