Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 3,129
- 4,285
Hadithi ya babu yangu Mzee Aweda na Uchaguzi wa mwaka 2014/2015.
Babu yangu Aweda aliwahi kuniambia kuwa kuna watu kumi walikuwa wanasafiri baharini kwa kutumia boti au mtumbwi. Mmojawao ni mhunzi halafu ni mtundu sana. Kutokana na tabia yake hiyo, akawa ana ng'oa mabati na mbao kwenye boti. Wao walimwacha wakisema hawezi kungóa mabati kiasi cha mtumbwi/boti letu kuzama kwa kuwa na yeye pia atazama na sisi majini. Wakamwacha, akaendelea. Wakiwa wamefikia robo tatu ya safari yao mtumbwi/boti likaanza kuingiza maji, nao wakaanza kujiokoa kwa kurudishia kila mbao na bati lililongólewa huku wakimlaumu mwenzao, lakini haikusaidia – walichelewa na maji yakawazidi. Wote wakazama na kufa baharini. Hadithi ya babu yangu Aweda inatufudisha nini kwenye kipindi hiki tunapoendelea na mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015?
Kuna watu wanadhani kuwa wao si wanasiasa, kwa hiyo mtaani/kijijini kwao, haijalishi mtu anayechaguliwa wala chama anachotoka. Haiwahusu. Mwaka kesho nani atakuwa Diwani, Mbunge au Rais haiwahusu – wengine hata kura hawapigi – wanasema haiwahusu. Kuna mwingine anajisemea moyoni kuwa yeye si mwanasiasa, yeye ni mwalimu, mkulima, mwanafunzi, Dakatari, mtanzania asiyetaka vurugu za wanasiasa, mwajiriwa katika shirika nzuri nk nk – wasichojua ni kwamba wanakosea sana kama wale wasafiri tisa wa hadithi ya Mzee Aweda.
Ukweli ni kwamba wanasiasa na viongozi serikalini, ndo wanaoamua ubora wa dawa unazokula iwe feki au nzuri, (Refer ARV Feki ziliripotiwa wiki hii), aina ya vifaa unayojengea iunguze nyumba au la, bei ya chakula chako iwe juu au chini, maji yawepo au la, Amani iendelee au vita vije, shule zifaulishe au zifelishe, ubora wa hospitali, bara bara, bei ya umeme ipande au ishuke, nauli ipande au ishuke nk nk. Hii ina maanisha kuwa kukaa kimya ni kufanya uamuzi mbaya kama wale wasafiri 9 na mwenzao.
Kwa hiyo basi,
Busara ya kawaida na mantiki au logiki, inanisukuma nihitimishe kuwa, kila mwenye busara hawezi kuacha kwenda kuchagua viongozi wazuri wa mtaa wake, na hawezi kuacha kupiga kura mwaka 2015 kwa sababu siasa inamhusu kuanzia anataka mpaka hataki - tofauti yetu itakuwa ni kiwango cha ushiriki tu. Na mtu makini hawezi kufanya ushabiki wa kivyama katika uamuzui wake bali hoja na sera nzuri za mgombea zinazotekelezeka na kubadili maisha yake ya kila siku.
Kutofanya hivyo rafiki zangu, ni sawa na kusema, mwenzetu huyu hawezi kutoboa boti letu likazama baharini kwa sababu na yeye atazama.
Wasiasa wengi tulio nao ni sawa na mhunzi mtundu niliyemtaja hapo juu. Watu wema ni lazima tuwajibike ili boti letu Kijijini au Tanzania yetu isizame-huu si muda wa kulaumu tu.
Ni ombi langu basi kwenu nyote,
kila moja akajiandikishe kuanzia tarehe 23 nov, 2014 hadi 28 Nov, 2014 na umshawishi na jirani yako ili tusiwe kama wasafiri 9 waliompuuza mwenzao akawazamisha, wakafa.
Mwanafalsafa mmoja alisema, Dunia inaharibika siyo kwa sababu ya uwepo wa watu wabaya (mafisadi), Hapana, Dunia inaharibika kwa sababu watu wema wamekaa kimya.
Tafakari,
Chukua hatua.