Hadithi ya umslopagaas

SURA YA 21

Tulipofika juu ya mwinuko tulisimama kidogo ili farasi wetu wapumzike kidogo, tukageuka kutazama vita chini yetu. Miali mikali ya jua lililokuwa likishuka liliangaza pote ikapatia wekundu.

Mzee Umslopagaas akasema, ‘’Tumeshinda! Tazama jeshi la ‘Bibi wa Usiku’ linarudi nyuma kila upande, wala halina imani tena, linapindika kama chuma kilichoyeyuka, tena watu wake wanapigana kwa nusu ya mioyo tu.

Lakini, ole wetu, vita havitakwisha kwa kushinda upande huu wala huu, maana giza linaingia na vikosi havitaweza kufuatafuata na kuua!’’ Akatikisa kichwa chake kwa huzuni.

‘’Lakini nadhani askari zake hawatapigana tena, maana wamekwisha ona kuwa nguvu zetu ni nyingi. Ah! I vyema kuishi. Leo nimepata kuona vita vilivyostahili kupiganwa, nami nimeona vita vingi.’’

Basi, huku nyuma tulikuwa tumeianza safari yetu tena, na tulipokuwa tukifuatana kando kando nilimweleza kwa nini tunakwenda Milosis, na jinsi maisha yote yaliyopotea siku hii yatakavyo kuwa yamepotea bure ikiwa hatufanikiwi katika safari yetu, akasema, ‘’Ah!

Lazima tuende mwendo wa maili mia moja kabla hakujapambazuka hali tunao farasi wawili hawa tu! Haya basi, mbio! Mbio! Mwanadamu anaweza kujaribu tu, Makumazahn, na labda tutawahi kufika kwa wakati unaofaa na kumpasulia mbali kichwa Yule mchawi (yaani Agon).

Ndiye aliyetaka kutuchoma moto, Yule mganga wa kuleta mvua. Na sasa anataka kumtega mama yangu (Nyleptha). Haya, vyema! Hakika, kama mama yangu yu hai au kama amekufa, nitampasulia mbali kichwa mpaka ndevu zake.

Ndiyo, naapa kwa Chaka nitafanya hivi! Akatikisa Inkosikazi alipokuwa akienda. Sasa giza likawa linazidi kuingia, lakini kwa bahati mwezi ulipanda halafu, tena njia ni nzuri.

Basi, tuliendelea mbele, na wale farasi wawili wenye nguvu walituchukua vizuri kwa hatua ndefu zisizobadilika maili kufuata maili. Hatukusema, ila tuliinama mbele shingoni pa farasi wetu tukazisikiliza pumzi zao zinavyovutwa na kujaza mapafu yao makubwa, na vishindo vya kwato zao. Basi, vivi hivi saa baada ya saa.

Halafu niliona ya kuwa farasi mzuri niliyempanda anaanza kupotewa na nguvu. Nikaitazama saa yangu, ilikuwa karibu saa sita za usiku, na tulikuwa tumemaliza zaidi ya nusu ya safari yetu.

Juu ya mwinuko palikuwa na chemchem niliyoikumbuka nikamwashiria Umslopogaas asimame hapo, maana nilikusudia kuwapumzisha farasi zetu na sisi wenyewe muda wa dakika kumi.

Basi, alisimama, tukashuka katika farasi zetu farasi walisimama wanatweta wakisimama kwanza kwa mguu huu halafu huu, na huku jasho linawatoka na mvuke wao ulionekana kama ukungu katika hewa kimya cha usiku.

Basi nilimwacha Umslopogaas awashike farasi, nikajivuta karibu na chemchem nikanywa maji yake matamu. Kisha, nilijitia maji kichwani na mikononi nikarudi, na Yule Mzulu akaenda naye kunywa maji.

Kisha, tukawachukua farasi wakanywe maji kidogo tu, wala si zaidi lo! Tulishindana nao mno kuwavuta wayaache maji!

Basi, kisha Umslopogaas alinisaidia nipande juu ya farasi na yeye mtu mwenye nguvu akarukia juu yake bila kuvigusa vikuku vya matandiko yake, tukaianza tena safari yetu. Kwanza taratibu mpaka farasi wakazoea, kisha mbio.

Basi, hivyo tulienda mwendo wa maili kumi tena, ndiyo tulipofika kwenye mwinuko wa mwendo wa maili sita au saba. Mara tatu farasi wangu alitaka kuanguka, lakini alipofika juu ya mwinuko alijikaza tena akaenda mbio kuteremka kwa hatua zilizokatika katika na huku anatweta sana.

Tulikwenda mwendo wa maili tatu nne zile mbio kuliko kwanza, lakini niliona ya kuwa ni juhudi ya mwisho ya farasi wangu.

Basi ghafla alishika sana hatamu katikati ya meno yake akaenda mbio sana kadiri ya yadi mia tatu nne, ndipo aliposita hatua mbili tatu akaanguka kichwakichwa, na mimi nilijitupa mbele yake kadiri nilivyoweza.

Nilifanya haraka kusimama nikamtazama farasi wangu, akanitazama kwa macho ya kusikitisha, kisha kichwa chake kikaanguka akaguna, akakata roho.

Moyo wake ulikuwa umepasuka. Umslopagaas alisimama, nikamtazama kwa fadhaa, maana hata sasa bado mwendo wa maili ishirini, tutafika namna gani kabla ya mapambazuko hali tuna farasi mmoja tu?

Ilikuwa kama haiwezekani, lakini nilikuwa nimesahau nguvu za kupiga mbio za Mzee Mzulu. Bila kusema neno akashuka katika farasi akanipandisha mimi.
 
Nikamuuliza, ‘’Wewe utafanya nini?’’

Akashika kikuku cha matandiko ya farasi, akajibu, ‘’ Nitakimbia.’’ Ndipo tulipoanza tena kupiga mbio kama zile za kwanza.

Yule farasi Nuru alienda mbio na kila hatua alimsaidia Yule Mzulu. Ilikuwa ajabu kumwona Umslopagaas akipiga mbio maili baada ya maili, na midomo yake ikiwa wazi na mianzi ya pua imepanuka kama ya farasi.

Kila maili tano tulisimama ili kupumzika kidogo, kisha tukazidi kuendelea. Baada ya kupumzika mara tatu, nikamuuliza, ‘’Je, unaweza kuendelea au nikuache unifuatie nyuma?’’ Alishika shoka lake akakielekezea kivuli cheusi mbele yetu, nikaona kumbe ni hekalu la jua, nalo halikuwa mbali zaidi ya maili tano. Akasema na huku anatweta ‘’Nitalifikia ama nitakufa.’’

Lo! Maili tano zile za mwisho. Ngozi ya ndani ya mapaja yangu ilichubuka, na kila mara farasi wangu alipojitahidi alinitesa.

Wala si hivyo tu, Nilichoka kwa kazi nyingi na kwa njaa na kwa kukosa usingizi, tena niliumia sana kwa dhoruba ile niliyopigwa upande wa kushoto wa kifua changu, ikawa kama kwamba kipande cha mfupa au kitu kingine kinanichoma taratibu mpaka katika pafu langu.

Tena, farasi maskini Nuru alikuwa karibu kwisha, lakini hatukuweza kukawia, maana dalili ya kupambazuka ilianza kuonekana.

Na sasa mbele yetu tuliona milango ya shaba ya nje ya mji wa Milosis, nikaingiwa na kitisho. Je, wakikataa kutufungulia milango?’’ Nikapiga ukelele na huku nikatoa neno la kifalme, ‘’Fungua! Fungua! Fungua! Tarishi! Tarishi! Ameleta habari za vita!’’

Askari wa zamu akauliza, ‘’Habari gani? Nani wewe unayesafiri upesi hivi?’’
Nikajibu, ‘’Ni bwana Makumazahn na Umslopogaas.

Fungua! Fungua! Nimeleta habari.’’

Basi, milango mikubwa ilifunguliwa kwa kishindo, na daraja la kupita likashushwa, tukapita ndani mbio mbio. Yule askari wa zamu akatuuliza, ‘’Habari gani, bwana wangu habari gani?’’

Nikajibu, ‘’Bwana Inkubu analifukuza jeshi la Sorais kama wingu mbele ya upepo.’’
Ndipo nilipozidi kwenda mbele mbio.

Haya, farasi jasiri juhudi zaidi kidogo tu! Jitahidi kidogo tu mzee Mzulu jasiri mno. Usianguke sasa, Nuru, endelea zaidi muda mfupi wa dakika kumi na tano tu, na wewe mzee Mzulu wa vita kadhalika, na majina yenu yataishi milele katika habari za nchi hii.

Basi, tulipita mbio kwa vishindo katika njia za mji. Sasa tulipita Hekalu la ua, maili moja tu imesalia, maili moja tu.

Ah! Mungu ashukuriwe, sasa tumelifikia jumba, lakini tazama, miali ya kwanza ya mapambazuko inaiangaza dari ya kuba la dhahabu la Hekalu. Je, nitawahi au tendo limekwisha tendwa na njia imezibwa?

Nami nikapiga ukulele nikitaja neno la kifalme, ‘’Fungua! Fungua!’’
Hapana jibu, na moyo wangu ukataka kufifia.

Nikaita tena, na mara hii sauti moja ilinijibu, nikafurahi, maana ilikuwa sauti ya Kara, Yule askari mwaminifu wa Nyleptha, ndiye Yule aliyepelekwa na Nyleptha kumshika Sorais siku ile alipokimbilia Hekaluni.

Nikasema, ‘’Ni wewe Kara? Mimi ni Makumazahn, waambie askari wa zamu waufungue mlango na kulishusha daraja upesi sana. Upesi! Upesi!’’

Basi hapo kulikuwa kimya kwa muda uliokuwa kama kwamba hauna mwisho, kisha, nusu ya mlango ikafunguliwa tukaingia uani, na pale pale farasi shujaa Nuru alianguka, nikafikiri amekufa.

Niliondoka, nikaiegemea nguzo , nikatazama pande zote. Sikuona hata mtu mmoja isipokuwa Kara, nayeye alionekana kwamba anataabika, na nguo zake zimetatuka tatuka.

Alikuwa ameufungua mlango na kulishusha daraja yeye peke yake. Nikamuuliza, ‘’Je, wako wapi askari wa zamu?’’

Akanijibu, ‘’Sijui. Muda wa saa mbili wakati nilipokuwa nimelala usingizini, nilishikwa, nikafungwa kamba na askari walio chini ya amri zangu, na ndiyo kwanza nimeweza kujifungua. Naogopa, naogopa sana ya kuwa tumesalitiwa.’’

Basi, maneno yake yalinitia nguvu mpya. Nikamshika mkono nikaenda na huku ninasitasita, na Umslopagaas alinifuata huku anapepesuka kama mtu aliyelewa.

Tukapita katika vyumba mpaka katika sebule kuu mpaka chumbani alimolala malkia. Kwanza tulifika chumba cha askari wa zamu hapana hata askari mmoja.

Kwa hakika wamekwisha tenda shughuli yao, nasi tumechelewa! Ukimya na upweke wa vyumba vile vikubwa ulikuwa wa kutisha mno, ukanielemea kama ndoto ovu.

Mbele, mbele katika chumba cha Nyleptha tukajiingiza huku tunapepesuka, tukiogopa mambo tutakayoyaona, tukaona kuna taa inawaka, tena, mtu ameichukua ile taa.

Oh! Mungu ashukuriwe, ni malkia mwenyewe, naye yu salama! Hapa alikuwa amesimama amevaa mavazi yake ya usiku ameamshwa na ghasia zetu za kupenya katika chumba chake, na uzito wa usingizi bado umo machoni mwake.

Akalia, ‘’Nani? Je, kuna nini Makumazahn, ni wewe? Mbona unahangaika hivi? Umekuja kunipa habari za msiba msiba wa bwana wangu ooh usiseme ya kuwa amekufa hakufa!’’ akalia na huku anaipunga mikono yake kwa mojonzi.

Nikasema, ‘’Nilimwacha Inkubu jana jioni amejeruhiwa, lakini anawaongoza askari juu ya Sorais; kwa hiyo moyo wako na utulie.

Sorais amesukumwa nyuma kila mahali, na askari zako wanashinda.’’ Akasema kwa shangwe, ‘’Nilijua, nilijua kuwa askari zangu watashinda; nao walimwita mgeni, wakavitikisa vichwa vyao nilipomfanya mkuu wa majeshi yangu! Ulimwacha jana jioni ulisema, na sasa hakujapambazuka bado! Hakika’’.

Nikasema, ‘’Nyleptha, jivike mavazi yako utupe divai tunywe, uwaite mabibi watumishi wako upesi kama unataka kuyaokoa maisha yako. Upesi! Usisite!’’

Basi, kusikia haya tu akafanya haraka kujitupia mavazi mengine akawaita mabibi watumishi wake, wakaja. Nikamwambia, ‘’Tufuateni kimya.’’ Basi, kwanza tulikwenda katika chumba cha nje, nikamwambia, ‘’Sasa tupeni divai tunywe na chakula maana tuna karibia kufa.’’

Chumba kile kilikuwa cha wakuu wa askari wa zamu na kulikuwa na meza kwa ajili ya wakuu hao.

Na Nyleptha na mabibi, wakatuletea divai na nyama toka kabatini, Umslopogaas na mimi tukanywa, tukaona uzima unaturudia tena. Kisha, nikasema, ‘’Sikiliza Nyleptha, wako mabibi wawili katika watumishi wako unaoweza kuwatumaini kabisa?’’
Akajibu, ‘’Hakika.’’

