Haitakuja tokea ngoma nyingine kali ya Club kama Mikasi ya Ngwair na Mchizi Mox

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Leo nilikuwa zangu Gheto nimepumzika nikaona bora nipige playlist zangu mbili tatu za kitambo nikumbuke Enzi

Aiseee kama bahati hivi nikajikuta nimeitupia ngoma ya Ngwair na Mchizi Mox ya kuitwa Mikasi,
Eeeh bhana eeh nikaisikia mara ya kwanza, nikaireplay mara ya pili nikaona haitoshi nikaweka Na Repeat kabisa ikawa inajirudia rudia na Playlist yangu ikawa imekomea hapo

Wakati nipo naisikia hiyo Ngoma mashairi yake, Mdundo ulivyogongwa na producer P funk(majani), mixing yake ilivyo na Quality mpaka leo na vitu vingine vingi

Nikawa najiuliza hivi huyu Ngwair alikuwa na IQ ngapi maana sio kwa uandishi ule wa Ngoma (Ningekuwa prof: direct baadhi ya ngoma kama hizi ningewasilisha Andiko wizara ya elimu ziwe zinafundishwa shuleni kwenye Fasihi kama wanavyofundisha mashairi )

Nikajiuliza Producer aliyetengeneza beat (Mdundo) na kufanya mixing alikuwa na IQ ya ngapi?

Uandishi wa Ngoma hiyo ya Mikasi ni uandishi bora kabisa wa Mashairi ambao muandishi wake alitumia akili kubwa sana kuwaza,

"kwanza picha linaanza mshikaji anatusimulia kuanzia siku yake ilivyoanza yaani kuanzia anaamka, nguo anazovaa baada ya hapo, mawasiliano ya washikaji zake, kukutana kwenda club, matendo ya humo club mpaka kuondoka kwao"

Ni story yenye mpangilio ambao haimchoshi hadhira kusikiliza zaidi na zaidi huku akipata burudani,

Mgonga beat (mdundo) ndio aliua kabisa.

Kwangu hii ngoma ya mikasi ni kati ya Ngoma yangu bora ya muda wote ya club kutokea Hapa Bongo.

Hongera kwake Ngwair (R. I. P Muhasisi wa east Zoo, East Chambers), hongera kwako Mchizi mox, hongera kwako P Funk(majani) na wote waliokuwa Nyuma ya hii ngoma.

Cc Zero IQ
 
Kuna nyimbo zinafaa kuimbwa mashuleni kila asubuhi, moja wapo ni hiyo ya mikasi. Unaanza wimbo wa taifa, kisha wa shule halafu mikasi then watoto wanaingia madarasani vichwa vikiwa active kukabili sequence and series.

Na kuna ule wa BBM yupo ngwair, Mr. Blue na Diamond.
Sio poa kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom