Hadithi ya umslopagaas

Hadithi ya umslopagaas

Basi mwishowe niliacha kutakafari juu ya mambo hayo nikayaacha yale yatakayotokea kesho katika mikono ya Mungu Mwenyenzi.

Basi mwishowe jua jekundu lilichomoza, na majeshi yaliamka kwa kishindo kikubwa na ngurumo yakajikusanya kufanya vita. Matengenezo yote yalikuwa mazuri ya kutisha, na Umslopogaas alikuwa ameliinamia shoka lake na kuyatazama na huku anachekelea kwa furaha.

Akasema, ‘’Makumazahn, sijaona namna yake, hata mara moja. Vita vya watu wangu vilikuwa kama michezo ya watoto vikilinganishwa na vita hivi namna vitakavyo kuwa. Je, waonaje watapigana hata mwisho?’’

Nikajibu kwa huzuni, ‘’Ndiyo, mpaka kufa. Uwe radhi Inkosikazi atakula shibe yake leo. Basi, wakati ulipita bila kuwapo dalili ya shambulio.


Kundi dogo la wapanda farasi lilipita mbele yetu polepole, na kwa dhahiri lilikuwa likichungulia namna tulivyopangwa na hesabu ya askari zetu, lakini hatukulishambulia, maana tulikuwa tumekwisha kusudia kukaa na kujitetea tu wala si kupoteza hata mtu mmoja.


Askari wetu walikula chakula chao cha asubuhi, wakasimama na silaha zao tayari, na saa zikapita. Saa sita watu walipokuwa wakila chakula cha mchana, maana tulifikiri wataweza kupigana vizuri zaidi kama hawana njaa, tulisikia kelele, ‘’Sorais! Sorais!’’ ilikuwa kama ngurumo ikitokea upande wa kuume wa adui zetu, nikatwaa darubini nikatazama, nikaweza kumwona Sorais mwenyewe anapita polepole mbele ya majeshi yake amezungukwa na wakuu waliokuwa wamevaa vizuri sana.


Na alipokuwa akipita, askari walimpigia ukelele wa shangwe kama ngurumo ya magari elfu kumi, au kama mvumo wa mawimbi ya bahari upepo ugeukapo na kuchukua sauti yake ghafla masikioni mwa mtu anayesikiliza, mpaka ardhi ilitikisika na hewa ilijaa wingi wa sauti.


Basi, tulisikia kuwa hii ndiyo alama ya kuanzisha vita, tukakaa kimya tukijiweka tayari. Wala hatukuwekwa sana. Mara, kama ndimi za moto zitokazo katika mdomo wa mzinga, vikosi viwili vya wapanda farasi vilitoka mbio, wakateremka mwinuko kutujia, kwanza pole pole kidogo, na kuongeza mbio walipokuwa wakija.


Lakini kabla hawajaufikia mto ule mdogo uliokuwa bondeni, Sir Henry aliipeleka amri kupeleka askari elfu tano wapanda farasi wenye panga kuwapiga, maana aliogopa kuwa wakiachiwa kuwashambulia askari wa miguu wa katikati kwa nguvu zao zote, hawataweza kustahimili. Basi nilipeleka askari wale, nikabaki nyuma pamoja na watu wangu waliosalia.


Basi, askari wale wapanda farasi elfu tano walikwenda wamepangwa mfano wa kabari na kuongozwa vizuri.


Na mkuu wao. Kwanza walikwenda taratibu muda wa yadi mia tatu, wakielekea sawasawa mbele, ndipo Yule mkuu wao alipowapeleka ghafla upande wakazidi kupiga mbio, nikaona kabari ile inapinda, na kabla kikosi cha adui hakijaweza kwenda upande au kujizuia, ilikipiga katikati kwa kishindo kikubwa mno.


Kabari ile ya wapanda farasi iliingia mpaka katika moyo wa kikosi, na wapanda farasi adui, walitupwa upande huu na huu kama udongo unavyotupwa jembe linapovutwa na ng’ombe likipita katika shamba, au kama maji ya bahari yanavyotupwa huko na huko kwa omo la merikebu inapokwenda mbio.