Nikasema, ‘’Vyema, waambie waende nje mjini, watoke kwa mlango wa upande, wakawaite wanaume waaminifu wowote wawezao kuwapata, na waje pamoja na silaha zao ili kuyaokoa maisha yako.

La usiulize habari sasa, fanya tu nikuambiayo. Kara atawapeleka mabibi na kuwafungulia mlango.’’

Akageuka akachagua wawili wa mabibi wale, akawaambia maneno niliyomwambia, akawapa pia orodha ya majina ya wanaume watakaowaendea. Nikasema, ‘’Nendeni upesi na kwa siri, nendeni, maana maisha yenu yamo hatarini.’’

Basi, walimfuata Kara, ambaye nilimwambia arudi upesi awezavyo akanikute kwenye mlango wa ua mkubwa wa kutokea penye ngazi kuu. Basi, mimi na Umslopogaas tulikwenda huko, na malkia na mabibi, wale wakatufuata.

Na huku tulipokuwa tukienda, tulimega chakula na katika kukimega nilisimulia habari jinsi nilivyojua hatari inayomjia, na jinsi tulivyomwona Kara, na jinsi askari wote wa zamu walivyokuwa wametoroka, naye yupo yeye peke yake pamoja na mabibi watumishi wake tu.

Katika jumba lile kuu, nayeye aliniambia ya kuwa habari zilivuma mjini ya kuwa jeshi letu limeangamia kabisa, na Sorais anakuja Milosis kwa shangwe, na kwa maneno hayo wanaume wote walimwacha.

Basi, ingawa mambo haya yamechukua muda mrefu kuyasimulia, lakini tulikuwa tumo jumbani kadiri ya dakika sita au saba tu, na ingawa dari ya Hekalu ambayo ni ndefu sana ilikuwa imaangazwa na miali ya jua, lakini hakujapambazuka bado, wala hakutapambazuka ila baada ya dakika kumi hivi.

Basi sasa tukawa katika ua na hapo jeraha liliniuma hata nikawa sina budi kumshika mkono Nyleptha, na Umslopogaas alitufuata kwa shida na huku anakula.

Sasa tulikuwa tumevuka ua, tumefika mlango mwembamba katika ukuta unaotokea penye ngazi kuu. Nilichungulia nikashangaa.

Mlango wa mbao umekwisha ondolewa, na milango ya shaba ya nje pia imekwisha ondolewa. Ilikuwa imeondolewa kabisa katika bawaba zake na kutupwa chini kabisa kadiri ya futi mia mbili.

Basi, pale mbele yetu palikuwa na nafasi ile ya juu ya ngazi kuu, na vile vipandio kumi vya marumaru nyeusi basi!
 
Nzuri
 
SURA YA 22

Tulitazama nikasema, ‘’Waona, wameuondoa mlango. Je, hakuna kitu tunachoweza kukitumia ili kuuziba mlango huu? Sema upesi maana watatufikia kabla hakuja pambazuka.’’

Nilisema hivi kwa sababu nilitambua kuwa lazima tupalinde mahali hapo kwa sababu hapakuwa na milango mahali pengine katika jumba, maana vyumba vimetengwa kwa mapazia tu.

Tena, nilijua kuwa tukiweza kupalinda mahali hapo hapana mahali pengine wauaji wanapoweza kuingilia jumbani; maana jumba halifikiki kabisa isipokuwa kwa ule mlango wa siri alioingilia Sorais usiku ule alipojaribu kumuua Nyleptha, na tangu usiku ule umekwisha zibwa na waashi.

Nyleptha, kama ilivyo, desturi yake, aligundua shauri, akasema, ‘’Najua upande wa pili wa ua viko vipande vya marumaru vilivyokatwa tayari watu wakazi walivileta kufanya msingi wa sanamu ya Bwana wangu Inkubu na tuvitumie hivyo kuuziba mlango.’’

Basi, nikaona shauri lake ni jema, nikampeleka mwanamke mmoja mtumishi ambaye baba yake ni tajiri mwenye watu wengi wa kazi, ajaribu kufanya shauri naye kutusaidia.

Tena, nikamweka mwanamke mwingine mtumishi asimame mlangoni, nasi tukauvuka ua kuvitazama vile vipande vya marumaru, hapo tukamkuta Kara ambaye alikuwa amekwisha watuma wale wanawake watumishi wawili wa kwanza.

Vipande vya marumaru vilikuwa vikubwa, na vingine vilikuwa vinene kadiri ya inchi sita, na uzito wake kadiri ya ratili themanini.

Tena kulikuwako namna ya machela zilizotumika kuyachukulia mawe yale, nikawapa kazi wanawake wanne waanze kuyachukua mpaka mlangoni. Umslopogaas akasema, ‘’Sikiliza Makumazahn, watu waovu hao wakija, mimi nitailinda ngazi kuu wasiipande mpaka mlango uishe kuzibwa. Kweli kitakuwa kifo cha kiume.

Wala usinikataze rafiki yangu, maana mwisho huu ulibashiriwa na mtu aliyekufa zamani sana.

Mchana ulikuwa mzuri, na sasa usiku na uwe mzuri pia. Tazama, nalala kidogo ili nipumzike. Watu watakapokaribia, niamshe wala si kabla ya wakati huo, maana nitahitaji nguvu zangu zote.’’

Asiseme neno tena, ila alitoka nje akajitupa chini sakafuni, na mara akashikwa na usingizi. Wakati huo na mimi pia nilishindwa na uchovu, ikawa lazima nikae karibu na mlango kusimamia mambo.

Wale wanawake waliyaleta yale mawe, na Kara na Nyleptha wakaanza kuyapanga ili kuuziba mlango.

Lakini ilikuwa lazima kuyachukua mwendo wa yadi arobaini, kisha kurudi yadi arobaini, na ingawa wale wanawake walifanya kazi kwa bidii sana, na wengine walichukua jiwe kubwa mikonononi mwao peke yao, lakini hata hivyo kazi iliendelea taratibu sana.

Mwangaza ukaanza kuzidi, na halafu katika kimya tukasikia vishindo vya watu waliovalia silaha wamefika chini ya ngazi. Ukuta tulioujenga katika nafasi ya mlango ulikuwa na kimo cha futi mbili tu, na kazi hii ilikuwa imechukua muda wa dakika nane, na sasa wamekwisha fika.

Vishindo vilikaribia, na katika mwangaza wa kijivu wa mapambazuko tuliweza kuona mistari mirefu ya watu kadiri ya hamsini wakipanda ngazi. Sasa walikuwa wamekwisha fika kituo cha katikati, na hapo walitambua kuwa kuna mambo yanayotendeka juu, wakasimama dakika mbili tatu kushahuriana, kisha, wakaanza kupanda tena kwa taratibu na kwa hadhari.

Sasa tulikuwa tumefanya kazi kadiri ya dakika kumi na tano, na ukuta ulipata kimo cha futi tatu. Ndipo nilipomwamsha Umslopagaas. Yule mtu mkubwa akaondoka, akijinyosha, akazungusha Inkosikazi kichwani, akasema, ‘’Ni vyema. Najiona kama ni kijana tena.

Nguvu zangu zote zimenirudia, ndiyo, kama taa inayopanda kabla haijazimika. Usiogope, nitapigana vyema, divai na usingizi vimenitia moyo mpya.’’

‘’Makumazahn, nimeota ndoto. Nimeota kuwa wewe na mimi tumesimama katika nyota na kuichungulia dunia chini ya miguu yetu, na wewe ulikuwa kivuli Makumazahn, maana mwangaza uliupenya mwili wako, lakini sikuweza kuona jinsi uso wangu ulivyokuwa.

Saa yetu imefika ee mwindaji mzee. Basi, na ije. Tumeish si haba, lakini ningependa kuona vita vingine kama vile vya jana.

‘’Wanizike kwa desturi ya kikwetu, Makumazahn, wayaelekeze macho yangu kuitazama nchi ya Wazulu .’’ akaushika mkono wangu, kisha akageuka tayari kuwakabili adui wanaokuja.

Ndipo niliposhangaa Yule mtu wa Zuvendi Kara alipanda kwa utulivu na uthabiti toka katika ukuta ule tunaojenga, akasimama karibu na Yule Mzulu, na huku anauchomoa upanga wake.

Yule Mzulu mzee akacheka, akasema,

‘’Je, na wewe umekuja pia! Karibu karibu shujaa! Aha! Namsifu Yule mtu anayeweza kufa kiume! Aha! Na nguvu za kuua na kishindo cha silaha! Aha! Tu tayari! Tunainoa midomo yetu kama tai, mikuki yetu inang’aa katika miali ya jua twaitikisa mikuki yetu tuna njaa ya kupigana.

Nani anayekuja kumwamkia Inkosikazi?

Nani anataka kumbusu yeye ambaye matunda ya kubusu kwake ni kufa? Mimi Gotagota, mimi muuaji, mimi mwenye mbio, mimi Umslopagaas mwenye shoka, wa kabila la kizulu, mkuu wa kikosi cha Nkomabakosi mimi Umslopagaas, mwana wa ulimi wa Mfalme, mwana wa Makedama, mimi, wa damu ya Mfalme Chaka, mimi, mshindi wa wasioshindika, mimi, nawaita kama kulungu aitwavyo, nawakaribisha, nawangojea. Aha! Ni wewe, ni wewe!’ Ahahaa!''
 
Aliposema au kuimba wimbo wake wa vita, wale watu wenye silaha walipanda juu kwa haraka, na katika mwangaza uliokuwa ukizidi niliweza kuwatambua Nasta na Agon, na mtu mmoja mkubwa mwenye mkuki mzito akaruka juu ya vipandio vile kumi vya ngazi mbele ya wenzake akajaribu kumpiga Umslopagaas kwa mkuki wake.

Umslopagaas akauepa, lakini hakuijongeza miguu yake, na kwa hivi kipigo kilimkosa, na mara ile Inkosikazi lilipiga juu ya kichwa cha Yule mtu likampasulia mbali kichwa, na maiti yake ikaporomoka ngazini.

Na alipoanguka, ngao yake ya ngozi ya kiboko ilimponyoka Yule Mzulu aliinama akaishika, na huku anaimba. Mara ile Kara shujaa naye akamuua mtu, ndipo yalipoanza mambo nisiyopata kuyaona kamwe.

Adui walipanda juu upesi upesi, mmoja, wawili, watatu pamoja, nao kadiri walivyofika juu, shoka lile lilipiga na upanga ule ulipunga, na adui walifingirika chini maiti au walikufa. Na vita vilipozidi kuwa vikali macho ya mzee Mzulu yalizidi kuwa mepesi na mikono yake kupata nguvu.

Aliita wito wa vita na majina ya wakuu aliowaua, na vipigo vya shoka la kutisha vilianguka imara na sahihi, vikipasuka kila vilipoangukia.

Kila kipigo mtu alianguka na kuporomokea ngazini kwa vishindo. Walimpiga na kumkata kwa panga na mikuki wakimjeruhi mara nyingi mpaka akatapakaa damu mwili mzima.

Lakini ngao ile ilikikinga kichwa chake na deraya alizovaa zilimlinda kiwiliwili, akaendelea kuilinda ngazi akisaidiwa na Yule shujaa mzuvendi.

Hatimaye upanga wa Kara ulikatika, akashikana na adui wakaporomoka ngazini pamoja, akakatwa vipande vipande, akafa kishujaa.

Umslopagaas hakusita wala kugeuka hata kidogo, akazidi kuwapiga adui mpaka wakarudi nyuma wameshangaa, wakifikiri kuwa huyu si mwanadamu.

Sasa ukuta ule wa vipande vya marumaru ulikuwa na kimo cha futi nne na nusu, na moyo wangu ulianza kupata tumaini tena nilipouegemea.

Lakini nilipomtazama Umslopagaas jinsi anavyopigana kwa ujasiri, niliyasaga meno yangu kwa uchungu kwa kuwa sikuweza kumsaidia. Sikuweza kufanya kitu, maana silaha zangu zilikuwa zimepotea vitani.

Na mzee Umslopagaas akaliegemea shoka lake, na ingawa alikuwa tayari kuzimia kwa udhaifu kwa ajili ya majeraha yake, aliwadhihaki, akawaita ‘wanawake’ Yule mzee shujaa aliwakabili wote peke yake!

Kwa muda hapana aliyethubutu kumshambulia, ingawa Nasta alijaribu kuwatia moyo, mpaka Yule mzee Agon alipoona kuwa ukuta huo utamalizika kujengwa, na hila zake zitashindwa, aliutikisa mkuki wake mkubwa akaruka juu ya ngazi iliyoteleza kwa damu.

Yule Mzulu alizitambua ndevu zake nyeupe akalia,

‘’Ah! Ah! Ni wewe mpelelezi wa wachawi! Njoo, njoo, nakungojea mganga mweupe, njoo! Njoo! Nimeapa kuwa nitakuua, nami nimezoea kutimiza viapo vyangu.’’

Agon akaja kwa nguvu akampelekea Umslopagaas mkuki wake kwa nguvu nyingi hata ukapenya ngao yake ukamchoma shingoni kama kumparaza.

