THE ISLAMIC WIFE
(Mke Muislamu)
Sehemu Ya 23
Mtunzi... MoonBoy
Simu No, +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →→↓↓
"ina maana mimi nalipia matibabu kila kitu... Kwa siku karibia laki nzima inaisha, kumbe haumwi??"
"Sasa unaniuliza au unapigia mstali... Hilo ndio jibu na sio swali tena"
"kumbeee??"
"yaani sasa hivi anachokifanya zena, ni wewe uwe mpole ili ale pesa zako vizuri mana utakuwa sio mkali tena.. Mana mwanaume akinywa pombe anakua mkali, sasa anakushawishi uache pombe ili uingie kwenye anga zake.. Mana hatoweza kukueka kiganjani ukiwa mlevi.... Na sasa ndio unaingia sasa kwenye kumi na nane zake... Utakoma baba, mwaka huu wako, nakupenda na nimediriki kukupa sehemu zangu lakini bado hunioni tu... Na ukiacha pombe, uatajiju, anazi hukua zote"
"Fadhila.... Basi basi..... Nitakutafuta niongew nawewe vizuri... Lakini kumbe ulilijua hilo mapema kwanini usiniambie Fadhila??"
"sasa we upo nae kila saa, mimi nitawezaje kukuambia?"
"kwahio zena anataka kuniweka kiganjani mimi"
"tena sio kidogo... Afu ana hasira na siku ile ulivyokuwa hutaki kuacha lile jenereta kule msikitini"
"Alaaaaaaaaaaaaaa.... Acha utani fadhila"
"Nakwambia usipokuwa makini, hata kufa utakufa jamani rahim wangu, si uachane nae, au kale kaweupe ka dukani ndio kanakuchanganya?"
ENDELEA.......
Kwa maelezo ya dokta pale alipoulizwa kuwa binaadamu anaetumia kilevi kama chakula, ili aache kunywa atatakiwa kukaa kwa muda gani na aweze kusahau kabisa,. Dokta akasema kuwa, kumwachisha mtu pombe kwa haraka haraka ni kitu kigumu sana, ila pia ni kirahisi kwasababu ya kitu fulani,.. Kwa kawaida mlevi kuacha inabidi apunguze kunywa pombe taratibu, kwa mfano jamali kaka yake rahim, kataamka kupunguza, lakini ipo siku ataacha kabisa, kwasababu kuacha kitu kunatokana na nia ulioinuia moyoni mwako,.. Na pia mtu aliozoe pombe akija kukaa wiki moja bila kugusa kinywaji hicho, basi ni lazima viugonjwa vya hapa na pele vimjie kwasababu ile mishipa ilio zoea pombe inatoa zile kemikali zilizobaki hivyo lazima nguvu zikuishe... Na hapa naelezea walevi na sio wanywaji, mana kuna walevi na wanywaji... Na mtu akisema anapunguza kunywa pombe, basi nafasi anayoishika ni nafasi ya mnywaji... Kutoka mlevi,.. Kwahio hapa naelezea mlevi yaani wale walioshindikana, siku haiishi bila kupata, na akikosa ni maumivu kwake, lakini mnywaji anaweza kukaa hata siku tatu bila kunywa na akawa sawa tu.. Mana yeye sio kuwa anataka kila siku, bali wanasema kutoa loku tu basi...
Sasa dokta alisema, rahim ili aweze kuacha pombe atatakiwa kuacha taratibu, lakini papo hapo familia ikadai kuwa kuna mtu anampenda sana, afu pia rahim ni mwepesi wa kutoa damu ili kumseidia mtu yeyote yule,.. Hivyo tukiitumia njia hio, huenda ikamseidia rahim kuacha pombe, hivyo waliianza kama kujaribu tu... Na dokta alisema akifikisha siku 37 bila kugusa pombe, basi hapo hatokaa kugusa pombe labda aanze upya, mana vile vimelea vinavyohitaji pombe mwilini vimeshakufa kwa kukosa taratibu zao za pombe, hivyo akinywa hapo kaanza upya, lakini kushawishiwa na mwili ni ngumu.... Jaribio hilo hawakuamini kama lingefaa, lakini wiki ilipoisha ndipo wakajua kumbe kweli rahim anampenda zena na yupo tayari kumwongezea damu,...
Sasa rahim keshafikisha siku 30, kasoro siku 7 tu, anakutana na fadhila mwana izaya asiekuwa na haya na asiojua kibaya... Akaanza kumpa siri yote juu ya zena kuumwa kwake, kuwa hio ilikuwa ni triki ya yeye kuacha pomne na sio kuwa zena anaumwa,.. Tena fadhila hakuishia hapo aliongea na maneno mengi sana juu ya zena, mpaka akamuingiza mwenzie kwenye ushirikina kuwa anataka kumweka rahim kiganjani, mara anakula hela zake tuuu... Rahim yote hayo alikuwa hayajui, lakini leo ndio kayajua... Nani alikuambia wana ndoa huachana hivi hivi??????.... Lazima kuwe na mtu nyuma yake, hawawezi kuachana hivi hivi bila sababu...
"Alaaaaaaaaaaaaaa.... Acha utani fadhila"
"Nakwambia usipokuwa makini, hata kufa utakufa jamani rahim wangu, si uachane nae, au kale kaweupe ka dukani ndio kanakuchanganya?"
Aliongea zena kuwa labda rahim anachanganywa na huo weupe wa dukani alionao zena, au inakuwaje..
"fadhila, please please.. Naomba niwahi hospitali kwanza.. Yaani nikifika navuruga wote"
Aliingea rahim huku akiwa na hasira ya kuua hata mtu,..
"sawa, we wahi tu... Lakini jua nakupenda rahim"
"tutakuja kuyamaliza... Sio kwa utamu ule nikuache aisee"
Aliongea rahim huku akiondoa gari kwa haraka ya kuwahi hospitalini,.. Huku nyuma fadhila alikuwa akijisemea kuwa.
"safi sana... Tayari nimesha mpasha moto, sasa zena imekula kwake, rahim ni wangu tu,.. Wacha ajishauwe kuwa mgonjwa, na sasa atakiona cha moto"
Fadhila aliongea hivyo huku akiondoka zake....
Sasa rahim alikuwa akielekea hospitali, Lakini cha ajabu, hakupitia huko, kitu cha kwanza alipitia sokoni kwanza akanunua matunda yaliohitajika, na hayo hayo matunda anataka yawe mtego kwa zena,..
"Kwanini anifanyie hivyo mtoto wa mwenzie, pesa zangu, mdomo wangu, dhambi ni zangu, sasa yeye vinamuhusu nini, kama ni kunipenda angenipenda tu kwanini astopishe starehe zangu?? naumwa mishipa inanitoka nikitarajia kumseidia mtu, kumbe ni hewa"
Aliongea rahim huku akikusanya matunda kwa hasira,... Alipomaliza kukusanya matunda, alilipia gharama zote,... Lakini sasa ujue kuwa kweli fadhila hakuwa mtu mzuri, rahim kapitia Supermarket kubwa mjini hapo, na kuenda upande wa vinywaji, kama kawaida yake, kachukuwa ile wine ya bei ghali, kisha akaenda pale kaunta...
"bei gani hii dada yangu"
Aliuliza bei ya wine hio, mana ilikuwa ni wine toleo jipya, mana ni nyeupe tofauti na zingine zilizo kama chai, sasa hio ni nyeupe inaendana kidogo na maji, lakini ni wine aina mpya...
"hio ni laki tatu"
"waoooo... Advantage Price for me"
Rahim aliona ni bei rahisi sana kwake, kwani aliingiza mkono mfukoni na kutoa waleti kwa furaha, mana leo ndio kwanzaa anaanza kurudia starehe zake, baada ya kupewa ukweli wote...
"brooo, unasema Advantage Price for You, wakati mimi nimeishindwa kuinunua"
Alikuwa ni jamaa mmoja aliokutana nae hapo kaunta, nae pia alikuwa akinunua vinywaji vidogo vidogo kwa ajili ya nyumbani kwake,...
