TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,721
- 10,224
Augustine Azuka 'Jay Jay' Okocha, Mchawi na Hizi yake kutoka Enugu
Usiku mmoja kule Kusini Mashariki mwa nchi ya Nigeria, Jimboni Enugu ile Agosti 14, 1973 alizaliwa Mchawi mmoja wa soka wakuitwa Augustine, ndio ni Augustine tu
Mitaa ya Enugu haikutaka kumwacha salama na jina lake la Augustine, wakaona kuna haja ya kumpachika jina la Jay Jay, ndipo wazungu na dunia tukaona isiwe kazi acha tumuite Jay Jay Okocha.
Mama yake Mzazi anakumbuka akimtuma dukani lazima atachelewa kurudi, atabetua chochote atakachokuta njiani, atasahau alichotumwa kama ataona watoto wanalipiga kandanda, alikua na uwezo wa kupiga danadana mpaka kitunguu au nyanya. 😊
Mechi za mtaani kwao ziligubikwa na majonzi kwa wapinzani, chenga zake zilitegua nyonga, watoto walivishwa na kuvuliwa makanzu, alifanya kila aina ya utukutu wa soka "football crimes".
Ushuhuda na maajabu waliokuwa wakishuhudia huko Enugu, Kusini Mashariki mwa Nigeria ulipaswa kutazamwa duniani kote, haikutosha klabu za Nigeria kuona mabalaa yake, bali burudani hii ilihamia duniani kote.
Jioni moja ya 1990, Okocha anasafiri mpaka Ujerumani Magharibi, kipindi hicho wametoka kutwaa kombe la dunia, Okocha safari yake ilikuwa kwenda kumpa salaam mshikaji wake alikua anakipiga Borussia Neunkirchen, ndipo hapa dunia ilimtambua.
Okocha alifika mazoezini kwa mshikaji wake, alikaa tu pembeni kutazama mazoezi yao, ila baadae Kocha alimualika afanye nao mazoezi, kilichotokea baada ya pale ni kusaini mkataba😂 ndipo hapo safari ilianza pale Bundesliga.
.
Alisainiwa baadae Frankfurt ya Jupp Hynkes, alifanya maajabu makubwa sana, aliwahi kupiga bao mbele ya Oliver Kahn kwa kumzunguka mara tatu🙌 moja kati ya bao bora mpaka kesho Ujerumani, fundi mmoja Mchawi kutoka Afrika.
Maajabu ya mguu wake yalienda mpaka PSG, pale alikutana na mafundi wenzake kama Dinho, Laurent Robert na Ali Bernabia😊 ila maajabu yote ya Dinho anakwambia yeye kwa Okocha anavua kofia, Dinho anakwambia hajawahi kumuona Jini Mpira kama Okocha.
Mtaalam wa step overs, free kicks na chenga za maudhi, mguu mwepesi na akili nyepesi, Mchawi mmoja kutoka Enugu pale Nigeria, aliyewahi kutimiza na kuweka rekodi pale Bolton.