hajielewi

Nyamayao

JF-Expert Member
Jan 22, 2009
6,966
2,352
wapo katika ndoa kwa miaka 4 sasa, wamejaaliwa baby gal, mume alikaa muda mrefu sana bila ya kazi coz kule alikokuwa anafanya alipata matatizo akafukuzwa kazi, kapelekwa shule kwa pesa ya mkewe, katafutiwa kazi nzuri na mkewe walikuwa na maisha mazuri/maelewano na kila jema, mume kaanza kubadilika, leo akirudi ni kumpiga mke, kesho ni kutafuta sababu ili mradi wagombane, mke kavumilia yote mpaka majuzi mume alivyomwambia" mama anakuja kutoka kijijini but samahani sana kukutaarifu kuwa anakuja na mke mwenzio kutoka kijijini nina twins nae wana mwezi 1, mama kaonelea waje tutambuzane coz nae ni mke wa ndoa kama ulivyo wewe"...wamekuja hapo ndani hapakaliki mama mkwe ni visa na vituko anasema yule mjukuu wa kwanza siowa mwanae bali wake ni hao twins wachangaa, maneno ya kejeli kutok kwa mama mkwe hana raha, imekuwa kero, rafiki yangu ni kulia kulia tu, anasema ana mpango wa kuwaacha hapo ndani akaanze maisha mapya, nilikosa ushauri wa kumpa.

tumsaidie jamani.
 
Last edited:
Suala la yeye kuachana na huyo mwanaume nadhani halina mjadala labda kama anapenda kukaa kwenye ndoa ya mitala. Mjadala hapo ni wa namna gani ya kuondoka na pia majaaliwa ya mtoto.
 
Mwambie atoe timu, nadhani kama bado hajakwaa virus bado vitakuwa njiani, yaani mwambie afanye fasta, kwani vipi tena wanawake si mnapenda uhuru wa kujiamulia sasa imekuwaje? The guy is a big tym sucka!!Mbona easy tu!
 
Aisee hii nayo ni kali!Huyo mama mkwe nae mshari sana na inawezekana wakwe ndo walimshinikiza mtoto wao aoe mke mwingine labda kuna tatizo kati ya huyo dada na wakwezake!Mbaya zaidi mme wake inaonekana anawasikiliza sana wazazi wake kuliko mke wake!Namuonea huruma huyo dada hana pa kukimbilia zaidi ya kusugua magoti namaanisha amwombe sana MUNGU!Pia kama mila za jamaa zinaruhusu mitaala hapo hana ujanja!avumilie tu kuishi kwenye uke wenza!
 
Jamani za leo, kwa kweli topic yako imenigusa sana Nyamayao, tena kabla sijasahau mbona PM yangu hujanijibu shostiiii! Sasa mwenzangu kuhusu huyo dada na maongezi yako inaonekana kabisa anajiweza kimaisha. Jamani mapenzi hayalazimishwi na kila shetani na mbuyu wake, ushauri wangu ni bora aondoke na mapemaaaa kabla haka kageni ketu(VVU) hakajaanza kumtambalia kwa kweli. Tena amshukuru Mungu kwa kujibu maombi yake tayari naendelee kumuomba atampa wake watakaye pendana kuliko. Jamani mpe pole shosti wetu mwaya na tunamtakia kila la kheri.
 
Mmh!..
Hamna jinsi hapo zaidi ya kuachana na huyo mwanaume maana anashuhudia vituko vyote wala hajahadithiwa.
Hamna mtu anayependa kuachana na mume/mke wake kiholela lazima kuna sababu maalum,hivyo hilo swala la huyo dada linaeleweka kabisa.
Maisha mafupi na kila mtu ana nafasi moja tu ya kuishi,ukifa hurudi tena duniani. Hivyo furahia maisha siyo kujitesa kisa penzi japo ni ngumu kumuacha mtu unayempenda.
Mshukuru Mungu una mtoto. angalia maisha yako yanapoenda,mlee vizuri mwanao.
Malipo duniani hata usipomlipa wewe atalipwa na mtu mwingine.