"kwahio, unaniambia unapenda sana hii wine mpya"
Aliuliza rahim huku jamaa akijibu kwa furaha
"yes... Kwasababu ile wine ya zamani ndio Nilikuwa nagonga mimi.. Sasa leo nikaiona inatangazwa kwenye TV, nikasema siiachi hii.. Lakini huezi amini nimeiacha kutokana na bei"
Rahim alicheka sana kusikia mtu anashindwa kununua kitu kwasababu ya pesa, alimuona yule jamaa ni masikini sana kwa kushindwa kununua wine hio... Sasa dharau za rahim ndio zinarudi upyaaaaaaaaaa
Rahim akiwa barabarani, hata gari hakuwa akiendesha vizuri, tena wakati huo ule mchupa wa wine upo katikati, ina maana tayari keshaunywa nusu yake,... Macho ya rahim sio yale tena, yalikuwa kama yanataka kudondoka vile, wine mpya huja na mambo mapya,.. Rahim mpaka hospitalini, gari yenyewe kuisimamisha imekuwa tabu, mpaka anataka kukanyaga wamama wa watu,...
"huyu mkaka vipi mbona anataka kutugonga"
Aliongea mama mmoja aliokuwa mja mzito,
"unasema we mwehu"
Wenzake walivyoona rahim anamrudia yule mama, walimtoa mana rahim hapo kinachomfanya awe hivyo ni pombe, na ndio karudia upyaaa,.... Wakati huo akina zena hawajui hili wala lile, tena walikuwa wanapiga stori za rahim...
"hizi zena... Kama rahim atatulia... Utakubali kuolewa nae"
Aliuliza bibi yake rahim, huku mama zena katulia tu kimyaa
Zena anajiskia aibu sana, mana hajaamini kama naweza kuolewa na mtu ampendaye na mbaya zaidi hata rahim anampenda zena,...
"bibi, mimi sina pingamizi kama mama na baba watakubali"
Aliongea zena huku akijificha kwa aibu, na ukumbuke zena haumwi wala nini,..
"we zena wewe, hebu acha dhambi zako, kama sisi hatupendi uwe na rahim, tusinge kuruhusu kuwa nae hata kwa sasa... Kwa nafasi uliofikia kwa rahim basi sisi hatuna shida... Ruksa tu, na hata baba yako kakubaliana na hilo, mana kusikiliza ushauri wa sulesh kuwa huu sio wakati wa kuchaguliana waume, ilimradi wamependana basi"
Mama zena aliongea hayo, na kumfanya zena atokwe na machozi ya furaha juu ya uamuzi wa wazazi wake kukubali kuolewa na rahim.. Masikini ya mungu wao wanapanga hili kumbe rahim anakuja na hili,... sasa zena alisikia sauti za wamama wanapiga kelele huko nje, tena walikuwa wakitukana sana juu ya mlevi huyo,...
"mbwa wewe, unakunywa mipombe yako huko unakuja kutudondokea sisi.. Mshenzi wewe"
Wakati huo rahim kudondoka chini, lakini chupa ya wine nzimaa na uzima wake, tena ina wine nusu..
Sasa huku ndani zena anazidi kulaani walevi
"yaani mama ninavyochukia walevi.. Hebu sikia huyo baba huko sijui kamfanyeje mke wake"
Zena aliongea akizani labda ni mlevi fulani tu kaja hospitali kwa mke wake,.. Kumbe sio cha nani wala nani, ni rahim wake huyo huyo, aliomkalia ugonjwa ndani ya siku 30 ili aache pombe na leo kapata ukweli, karudia pombe upyaaa... Tena bora hata zamani, mana wine za zamani zilikuwa zikiuzwa laki moja, zingine laki mbili.. Sasa hii mpya ina ukali wake, inauzwa laki tatu...
"we mama ntakutia teke la tumbo"
Aliongea rahim huku akijitahidi kuamka,...