Ndani ndani zaidi, na kikosi cha adui kilipinda kama nyoka anavyojipinda aumizwapo ili ailinde sehemu yake ya katikati ndani zaidi. Kumbe watu wetu wemepita na kutokeza upande wa pili, waka geuka wakashambulia tena adui waliotawanyika kama povu mbele ya upepo wenye nguvu, na huku askari zetu wote wanatazama na kupiga kelele za shangwe.


Hata mwishowe, kikosi kile cha adui kilivunjika, kikageuka kikarudi mbio katikati ya farasi wengi wasio na askari, na miali ya panga zinazopungwa huko na huko, na kelele za shangwe za askari waliokuwa wakiwafukuza. Kikarudi mbio kutafuta salama nyuma ya askari wenzao.


Basi, jeshi lililokuwa likija mbele lilifunguka kukipa nafasi ya kuingia, na askari zangu walirud, wamepata hasara ya watu kadiri ya mia tano nami nilifikiri si wengi kwa kadiri ya ukali wa vita vilivyokuwa.


Basi, sasa vikosi vya upande wa kushoto wa adui vilivyokuwa karibu vyote ni vya watu wa Nasta, vilikuwa vikitujia, na huku tukasikia kelele ‘’Nasta’’ na ‘’Sorais’’ tukaona bendera zinapepea, na panga zinapungwa, vikatujia kama makundi ya siafu.


Nilipewa amri tena nijaribu kuwapinga kwa kupeleka vikosi vya wapanda farasi, nikafanya kadiri nilivyoweza kupeleka vikosi vya watu elfu moja.


Vikosi hivyo viliwatia adui kama kisu kinachong’aa na kuingia katika moyo wao, lakini tulipata hasara ya watu wengi, maana sasa askari wa adui hawakushikamana kama katika shambulio la kwanza, ila walifunguka wakaacha nafasi ili wapanda farasi wapite katikati, kisha walijitupa chini wakawakata miguu farasi walipokuwa wakipita.


Basi kadiri tulivyoweza kufanya, adui walizidi kutukaribia, mpaka wakakishambulia kwa nguvu kikosi cha Bwana Good. Tena, wakati huo huo nikasikia kishindo kilichonifaamisha kuwa adui wameshambulia katikati na kwa upande wa kushoto pia.


Nilijiinua katika vikuku vya miguu juu ya farasi wangu nikatazama upande wa kushoto, nikaona mng’aro wa panga zinazopungwa na wa ncha za mikuki inayosukumwa upeo wa macho yangu.


Basi, hapo majeshi yalitikisika huku na huku yakishindana, pengine yakirudi nyuma, pengine yakisukumwa mbele, katika fujo ya kushambulia na kujitetea. Basi, vivyo hivyo vita viliendelea kwa muda wa saa nne bila kituo, na mwisho wa wakati huo tulikuwa haujaendelea mbele wala kurudi nyuma.


Mwishowe mashambulio yalififia na jeshi la Sorais lilirudi, nikaanza kufikiri askari zao wamechoka. Lakini sivyo, sasa Sorais aliwapanga wapanda farasi vikosi vidogo vidogo wakatushambulia kwa nguvu kila mahali, ndipo wakati huo, huo alipopeleka mbele tena jeshi kubwa.


Sorais mwenyewe alikuwa akiamrisha. Basi, wakaja mbele kama mawimbi makubwa yenye nguvu nyingi mno, wakapambana na askari wa katikati ya kidari cha jeshi letu. Basi, askari wa sehemu ya katikati ya jeshi letu walipinda kama upinde, wakafunguka, na kama askari wale elfu kumi wasingalikuwa wamewekwa nyuma kuwategemeza, wangaliangamia kabisa.


Kikosi cha Bwana Good pia kilisukumwa nyuma na sehemu moja ilivunjika, na nusu ya askari wakapotea. Lakini shambulio lilikuwa lenye nguvu mno na nguvu zake hazikuweza kuendelea hivyo. Mara ikawa kama vita vinageuka, na kwa muda mfupi ilikuwa kama pande zote mbili zimesimama tu.

Ndipo vita vilipoanza kuiendea kambi ya Sorais. Tena, wakati huo huo kikosi cha Nasta kikarudi nyuma, sijui kama askari zake walikata tamaa kwa ajili ya hasara waliyoipata, au kama ni hila waliyofanya.

Lakini hapo, kikosi cha Bwana Good kilipaacha mahali pake kikashambulia na huku kinapiga kelele.

Na mara ilea dui waligeuka wakashambulia tena kwa nguvu. Basi, adui walikizunguka kile kikosi kikaangamia kabisa, nikaona kuwa Bwana Good amepanda farasi mkubwa yu katika hatari ya kuuwa.

Baada ya dakika chache kikosi kizima kilitawanyika nami sikuweza kumwona Bwana Good katika mauaji ya kutisha yaliyofuata.


Halafu nikaona farasi mweupe anatoka mbio katika fujo, akanipita mbio hana mtu mgongoni, nikamtambua ni farasi wa Bwana Good. Basi, hapo sikusita zaidi, wala sikungoja kupewa amri, ila niliwaamrisha watu wangu kadiri ya elfu nne au tano, tukawashambulia wale watu wa Nasta wenye panga.


Walituona tunakuja, tena, walionywa kwa vishindo vya miguu ya farasi zetu, wakageuka wakatungojea. Wala hawakukubali kurudi nyuma hata kidogo, tukajaribu kuwakanyaga, tukawapigapiga, tukawatenga lakini walionekana kama wainukao tena, wakawashambulia farasi wetu kwa panga zao kali, wakaikata miguu yao, kisha wakawashambulia askari walipoanguka chini wakawakata vipande vipande.


Farasi wangu akauawa, lakini kwa bahati nilikuwa na mwingine aliyewekwa pamoja na askari nyuma, ikawa sina budi kufanya niwezavyo. Baadaye kidogo nilijiona katikati ya askari wa Bwana Good waliosalia ambao walikuwa wamemzunguka na sasa wanapigana kuyaokoa maisha yao.


Ndipo nilipojikwaa nikatazama chini nikaona rodi ya Bwana Good, alikuwa ameangushwa kigotigoti, na mtu mkubwa sana alikuwa amesimama anapunga upanga mkubwa tayari kumpiga. Sijui namna nilivyoweza, lakini niliwahi kumuua Yule mtu kwa sime ya Kijivuni niliyokuwa nayo.

Lakini nilipokuwa nikifanya hivyo alinipiga dharuba moja upande wa kushoto wa kifua, na ingawa nilikuwa nimevaa deraya chini ya nguo zangu, lakini nilitambua ameniumiza vibaya sana.

Kwa dakika moja niliangukia mikono na magoti katikati ya maiti na watu waliokuwa wakifa, na moyo wangu ulielea nikataka kuzirai.

Nilipokuja juu tena, niliona ya kuwa askari wa Nasta, au wale waliosalia, wanarudi nyuma ya mto, na Bwana Good amesimama karibu na huku anachechemea, akasema, ‘’Lo! Tulikuwa karibu kufa, lakini asante tumepona.’’

Nikakubali, lakini nilijua ya kuwa nimeumia vibaya. Basi, hapo tuliona vikosi vyetu vya wapanda farasi wenye panga vya upande wa kuume na vya kushoto vilivyo wekwa nyuma, vikitoka mahali pao kama mishale na kuwangukia askari wa Sorais waliokuwa sasa wametawanyika, na shambulio hilo ndilo lililovimaliza vita.


Baada ya kupita dakika mbili tatu, adui walikuwa wakirudi nyuma kuuvuka ule mto mdogo, wakajipanga huko tena. Kisha, kukawa kimya kidogo, nikawahi kumpata farasi wangu wa pili. Aliyekuwa nyuma, nikapewa amri na Sir Henry kushambuliwa mbele. Basi hapo tulifanya kelele moja kwa moja, tukazipepea bendera zetu, tukapunga panga na mikuki, tukawafutia adui tukawafukuza.


Tulipokuwa tukipita juu ya chungu za maiti na watu waliokuwa wakikata roho nilimwona mtu mmoja ananijia mbio sana amepanda farasi, akaniita kwa sauti ya hofu! Nikasimama, nikamuuliza ana habari gani.

Akaniambia kuwa ana habari ya haraka sana! akaniambia, ya kuwa Malkia Nyleptha atauawa kwa hila katika jumba la Milosis mara kutakapopambazuka kesho. Aliniambia kuwa askari wa zamu watapaacha mahali pao, na makuhani watamuua Malkia. Nikashtuka kwa ushangao, nikamuuliza, ‘’ Unasemaje?’’

Akasema, ‘’Ni kweli, Yule shetani Nasta aliondoka usiku akafanya shauri na Agon. Askari wa zamu wataufungua mlango, na Nasta na makuhani wa Agon wataingia na kumuua Malkia.’’

Basi, nilimchukua Yule mtu nikaenda naye mbio mbio mpaka nilipomwona Sir Henry katikati ya wakuu wengine. Mara nilipomwona, askari walikuwa wanaanza kuendelea mbele tena.

Kichwa chake kilifungwa kwa kitambaa chenye damu, lakini niliona ya kuwa macho yake na kama desturi yake, na karibu naye Umslopogaas alikuwa amesimama amelishika shoka lake, jekundu kwa damu, lakini yeye alionekana mzima kabisa.
Sir Henry akauliza, ‘’Kuna nini Quatermain?’’

Nikajibu, ‘’Wanafanya hila kumuua Malkia mara kutakapo pambazuka kesho. Mtu huyu aliyetoroka toka upande wa Sorais alisikia habari za hila wanazotaka kuzifanya.’’

Rangi ya uso wa Sir Henry ilibadilika, akawa mweupe sana, akasema, ‘’Kutakapo pambazuka, na sasa jua linashuka kunapambazuka saa kumi, na toka hapa mpaka huko ni mwendo wa maili mia moja. Tutafanya nini?’’

Basi, nilifikiri shauri, nikamuuliza, ‘’Je farasi wako amechoka?’’ akajibu, ‘’La, ndiyo kwanza nimpande, tena amekwisha kula.’’

Nikasema, ‘’Na farasi wangu pia hajafanya kazi leo. Basi, shuka chini umwache Umslopogaas ampande, tutafika Milosis kabla hakujapambazuka, na kama hatuwahi kufika, basi tumeshindwa.

Sir Henry akataka kwenda pamoja nasi, Nikamwambia! Hapana, hapana, wewe huwezi kuacha vita sasa. Watu wasipokuona watakufa moyo na vita vitapotea. Askari wangefikiri umekimbia. Basi, upesi, upesi.’’

Basi mara ile alishuka, na Umslopogaas alipanda mahali pake. Nikasema, ‘’Kwa heri. Peleka wapanda farasi elfu moja watufuatie baada ya saa moja ikiwezekana tena peleka mkuu apashike mahali pangu umweleze sababu niliyotoka.’’


Akasema, ‘’Utafanya uwezavyo kumwokoa Nyleptha, Quatermain?’’
Nikajibu, ‘’Ndiyo, kadiri ninavyoweza kufanya. Sasa nenda, unaachwa nyuma.’’
Basi, alitutazama mara moja tu, kisha akageuka akawafuata watu wake akaenda upesi kujiunga na askari zake.


Na Umslopogaas na mimi tukatoka mahali pale kama mishale inavyotoka katika upinde, na baada ya kupita dakika chache, tulikuwa tumetoka kabisa mahali pale pa mauaji na harufu ya damu, na sauti za vita zikawa kama mvumo wa bahari ya mbali katika masikio yetu.
 
Kitambo sjaweka mguu humu

Gurudumu langu lilikwamia pale Bwana Good alipopigwa kiatu
 
Vile vile, jua lishukapo jioni, miali ya mwisho hupenya kati dirisha lililo katika ukuta nyuma ya madhabahu ya magharibi.