Yule Mzulu aliitupilia mbali ngao yake iliyochomwa kwa mkuki, na dakika ile ilikuwa dakika ya mwisho ya Agon, maana kabla hajaweza kuuchomoa mkuki wake na kupiga tena, Umslopagaas alilia.

‘’Na hiki ni chako, mfanya mvua,’’ akashika Inkosikazi kwa mikono miwili akalipunga juu sana akaliteremsha kwa nguvu, akampasua kichwa mzee Agon, na Agon alikufa, akaporomoka mpaka kwenye maiti za wauaji wenzake.

Na hapo alipoanguka, sauti kuu ilitoka chini ya ngazi, nikatazama juu ya ukuta ule tuliokuwa tukiujenga, nikaona askari wenye silaha wanakuja kutuokoa, nikaitikia sauti zao. Basi, hapo wale waliotaka kutuua waligeuka wapate kukimbia wasiweze, wakauwa wote. Mtu mmoja tu alisalia, ndiye Yule mkuu Nasta.

Kwa muda alisimama ameuegemea upanga wake mrefu, kama kwamba amekata tamaa, kisha alilia kwa sauti ya kutisha sana akamrukia Yule Mzulu, akaupunga upanga wake kwa nguvu nyingi kukizunguka kichwa chake, akampiga dhoruba moja hata ukapenya deraya ya chuma ukaingia mbavuni mwake Umslopagaas, na kwa muda kidogo alisimama kama amepooza, na shoka lake lilianguka chini.

Basi, hapo Nasta aliuinua upanga wake tena akaruka mbele ili ammalize Umslopagaas, lakini hakujua jinsi alivyo adui yake.

Maana Yule Mzulu alijitikisa akatoa sauti ya ghadhabu akamrukia Nasta kooni, kama nilivyoona simba aliyejeruhiwa akiruka.

Alimpiga pale mguu wake ulipofika juu ya kipandio cha juu ya ngazi, akamshika kwa mikono yake mirefu kama kwamba ni kamba ya chuma, wakavingirika pamoja wakishindana vikali.
 
Nasta alikuwa mtu mwenye nguvu nyingi, tena anapigania maisha yake, lakini hakuweza kumshinda Yule Mzulu ingawa alijeruhiwa vibaya, maana nguvu zake ni za fahari.

Basi, mwisho ukafika. Nilimwona mzee Umslopagaas akifanya juhudi akasimama wima, akajitahidi akamwinua Yule Nasta na huku anashindana mikononi mwake, akatoa sauti ya shangwe, akamtupa chini apondwe juu ya mawe yaliyoko chini kadiri ya futi mia mbili.

Basi, watu wale walioitwa na watumishi mabibi tuliowapeleka walikuwa wamekwisha fika na sauti kubwa zilitufaamisha kuwa watu wa mji wameamshwa, na wanaume na wanawake pia wanakuja wanataka kuingia.

Wengine katika mabibi hodari wa Nyleptha waliosaidia kuujenga ule ukuta walikwenda wawapitishe katika mlango wa upande, na wengine wakaanza kuubomoa ukuta ule tulioujenga kwa kazi ngumu.

Ukuta ulibomolewa upesi na Umslopagaas akaingia mlangoni amefuatwa na umati wa watu waliokuja kutusaidia.

Yule mzee Mzulu alikuwa wa kutisha sana, amefunikwa kwa meraha, nikajua kwa mcho yake ya kuwa anakufa. Damu ilimchuruzika usoni.

Alikuwa na jeraha shingoni pale alipochomwa na mkuki wa Agon na jeraha jingine mkononi, na katika ubavu wa kuume palikuwa na jeraha la urefu wa inchi sita pale upanga mkubwa wa Nasta ulipoingilia mpaka ndani kabisa.

Sasa, Yule mzee mkali aliendelea amelishika shoka lake mkononi, na wale wanawake walisahau kuogopa kuona damu, wakampigia kelele za shangwe alipokuwa akipita, lakini asisite wala kuwaangalia.

Huko alikwenda akipepesuka na mikono yake imenyoshwa mbele, na sisi tulimfuata. Alipita katika vichochoro, akazunguka mahali mawe yale yalipokuwapo, akapita katika mapazia ya mlango mpaka katika sebule kubwa ambayo sasa ilikuwa inajaa watu waliokuwa wakiingia kwa mlango wa upande mwingine.

Alipita moja kwa moja katika sebule na huku anaacha alama ya damu nyuma yake, mpaka alipoufikia ule mwamba mtakatifu uliopo katikati, na hapo ikawa kama kwamba nguvu zake zinamwishia, akasimama akaliegemea shoka lake. Kisha, akapaza sauti yake, akasema kwa sauti kuu,

‘’Nakufa, nakufa lakini vilikuwa vita vya kifalme.
Wako wapi wale walioipanda ngazi kuu? Siwaoni. Wewe upo Makumazahn, au umekwisha nitangulia katika mahali pa giza ninakokwenda mimi? Damu inanipofusha naona kizungu zungu, nasikia ngurumo ya maji. Ninaitwa!’’

Ndipo alipoonekana kama kwamba amepata wazo jingine, akalinua shoka lake jekundu akalibusu bamba lake. Akalia,

‘’Kwa heri Inkosikazi. Hapana, hapana, tuta kwenda pamoja, hatuwezi kuagana mimi na wewe. Tumeishi pamoja siku nyingi, wewe na mimi. Hapana mwingine atakayekushika.

‘’Pigo jingine moja tu! Pigo lililonyooka! Pigo lenye nguvu!’’

Akajinyosha urefu wake wote, akapiga ukelele uliotikisa hata moyo, akaliinua shoka lake juu ya kichwa chake kwa mikono yake miwili, akalizungusha kichwani mpaka lilionekana kama ni duara ya nuru.

Ndipo alipolipiga kwa nguvu za kutisha sana juu ya mwamba mtakatifu. Cheche za moto ziliruka juu, na nguvu zilikuwa za ajabu hata mwamba ule wa marumaru ulipasuka kwa kishindo ukavunjika vipande vipande, na kipini chake tu.

Vile vipande vya mwamba mtakatifu vikaanguka chini kwa kishindo kikubwa, ndipo Yule mzee Mzulu shujaa alipoanguka chini, amekufa lakini angali ameshika sehemu ya kipini cha Inkosikazi mkononi mwake.

‘’Basi, ndivyo alivyokufa Yule shujaa.’’

Sauti ya mastaajabu na ushangao iliwatoka wote waliyoyashuhudia mambo hayo, kisha mtu mmoja akalia, ‘’Bashiri, bashiri! Ameuvunja mwamba mtakatifu!’’ na hapo pakatokea mnong’ono.

Nyleptha akasema, ‘’Ndiyo, ndiyo watu wangu. Ameuvunja mwamba mtakatifu, na tazama, ubashiri umetimia, maana mfalme mgeni anatawala katika Zuvendi. Inkubu, bwana wangu, amelisukuma nyuma jeshi la Sorais, nami simwogopi tena, naye Yule aliyeiokoa taji ndiye atakayeipata.’’

