Haika Lawere wa 'Mbezi Garden' apewa Talaka

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
16,095
Reaction score
24,323
Anaandika MUME (Phares Magesa):

Watu wengi kwa muda mrefu zaidi ya miaka 4 sasa wamekuwa wakiuliza maswali katika baadhi ya posts zangu mama wa watoto hawa mbona hawamuoni ? kwenye picha nyingi ukiacha chache chache sana za matukio muhimu au labda hata kwenye posts za mama yao pia labda baadhi ya watu nao wanauliza/wanajiuliza swali kama hilo .

Ukweli upo hivi;

Mwaka 2001 Phares Magesa na Haika tulioana na ndoa ilifungwa katika Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), mtaa wa Ally Khan, Upanga karibu na DIT au Regency Hospital, sherehe ya harusi baadae ilifanyika ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na watu takribani 1,000 wakati ule, sherehe ilifana sana MC alikuwa FomaFoma.

Wakati namuoa Haika alikuwa ni Mwanafunzi anasomea Shahada ya kwanza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na akamaliza vizuri licha ya kuwa kwenye ndoa akiwa mwanafunzi, na tukiwa ndani ya ndoa nikamshauri asiridhike na elimu aliyoapata na nikamruhusu akasome Shahada ya Uzamili, akaenda Salford University, Uingereza nako pia akamaliza vizuri masomo yake na kwa neema ya Mungu baada ya hapo tukajaliwa watoto wazuri watatu, wawili wa kiume Paxton na Haris na mmoja wa kike Princess.

Mungu amekuwa mwema sana kwetu ametusaidia sana kwa kutuwezesha kufanya kazi na biashara zetu kila mmoja kwa bidii, maarifa, nidhamu na kujituma kwa hali ya juu na kufanikiwa kadri Mungu alivyotujalia.

Baada ya kuwa katika ndoa kwa miaka 21, yaani 2001 hadi 2022 Mahakama ya Mwanzo, Kawe, Kinondoni ilihitimisha shauri la talaka lililokuwa mahakamani hapo kwa takribani mwaka mmoja na kuanzia 2022 kila mmoja akawa huru na kwa sasa tunashirikiana vizuri kulea watoto wetu (Co-Parenting) na tunashukuru Mungu kwa yote.

Ushauri kama hakuna sababu ya msingi ya kuachana na mwenza wako, sishauri wanandoa wowote hasa kama mkiwa na watoto kufikia kirahisi uamuzi wa kuvunja ndoa ni mpaka pale itakapokuwa hiyo ndio njia salama na ya lazima kwa mustakabali mwema wa pande zote tatu yaani Mke, Mme na Watoto.

Usiingie kwenye ndoa kwa nia ya kutaka kuonekana na wewe umo au kwa nia ya ku trend, pia usiachane na mtu kwa sababu hizo hizo.

Mbarikiwe wote mlio kwenye ndoa zidumu na mnaotaka kuingia pia ndoa zidumu,tumtangulize Mungu na kujali famlia zetu.

 
Ujibiwe mkuu
Hawa watto wamesoma FEZA , ni wanafunzi bora Tanzania na pia ni wapo vyuo vikubwa Ulaya kuiwakilisha Tanzania.
Mama yao ni mmilii wa Mbezi Garden , wamegawana na mume baada ya kuachana lakini ni muhimu sana kwa wanaume kuwa makini na hizi ndoa za kuoana mkiwa chuo, unakuta binti ni bikra ama wewe ndio mwanaume wa pili kupita hapo, ikifika siku DUNIA IKAMFUNGUKIA mnaachana maana atakutana na fupi, ndefu, nyembamba na nene.
 
Umeandika ka chawa wa kizimkazi
 
watu wamedumu kwenye ndoa 21yrs alf wanaachana kirahisi tu🤦‍♀️ na wanaamua kumove on kila mtu anaendelea na issue zake,,,

nimejifunza kitu hapa Hata najua basi pita na huku we mkenya ujifunze vitu
Mwanamke ameolewa akiwa chuo IFM, alikuwa hajaichezesha, amepata hela na umaarufu, fungua code mwenyewe.
 
Ikifika hapa ndio utajua TEAM KATAA NDOA WANA FACTS. Hapo huyo mjuba hajataka kutueleza namna walivyopiga pasu mali za ndoa "Merital properties". Hapo huyo bidada kaondoka na settlement ya maana, mali na biashara bila kujali nguvu yake katika kuchuma hizo mali. Kapata mali kwa kuhama "by induction"

Nje ya mada: Taraka ni wizi kwa mwanaume. Hongera sana Haika, unapiga hesabu zako vizuri. Kina manka, haika ni mabingwa wa hizi kazi. Oa tena mkali, uibiwe tena.
 
Eeh Boss Phares imekuaje tena?
Hii kesi inafanana na Ile ya Tajiri Mosha

Mosha alikuwa mjanja, Mosha mali nyingi aliziweka kwenye makampuni ambayo mkewe aliyakuta. Mosha kaokoa mali kibao kupigwa pasu. Usipojua kuficha mali ukiwa kwenye ndoa za mitego, zitaibiwa kwa talaka.

Hili somo mzee wangu akishanieleza sana. Talaka ni wizi, ni ufilisi wa wazi. Talaka inakutoa upepo. Unapoteza mali kwa mujibu wa sheria. Unapigwa pasu jasho lako ulilotoa kwa miaka mingi. Mali yote uliyochuma ukiwa na nguvu inaondoka, inakuwa sio yako tena na wengine wanaenda kuila. Kama una 100 basi unabaki na 40. Tragedy of miscalculation
 
Mbezi garden ni ya Familia ya kina Haika.Baba yao aliwaachia alipofariki dunia. Magesa kaikuta hiyo hoteli kwenye hiyo familia.
 
watanzagiza wamegawanyika sehemu kubwa 2, muslims au mila mila and asilimia ndoogo sana Christian, na mila mila ni de facto muslim, na ndiyo maana wanatawaliwa na kupagazwa na foreign muslims kama rostamu au zanzibaris ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…