Tunaisibiria kwa hamu kuuTupo pamoja mkuu kesho kunapo majaaliwa!
NzuriNikamuuliza, ‘’Wewe utafanya nini?’’
Akashika kikuku cha matandiko ya farasi, akajibu, ‘’ Nitakimbia.’’ Ndipo tulipoanza tena kupiga mbio kama zile za kwanza.
Yule farasi Nuru alienda mbio na kila hatua alimsaidia Yule Mzulu. Ilikuwa ajabu kumwona Umslopagaas akipiga mbio maili baada ya maili, na midomo yake ikiwa wazi na mianzi ya pua imepanuka kama ya farasi.
Kila maili tano tulisimama ili kupumzika kidogo, kisha tukazidi kuendelea. Baada ya kupumzika mara tatu, nikamuuliza, ‘’Je, unaweza kuendelea au nikuache unifuatie nyuma?’’ Alishika shoka lake akakielekezea kivuli cheusi mbele yetu, nikaona kumbe ni hekalu la jua, nalo halikuwa mbali zaidi ya maili tano. Akasema na huku anatweta ‘’Nitalifikia ama nitakufa.’’
Lo! Maili tano zile za mwisho. Ngozi ya ndani ya mapaja yangu ilichubuka, na kila mara farasi wangu alipojitahidi alinitesa.
Wala si hivyo tu, Nilichoka kwa kazi nyingi na kwa njaa na kwa kukosa usingizi, tena niliumia sana kwa dhoruba ile niliyopigwa upande wa kushoto wa kifua changu, ikawa kama kwamba kipande cha mfupa au kitu kingine kinanichoma taratibu mpaka katika pafu langu.
Tena, farasi maskini Nuru alikuwa karibu kwisha, lakini hatukuweza kukawia, maana dalili ya kupambazuka ilianza kuonekana.
Na sasa mbele yetu tuliona milango ya shaba ya nje ya mji wa Milosis, nikaingiwa na kitisho. Je, wakikataa kutufungulia milango?’’ Nikapiga ukelele na huku nikatoa neno la kifalme, ‘’Fungua! Fungua! Fungua! Tarishi! Tarishi! Ameleta habari za vita!’’
Askari wa zamu akauliza, ‘’Habari gani? Nani wewe unayesafiri upesi hivi?’’
Nikajibu, ‘’Ni bwana Makumazahn na Umslopogaas.
Fungua! Fungua! Nimeleta habari.’’
Basi, milango mikubwa ilifunguliwa kwa kishindo, na daraja la kupita likashushwa, tukapita ndani mbio mbio. Yule askari wa zamu akatuuliza, ‘’Habari gani, bwana wangu habari gani?’’
Nikajibu, ‘’Bwana Inkubu analifukuza jeshi la Sorais kama wingu mbele ya upepo.’’
Ndipo nilipozidi kwenda mbele mbio.
Haya, farasi jasiri juhudi zaidi kidogo tu! Jitahidi kidogo tu mzee Mzulu jasiri mno. Usianguke sasa, Nuru, endelea zaidi muda mfupi wa dakika kumi na tano tu, na wewe mzee Mzulu wa vita kadhalika, na majina yenu yataishi milele katika habari za nchi hii.
Basi, tulipita mbio kwa vishindo katika njia za mji. Sasa tulipita Hekalu la ua, maili moja tu imesalia, maili moja tu.
Ah! Mungu ashukuriwe, sasa tumelifikia jumba, lakini tazama, miali ya kwanza ya mapambazuko inaiangaza dari ya kuba la dhahabu la Hekalu. Je, nitawahi au tendo limekwisha tendwa na njia imezibwa?
Nami nikapiga ukulele nikitaja neno la kifalme, ‘’Fungua! Fungua!’’
Hapana jibu, na moyo wangu ukataka kufifia.
Nikaita tena, na mara hii sauti moja ilinijibu, nikafurahi, maana ilikuwa sauti ya Kara, Yule askari mwaminifu wa Nyleptha, ndiye Yule aliyepelekwa na Nyleptha kumshika Sorais siku ile alipokimbilia Hekaluni.
Nikasema, ‘’Ni wewe Kara? Mimi ni Makumazahn, waambie askari wa zamu waufungue mlango na kulishusha daraja upesi sana. Upesi! Upesi!’’
Basi hapo kulikuwa kimya kwa muda uliokuwa kama kwamba hauna mwisho, kisha, nusu ya mlango ikafunguliwa tukaingia uani, na pale pale farasi shujaa Nuru alianguka, nikafikiri amekufa.
Niliondoka, nikaiegemea nguzo , nikatazama pande zote. Sikuona hata mtu mmoja isipokuwa Kara, nayeye alionekana kwamba anataabika, na nguo zake zimetatuka tatuka.
Alikuwa ameufungua mlango na kulishusha daraja yeye peke yake. Nikamuuliza, ‘’Je, wako wapi askari wa zamu?’’
Akanijibu, ‘’Sijui. Muda wa saa mbili wakati nilipokuwa nimelala usingizini, nilishikwa, nikafungwa kamba na askari walio chini ya amri zangu, na ndiyo kwanza nimeweza kujifungua. Naogopa, naogopa sana ya kuwa tumesalitiwa.’’
Basi, maneno yake yalinitia nguvu mpya. Nikamshika mkono nikaenda na huku ninasitasita, na Umslopagaas alinifuata huku anapepesuka kama mtu aliyelewa.
Tukapita katika vyumba mpaka katika sebule kuu mpaka chumbani alimolala malkia. Kwanza tulifika chumba cha askari wa zamu hapana hata askari mmoja.
Kwa hakika wamekwisha tenda shughuli yao, nasi tumechelewa! Ukimya na upweke wa vyumba vile vikubwa ulikuwa wa kutisha mno, ukanielemea kama ndoto ovu.
Mbele, mbele katika chumba cha Nyleptha tukajiingiza huku tunapepesuka, tukiogopa mambo tutakayoyaona, tukaona kuna taa inawaka, tena, mtu ameichukua ile taa.
Oh! Mungu ashukuriwe, ni malkia mwenyewe, naye yu salama! Hapa alikuwa amesimama amevaa mavazi yake ya usiku ameamshwa na ghasia zetu za kupenya katika chumba chake, na uzito wa usingizi bado umo machoni mwake.
Akalia, ‘’Nani? Je, kuna nini Makumazahn, ni wewe? Mbona unahangaika hivi? Umekuja kunipa habari za msiba msiba wa bwana wangu ooh usiseme ya kuwa amekufa hakufa!’’ akalia na huku anaipunga mikono yake kwa mojonzi.
Nikasema, ‘’Nilimwacha Inkubu jana jioni amejeruhiwa, lakini anawaongoza askari juu ya Sorais; kwa hiyo moyo wako na utulie.
Sorais amesukumwa nyuma kila mahali, na askari zako wanashinda.’’ Akasema kwa shangwe, ‘’Nilijua, nilijua kuwa askari zangu watashinda; nao walimwita mgeni, wakavitikisa vichwa vyao nilipomfanya mkuu wa majeshi yangu! Ulimwacha jana jioni ulisema, na sasa hakujapambazuka bado! Hakika’’.
Nikasema, ‘’Nyleptha, jivike mavazi yako utupe divai tunywe, uwaite mabibi watumishi wako upesi kama unataka kuyaokoa maisha yako. Upesi! Usisite!’’
Basi, kusikia haya tu akafanya haraka kujitupia mavazi mengine akawaita mabibi watumishi wake, wakaja. Nikamwambia, ‘’Tufuateni kimya.’’ Basi, kwanza tulikwenda katika chumba cha nje, nikamwambia, ‘’Sasa tupeni divai tunywe na chakula maana tuna karibia kufa.’’
Chumba kile kilikuwa cha wakuu wa askari wa zamu na kulikuwa na meza kwa ajili ya wakuu hao.
Na Nyleptha na mabibi, wakatuletea divai na nyama toka kabatini, Umslopogaas na mimi tukanywa, tukaona uzima unaturudia tena. Kisha, nikasema, ‘’Sikiliza Nyleptha, wako mabibi wawili katika watumishi wako unaoweza kuwatumaini kabisa?’’
Akajibu, ‘’Hakika.’’
Nikasema, ‘’Vyema, waambie waende nje mjini, watoke kwa mlango wa upande, wakawaite wanaume waaminifu wowote wawezao kuwapata, na waje pamoja na silaha zao ili kuyaokoa maisha yako.
La usiulize habari sasa, fanya tu nikuambiayo. Kara atawapeleka mabibi na kuwafungulia mlango.’’
Akageuka akachagua wawili wa mabibi wale, akawaambia maneno niliyomwambia, akawapa pia orodha ya majina ya wanaume watakaowaendea. Nikasema, ‘’Nendeni upesi na kwa siri, nendeni, maana maisha yenu yamo hatarini.’’
Basi, walimfuata Kara, ambaye nilimwambia arudi upesi awezavyo akanikute kwenye mlango wa ua mkubwa wa kutokea penye ngazi kuu. Basi, mimi na Umslopogaas tulikwenda huko, na malkia na mabibi, wale wakatufuata.
Na huku tulipokuwa tukienda, tulimega chakula na katika kukimega nilisimulia habari jinsi nilivyojua hatari inayomjia, na jinsi tulivyomwona Kara, na jinsi askari wote wa zamu walivyokuwa wametoroka, naye yupo yeye peke yake pamoja na mabibi watumishi wake tu.
Katika jumba lile kuu, nayeye aliniambia ya kuwa habari zilivuma mjini ya kuwa jeshi letu limeangamia kabisa, na Sorais anakuja Milosis kwa shangwe, na kwa maneno hayo wanaume wote walimwacha.
Basi, ingawa mambo haya yamechukua muda mrefu kuyasimulia, lakini tulikuwa tumo jumbani kadiri ya dakika sita au saba tu, na ingawa dari ya Hekalu ambayo ni ndefu sana ilikuwa imaangazwa na miali ya jua, lakini hakujapambazuka bado, wala hakutapambazuka ila baada ya dakika kumi hivi.
Basi sasa tukawa katika ua na hapo jeraha liliniuma hata nikawa sina budi kumshika mkono Nyleptha, na Umslopogaas alitufuata kwa shida na huku anakula.
Sasa tulikuwa tumevuka ua, tumefika mlango mwembamba katika ukuta unaotokea penye ngazi kuu. Nilichungulia nikashangaa.
Mlango wa mbao umekwisha ondolewa, na milango ya shaba ya nje pia imekwisha ondolewa. Ilikuwa imeondolewa kabisa katika bawaba zake na kutupwa chini kabisa kadiri ya futi mia mbili.
Basi, pale mbele yetu palikuwa na nafasi ile ya juu ya ngazi kuu, na vile vipandio kumi vya marumaru nyeusi basi!
Inaendelea mkuuMkuu ndo imeisha hapa???
Hakuna noma kiongozi..Inaendelea mkuu
Mungu akipenda leo nitaimaliziaNatumai inaendelea au!?