Na huing’arisha madhabahu ya katikati kisha hutua kwa muda kidogo juu ya madhabahu ya mashariki. Ni kama ahadi inayoweka mapambazuko ya jioni, na ahadi inayoweka jioni kwa mapambazuko.

Isipokuwa kwa madhabahu hizi tatu, nafasi iliyo chini ya kuba hili kubwa ni wazi kabisa, bila pambano lolote.

Basi, hili ndiyo namna lilivyo hekalu lile zuri, lakini siwezi kulieleza zaidi jinsi lilivyo la ajabu na utukufu.

Mlangoni pa hekalu, tulipokewa na kundi la skari walio onekana kuwa wapo chini ya amri ya kuhani. Tuka pelekwa katika sehemu moja ya hekalu tukaachwa humo muda wa nusu saa.

Hapa tulifanya shauri pamoja, tukatambua ya kuwa tumo katika hatari ya kupoteza maisha yetu, tukakusudia kujilinda tuwezavyo na kuyapigania vikali maisha yetu.

Uslopogaas alisema kuwa yeye atamuua Yule kuhani mkuu Agon kwa kumpasulia mbali kichwa kwa Inkosikazi.

Mahali tuliposimama tuliweza kuona umati wa watu waliokuwa wakihudhuria hekaluni, kama kwamba wanatazamia jambo kuu, nikahofia ya kuwa sisi tumo katika jambo hilo.

Basi, karibu na saa sita, kuhani alikuja akafanya ishara, na mkubwa wa askari alituashiria ya kuwa tunatakiwa kwenda mbele, tukaenda mbele kwa ujasiri tulivyoweza.

Mara tulitoka katika ile sehemu ya hekalu, tukapita katikati ya umati mkubwa wa watu waliokuwa wamehudhuria, mpaka tukawa tumesimama juu ya utando wa shaba ulio katika sakafu mbele ya madhabahu kuu kwa upande wake wa mashariki.

Kwa kadiri ya futi thelathini kuizunguka madhabahu, kamba zilifungwa ili kufanya nafasi na kuwazuia watu wasiingie ndani.

Na katika nafasi hiyo makuhani wengine walipangwa mfano wa duara, wameshika panda mikononi mwao, wamevaa mavazi meupe yenye mahazamu ya dhahabu, na mbele yetu, Agon kuhani mkuu, alikuwa amesimama amevaa kofia yake ya nakshi na urembo. Yeye pekee alikuwa amevaa kofia, bali wote wengine walikuwa vichwa wazi.


Tulisimama juu ya sehemu ile ya shaba, wala hatuna habari hata kidogo kuna nini chini yake kilichotengenezwa kwa ajili yetu.

Nilisikia sauti ikitoka chini sakafuni, lakini sikuweza kukisia ni kitu gani.
Basi, hapa kukawa kimya, nikatazama huku na huko niwaone wale Malkia wawili Nyleptha na Sorais. Nisiwaone.

Lakini niliona nafasi ipo wazi upande wa kulia, nikakisia ya kuwa nafasi ile imewekwa kwa ajili yao.

Tulingoja, na halafu tulisikia panda inalia mbali sana juu katika kuba. Kisha, tulisikia mnong’ono wa watu waliokuwapo, tukatazama tukaona Malkia wale wawili wanakuja pamoja.

Nyuma yao wakuu wengine waliandamana nikamwona Yule Nasta, na nyuma yao askari wapatao hamsini walifuata.

Nilifurahi sana nilipowaona askari wale. Basi, baada ya muda mfupi, walikuwa wamekwisha fika na kusimama mahali pao, Malkia wawili kwa mbele, na wakuu kwa upande wa kuume na wa kushoto, na askari wamejipanga katika mfano wa nusu duara nyuma yao.

Kasha, kukawa kimya kwa muda mrefu, na Nyleptha alinitazama; nikafikiri ya kuwa anajaribu kunijulisha habari, nikamwangalia sana.

