Haki inanisumbuwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki inanisumbuwa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ngekewa, Mar 22, 2012.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Najuwa tuko wengi tunaoamini utaratibu wa mwanamme kuwa na haki ya kutowa talaka. Mlio kwenye kundi hili nawaombeni ushauri wenu kwa vile mtanielewa nini kinachonisibu.

  Mwenzangu, nikimaanisha mama watoto wangu ana nifanyia visa eti kwa kuwa mimi ndie ninaeweza kutowa talaka kwake!
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kuwa nina sababu nyingi zinazonifanya nishindwe kutowa talaka,nae analijuwa hilo!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Kwa nini mwanamke hawezi kutoa talaka?

  Mimi nilidhani mume ama mke ndo anaweza kuomba talaka (kwa kufungua shauri mahakamani) na ni jaji ndiyo mwenye kuitoa. Au sielewi?
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  unalo hilo,kama stori zako ndio zile za kuongeza mke wa pili kisa dini inaruhusu wacha akufanyie visa....she is just frustated,anataka ujirudi ulipokosea....sidhani kama anataka talaka,angekuwa anaitaka angeshakuburuza mahakamani au kwa wazeee....
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Uko sahihi kabisa kuwa mwanamke anaweza kudai talaka lakini hawezi kutowa talaka! Hili la mahakama linakuja baada ya kukosa makubaliano.
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wallahi kama angefanya hivyo ningehisi afuweni.
  Pengine sasa mnaweza kuona kwanini niliamuwa kutaka kuowa mke wa pili. Kuna mtu nilipomweleza matatizo yangu alinishauri hivyo.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Sasa mwanamme anatoaje talaka? Sheria inampa mamlaka ya kutoa? Na kama mwanamme anatoa talaka ina maana jaji hana umuhimu katika shauri la talaka?
   
 8. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  wanasema za kuambiwa changanya na zako
   
 9. j

  jobseeker Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijui kwa dini nyengine lakini kwa dini ya kiislamu mume ndie anaetoa talaka na hakuna hata haja ya kushirikisha jaji au mahakama. Anachotakiwa ni kuwa na mashahidi anapofanya hicho kitendo, infact anatakiwa kutamka tu mfano "fulani binti fulani nimekuwacha, wewe si mke wangu" and thats wameachana, yanayofuata baadae mambo ya kuregister na mengineyo yanategemea na sheria za nchi mliopo. Kwa ufupi mume akishatamka tu kuwa nakuacha basi ndio mke ameachika hata kama mume hakuweka signature popote pale.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Duuh! Kama ni kweli hivyo ndivyo ilivyo basi kaazi kweri kweri.

  Yaani kwa hiyo ina maana mwanamke anaweza akawa kwenye abusive marriage na asijichomoe toka kwenye hiyo hali hadi mumewe apende? Hata akipigwa mangumi na kung'olewa meno hana jinsi....ni kuvumilia na kusamehe saba mara sabini?

  I am trying to make sense of that nonsense but I just can't.
   
 11. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  shauri lako,ngoja na huyo mke wa pili aje na visanga vyake....ukienda huku gubu,ukirudi huku gubu. ndio kiranga kitakavyokukoma....kama mkeo shida yake talaka si umpe tu na wewe uwe free kumuoa unayemtaka???......holding onto dead relationship...is not healthy,not for you,not for anybody else.
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mkuu Divorce ni swala la kisheria zaidi kwa dini zote mbili uislamu na ukristo, na marriage certificate kwa dini zote zinatolewa na serikali hivyo basi mbele ya court of law kama hakuna divorce document ya mahakama hapo mwanamke ana uwezo wa kuclaim madai yoyote anayostahili kuclaim mke.

