Haiti na Kilosa: Mtaji wa kisiasa/kibiashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haiti na Kilosa: Mtaji wa kisiasa/kibiashara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GY, Jan 19, 2010.

 1. GY

  GY JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Si wote wanaokimbilia Haiti na Kilosa wanalengo la kusaidia. Ni mapema mno kufanya kama wafanyavyo mataifa makubwa kuhusu Haiti, kwani kwayo ajenda ya kusaidia ni tofauti kabisa

  Vyovyote iwavyo, ya Haiti ni janga lisilokuwa limetarajiwa, lakini ya Kilosa tulijua muda mrefu kuwa kuna mvua nyingi kuliko kawaida ivo hatari ya mafuriko. Serikali inawizara na bajeti ya kushulikia maafa, na mafuriko ya wilaya moja hayawezi kuishinda wizara kumudu mpaka kutoa nafasi kwa kila atakaye kupanda juu kisiasa na kibiashara kupitia tatizo hili apate upenyo

  Nasema ivi, ya Haiti sawa, lakini ya Kilosa situmi hata msg moja kuchangia wakati tatizo li ndani ya serikali. wacha hao wanaotaka kutumia suala hili dogo wapate kujitangaza kibiashara na kisiasa wafanye ivo. Si tumeambiwa Libya wanajenga nyumba 200 kwa Tsh 1.5 bilion. Iwapi mizania ya kulinganisha hifadhi ya familia 200 na ile moja ya gavana wa benki kuu kwa gharama ileile?

  Tusidanganywe, serikali inuwezo wa kukabiliana na hili la kilosa, tusichange!

  Narudia...Tusichange
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Generation.. japo mawazo yako tunaweza kuyaonesha kuwa yana makosa lakini nina uhakika mkubwa kuwa mawazo yako yanawakilisha mawazo ya watu wengi ambao hawawezi kuguswa na majanga yanayotokea Tanzania kwa sababu wanaamini kuwa "serikali" ina uwezo wa kufanya kila kitu.

  Mawazo kama hayo yalioneshwa kuwa yanamakosa kule New Orleans kama yanavyoonekana kuwa yana makosa kule Haiti! Hakuna serikali duniani ambayo inaweza kushughulikia majanga ya asili kwa ukamilifu wote peke yake. Leo hiii tunaona jinsi ilivyo ngumu kusaidia watu wote kule Haiti licha ya uwepo wa mlundiko wa mataifa makubwa na yenye nguvu.

  Kufikiria kuwa serikali ya Tanzania ina uwezo wa kushughulikia majanga ya mafuriko na hivyo iachwe peke yake ni kujitakia mabaya na kujaribu kuwalaani Watanzania wenzetu katika vifo na madhara yasiyohesabika. Hivyo, mawazo yako yakikubaliwa au kukumbatiwa na watu ni ya hatari na kimsingi yanawafanya watu wawe na tumaini la uongo kuwa serikali "itawasaidia".

  Hii ndiyo sababu hata Marekani taifa kubwa wakati wa Septemba 11 na hata sasa wametegemea sana juhudi za taasisi huru za misaada kama Msalaba Mwekundu kuliko kutegemea FEMA! Kuwa na fedha peke yake siyo suluhisho la kutatua matatizo. Unahitaji watu wenye wito, moyo, na utayari wa kwenda kusaidia! Na hadi hivi sasa hakuna watu walio na sifa hizo zaidi ya watu wa Red Cross.

  hii ndiyo sababu sisi wengine tumeamua kuchangia na kuwasaidia Watanzania siyo Kilosa tu bali Bariadi, Hedaru, n.k kwa kupitia chama cha Msalaba Mwekundu.
   
