Msumbuji: Raia waandamana kupinga matokeo uchaguzi, Wawili wauawa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Watu wawili wameuawa katika maandamano nchini Msumbuji ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa mitaa.

Shirika lisilo la kiserikali la Centre for Public Integrity - CIP limesema polisi waliwafyatulia risasi za moto waandamanajai katika miji kadhaa.

Kundi kuu la upinzani nchini humo likiongozwa na chama cha RENAMO liliitisha maandamano baada yamatokeo ya uchaguzi wa Oktoba 11 kutolewa na maafisa wa uchaguzi Alhamisi, yakionyesha kuwa chama tawala cha Frelimo kilitangazwa mshindi katika manispaa 64 kati ya 65.

Maandamano yalipangwa katika mji mkuu Maputo na katika miji ya kaskazini ya Nacala na Nampula, huku polisi wakiwafyatulia risasi waandamanaji katika maeneo mengine.

Taarifa ya CIP imesema polisi mmoja alidaiwa kushambuliwa na umma katika mji wa NAMPULA na kujeruhiwa vibaya na kufariki hospitalini.

Imesema mwanaume moja aligongwa na kitu kizitona kuuawa katika mji wa Nacala. Watu wengine wawili walipigwa risasi na kujeruhiwa katika maandamano ya eneo hilo.

DW
 
Kwanini mpaka muitolee mfano Tanzania?
Mna agenda ya siri sio bure
 

Attachments

  • inbound1469246696365638972.jpg
    inbound1469246696365638972.jpg
    116.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom