Husna Muba
JF-Expert Member
- Jan 28, 2017
- 14,524
- 44,576
THE ISLAMIC WIFE
(Mke Muislamu)
Sehemu Ya 1
Mtunzi... MoonBoy
Simu No, +255714419487 WhatsApp
Inapoanzia Rasmi
NDUGU WASOMAJI WANGU... SIMULIZI HIII... HAITOKUWA NA VIPENGELE VIREFU, KAMA ILIVYO KATIKA SIMULIZI ZINGINE... HII ITAKUWA FUPI FUPI, KUNA SABABU ZILIZOPO NJE YA UWEZO WANGU NA NDIO MAANA IMEKUWA HIVYO..
HAYA TUANZENI RASMI HADITHI, SIMULIZI, STORY... AU VYOVYOTE UTAKAVYO IITA SAWA TU.....
SIMULIZI yetu inaanza Katika Chuo Binafsi ambacho ni chuo kikubwa sana kilichopo jijini Arusha,.. Wanafunzi walikuwa ni wengi sana na leo ni siku yao ya kupata likizo ndogo, yaani ule mwezi wa sita.. Mana kuna vyuo vingine hufunguliwa mwezi wa sita au saba lakini pia vipo vingine hufungwa miezi hio,.. Inategemea na utaratibu wa vyuo binafsi, yaani sio vyuo vya serikali...
Wanafunzi wengi sana walikuja kupokelewa na wazazi wao, walezi wao, au hata marafiki zao..
Nje ya geti la chuo hicho kulisimama magari makubwa makubwa, yaani sio malori, namaanisha magari ya thamani kubwa na mmoja wapo alikuwa ni Jamali aliokuja kumpokea mdogo wake,.. Gari aliokuja nayo ni gari aina ya VOGUE DISCOVERY V807
Gari yenye thamani kubwa sana duniani japo zipo zaidi ya hio lakini hizo ni babu kubwa na ukiona mmiliki wa gari hio usije kumdharau, sio tajiri wa mchezo mchezo,...
"aahhh dogo langu la faida.. Niambie sasa"
Alikuwa ni jamali aliomkumbatia mdogo wake wa kiume aitwae RAHIM, ukipenda unaweza kumwita RAM au RAMY... Ramy huyu ndio yule yule kijana tuliomzoe katika simulizi zilizopita na zinazokuja... Anaitwa Sharbiny Rashidy Kingazi, katika simulizi hii kutumia jina la Rahim,.. Ni mtoto wa kitajiri wacha mchezo, hata hiki chuo anachosoma hapa, ada yake ya mwezi mmoja tu unakula mpaka kufa kwako...
"niaje broo"
"nisalimie weweee, au kisa umepanda hewani tumelingana si ndio"
Aliongea jamali kumtaka rahim amsalimie mana ni kaka yake, na ni kweli wamelingana utafikiri wamezaliwa siku moja, kumbe wamepisha kama miaka 7 hivi au 8, basi rahim aliingiza begi lake la nguo kisha wakaondoka zao...
Walifika nyumbani kwao..... Hilo jumba lao sijui hata ulishawahi kuliona wapi, ni jumba haswa, yaani sio kijumba cha mchezo mchezo, yaani ni familia yenye pesa sana, ila kwa hasara zaidi ni kwamba hawaijui dini, wapo kama wapagani vile... Hua wao wanachojua ni pesa na starehe kwa kwenda mbele,... Geti lenyewe hakina mtu wa kufungua, bali kila mmoja kuna saa maalumu kaivaa hio ni spesho kwa familia hii,.. Na kama huna saa basi Utapiga kengele uje ufunguliwe, lakini kama una saa basi ni mwendo wa kuminya ukiwa humo humo ndani ya gari,..
Mama mzazi wa watoto hao alipomwona mtoto wake wa mwisho alimkimbilia sana na kumhag, (kukumbatiana)... Mama alifurahi sana kumwona mtoto wake,..
"weee ram umekonda mwanangu"
Aliongea mama yake ram au ramy.. Na wala ram hajakonda ila si unajua tu mambo ya akina mama, kupenda sana watoto wao wa kiume hata akinenepa atasema kakonda, ni upendo wa wazazi tu...
Basi waliingia ndani kisha akaandaliwa madiko diko ya maana, lakini ram alikuwa hatulii, moja haikai mbili haikai,....
