Haki inapozuiliwa na mtutu wa bunduki Nigeria

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Waandamanaji mjini Lagos waliweka vizuwizi na kufunga barabara katika mji huo mkubwa wa kibiashara

Waandamanaji mjini Lagos waliweka vizuwizi na kufunga barabara katika mji huo mkubwa wa kibiashara
Watu kadhaa walioandamana dhidi ya polisi wakatili wameripotiwa kupigwa risasi na kufa na huku wengine wakiwa wamejeruhiwamjini Lagos, Nigeria.

Walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa wameona miili ipatayo 20 ilikuwa imetapakaa na wengine 50 wamejeruhiwa baada ya wanajeshi kufyatua risasi.

Shirika la kimataifa la Amnesty limesema limepata habari za kuaminika kuhusiana na vifo hivyo.

Maafisa wameahidi kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo.

Amri ya kutotoka nje ndani ya saa 24 imewekwa mjini Lagos na miji mingine.

Waandamanaji sasa wamezunguka vituo vya polisi , kikosi maalum cha Sars, kimekuwa kikiendelea kwa muda wa wiki mbili .

Kutokana na mapigano ya risasi yanayoendelea , aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Marekani bi. Hillary Clinton amemtaka rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kuacha kuwaua vijana asitishe maandamano ya Sars.

#EndSARS ".

Mcheza mpira Nigeria Odion Jude Ighalo, ambaye anaichezea Manchester United, ameishutumu serikali ya Nigeria kwa kuua wananchi wake.

Alisema hayo kupitia ukurasa wa tweeter kwa kuweka video.

Walioshuhudia tukio hilo walizungumzia wanaume ambao hawakuwa katika sare ambao walipiga risasi jioni ya siku ya Jumanne.

Askari wenye silaha walikuwa wakiwazuia waandamanaji kabla ya risasi kuanza kupigwa , mwandishi wa BBC Nigeria Nayeni Jones anaripoti.

Video katika mitandao ya kijamii ilikuwa ikionesha tukio hilo mubashara.

Shuhuda ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa majira ya saa moja kasoro usiku walianza kupiga risasi katika maandamano ambayo yalikuwa ya Amani.

Walikuwa wanapiga risasi moja kwa moja kwetu, lilikuwa tukio baya . Kuna mtu alipigwa risasi na kufa hapo hapo.

Walipiga risasi kwa muda was aa moja na nusu na baada ya hapo askari walichukua miili ya waliouawa.

Askari walikuwa wameweka zuio kwa waandamanaji hivyo magari ya wagonjwa yalishindwa kufika katika eneo la maandamano.

Askari walikuwa wameweka zuio kwa waandamanaji hivyo magari ya wagonjwa yalishindwa kufika katika eneo la maandamano.

Watu wengine wanne walioshuhudia waliiambia Reuters news agency kuwa askari waliwapiga risasi waandamanaji .

Mmoja wao Alfred Ononugbo, 55, alisema: "Walianza kupiga risasi katika mkusanyiko huo .

Niliona risasi zikipiga watu wawili.

Katika ujumbe wa tweet wa , Amnesty International Nigeria wamesema kuwa wana ushahidi tosha unaoonesha polisi wakitumia mabavu dhidi ya waandamanaji mjini Lagos".

Msemaji wa Amnesty International Isa Sanusi alisema wana video inayoonesha polisi wakiwaua wananchi, wanajaribu kuhakiki ni wangapi.
 
Naona sasa watu Wanavamia vituo vya polisi aise wanachoma moto....
Kuwazuia raia mamilion wa Nigeria ni ngumu sana
Labda utawala uliyopo upishe ukae pembeni
Maana watu wanachoma mpaka maofisi na miradi ya serikali

Ova
 
La msingi ni Buhari kujiuzuru tu maana hayo maandamano yameshafikia point of no other agreement rather than resignation.
Kwa ustawi na kuepuka vifo vingi zaidi vya raia na kuikaribisha mahakama ya kimataifa nchini Nigeria rais angejiuzuru tu.
 
Wanaandamana huku raisi na wakuu wa polisi wanagonga vikombe vya kahawa ikulu

Unapoteza maisha kwa upumbavu wa kijinga ili uridhishe umma eti we mpenda haki

Hii dunia haina haki, haki utaipata mbinguni.
 
Nchi za Africa magharibi haziishi machafuko.
muda simrefu utasikia jeshi limekamata nchi Nigeria.
 