Akageuka akauweka mkono wake begani mwangu akasema, ‘’Na bwana huyu, ingawa alijeruhiwa katika vita vya jana, alisafiri pamoja na Yule mzee shujaa ambaye amelala hapa sasa, kwa mwendo wa maili mia moja katikati ya kuchwa jua na kupambazuka kwake ili aniokoe katika hila za watu wenye ukatili.

Ndiyo, naye ameniokoa, ingawa nilikuwa karibu kuuawa, na kwa hivi kwa ajili ya matendo waliyoyafanya matendo ya utukufu ambayo hayapo katika habari za nchi yetu na kwa hivi nasema, jina la Makumazahn na jina la marehemu Umslopagaas, ndiyo, na jina la Kara, mtumishi wangu aliyemsaidia kuilinda ngazi kuu.

Yataandikwa kwa herufi za dhahabu juu ya kiti changu cha kifalme, nayo yatakuwa matukufu siku zote mpaka nchi yetu itakapokwisha.

Mimi, Malkia, nimesema haya.’’

Watu walipoisikia hotuba hii ya uhodari, walipiga vigelegele vya shangwe, na mimi nikasema kuwa tumefanya yaliyotupasa tu, kama ilivyo desturi ya Waingereza na Wazulu, wala si jambo la kusifiwa zaidi na waliposikia haya walizidi kupiga vigelegele vya shangwe.

Ndipo nilipoongozwa na kusaidiwa kuuvuka ua wa nje mpaka chumbani kwangu, ili nilazwe kitandani.

Na nilipokuwa nikienda nikamwona Yule farasi shujaa nuru aliyekuwa amelala chini vile vile alivyolala tulipoingia, nikamwambia wale waliokuwa wakinisaidia waniongoze ili nimtazame mnyama Yule mwema kabla hawajamchukua.

Na nilipokuwa nikimtazama, nilistaajabu, maana aliyafumbua macho yake, akakinua kichwa chake kidogo, akalia kidogo.

Nikataka kupiga ukelele wa kuraha nilipotambua kuwa hakufa, lakini nilikuwa sina nguvu ya kupiga ukelele.

Hata hivyo, masaisi waliitwa, wakamtunza Yule farasi, na baada ya kupita siku kumi na nne alikuwa amekwisha pona na kupata nguvu tena, naye anasifiwa na watu wote wa Milosis, ambao kila wamwonapo huwaonyesha watoto wao na kuwaambia kuwa huyu ni farasi aliyeyaokoa maisha ya Malkia wetu.

Basi, nililala kitandani, nikaogeshwa, na mavazi yangu ya deraya yakavuliwa. Wale walionisaidia waliniumiza sana waliponivua mavazi, wala si jambo la kustajabia, maana palikuwa na maumivu makubwa katika upande wa kushoto wa kifua na mbavu zangu kwa sababu ya jeraha kuambatana na deraya yangu.

Hapo, sikuwa na habari za mambo mengine mpaka niliposikia vishiko vya wapanda farasi waliofika nje ya jumba baada ya kupita muda wa saa kumi.

Nilijiinua nikauliza kuna habari gani, nikaambiwa kuwa jeshi la wapanda farasi lililotumwa na Sir Henry kumsaidia Malkia limefika toka vitani.

Walikuwa wametoka saa mbili baada ya kushuka jua. Walipotoka, mabaki ya jeshi la Sorais walikuwa wakiukimbilia mji wa Marstuna wakifuatiwa na wapanda farasi wetu.

Sir Henry alikuwa amefanya kambi yake katika kambi ile ile aliyoipanga Sorais usiku uliotangulia, naye alikusudia kuuendea Marstuna asubuhi.

Basi, nilipoyasikia hayo niliona kuwa naweza kufa mwenye moyo mwepesi, kisha sikuwa na habari tena nikazirai. Nilipoamka tena, kitu cha kwanza nilichokiona ni rodi ya Bwana Good, nikasikia sauti yake, ‘’Je, waonaje rafiki yangu?’’

Nikauliza kwa sauti ndogo, ‘’Unafanya nini hapa? Kwa nini hukuenda Marstuna? Je, umetoroka nini?’’ akajibu kwa shangwe, ‘’Marstuna? Ah! Marstuna imepigwa na kutekwa sasa siku saba zimepita umelala umezirai kwa muda wa siku kumi.’’

Nikauliza, ‘’Na Sorais’’ Akajibu, ‘’Sorais! Sorais ni mfungwa, watu wake walimhaini. Analetwa hapa, sijui watamfanya nini, maskini!’’

Nikauliza, ‘’Sir Henry yupo wapi?’’

Akajibu, ‘’Yupo pamoja na Nyleptha. Atakuja kukutazama kesho, mabwana waganga waliona kuwa afadhali asije leo.’’

Basi, kesho yake Sir Henry na Nyleptha wakaja kunitazama, na Sir Henry akanieleza habari zote zilizotokea tangu Umslopagaas na mimi tulipoondoka mbio vitani ili kuyaokoa maisha ya Malkia.

Nikauliza, ‘’Sorais atafanywa nini.’’ Mara uso wa Nyleptha ulikunjika akakasirika, lakini Sir Henry akaanza kusema maneno mengine, akasema, ‘’Nadhani utapata nafuu tena siku hizi hizi.’’

Nikatikisa kichwa changu, nikasema, ‘’La, usijidanganye, labda nitaweza kupata nafuu kidogo, lakini sitapona tena.

Sir Henry, mimi ninakufa. Labda nitakufa polepole, lakini kufa lazima nife. Unajua ya kuwa asubuhi yote nimetema damu? Nakuambia kuwa kuna kitu kinacho ni choma kwenye upande huu wa pafu langu, naweza kukisikia.

Basi, usihuzunike, nimeishi siku nyingi, na siku zangu za kufa zimefika tayari, ni kama ilivyo desturi kwa kila mwanadamu siku yake yakufa ikifika hakuna wakuizuia.’’

Basi, hapo Nyleptha akaanza kulia, Sir Henry akabadili mazungumzo, akaniambia kuwa tiyari wame fanya picha ya Umslopagaas ili wachore sanamu kubwa ya marumaru nyeusi mfano wake kuonyesha namna alivyouvunja ule mwamba mtakatifu, tena watatengeneza sanamu kubwa nyingine kwa marumaru nyeupe ya Yule farasi Nuru na mimi namna tulivyoonekana tulipofika uani akianguka chini mbele yangu.

Tangu wakati huo nimeziona sanamu zile, maana ninapoandika haya miezi sita imepita tangu vita vilipokwisha, nazo karibu zitakuwa tayari. Ni nzuri sana na hasa ile ya Umslopagaas, ambayo imefanana naye sana.

