Hakatwi mtu hapaaa! Lowassa anaaminika kwa wengi

12STONE

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,184
398
Dalili ya Mvua ni Mawingu,Wingi ama ukubwa wa Mvua hutegemea sana Mwonekano wa Mawingu ukoje angani.

Wanaona wapambe wa makundi ya wataka Urais ndani ya CCM wakitaabika sana na kutumia muda wao mwingi,nguvu zao nyingi,Propaganda zao chafu iwe kwenye mitandao ya Kijamii,Runinga,Radioni ama Magazetini ili kujitahidi kumdhibiti EDWARD NGOYAI LOWASSA ASIYEZUILIKA KWA SAFARI YAKE YA MATUMAINI ALIYOIANZISHA PAMOJA NA WANANCHI KUELEKEA MAGOGONI.

Wako wachache sana waliobakia na Imani za kiwendawazimu kuwa Jina LOWASSA LITAKATWA MAPEMA SANA.Kama ndio ilivyo,basi huo nao utakuwa ni Uchizi na kujiondoa Akili kwa VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Gonja niulize Maswali,najua mtayajibu tu.

1.Je! Ni kweli Mnapuuza Nguvu alonayo HON.EDWARD N.LOWASSA NDANI NA NJE YA CCM???

2.Mnaona jinsi anavyokubalika na kupata WADHAMINI WENGI KULIKO WATANGAZA NIA WOOTE??

3.Mnafikiri ni vyepesi kiasi hicho kulikata jina EDWARD???

4.Nini faida na hasara ya kulikata jina la LAIGWANANI LOWASSA???

Kuna mbinu za kizamani sana mnajaribu kizitumia mkidhania mtabaki salama kwa kufanya maamuzi yao kitoto na kizembe dhidi ya EDNGOLO.
Mkiupindisha ukweli UKAWA Watangaza USHINDI WAO saa tatu asubuh mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu 25 Octoba 2015.

Mnahaha sana kufuta nyayo za huyu mtu na hakuna hata unyayo ambayo umefutika,Kila mnalopanga linaharibika mara baada ya kuinuka tu kwenye viti mlokalia.Mitego yote haijamnasa anawatangulia maili 12 mbele,KAMWE HAMTAMWEZA EDO NI MTU WA WATU,Mkijitahidi sana kwa shingo ngumu kuonyesha ninyi ndio wenye kisu cha kukatia virigisi,HII CHAMA ITAMFIA JK MIKONONI MWAKE.BUSARA NI HII.

NAWASHAURI BURE:-
Hili game liacheni liwe fair dk 90 hadi 120 pakiwa bado hali ni tete matokeo hayasomi nendeni naye hata kwenye PENALTY ILI AWE MSHINDI.

-Msisahau WATANZANIA HAWAHITAJI RAIS MLINDA MASLAHI YA MTU AWAYE YOTE.
-Wakimkosa Rais wamtakaye ndani ya CCM Watampata UKAWA.

Mnaona wenyewe alivyopokelewa na kudhaminiwa na watu sio haba ,SAUTI ZA WATU NI SAUTI YA MUNGU.

Msiingize Udini,Ukanda wala Ukabila maana kote huko huyu jamaa ANAKUBALIKA.

MAFURIKO HAYAZUILIWI KWA MKONO,NA KWA STYLE HII HAKATWI MTU HAPAA LOWASSA MPAKA MAGOGONI.
 
Safari ya matumaini iliyoishia njiani, hakuna aliyechukua form ya Urais wa Monduli akajaribu huko kusiko na utitiri wa wagombea.
 
Safari ya matumaini iliyoishia njiani, hakuna aliyechukua form ya Urais wa Monduli akajaribu huko kusiko na utitiri wa wagombea.

imeku-pain sana leo utalala usingizi wa mang'amung'amu.
 
Usingizi wa mang'amung'amu utalala weye unayehangaika kumpigia chapuo huyu fisadi ambaye ameshakuweka kwenye payroll yake. Mtu hata kuongea hajui na historia ya nchi haijui juzi karopoka eti miaka 58 tangu tupate uhuru kwi kwi kwi kawahini kuchukua form ya kugombea Urais wa Monduli msije mkakosa na kule pia.

kakojoe ulale

lowassa is too big for you
 
Fisadi Lowassa aliulizwa kuhusu mabilioni aliyokuwa anatoa rushwa kwenye nyumba za ibada kayapata wapi, akadai si pesa zake ni za marafiki zake. Akaambiwa aweke list ya majina ya hao marafiki zake na kiasi alichotoa kila mmoja mpaka kesho kutwa anang'aa macho kuiweka hadharani hiyo list aliyoombwa miezi chungu nzima iliyopita.

Billioni zipi wew ushahidi unao?
 
"Lowasa ni Muongo wa jamhuri ya muungano wa Tanzania"-Makongoro akiwa Shinyanga
 
SIJAWAHI ONA JAMBO LA AINA HII KABISA YAANI WAGOMBEA WOTE WA URAIS KUMSHAMBULIA MGOMBEA MMOJA TU TENA KWA NGUVU NGUVU ZOTE BILA AIBU,YAANI NINYI NYOTE 30 NA USHEE KUANGUASHA GADHABU ZENU KWA KIUMBE MMOJA TU/hakika haijapata tokea
 
kakojoe ulale

lowassa is too big for you

Network imekupotea? uko juu ya mti? mbona umeandika mara nyingi inachokionesha humu ni chuki binafsi dhidi ya Lowassa,mzuka umepanda na unatokwa na povu kweli huku pressure inapanda na kushuka angalia usije dondoka huko uliko MWAKA HUU IMEKULA KWENU LOWASSA NDIO HABARI INAYOSOMEKA NA KUELEWEKA.
 
Lowassa kuingia Ikulu ni ndoto.

Ndio ni ndoto yake ya siku nyingi hajakurupuka kama wengine,anajua Akiingia Ikulu Aanze na nini na aishie na kipi.

MEMBE alisema Urais mpaka AOTESHWE kaa BABU WA LOLIONDO,Hakusubiri aoteshwe kafyatuku ovyo kuusaka Urais na Msaada wa fedha kutoka Mashariki ya mbali.
 
Tukimkosa lowasa ndani ya ccm tutampata nje ya ccm, lowasa tosha tumechoka kulima kwa jembe la mkono tumechoka na manyanyaso ya mgambo wajiji.
 
Fisadi Lowassa aliulizwa kuhusu mabilioni aliyokuwa anatoa rushwa kwenye nyumba za ibada kayapata wapi, akadai si pesa zake ni za marafiki zake. Akaambiwa aweke list ya majina ya hao marafiki zake na kiasi alichotoa kila mmoja mpaka kesho kutwa anang'aa macho kuiweka hadharani hiyo list aliyoombwa miezi chungu nzima iliyopita.

Aliambia na nani???

Aweke hadharani ili iweje?
 
Back
Top Bottom