  Ndio maana wakristo wanasema ndoa ya kanisa utenganishwa na kifo tu, lakini mkristo ukiamuwa kuachana na mume/mke unakwenda kuflame kesi mahakamani na Jaji ana mamlaka ya kuvunja ndoa hiyo kitu utakachomis wewe ni kwamba kanisa litakuwekea pingamizi kufunga ndoa nyingine kwahiyo utapaswa kufunga ndoa ya kiserikali au kimila tu. thats it
  NB: Mambo haya ya ndoa kwa Nyumbani Tanzania yanaendeshwa kwa kutumia busara zaidi kuliko sheria kama walivyo wenzetu mamtoni ambao wao wanaongozwa na sheria tu.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Kuna siku Mwanakijiji alianzishaga mada kuhusu kulegeza sheria ya ndoa Tanzania na kugusia kama kuwepo na kipengele cha "no-fault" divorce, na mimi nilipounga mkono watu hawakunielewa kabisa.

  Ila sijabadili mtazamo. No-fault divorce bado naifagilia, tena sana tu. Na kwa Tanzania ndoa nyingi ni maigizo tu. Wanandoa wanazini kuliko ambavyo watu wako tayari kukiri.

  Midanguro (gesti) imejaa kila kona na patrons wake wengi nadhani ni wanandoa. If that's not the apex of hypocrisy, then what is?
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  uki deal na wanawake kwa kiburi cha 'haki yangu'
  watakusumbua sana....

  wanawake nenda nao kama watoto wadogo...
  wape 'pipi' na 'ice cream' kila mara...na 'uwaimbie imbie nyimbo'...
  ndo wanaenda...
   
 15. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hahahaaa imebidi nicheke....NN, Matola amekujibu vizuri.
  Tatizo kuna watu hawaelewi na wengine wanapotosha wenzao kuwa mwanaume ndio anaetoa talaka(kwa waislam sawa) lakini kisheria mnakua mmeshapitia ngazi kadhaa mpaka kufikia mahakamani na anaetoa talaka ni hakimu anaeona kuwa kweli nyie vilaza wawili hamuwezi kuendelea kuishi pamoja na si ww(mwanamke/mwanaume)na hamna signature yoyote unayoweka!!! Kila mtu anapewa karatasi lake mnaingia mitini....waiiii watu bwana wanadanganyana sana.
   
 16. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umegusa penyewe na ukikaa na hao wanandoa wanakutajia na mida yao mizuri ya kuzuka huko ili husband/wife asijue teh teh teh teh......bongo tambarare!
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaaaa Wabongo tuko wasanii sana. Halafu kuna kitu kingine nimgendua.

  Hizi gesti zina biashara nzuri sana na ndiyo maana huwa zinadumu kwa muda mrefu. Na hii longevity ni kwa sababu demand yake ipo muda wote kwa sababu ya watu kucheat.

  Kuna gesti moja ipo Sinza karibu na Meeda pale inaitwa La Paloma. Hii gesti bana ina zaidi ya miaka 20 na mpaka leo hii ipo. Gesti yenyewe ukiiona imechoka vibaya. Hutumiwa sana na wale wadada poa wa pale Meeda.

  Nadhani ni eneo (gesti) ambalo linafaa katika kuwekeza. Ni biashara iliyo recession proof.
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Kwa mimi mwenye experience ya kutafuna wake za watu muda mzuri wa kumla mke wa mtu ni kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni make sure umemrelease na kwa wanaume walioowa sishauri uchukuwe demu baada ya kupombeka usiku ndio unaenda naye kwenye game ukinogewa ni lazima ulale nje au urudi home alfajili, hapa unaaribu ndoa yako mwenyewe. kwahiyo mwanaume unashauriwa uache kazi ufanye kazi mida ya kucheat walio kwenye ndoa ni saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni, saa 12 jioni upo kwa mkeo kimyaa!!
   
 19. huzayma

  huzayma Senior Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtu anakutia panzi wa roho uko nae tu, dah! mie uvumilivu wa namna hiyo Mungu ameninyima , we muache bwana life is too short, kwanini uishi kwa kujitesa na uwezo wa kuepuka mateso unao.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Sasa katika hiyo time-frame ya saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni utammegea wapi? Nyumbani kwako?
   
Loading...