Jicho lake lilitazama jicho langu, kasha likajongea, na kutazama ile sehemu ya shaba ambayo tulikuwa tumesimama juu yake, kasha, alikijongeza kichwa chake polepole upande.

Sikufahamu maana yake, akaifanya ishara ile ile tena. Ndipo nilipofahamu ya kuwa anatuonya tusisimame juu ya mlango huo wa shaba.

Akatazama tena, nikaona kuwa ndiyo maana yake hakika, yaani ya kuwa ipo hatari katika kusimama juu ya mlango huo.

Sir Henry alikuwa amesimama upande wangu mmoja na Umslopogaas upande wa pili.

Basi, niliyakaza macho sawasawa mbele yangu, lakini niling’ona kwa sauti ndogo sana kwanza kwa Kizulu, kisha kwa Kiingereza nikawaambia warudi nyuma kidogo kidogo mpaka wawe wamesimama juu ya sakafu wala si juu ya mlango wa shaba.

Basi, sote tulianza kujongea polepole kabisa polepole wala hapana mtu aliyetuona isipokuwa Nyleptha na Sorais tu.

Kisha, nilimtazama tena Nyleptha nika mwona anakiinamisha kichwa chake kidogo sana kama kwamba ananijulisha ya kuwa nimefanyaalivyotaka.

Basi, huku nyuma macho ya Agon yalikuwa yamekazwa mbele kuitazama madhabahu, kama kwamba ametoa kila wazo katika akili zake isipokuwa la kazi iliyoko mbele yake! Na macho yangu yalikuwa yamekazwa kuutazama mgongo wake.
Aisee
 
SURA YA KUMI NA SABA


Basi sasa udhia ule ambao mpaka sasa ulikuwa kama wingu dogo tu! Ulianza kudhihirika kabisa, ndiyo pengo alilo nalo Sorais kwa Sir Henry.

Nyleptha alikuwa mwenye tabia ya wivu sana, alikua anaudhika mno kila mara Sorais alipomfanyia Sir Henry fadhili, lakini hata hivyo hakukubali Sir Henry amwambie Sorais ya kuwa anataka kumwoa dada yake.

Angalimruhusu labda mambo yangalitokea vingine. Tena, Sir Henry alijua kuwa Bwana Good anampenda Sorais, na kwa kweli alikuwa ameanza kudhoofu kwa ajili ya kumpenda.

Mambo yaliendelea hivyo, ikawa jinsi Sir Henry anavyojaribu kumwepuka Sorais, ndivyo Sorais, alivyozidi kumfuata nakumwonyesha jinsi gani anavyo mpenda, mpaka mambo yakawa mabaya sana.

Ilikuwa kama kwamba Sorais hana habari ya kuwa Sir Henry anampenda Nyleptha, nikaihofia sana siku atakayoamka na kuyatambua hayo.


Maana Sorais ni mwanamke mwenye tabia ya ukatili sana. Basi, wakati niliouhofia ukawadia kama nilivyojua kuwa lazima utafika.

Siku moja Bwana Good alikuwa anakwenda kuwinda, na Sir Henry na mimi tulikuwa tunazungumza, mara tarishi wa jumbani alileta barua kumwambia Sir Henry afuatane naye mpaka chumbani kwa Malkia Sorais.

Sir Henry aliguna, akasema, ‘’Je, wewe huwezi kwenda mahali pangu?’’ Nikamjibu, ‘’La, mimi siendi, afadhali kumkabili tembo aliyejeruhiwa kwa bunduki ya marisaa kuliko kumkabili Sorais.

Mimi simo! Kama wewe ni mzuri hata kuwafanya wanawake wakupapatikie, basi matokeo yake ni juu yako mwenyewe.’’

Mimi sikubali kuwa mahali pako hata kama utanipa ufalme.’’
Basi, aliondoka akamfuata Yule tarishi, na mimi nilibaki nikimngojea.

Baada ya kupita muda wa dakika arobaini na tano, alirudi amefadhaika sana. Nikamuuliza habari za huko, akasema na sauti yake ilipwaya , ‘’Habari ni mbaya! Kweli matata yapo karibu sasa.