"mamy, gari yangu ipo wapi pale mbona siioni"
Aliuliza ram, mana familia yote kila mmoja ana gari yake,
"baba yako kasafiri nayo.. Alafu wataka uende wapi na hujala"
Aliongea mama huku akimshika mkono kumzuia asitoke
"mama nimewamisi sana machizi wangu"
"kula kwanza"
"mama nitakula nikirudi"
Ram ni mtoto alielelewa katika mazingira ya kuachiwa sana kiasi cha kwamba ni yeye na starehe ni yeye na pesa... Hata mlango wa msikiti haujui toka kuzaliwa kwake,.. Hajui hata neno la Quran tukufu, yeye anajua starehe tu,..
Ram alitoka na gari ya baba yake, na kuelekea zake mjini kwa marafiki zake,... Aliwachukuwa washkaji zake kisha haoo, mwendo wa kwenda katika club kubwa kubwa zenye starehe za kila aina,.. Vinywaji alivyokuwa akivinunua, ni vinywaji vya gharama kubwa sana, usishangae ram kuacha milioni moja kwa masaa mawili tu... Walikunywa sana na kila mmoja aliondoka na mschana wake anaemjua...
Ram alirudi nyumbani usiku sana kama saa 6 hivi, kaingiza gari viziri na wakati huo alikuwa kalewa sana, mana kanywa vile vinywaji vya gharama kubwa ambavyo havileweshi sana kama utagusa gusa tu, lakini ukinywa nyingi hata kutembea utashindwa,..
"mamaaaa"
Ram aliita huku akishindwa hata kutoka kwenye mlango wa gari kwa kulewa,.. Mama yake alikuwa sebuleni hata kulala hajalala mana Mziwanda wake hajarudi,.. Japo ni tabia ya ram kila anapokuwa nyumbani kwa likizo hizi hua anakuwa mtu wa starehe sana na mama yake keshamzoea kihivyo yani,
"rahim mwanangu, leo umekunywa sana kwanini lakini"
Aliongea mama yake huku akimtoa katika gari
"mamaaa... Gambe (unywaji) la leo tamu mno"
"lakini umezidisha baba"
Mama akaanza kumkokota mtoto wake mpaka ndani,.. Na kwakuwa alikuwa kashiba alipotoka, basi mama hakuhangaika na kupika, japo wafanyakazi wapo wengi sana lakini kwa watoto wake hua anawapikia mwenyewe, eti haamini kama wanaweza kuwapikia watoto wake, hivyo anawapikia mwenyewe.... Ndani ya jengo hilo kuna wafanyakazi wengi sana na kila mtu ana kazi yake... Yaani watoto wa hii nyumba wakiamka tu ni wao na kula na starehe kwa wingi, hawana kazi wanajua hawa... Tena hapo ndani penyewe kuna kaunta utafikiri baa,.. Kama mtu una hamu ya wine basi unaingia kaunta na kujisevia... Na hapo kaunta hakuna Serengeti, hakuna Eagle, hakuna Safari, hakuna Kilimanjaro, Hakuna Tusker,.. Yaani hakuna kinywaji cha elfu 3 au 5...yaani hapo ni mwendo wa wine, wiski yaani vile vinywaji vinavyo anzia na bei ya shilingi laki moja na kuendelea
**************************************
Ikiwa ni siku ya ujumaa, iliotukuka umma ulishangaa kumwona shekhe fulani leo akiingia msikitini,.. Kila mtu alishangaa sana kwa kumwona shekhe aliovalia ki Nigeria,.. Wapo waliofurahia ujio wake lakini hakuna aliochukia ujio wake na wapo walioshangazwa na ujio wake...
"as Salaam Aleykum"
Aliwasalimia watu wote waliopo msikitini, tena alifika muda muafaka, katika swala ya Ijumaa mchana kweupee
"aahhh shekh rahim"
Aliitwa na imamu wa msikiti huo kisha akapewa nafasi ya kuswalisha ijumaa ya leo...
"naam mzee wangu"
"nina furaha sana kuwa na kijana mtiifu kama wewe.... Leo sijiskii vizuri hivyo nipo nyuma yako leo"
Aliongea imamu huyo huku rahim anajua maana ya kukaa nyuma yako, yaani kampa nafasi ya kuswalisha Al Ijumaa kareem,.. Huezi amini alikuwa ni rahim ndie mswalishaji wa Ijumaa ya leo,... Sasa hapa inakuwaje, mbona rahim tunaemjua sisi ni mtu wa starehe tu na hajui cha msikitini wala nini... Sasa mbona hapa anaonekana kuswalisha tena anaswalisha umati wa watu wasiopungua 300,... Sasa huyu ni rahim yupi na yule sharobaro mhuni ni rahim yupi?