mpendwa wangu sijapata PM yako jamani, plz nitumie tena love, unajua Aunty Lao hii kitu inaumiza kupitiliza, yaani akikaa ni kuliaa tu, aliacha kusomesha wadogo zake ili amsomeshe kwanza mumewe wajikwamue,matokeo yake ndio haya! inaumiza sana anajuta lakini ndio hivyo tena, uwezo wa kimaisha anao, na ndio plan yake kuondoka but akifikiria hiyo nyumba mume alikuwa na kiwanja mke akaona ni bora ajenge hapo wakae kwao, nyumba ni nzuri sana kajenga kwa nguvu zake kwa mama yake mzazi ni ka nyumba ka kawaida tu, analia kwa mengi! ningejua ningesomesha wadogo zangu nipate baraka za wazazi, ningejua ningemjengea mama yangu nyumba kama hii anipe baraka..ningejua...ningejua....
Investing for the future - would be wife/hubby!
Hii kitu ya kumsomesha potential wife or hubby haijakaa sawa jamani.Hii ni mara ya kwanza kwangu kusikia mwanamke akimsomesha mwanaume ili hatimaye waje wakae na kujenga maisha.Nimeona wanaume wengi wakilia mwisho wa siku kwa vile waliwekeza kumsomesha msichana.Alipohitimu tu akatoka barutiii!
May be kuna somo hapa... kwamba wakati uko busy kujinyima umsomeshe mtu... hata kama hakupendi anajifanya anakupenda ili usimchomolee fuse! Akifanikiwa kupata elimu yake humuoni tena.Sina maana kutonesha jeraha ila nimeona niliseme hapa maana wanaume wengi wamelizwa na wasichana/wachumba zao.
wapo katika ndoa kwa miaka 4 sasa, wamejaaliwa baby gal
...mume alivyomwambia" but samahani sana kukutaarifu kuwa anakuja na mke mwenzio kutoka kijijini nina twins nae wana mwezi 1, mama kaonelea waje tutambuzane coz nae ni mke wa ndoa kama ulivyo wewe"...
...mama mkwe ni visa na vituko anasema yule mjukuu wa kwanza siowa mwanae bali wake ni hao twins wachangaa, maneno ya kejeli kutok kwa mama mkwe hana raha, imekuwa kero, ...
mpendwa wangu sijapata PM yako jamani, plz nitumie tena love, unajua Aunty Lao hii kitu inaumiza kupitiliza, yaani akikaa ni kuliaa tu, aliacha kusomesha wadogo zake ili amsomeshe kwanza mumewe wajikwamue,matokeo yake ndio haya! inaumiza sana anajuta lakini ndio hivyo tena, uwezo wa kimaisha anao, na ndio plan yake kuondoka but akifikiria hiyo nyumba mume alikuwa na kiwanja mke akaona ni bora ajenge hapo wakae kwao, nyumba ni nzuri sana kajenga kwa nguvu zake kwa mama yake mzazi ni ka nyumba ka kawaida tu, analia kwa mengi! ningejua ningesomesha wadogo zangu nipate baraka za wazazi, ningejua ningemjengea mama yangu nyumba kama hii anipe baraka..ningejua...ningejua....
Anataka ushauri gani ilihali kila kitu kiko wazi kwamba hatakiwi? Ila naomba kufahamishwa hali yake ya uchumi kwasas ikoje maana ulisema alimfadhili mumewe kusoma, kama ipo bomba basi aende akaanze maisha upya siamini kama mtoto mmoja atamshinda kumtunza.
Ila kuna kitu nimejifunza ( ikizingatiwa ilikuwa nimeiona na kuisikia kwa wanawake zaidi) kuwa kumsomesha mwenza wako ni hatari kuliko hatari yenyewe, kwani akifanikiwa kimaisha kwa msaada uliompa basi kuucha ni wajibu.
Aksante mtoa mada
Jamani yote yaweza kutokea 1. kuwa anajaribu kupata sympathy na 2 ni kweli yametokea. Katika dunia ya sasa si ajabu kabisa kwa haya kutokea. Ndoa zina mambo na kuta nne zinaficha mengi. Naungana mkono na dada Dina hapo kuwa si rahisi kumshauri mtu katika hili lakini yeye mwenyewe atizame future yake na mtotot. Hali ikishafika hivi si rahisi kubadilika na kurudia hali ya kawaida labda MUNGU aingilie kati.
Binadamu tu wepesi wa kusahau mema tuliyotendewa na wenzi wetu.