 3. GY

  GY JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mwanakijiji

  I hope u know better than me kuwa nchi uliyoitaja kama mfano ziko highly committed na welfare za wananchi wao in such a way hata wanaweza kujustfy kupelekea misaada nje ya nchi yao. Hilo halina haja ya kulihoji. Mmekuwa very sympathetic na mafuriko yaliyokumba maeneo mbalimbali nchini Tanzania, mafuriko ambayo vyombo mbalimbali vilishayasema muda mrefu tu kuwa yatakuja. Pamoja na misaada mbalimbali na harambee kama hii ya kwenu bado mwenye dhamana ya kusimamia welfare za wananchi ni serikali, nyinyi mnasupplement tu.
  Harambee yenu haitachangiwa na kina Benno Ndulu, Jeetu Patel au Basil Mramba. Itachangiwa na kina Mwarami na Chausiku na Joni ambao wao pia mvua ikinyesha kidogo tu Darisalama na jangwani kufurika wataingia kwenye shida hiyohiyo. Hawa ndio ambao watawachangia hizo msg za sh 150, na ni hao hao ambao huchukuliwa kuku na mbuzi wao pale wanapokosa uwezo wa kuchangia ujenzi wa shule za kata. Na hata mkishafanikiwa kupata hizo bilioni 10 mkapeleka kwenye mafuriko, kesho utasikia serikali imenunua jengo la ubalozi wa Tanzania huko Trinidadi and Tobago kwa sh bilioni 20, au raisi anawasha gulfstream na msururu wake, kwa gharama ya karibu bilioni 2,anaenda china kuwaomba waje watujengee uwanja wa judo pamoja na kututafutia kocha wa mchezo wa rede.

  Unajisikiaje kuisaidia familia ambayo wazazi wake kila siku unawapita baa wakinywa serengeti baridi ili kuichangia Taifa Stars. Unasaidia kuondoa tatizo au unaliongeza. Ifike mahali tuisusie serikali msiba japo mmoja ili wajue kuwa kweli nyie pia mnaumizwa na utumiaji wa kilafi wa pesa za masikini wa kawaida kabisa

  Ipo thread yako moja nilipata kuisoma na kuifurahia sana, ilikuwa inahoji impact ya misaada toka kwa nchi wahisani/wafadhili, je inatusaidia au inatumaliza. Uhisani ni uhisani tu sio lazima utoke nje, hata ukitoka ndani bado unaweza kuwa na impact ile ile. Sijui katika thread ile ulipata picha gani.

  Mtamaliza hili la mafuriko, mtahamia kwenye harambee ya kuchangisha watu ili mnunue madawati ya shule za msingi ambayo hata mwalimu mmoja haina. Na wakati mkiendelea kuwakamu hao masikini wa kawaida kwa msg za sh 150, wenzenu wataendelea kuweka tiles mpaka kwenye fensi ya majengo yaliyojengwa na kutumiwa na kile chombo ambacho ni "the nerve centre of the national economy na kinachoongozwa na the best trained people who are also individuals of the highest integrity in society

  Tusifungue macho kuona na mdomo kusema ikiwa tu jambo limefanywa na wengine, na pale tunapofanya sisi basi lazima iwe tupo sahihi

  Ninapoliona hili ni mtaji wa kisiasa na kibiashara ninaonekana wa ajabu sana kwa sasa, lakini tuvute subira halafu baada ya muda wote tutakubaliana kuwa hili ni zaidi ya sympathy. Na ndio maana hata hiyo michango haipelekwi kimya kimya pale red cross Ali Hasan Mwinyi road, inapelekwa kwa mbwembwe na suti kule kilosa, ikipokewa na wanasiasa walewale

  Ni hayo tu
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hiii ndiyo demokrasia bwana. Na kwa kweli hiari inashinda utumwa. Kwa kuwa kila mtu anayonafasi ya kujichagulia analolipenda basi well, tuache mambo yawe hivyo.
  Naamini kabisa, tena kwa dhati kutoka moyoni mwangu kuwa tabia tuliyonayo ya kuona kila kila jambo halituhusu na ni sual la serikali, limetufanya tumetengeneza matatizo makubwa yanayoturudi wenyewe kuliko tunavyofikiri.
  What a country kama leo serikali na wananchi wote tungeungana kuona wenzetu wanasaidiwa maana walipo wanaadhirika? Nimeshaona mimi mgonjwa aliyehitaji milioni 30 tu akafanyiwe upasuaji jinsi ambavyo alitelekezwa na laiti kama watu wasingelijitolea kutoa chochote basi tungemsahau hii leo.Guess what! Waliomchangia hawakuwa kina Mramba wala Patel. Ni watu wa kawaida wanaojua umuhimu wa kufanya lile jambo na likatekelezeka.
  Kwanini Libya iweze na sisi tushindwe? Mimi sioni kama kila kitu hakiwezekani maana tulipofikia sasa ni kwamba mindset zetu zimetufanya tu relax na tumerelax kwelikweli.
  Well, nakubaliana na uamuzi wako kabisa ila mimi binafsi ambaye si mwanasiasa wala sitegemei siku moja itakuwa hivyo, nitajitoa pale ntakapoona nahitajika.
   