Ndipo waliponiambia kuwa usia wa Umslopagaas umetimizwa, alizikwa kwa desturi ya Kizulu.
 
SURA YA 23

Baada ya kupita siku saba tangu Nyleptha alipokuja kunitazama niliweza kupata nafuu kidogo, na Sir Henry aliniletea habari kuwa Sorais ataletwa mbele yao katika chumba cha Malkia kwenye saa sita, akaniomba nihudhurie kama nikiweza.

Basi, nilivutwa na udadisi kumwona Yule mwanamke mzuri maskini tena, nikaenda na huku ninasaidiwa na watumishi. Nilipofika, watu wengine walikuwa hawajafika bado isipokuwa wakuu wachache tu.

Nilipokwisha kukaa kidogo, Sorais akaletwa na kundi la askari, mzuri, mshupavu, lakini uso wake wa kiburi ulionyesha namna alivyotaabika, alikuwa amevaa mavazi ya kifalme kama desturi, naye ameshika mkuki ule mdogo mkononi mwake. Halafu kidogo Nyleptha akaja amefuatana na Sir Henry, na Bwana Good, wakakaa.

Nyleptha alikaa kimya kidogo, kisha akasema, ‘’Salamu Sorais dada yangu! Tazama jinsi ulivyo upasua ufalme wetu kama kitambaa, umewaua watu wangu elfu nyingi, umefanya hila ovu mara mbili kuniua, tena, umeapa kumuua bwana wangu na wenziwe na kunitupa mimi toka juu ya ngazi kuu mimi chini yake.!

Kweli dada yangu nini kimekupata hata ufikirie kuniua? Ni wivu tu wa mapenzi ulio tutenganisha? Au kuna kitu kingine! Je, unalo neno la kusema kutoa sababu usiuawe? Sema, ee Sorais!’’

Sorais akajibu kwa sauti thabiti, ‘’Sina neno la kusema ila laiti ningalishinda kuliko kushindwa. Basi, nifanye upendavyo.’’ Akajivuta juu akaukunja uso wake na huku anauchezea ule mkuki mdogo wa fedha.

Nyleptha akasema, ‘’Sorais, tangu mwanzo nimekuwa dada mwema kwako. Watu walipozungumza juu ya habari za kuwapo Malkia wawili, mimi niliwaambia waache ukae kitini pamoja nami, maana tulikuwa mapacha ingawa mimi nilizaliwa kwanza.

Tulipokuwa watoto tulicheza pamoja tulilala kitanda kimoja na huku tumekumbatiana, na kwa hiyo moyo wangu unakuonea huruma sana hata naumia kwaajili yako. Sorais,kwa uovu wa mambo uliyoyafanya wewe ukiwa hai nchi haitakuwa na amani. Lakini hata hivyo hufi, maana bwana wangu mpenzi ameomba usiuawe.

Basi, nakutoa na kukuweka katika mikono yake akufanye apendavyo.’’
Sorais alibadilika rangi, asiseme neno. Kisha Sir Henry akasema, na huku anamtazama Bwana Good.

‘’Nafahamu ya kuwa wewe ulimpenda Malkia Sorais, sijui namna unavyoona sasa. Lakini labda mambo yatakwisha vizuri ukimwoa. Anazo mali zake na nchi zake mwenyewe, na sisi hatutamdhuru.’’

Bwana Good akajibu, ‘’Kwangu mimi, naweza kusahau mambo yote yaliyopita, yaani ikiwa yeye atanikubali. Ni tayari kumwoa hata kesho, nami nitajaribu kuwa mume mwema kwake.’’

Basi, sasa watu wote walimtazama Sorais, na huku yeye amesimama na kutabasamu kidogo. Kisha akamtazama Nyleptha akasema, ‘’Nakushukuru ee dada yangu Malkia mwenye huruma, na kwa ajili ya mapenzi yote ulionionyesha tangu utoto wangu.

Ustawi, amani na neema ziandamane na njia zako. Uishi na kutawala siku nyingi, ee Malkia mkubwa mtukufu, na upendo wa mume wako uhifadhiwe, na watoto wako wanaume na wanawake wawe wengi.

Nakushukuru bwana wangu Inkubu Mfalme nakushukuru kwa kuwa umeikubali zawadi na kuitia tena katika mikono ya mwenzako Bwana Bougwan.

Mwisho, nakushukuru sana wewe Bwana Bougwan kwa kuwa umekubali kunipokea tena.
Nakushukuru mara elfu, wewe ni mtu mwema mwaminifu. Na sasa nimekwisha kuwashukuru wote, ninalo neno moja la kusema.

‘’Malkia Nyleptha, huwezi kunifahamu hata kidogo ukifikiri nitaridhika na mambo yalivyo. Naidharau huruma yako, tena, nakuchukia kwa ajili yake. Natupa mbele yako misamaha yako kana kwamba ni nyoka na mimi niliyesimama hapa, nimesalitiwa, nimeachwa nimetukanwa, mimi peke yangu nitakushinda.

Namdhihaki, namchukia kila mmoja wenu. Na hili ndilo jibu langu.’’ Na mara ile kabla mtu hajaweza kukisia anachotaka kufanya, alijichoma kwa mkuki wake mdogo wa fedha aliouchukua mkononi, akajichoma mbavuni kwa nguvu nyingi, akaanguka chini.

Nyleptha alipiga ukulele wa uchungu, na Bwana Good akataka kuzimia, na sisi sote wengine tukamkimbilia Sorais.

Lakini ‘’Bibi wa Usiku’’ alijiinua akauegemea mkono mmoja, akautazama uso wa Sir Henry kwa macho yake mazuri dakika moja, kama kwamba anataka kumwambia neno, kisha kichwa chake kikaanguka chini, akaugua, na roho yake ikamtoka.

Siwezi kueleza hali iliyotokea hapo! Maskini Bwana Good maana aligeuka kama mfu.

Basi, alizikwa kwa desturi ya kifalme, na huu ndio mwisho wake. Baada ya kupita mwezi mmoja tangu mambo hayo yalipotokea, palikuwa na tamasha kuu katika Hekalu la Ua, na Sir Henry akatawazwa kuwa mfalme wa Zuvendi.

Mimi mwenye sikuwapo, maana ugonjwa ulinizidi sana, lakini Bwana Good alikuwapo akanieleza habari za mambo yaliyofanyika.

Aliniambia kuwa Nyleptha alikuwa mzuri sana, na Sir Henry akaonekana kuwa Mfalme halisi, na watu wote walimshangilia na kumfurahia.