Bel.
 
wapo katika ndoa kwa miaka 4 sasa, wamejaaliwa baby gal, mume alikaa muda mrefu sana bila ya kazi coz kule alikokuwa anafanya alipata matatizo akafukuzwa kazi, kapelekwa shule kwa pesa ya mkewe, katafutiwa kazi nzuri na mkewe walikuwa na maisha mazuri/maelewano na kila jema, mume kaanza kubadilika, leo akirudi ni kumpiga mke, kesho ni kutafuta sababu ili mradi wagombane, mke kavumilia yote mpaka majuzi mume alivyomwambia" mama anakuja kutoka kijijini but samahani sana kukutaarifu kuwa anakuja na mke mwenzio kutoka kijijini nina twince nae wana mwezi 1, mama kaonelea waje tutambuzane coz nae ni mke wa ndoa kama ulivyo wewe"...wamekuja hapo ndani hapakaliki mama mkwe ni visa na vituko anasema yule mjukuu wa kwanza siowa mwanae bali wake ni hao twince wachangaa, maneno ya kejeli kutok kwa mama mkwe hana raha, imekuwa kero, rafiki yangu ni kulia kulia tu, anasema ana mpango wa kuwaacha hapo ndani akaanze maisha mapya, nilikosa ushauri wa kumpa.

tumsaidie jamani.

Just curious...what is Twince?!...
 
Aisee hii nayo ni kali!Huyo mama mkwe nae mshari sana na inawezekana wakwe ndo walimshinikiza mtoto wao aoe mke mwingine labda kuna tatizo kati ya huyo dada na wakwezake!Mbaya zaidi mme wake inaonekana anawasikiliza sana wazazi wake kuliko mke wake!Namuonea huruma huyo dada hana pa kukimbilia zaidi ya kusugua magoti namaanisha amwombe sana MUNGU!Pia kama mila za jamaa zinaruhusu mitaala hapo hana ujanja!avumilie tu kuishi kwenye uke wenza!

hakuwa na ugomvi nao kabisa but inaonekana mama mkwe alikuwa ana pretend kumpenda mka mwana wake, kuna siku tulienda kijijini kwa huyo mama mkwe alikuwa amefiwa na kakake yani mjomba wa mume, mama mkwe alionyesha upendo wa ajabu kwa mka mwana wake kumbe ni ku pretend tu mana rafiki yangu ndio alikuwa anahudumia msiba mpaka walipovunja tanga, coz mume alikuwa hana kitu, mama mkwe ni kama hivyo tena, nilihamaki nilivyoambiwa huyo mama kafanya alichofanya.
 
Jamani za leo, kwa kweli topic yako imenigusa sana Nyamayao, tena kabla sijasahau mbona PM yangu hujanijibu shostiiii! Sasa mwenzangu kuhusu huyo dada na maongezi yako inaonekana kabisa anajiweza kimaisha. Jamani mapenzi hayalazimishwi na kila shetani na mbuyu wake, ushauri wangu ni bora aondoke na mapemaaaa kabla haka kageni ketu(VVU) hakajaanza kumtambalia kwa kweli. Tena amshukuru Mungu kwa kujibu maombi yake tayari naendelee kumuomba atampa wake watakaye pendana kuliko. Jamani mpe pole shosti wetu mwaya na tunamtakia kila la kheri.

mpendwa wangu sijapata PM yako jamani, plz nitumie tena love, unajua Aunty Lao hii kitu inaumiza kupitiliza, yaani akikaa ni kuliaa tu, aliacha kusomesha wadogo zake ili amsomeshe kwanza mumewe wajikwamue,matokeo yake ndio haya! inaumiza sana anajuta lakini ndio hivyo tena, uwezo wa kimaisha anao, na ndio plan yake kuondoka but akifikiria hiyo nyumba mume alikuwa na kiwanja mke akaona ni bora ajenge hapo wakae kwao, nyumba ni nzuri sana kajenga kwa nguvu zake kwa mama yake mzazi ni ka nyumba ka kawaida tu, analia kwa mengi! ningejua ningesomesha wadogo zangu nipate baraka za wazazi, ningejua ningemjengea mama yangu nyumba kama hii anipe baraka..ningejua...ningejua....
 