Nilipomfuata Yule tarishi, alinichukua mpaka chumbani kwa Sorais, nika mkuta peke yake ameketi kitandani anapiga gambusi.

Nilisimama mbele yake, na kwa muda kidogo hakuniangalia ila aliendelea kupiga gambusi na kuimba tu, kisha alinitazama na kucheka. Akasema, Umekuja.

Nilifikiri labda umeenda kushughulika na mambo ya dada yangu Nyleptha. Maana siku zote unashughulika naye, nami naona bila shaka kuwa wewe ni mtumishi mwema na mwaminifu.

Basi, sikusema neno, ila nilikiinamisha kichwa tu. Akasema ‘’Nataka kusema nawe, basi keti ustarehe’’ akajijongeza kitandani afanye nafasi niketi. Nikasema ya kuwa sistahili kuketi pamoja na Malkia.

Akasema, ‘’Keti.’’

Basi, nikaketi, akaanza kinitazama sana kwa macho yake makubwa meusi, kisha akasema, ‘Inkubu, unapenda uwezo?’ Nikamjibu ya kuwa nadhani wanaume wote hupenda uwezo wa namna namna.

Akasema, ‘Utaupata. Unapenda utajiri?’ Nikamjibu ya kuwa napenda utajiri kwa ajili ya vitu vinavyoletwa nao.

Akasema, ‘Utaupata.unapenda uzuri?’ Nikajibu kuwa napenda kazi za sanaa na za ustadi na kadhalika.

Akaukunja uso wake. Basi,ikawa sasa nimefadhaika hata nilikuwa ninatetemeka, nikajua ya kuwa mambo mabaya yatatokea, maana nilikuwa kama nimeduwaa, wala sikujiweza.

Mwisho akasema, Inkubu, wataka kuwa mfalme ‘’Tazama u mgeni, mimi ninafikiri kukufanya mfalme wa Wazuvendi wote, na mume wake Sorais.

La! Nyamaza kwanza unisikilize vyema. Siwezi kudhubutu kumwambia hivyo hata mtu mmoja katika watu wangu hisia za moyo wangu. Lakini wewe ni mgeni na kwa hivi nimeweza kusema nawe bila kuona haya.

Tena nakumbuka yote ninayoweza kukupa, na kutambua jinsi ilivyo vigumu kwako kuniposa.

Tazama, ufalme umewekwa miguuni pako, Bwana wangu Inkubu, na pamoja na ufalme, mwanamke ambaye wengine wametamani kumposa. Na sasa nijibu, Ee mteule wangu, na maneno yako yatakuwa matamu masikioni mwangu.’’

‘’Nikasema, Ee Sorais, nakuomba usiseme namna hii, maana mambo hayo hayawezi kuwa. Nimekwisha mposa dada yako, nami nampenda yeye! Yeye tu.’’

Basi, nilipokuwa nikisema, Sorais aliuficha uso wake kwa mikono yake, na alipoyasikia maneno yangu, aliuinua uso wake pole pole, nilipouona uso wake nilifadhaika sana, maana uso wake ulikuwa mweupe kabisa na macho yake yaling’aa kama balbu.


Akaondoka, akasimama na kuvuta pumzi kama kwamba roho yake inataka kumtoka. Mara alikitazama kisu kilichokuwapo mezani, kisha akanitazama mimi kama kwamba anafikiri kuniua pale pale lakini hakukitwaa.

Mwishowe akasema neno moja tu, ‘Nenda!’ Nkaondoka, Nikashukuru kutoka chumbani humo salama.

Sasa je, nitafanya nini?’’ Nilikitikisa kichwa changu, maana mambo yamekwisha kuwa mabaya sana. Hata katika Jehanamu hakuna ukali kama wa mwanamke aliyekataliwa! Na hasa kama ni mwanamke kama Malkia Sorais. Nikahofia yale yatakayotokea, na pamoja nayo hatari ya maisha yetu.