Sasa kule ndani zena kasikia sauti ya rahim
"mama, huyo sio rahim kweli, mbona ni sauti yake"
Zena alimuuliza mama yake huku mama akicheka na kusema kuwa
"hahahahah, rahim sio rahisi kulewa.. Kwa elimu ya dini alioipata kwa kifupi hawezi kuwa hivyo"
"mamaaa... Atakuwa ni yeye tu"
Wakati huo huku nje, rahim kakazana kutishia watu
"ntaua mtu nyie... Tena ntaua wawili wawili, mama na mtoto wake... Njoo sasa"
Macho haya amki kwa kuzidiwa na kilevi,.. Huku ndani zena anajikongoja kutoka, ili kama ni rahim basi aendelee kujua kuwa bado anaumwa, mana anajua rahim hajui mpango unaoendelea hapo...
Masikini ya mungu zena hajaamini kumuona rahim ndio anadondoka na chupa ya wine... Zena alirudi wodini haraka huku akimlalia mama yake, na wakati huo rahim nae ndio anaingia katika wodi hio,.. Mama zena haamini, bibi yake mwenyewe haamini kwa kile alichokifanya rahim
"mama... Naomba unisamehe mama yangu,.... Nilikuhakikishia kumfanya rahim aache pombe ili awe mume wangu,.. Lakini kumbe ilikuwa ni ngumu... Mama nisamehe mama yangu... Simtaki tena mama simtaki"
Aliongea zena na wakati huo hatamani hata kumwangalia rahim,.. Bibi yake rahim aliamka na kumchapa rahim kibao, huku akisema
"mtoto wa watu akupende vipi.. Siku 30 kazungushiwa mipira hapa ilimradi uache pombe,... Leo zimebaki siku 7, unakuja na chupa ya pombe"
Aliingea bibi wakati huo rahim walaaa hata hasikilizi mtu
"kwani hii si wine yangu... Matumda yenu nimeleta yapo Kwenye gari"
Mara mzee mvungi kaingia kwa shangwe, lakini alishangaa kumkuta rahim ananing'inia na chupa ya wine, tena wakati huo rahim anapiga funda za kutosha mbele yao....
"alafu nasema hivi.... Wewe dokta.. Nataka unipigie mahesabu ya huyu mtu kukaa hapa hospitalini,.. Nataka kuanzia siku ile ya kwanza mpaka leo... Naitaka pesa yangu,.. Mimi sijui utatoa wapi.. Nataka pesa yangu.. Unajifanya unaumwa kumbe huumwi,.. Mamilioni ya pesa yanatoka hapa kumbe huumwi... Sasa nataka pesa zanguuuuuuuu... Shenzi taipu.. Nyau wewe"
Zena alimuangukia baba yake na kumuomba msamaha juu ya jambo hilo,... Baba haamini maskio yake kwa pesa inayotakiwa kulipwa... Ataitoa wapi, na maisha yao ndio hayo ya hali ya chini..
"kachukueni yale Matunda muendelee kuongeza gharama"
Aliongea rahim kisha akaketi kitandani na kukishika kile kitanda huku akisema,....
"mgonjwaaaaaaaaa...... Mgonjwaaaaaaaaa...... Jamani mgonjwa upo wapi jamani... Jamani mgonjwa hutaki damu yangu tena "
Sasa hapo rahim hata kuchizika kulikuwa kunakuja bila hata breki, mana anapiga funda moja la wine, huku akiita mgonjwa yupo wapi ampe damu....
"sikiliza kijana wangu... Tupe siku mbili au tatu.. Tukauze mashamba na viwanja vyetu vyote... Tukulipe pesa yako"
Baba zena aliongea maneno hayo kwa uchungu huku akiichukuwa familia yake na kuondoka.... Lakini kabla hawajaondoka,.. Rahim alisimama na pombe pombe zake kichwani kana kwamba kuna kitu anataka awaambie,... Lakini sasa kabla ya rahim kuongea lolote, kulisikika sauti ya kizibo kilicho dondoshwa makusudi na rahim, huku familia ya mzee mvungi inageuka na kuangalia kulikoni kwa kelele hizo...
Zena ndio wa kwanza kuona kizibo kile,... Lakini sasa kumbe kizibo hicho hicho kina maana kubwa tu,.. Mana zena alipokiona alitikisa kichwa, kumaanisha kuwa hakubaliani na kizibo hicho....
Je?... Kizibo kina nini??...au kimeandikwa nini???.. Au kina maana gani kuwepo hapo????... Na Mbona zena kakataa kwa kuona kizibo tu???