- I was once told " kila chenye mwanzo kina mwisho " e.g. barabara ya Cairo -to- Cape. I'm not certain if these wise word applies to "marriage".

- Hawa walikuwa "wameoana" au ni "sogea tuishi"?

- Je umeweza kupata undani ya maisha yao .. before "ndoa"? Is it possible kwamba mwanamume alimsomesha mwanamke wakati wakiwa "wachumba"?

- Ni mtizamo tu!
 
Akina baba na mama zao, mmh mpaka wakati mwingine wanashindwa kujiamulia mambo yao wenyewe.....Si ajabu aliambiwa kuna binti mashallah yupo kijijini tena ana uzazi nje nje sio huo wa mkewe wa kubania....

Tatizo la kutoa ushauri maeneo haya ni moja, tunaweza tukawa tunaona kuwa kwa mtazamo wetu huyo bibie ajifungashie kilicho chake aanze, asije akalibamba limuheshimiwa (VVU) huku anajiona. Pitia jioni maeneo ya barazani kwao, aah wenyewe wameshikana mikono na tabasamu tele mdomoni, mtoa ushauri unabaki kukwepesha macho......
 
labda huyo mke si kabila lao!maana kuna wazazi wengine hawapendi watoto wao waoe kabila tofauti na lao!
 
mpendwa wangu sijapata PM yako jamani, plz nitumie tena love, unajua Aunty Lao hii kitu inaumiza kupitiliza, yaani akikaa ni kuliaa tu, aliacha kusomesha wadogo zake ili amsomeshe kwanza mumewe wajikwamue,matokeo yake ndio haya! inaumiza sana anajuta lakini ndio hivyo tena, uwezo wa kimaisha anao, na ndio plan yake kuondoka but akifikiria hiyo nyumba mume alikuwa na kiwanja mke akaona ni bora ajenge hapo wakae kwao, nyumba ni nzuri sana kajenga kwa nguvu zake kwa mama yake mzazi ni ka nyumba ka kawaida tu, analia kwa mengi! ningejua ningesomesha wadogo zangu nipate baraka za wazazi, ningejua ningemjengea mama yangu nyumba kama hii anipe baraka..ningejua...ningejua....

Hakuna haja ya kukaa na kujuta kwani nina uhakika wakati anayafanya hayo alijua anafanya kitu sahihi,kwa sababu imekuwa ndivyo sivyo ni kujipanga upya na kuangalia nini cha kufanya,MAISHA NI LAZIMA YAENDELEE.Mpe pole sana,sometime life is not fair.
 
- I was once told " kila chenye mwanzo kina mwisho " e.g. barabara ya Cairo -to- Cape. I'm not certain if these wise word applies to "marriage".

- Hawa walikuwa "wameoana" au ni "sogea tuishi"?

- Je umeweza kupata undani ya maisha yao .. before "ndoa"? Is it possible kwamba mwanamume alimsomesha mwanamke wakati wakiwa "wachumba"?

- Ni mtizamo tu!

hapana! mwanamke alisomeshwa na wazazi wake, ni mtu wangu wa karibu sana naweza kukueleza machache! walipokutana mwanaume kwa wakati huo ndio alikuwa na kazi mwanamke ndio amemaliza chuo, wakaingia uchumba, mwanzoni mwa ndoa mwanaume akapata matatizo, mwanamke ndio akaamua kumpeleka skul, ndoa yao ilikuwa na kila jema! sijui shetani gani jamani.
 
labda huyo mke si kabila lao!maana kuna wazazi wengine hawapendi watoto wao waoe kabila tofauti na lao!

ni makabila tofauti! nadhani mama mkwe ndio anajua ukweli wa hili jambo kwamba kwanini kaamua kufanya hivyo, kama ni kabila hilo alijua kuanzia mwanae alivyoenda kijijini kumtambulisha mchumba, mbona kwa wakati huo asiseme ni kabila tofauti simtaki?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom