hahah Vibuti vyengine bana!! (Single mwaka mzima)

Habari zenu wanaJamii.. Nina imani mko Salama kabisa..

Kwa mara nyengine tena nimekuja na story hii.. inayohusu, ni namna gani nilivyouanza na kuumaliza mwaka wa 2018.

Nirudishe Historia nyuma kidogo mpaka mwaka 2017, ambapo kuanzia mwezi wa 9 mpaka wa 11, niliachana na mabinti wanne ambao nilikuwa nao kwenye mahusiano.. Na mwezi wa 12 nikapata binti mwengine.. ambaye huyu mahusiano yake kidogo yalikuwa serious, kwa maana pia alisisitiza kunipeleka mpaka kwao na alinitambulisha.

Maisha yakaenda na Mwezi ukafika Mwishoni.. Yaani kuukaribisha mwaka 2018 sasa.

Kama ishara ya shukrani na Upendo nikaamua kujitutumua nikamnunulia yule binti simu flani kali ili akaribishie mwaka.. ingawa sikuwa nimemkabidhi

Usiku wake nikaenda mpaka Chuo alichokuwa anasoma.. Nikapaki ndinga nikawa nimekaa naye hapo huku tukisubiri mwaka mpya uingie.. Sasa ile saa tano na nusu inafika.. kidogo wakaja jamaa wawili waliovalia nguo za kiaskari na wakapiga lock Gari yangu, na kuanza kunizingua vibaya, hadi yule binti akaanza kupata wasiwasi.. ila mimi nikawa nawajibu kawaida tuu, na nikafunga gari ..nikasepa zangu kwenye kituo chao kidogo cha polisi ili niepushe utata nikiwa na yule Binti wa watu..

Tuliyazungumza yakaisha na hapo ndipo nilipopata nafasi ya kwenda kutoa gari yangu na kuagana na yule binti mida ya saa 6 na nusu.. yaani mwaka mpya 2018.

Ule mwaka ukawa umeingia kwa style hiyo ya shari.. na yule binti kiukweli alionekana amechukizwa, hivyo hakutaka kuzungumzia jambo lolote na hata zawadi yake hakutaka kuipokea.. basi nikaamua kumpeleka hadi kwenye malazi yake na kumwacha hapo nikiwa bado nambembeleza..

Cha kushangaza kesho yake naamka asubuhi mida ya saa 3 napokea Text inasema ..PLEASE CAN WE END THIS AND JUST BE FRIENDS.. nilishangaa sana na kuishia kucheka tuu.. na nilishukuru kwa upande mwengine kwa maana Simu yangu aina ya iPhone 6s ilipona.. maana sikutaka kubembelezana naye..

Ila nahisi lilikuwa Gundu, kwa maana tangu pale.. sikupata binti hadi mwaka huu tarehe 2 mwezi wa 1..

Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu kwani garii ilifanyaje hadi wa kakuzengua
 
No! Nlilokuwa nasema ni kwamba, kuna mdau amesema watu wengi wanayo magari kitu ambacho napingaaa tena kwa nguvu zote. Hata kama ni mikweche lakini sio wengi ambao wana magari hususan kutoka hapa JF. Kwani wewe ushakutana na watu wangapi wa hapa?? Trust me hali za watu humu ni mbaya
Hata wenye ambao hawana ata driving license utaskia anakwambia nikaenda na ndinga, nikapaki sjui manini nini, ulimbukeni mtupu.....wenye magari hawayaongelei hata
 
Hahahahahaha. Sasa vijana tukisema hatuna magari mnatukataaa. Tufanyeje sasa??
 
Habari zenu wanaJamii.. Nina imani mko Salama kabisa..

Kwa mara nyengine tena nimekuja na story hii.. inayohusu, ni namna gani nilivyouanza na kuumaliza mwaka wa 2018.

Nirudishe Historia nyuma kidogo mpaka mwaka 2017, ambapo kuanzia mwezi wa 9 mpaka wa 11, niliachana na mabinti wanne ambao nilikuwa nao kwenye mahusiano.. Na mwezi wa 12 nikapata binti mwengine.. ambaye huyu mahusiano yake kidogo yalikuwa serious, kwa maana pia alisisitiza kunipeleka mpaka kwao na alinitambulisha.

Maisha yakaenda na Mwezi ukafika Mwishoni.. Yaani kuukaribisha mwaka 2018 sasa.

Kama ishara ya shukrani na Upendo nikaamua kujitutumua nikamnunulia yule binti simu flani kali ili akaribishie mwaka.. ingawa sikuwa nimemkabidhi

Usiku wake nikaenda mpaka Chuo alichokuwa anasoma.. Nikapaki ndinga nikawa nimekaa naye hapo huku tukisubiri mwaka mpya uingie.. Sasa ile saa tano na nusu inafika.. kidogo wakaja jamaa wawili waliovalia nguo za kiaskari na wakapiga lock Gari yangu, na kuanza kunizingua vibaya, hadi yule binti akaanza kupata wasiwasi.. ila mimi nikawa nawajibu kawaida tuu, na nikafunga gari ..nikasepa zangu kwenye kituo chao kidogo cha polisi ili niepushe utata nikiwa na yule Binti wa watu..

Tuliyazungumza yakaisha na hapo ndipo nilipopata nafasi ya kwenda kutoa gari yangu na kuagana na yule binti mida ya saa 6 na nusu.. yaani mwaka mpya 2018.

Ule mwaka ukawa umeingia kwa style hiyo ya shari.. na yule binti kiukweli alionekana amechukizwa, hivyo hakutaka kuzungumzia jambo lolote na hata zawadi yake hakutaka kuipokea.. basi nikaamua kumpeleka hadi kwenye malazi yake na kumwacha hapo nikiwa bado nambembeleza..

Cha kushangaza kesho yake naamka asubuhi mida ya saa 3 napokea Text inasema ..PLEASE CAN WE END THIS AND JUST BE FRIENDS.. nilishangaa sana na kuishia kucheka tuu.. na nilishukuru kwa upande mwengine kwa maana Simu yangu aina ya iPhone 6s ilipona.. maana sikutaka kubembelezana naye..

Ila nahisi lilikuwa Gundu, kwa maana tangu pale.. sikupata binti hadi mwaka huu tarehe 2 mwezi wa 1..

Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulipigwa umeogopa kusema umemeza tu ili tusikucheke na zawadi uliomletea haikuwa ni iphone 6 ni kitochi au nokia ya tochii .
Ukiona mtu anajisifu ni uongo.
🤣🤣🤣🤣🙄🙄
 
Back
Top Bottom