Nikasema, ‘’Lazima Nyleptha aambiwe habari hizo haraka, nami naona afadhali nimwambie mimi; maana ukimwambie wewe haikosi atashuku neno. Nani mkubwa wa zamu usiku huu?’’

Akajibu Sir Henry ‘ni Kara’ Nikasema. ‘’Vyema, naona hapana anayeweza kumdhuru Nyleptha. Usishangae, maana mimi nadhani bila shaka Sorais atajaribu kumdhuru.

Je, tumwambie Bwana Good habari za mambo yaliyotokea?’’
Sir Henry akasema, ‘’Sijui, maana habari hizi ndizo zitamuumiza sana hasa kwa jinsi anavyompenda Sorais.’’


Nikasema, ‘’Kweli, na labda hapana haja kumwambia. Atapata habari mwenyewe upesi. Sasa, sikiliza maneno yangu! Bila shaka sasa Sorais atajipanga upande wa Nasta analiyenuna huko katika nchi yake ya kaskazini, na vita vitatokea ambavyo namna yake havijatokea katika nchi ya Zuvendi kwa miaka mingi.


Tazama! ‘’nikamwonyesha natarishi wawili wanaotoka mbio chumbani mwa Sorais. Nikasema, ‘’Nifuate,’’ nikapanda ngazi ya kufikia juu ya mnara wa kulinda zamu, nikachukua darubini nikatizama juu ya ukuta wa jumba.


Tukamwona tarishi anakwenda mbio Hekaluni. Hakosi anampelekea habari kuhani mkuu, Agon. Sikumwona Yule tarishi wa pili. Lakini halafu kidogo, niliona mpanda farasi anakwenda mbio sana kupita katika mlango wa bustanini wa mji, nikatambua ni Yule tarishi wa pili.


Nikasema, ‘’Ah! Ama Sorais ni mwanamke wa juhudi. Anafanya mambo upesi, tena kwa ustadi na kwa nguvu.

Umefanya kama kumtukana, na sasa damu ya watu itamwagika kama mito kabla jua halijafutika , na damu yako pia akiweza kukushika.

Basi, nakwenda kumwambia Nyleptha. Wewe kaa hapa hapa ujaribu kutulia tena.’’
Nikaondoka.

Nilipata ruhusa kuonana na Nyleptha upesi. Alikuwa akimtazamia Sir Henry, na aliponiona mimi alisema, ‘’Bwana wangu mgonjwa? Makumazanh! Hata haji kunitazama. Natumaini si mgonjwa.’’

Nikamwambia ya kuwa hajambo, ndipo nilipoanza kumwambia habari zile toka mwanzo mpaka mwisho.

Lo! Angalia basi jinsi alivyoghadhabika! Akasema,
‘’Umethubutuje kunijia na kuniambia hadithi ya uongo kama hii? Kusema kuwa Bwana wangu alikuwa akishughulika na dada yangu Sorais! Ni uongo kabisa.’’
Nikamjibu, ‘’Niwie radhi Malkia, nilisema kuwa Sorais ndiye aliyekuwa akishughulika na Bwana wako.’’

Akasema, ‘’Usinitandazie utando wa buibui wa maneno. Si mamoja pia? Mmoja hutoa, mwingine hupokea na zawadi hupitishwa, si haja kugundua mwenye hatia ni nani! Sorais! Ee jinsi ninavyomchukulia Sorais Malkia, tena ni dada yangu. Hakika hangalifanya mambo hayo kama asingalivutwa.’’

Nikajibu, ‘’Nyleptha, unajua kabisa kuwa maneno yako ni ya upuuzi mtupu, na wakati huu si wakati wa kufanya upuuzi.’’

Akaupiga mguu wake chini kwa hasira, akasema, ‘’Unathubutuje kusema maneno kama haya? Je, Bwana wangu mwongo amekutuma unitukane hata na mimi? Wewe ni nani? si mgeni! hata kuthubutu kusema na mimi Malkia, tena kwa maneno kama haya?’’
Oooohoooo
 
Back
Top Bottom