La msingi ni Buhari kujiuzuru tu maana hayo maandamano yameshafikia point of no other agreement rather than resignation.
Kwa ustawi na kuepuka vifo vingi zaidi vya raia na kuikaribisha mahakama ya kimataifa nchini Nigeria rais angejiuzuru tu.
Kweli kabisa,inasemekana huyo tinubu anataka kula kona kwa kutumia ndege binafsi...maana raia huko Wana muwinda
Ila all in all Buhari ajiuzulu anawapa wakati mgumu vyombo vya ulinzi huko,Ona vituo vya polisi vinachomwa moto,magereza yanavunjwa akijifanya kukaza Hali itakuwa mbaya zaidi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mnamlaumu buhari bure, kwenye vita hiyo mzungu anahusika kwa asilimia kubwa Sana kutokana na utajiri uliopo punde utashangaa kusikia raia nao wanamiliki silaha, issue ya msingi ni kuondoa/kuvunja makundi ,na namna yakuyaondoa ni ipi,hekima ya kiongozi inahitajika
 
Ni bora nchi ichafuke kuliko kuwa colonized na mtu mweusi.
 
Mnamlaumu buhari bure, kwenye vita hiyo mzungu anahusika kwa asilimia kubwa Sana kutokana na utajiri uliopo punde utashangaa kusikia raia nao wanamiliki silaha, issue ya msingi ni kuondoa/kuvunja makundi ,na namna yakuyaondoa ni ipi,hekima ya kiongozi inahitajika
Kwani mkuu Aliyekua anapiga na kuua raia ni SARS au mzungu? Au mzungu ndo aliwatuma wavunje sheria na kuwafanyia unyama raia wao? Watu wamechoshwa na unyanyasaji wanadai haki zao eti lawama unazipeleka kwa mzungu!
 
Mnamlaumu buhari bure, kwenye vita hiyo mzungu anahusika kwa asilimia kubwa Sana kutokana na utajiri uliopo punde utashangaa kusikia raia nao wanamiliki silaha, issue ya msingi ni kuondoa/kuvunja makundi ,na namna yakuyaondoa ni ipi,hekima ya kiongozi inahitajika
Ujinga mtupu, ni mjinga pekee ndiye atakae amini ulichokiandika hapa.
 
Maandamano yalikuwa ya kupinga ukatili wa polisi ila wanaelekea kuyageuza kuwa ya kisiasa kwa maslahi ya wachache.
Hii ni kwa kiasi flani imesababishwa na ujinga na upumbavu wa viongozi. Kwa mfano kama wangekubali matakwa ya waandamanaji mapema wakatenda haki yasingefika huku. Pia kutumia risasi za moto ndo wameharibu kabisa mkuu
 
Viongozi wengi wa Africa ni shida mno kwao linapokuja suala la kuwajibika au kutenda haki!
Katiba mbovu ndio chanzo cha matatizo mengi katika nchi za Africa!
Wapigania uhuru wa bara la Africa walikosea kitu kimoja, Hii Africa tulipaswa kuwa na katiba moja ambayo ingetumika Africa nzima!
Africa nzima tungetumia katiba kama ile ya Ghana au Sauth Africa, Bara letu lingekuwa mbali sana!
 
Maandamano yalikuwa ya kupinga ukatili wa polisi ila wanaelekea kuyageuza kuwa ya kisiasa kwa maslahi ya wachache.
Mkuu hata kama wana taka kubadilisha uongozi mm nawaunga mkono ile nchi imejaa ufisadi wa kutisha mno.
Yaan ukiangilia utajiri ilio nao nchi hiyo na maisha ya wangeria yalivyo kwakweli wana haki ya kuwatia adabu viongozi wao.
 
Wanaandamana huku raisi na wakuu wa polisi wanagonga vikombe vya kahawa ikulu

Unapoteza maisha kwa upumbavu wa kijinga ili uridhishe umma eti we mpenda haki

Hii dunia haina haki, haki utaipata mbinguni.
Hivi ww mjinga unajua ni watu wangapi wamekufa mpaka ww kuwa huru ndani ya nchi yako?
Hivi unajua ni watu wangapi wamekufa kwa ajili ya kukomesha utumwa kwa mtu mweusi kama ww ?
Hivi unajua ni watu wangapi wamekufa kwa ajili ya kutetea thamani ya mtu mweusi kama ww, angalau mtu mweusi naye anaonekana ni binadamu badala ya mnyama?
Hao nilio wataja ni watu walio kufa miaka mingi iliyo pita lakini ww sasa hivi unanufaika na kufa kwao.
Je hao watu wangekuwa na fikira za kupumbavu kama za kwako leo hii ungekuwa unauzwa kama nyanya kwenda kulima mashamba ya wazungu.
Siku zote unapo pigania haki haujipiganii ww kama ww bali una pigania kizazi chako cha mbeleni.
 
Wanaandamana huku raisi na wakuu wa polisi wanagonga vikombe vya kahawa ikulu

Unapoteza maisha kwa upumbavu wa kijinga ili uridhishe umma eti we mpenda haki

Hii dunia haina haki, haki utaipata mbinguni.
Hapa ni makalio yamefikiri halafu yakaandika.
 
Back
Top Bottom