Mama huu sio mwisho wa dunia na wala huyo s mwenye kengele peke yake!! kaza moyo songa mbele tena na tikeeti unayo kabisa.. ningekuwa mimi............ah kama nanawa vile maana ishakuwa wizi mtupu
wapo katika ndoa kwa miaka 4 sasa, wamejaaliwa baby gal, mume alikaa muda mrefu sana bila ya kazi coz kule alikokuwa anafanya alipata matatizo akafukuzwa kazi, kapelekwa shule kwa pesa ya mkewe, katafutiwa kazi nzuri na mkewe walikuwa na maisha mazuri/maelewano na kila jema, mume kaanza kubadilika, leo akirudi ni kumpiga mke, kesho ni kutafuta sababu ili mradi wagombane, mke kavumilia yote mpaka majuzi mume alivyomwambia" mama anakuja kutoka kijijini but samahani sana kukutaarifu kuwa anakuja na mke mwenzio kutoka kijijini nina twins nae wana mwezi 1, mama kaonelea waje tutambuzane coz nae ni mke wa ndoa kama ulivyo wewe"...wamekuja hapo ndani hapakaliki mama mkwe ni visa na vituko anasema yule mjukuu wa kwanza siowa mwanae bali wake ni hao twins wachangaa, maneno ya kejeli kutok kwa mama mkwe hana raha, imekuwa kero, rafiki yangu ni kulia kulia tu, anasema ana mpango wa kuwaacha hapo ndani akaanze maisha mapya, nilikosa ushauri wa kumpa.
tumsaidie jamani.
mpendwa wangu sijapata PM yako jamani, plz nitumie tena love, unajua Aunty Lao hii kitu inaumiza kupitiliza, yaani akikaa ni kuliaa tu, aliacha kusomesha wadogo zake ili amsomeshe kwanza mumewe wajikwamue,matokeo yake ndio haya! inaumiza sana anajuta lakini ndio hivyo tena, uwezo wa kimaisha anao, na ndio plan yake kuondoka but akifikiria hiyo nyumba mume alikuwa na kiwanja mke akaona ni bora ajenge hapo wakae kwao, nyumba ni nzuri sana kajenga kwa nguvu zake kwa mama yake mzazi ni ka nyumba ka kawaida tu, analia kwa mengi! ningejua ningesomesha wadogo zangu nipate baraka za wazazi, ningejua ningemjengea mama yangu nyumba kama hii anipe baraka..ningejua...ningejua....
Suala la yeye kuachana na huyo mwanaume nadhani halina mjadala labda kama anapenda kukaa kwenye ndoa ya mitala. Mjadala hapo ni wa namna gani ya kuondoka na pia majaaliwa ya mtoto.
Nyamayao, heshima yako dadangu.
Kuna dada niliwahi kumsaidia kupata haki zake hapo Dar. Mume waliyekuwa wamezaa mtoto mmoja wa kiume aliamua kuoa mwanamke mwingine. Huyo dada ndiye aliyemnyanyua jamaa kutoka mavumbini. Dada aliweza kupata nyumba yake at the end of the day.
Tukirudi kwenye suala la huyu dada, anazo haki zote za msingi ( haijalishi kama alifunga ndoa au la almradi tu waliishi kinyumba na kujulikana kama mume na mke(Presumption of Marriage).
Anaweza kufungua kesi ya madai kudai haki zake na tena kama yeye ndiye aliyekuwa mtafuta ridhki mkuu ( Bread winner) basi hapo anaweza kupata bingo ya nguvu kwenye mgawanyo wa hizo mali (kama akiamua kufuatilia haki zake).
Sheria ya ndoa ya 1971 inamlinda huyo dada vizuri tu.
Tukiachana na upande huo wa madai, tuje kwenye suala la maisha ( social life). Mwambie huyo dada amrudie mja wake manake asije kujikuta anaingia kwenye shimo jingine kwani mabazazi ni wengi humu duniani.
Mpe pole sana na mwambie hiyo ni sehemu ya maisha na akubali kwamba ni kweli yamemtokea na asimame kidete kumwonesha mtalaka wake mtarajiwa kwamba yes she can get there without him na asiruhusu hali ya kujiona yeye si kitu ten! We all stumble in life but never fall.
Shadow.
Mambo ya mitala siku hizi yamepitwa na wakati, hiyo nyumba inabidi aachane nayo.Kwakuwa bado ana uwezo wa kufanya kazi Mungu atamsaidia tu. Kubaki kwenye hiyo nyumba ni kujiongezea matatizo tu. Ila kabla ya kuanza ahakikishe anawasiliana na wanasheria ili wampe mwongozo haki itendeke, huyo mama mkwe asije akadhani kuwa atafaidi kilichomo humo ndani kwa kumuondoa huyo dada. Na kuhusu huyo mtoto wala asijali.Kwa kuwa mama mkwe ameshasema kuwa huyo mtoto sio wao, aanze naye (ni wake 100%). Na ikiwezekana wakaandikishane kabisa. Maana watu wamezoea kukataa watoto, baadae wakiona watoto wamefanikiwa wanajitia kujipendekeza