 5. GY

  GY JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Asante kwa maoni yako. Demokrasia inataka hivyo, tukubaliane kutokukubaliana
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  completely silent on this...Sitofungua mdomo wangu...No!
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  no comment mwanakijiji upo sahihi
   
 8. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu kama nimekuelewa vizuri..! na wewe pia una hatia ya kosa lilelile unalowashutumu hao unaowashutumu..! kwasababu hujaangalia kama msaada unaoutoa umewafikia walengwa bali nini wanapata wanaoratibu ukusanyaji wa michango au watoa misaada!

  Hivi wangeenda kimya kimya bila uthibitisho wa picha au kutangaza (ili wasionekane wana malengo ya kisiasa kama unavyodai) na waliochanga wakahoji mbona hatujaona mkikabidhi misaada tuliojitolea wala kusikia chochote kuhusu makabidhiano ya misaada hiyo wangejibu nini..? Wangejitetea vipi kuhusu suala la transparency..?

  Mkuu generation Y kama tuna nia hasa ya kusaidia tusiangalie ni nini hasa waratibu watapata(iwe umaarufu wa kisiasa au nafasi za kibiashara) bali ungeangalia je msaada uliotoa umewafikia walengwa..? kwakua kama misaada inafika lengo letu la msingi limetimia..! Hayo mengine ya kuangalia "Juma" kapata umaarufu kupitia michango yetu sidhani kama yatatusaidia sana!
  Hata wakipata umaarufu tatizo liko wapi? maana wao ndio wamekua mstari wa mbele kuhamasisha hili, basi wanastahili sifa kwenye hilo!
   
 9. GY

  GY JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Umeelewa sehemu ndogo sana ya argument yangu
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Generation-Y sio wote wanao saidi Kilosa wanamlengo au wanajihusisha na siasa, mi nimechangia wahanga wa Kilosa na nitaendelea kuchangia kadri ya uwezo wangu, mi sitokei Kilosa na sina uhusiano wowote na siasa na sioti kugombea nyazifa yoyote ile ila nimetoa mchango wangu kwa kuguswa kama Mtanzania ndo maana nimeamua kuchangia kile kidogo nilicho nacho tuwe na mioyo ya kusaidiana ili tuweze kujikomboa gonjwa kubwa linalo likumba Taifa letu la Maradhi, Umaskini na Ujinga kumsaidia mtu si lazima awe ndugu yako au muwe mnatoka sehemu moja la hasha sisi sote ni binadamu leo wewe unakula unashiba lakini kuna jilani zako hapo mlo mmoja tu wanaupata kwa taabu.
  Kutoa ni moyo na si utajiri ndugu yangu.
   
 11. GY

  GY JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Maadui wa Taifa wako zaidi ya watatu uliowataja hapo juu, tuna adui mpya UFISADI. Tuungane kupambana nae pia
   
 12. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Elewesha tafadhali wapi nimeelewa kidogo?? wapi sijakuelewa??
   
 13. GY

  GY JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Umechukua toka kwenye majibu yangu kwa Mwanakijiji, sehemu ya mwisho tu ya ile post. Comment zako zimelenga hapo tu, hazikutazama nilipoanzia na nilichokuwa najaribu kukileta kwenye hoja. Irudie tu kuisoma halafu utaelewa zaidi.
   
 14. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu Generation pote umesema lakini hayo niliyoyanukuu hapo juu sina namna ya kuyapinga.
   
 15. GY

  GY JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Nashukuru kwa kuliona hilo mkuu
   
 16. GY

  GY JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Tumesikia jana tena raisi ameenda Uswisi kuhudhuria mkutano wa hali ya uchumi. Tanzania, nchi masikini namba 2 duniani inaenda kushiriki mkutano wa hali ya uchumi duniani.

  Hayo ndio walio tayari kuyalipia, safari za kwenda kwenye mikutano ambayo sisi sio participants kabisa, ila tunakuwepo tu.

  Kwanini asiseme kuwa kwa kuwa hali ya uchumi ni mbaya na sasa ivi nchi yake imekumbwa na mafuriko basi pesa za hiyo safari kama anazo azipeleke kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko?

  Au hii safari tunalipiwa?
   
Loading...