Tena, aliniambia kuwa Yule farasi Nuru alikuwa katika andamano, na watu wote walikuwa wa kiimba ‘’Yu wapi Makumazahn yu wapi Makumazahn!’’ mpaka sauti zao zilipwea, wala hawakukubali kunyamaza mpaka walipoambiwa kuwa ungonjwa umemzidi, na kwa hivyo hukuweza kuja.

Basi, baada ya mambo hayo, niliomba nihamishwe katika nyumba ninamokaa sasa ninapoandika maneno haya. Ni nyumba nzuri mwendo wa maili mbili kutoka mji wa Milosis. Miezi mitano imepita tangu nilipohamishiwa hapa, na wakati huo wote nimelala kitandani na kujizungumza kwa kuyaandika maneno haya yanosimulia habari za safari yetu.

Labda habari hizi hazitasomwa na mtu, lakini si kitu, maana kazi ya kuziandika imenisaidia kuvumilia maumivu ya saa nyingi. Lakini namshukuru Mungu ya kuwa saa nyingi hazibaki sasa.

Tangu nilipoyaandika maneno hayo ya juu, juma moja limepita, na sasa naitwaa kalamu yangu mara ya mwisho maana najua mwisho wangu u karibu. Akili zangu bado zi timamu, na hata sasa ninaweza kuandika lakini kwa shida sana.

Maumivu katika pafu langu yamenizidi sana juma hili, lakini sasa yametulia na naona kama upande huu wa pafu langu umekufa ganzi. Tena, pamoja na maumivu, hofu ya kufa imeniondokea, naona kama kwamba ninakwenda kulala katika mikono ya raha isiyoelezeka.

Mambo yote yanabadilika machoni pangu. Giza linakaribia na mwangaza unafifia. Lakini ni kama kwamba naweza kulipenya giza, na hata sasa ninaanza kuona shangwe ya watu wengi waliokwisha fariki walio tayari kunipokea.

Mtoto wangu Harry naye yupo pamoja na wengine, na zaidi ya wote ni mke wangu mpenzi, Yule mwanamke mzuri kuliko wote walionifurahisha kwenye dunia hii.

Jua linashuka na kulifanya kuba kubwa la Hekalu kuwa kama moto mkubwa unaowaka, na vidole vyangu vinachoka. Basi, kwa wote walionijua au waliozijua habari zangu, na wote wanaoweza kumkumbuka mzee mwindaji kwa huruma, naunyosha mkono wangu toka nchi ya mbali na kuwapa kwa heri.

Na sasa naiweka roho yangu katika mikono ya Mwenyezi Mungu aliyenileta duniani. Na kama wasemavyo Wazulu, ‘’Nimesema.’’
 
SURA YA 24

Mwaka mzima umepita tangu rafiki yangu mpenzi Allan Quatermain alipoliandika neno lile ‘’Nimesema’’ mwisho wa taarifa ya mambo yaliyotupata.

Nisinge penda kuyaongeza maneno yake, lakini kwa namna ya ajabu ipo, njia ambayo kwayo labda maandiko yake yataweza kupelekwa Uingereza.

Kweli ni jambo la kubahatisha tu, lakini Bwana Good na mimi tunafikiri afadhali na tubaatishe, kwa muda wa miezi sita wameshughulika katika mipaka ya Zuvendi ili waone kwamba ziko njia nyingine za kutokea na kuingilia katika nchi hii, na moja imeonekana.

Njia hii ndiyo ile aliyopita Yule mtu maskini aliyefika kwa Bwana Mackenzie, nayo ilijulikana na makuhani wa nchi tu, wakaificha kabisa.

Sasa njia hii itazibwa kabisa, lakini kabla ya kuiziba tunapeleka tarishi ayachukue maandiko ya Bwana Allan Quatermain na barua kadha wa kadha toka kwa Bwana Good, kwa rafiki zake, na toka kwangu kwenda kwa ndugu yangu George Curtis.

Nasikitika sana ya kuwa sitamuona tena ndugu yangu, na katika barua yangu namwambia kwa kuwa yeye ni mrithi wangu, basi azichukue mali zangu zote.

Lakini sasa nataka kuongeza maneno kidogo juu ya mzee Quatermain. Alifariki asubuhi na mapema siku iliyofuata ile ambayo aliyaandika maneno ya mwisho ya sura iliyotangulia. Nyleptha, Bwana Good na mimi tulikuwapo alipofariki.

Saa moja kabla hakujapambazuka ilikuwa dhahiri ya kuwa anakufa, tukahuzunika mno.
Kulipopambazuka, aliomba ainuliwe aweze kulioa jua mara ya mwisho linavyotoka, akalitazama sana kwa muda, kisha akasema, ‘’Katika muda wa dakika chache nitakuwa nimekwisha ipita milango ile ya dhahabu.

Ninakwenda safari ya ajabu kupita zile zote tulizokwenda pamoja. Mungu awabariki, nitawangojea huko.’’ Akaugua, akalala, akafariki dunia.

Basi, hivyo ndivyo alivyo fariki mtu ambaye nadhani tabia yake ilikuwa nzuri kuliko tabia za watu wote niliopata kuonana nao. Bwana Good alisoma ibada ya kuzika wafu, na Nyleptha na mimi tulikuwapo.

Kisha kwa kuwa watu wote waliomba sana, maiti yake ilichukuliwa kwa sherehe nyingi na kuchomwa moto kama ilivyo desturi ya Wazuvendi.

Basi, dakika chache kabla ya kushuka jua, maiti iliwekwa juu ya milango ya shaba mbele ya madhabahu, tukasimama huko kuungojea mwali wa mwisho wa jua linaloshuka.

Halafu mwali wa mwisho ulipenya dirishani, ukauangazia uso wake kama mshale wa dhahabu, ukafanya kama taji ya dhahabu juu ya paji lake, ndipo panda zililia, na milango ilifunguka, na maiti ya rafiki yetu mpenzi ilianguka chini motoni .

Basi, huu ulikuwa mwisho wa maisha ya ajabu ya mwindaji Quatermain. Tangu mambo hayo yalipotokea, tumestawi sana.

Bwana Good anashughulika kuunda merikebu za vita za kusafiri katika ziwa la Milosis, na ziwa jingine, na kwa merikebu hizo tunatumaini kuzidisha biashara na kuwatuliza watu wengine wenye matata wanaokaa kando kando ya maziwa hayo.

Maskini Bwana Good! Mara nyingi huuzunika sana kwa kile kifo kibaya cha Malkia Sorais, maana alimpenda sana.

Lakini natumaini ipo siku machungu yake yataisha na kuhuzunika kwake kutaisha. Maana Nyleptha anamtafutia mke atakayemfaa. Na kwa habari zangu mimi, nadhani afadhali nisijaribu kuzisimulia, maana sijui nianzie wapi.

Cheo changu cha Kifalme kina madaraka makubwa sana, lakini natumaini kufanya mema siku zote, nami nimekusudia mambo mawili makubwa, yaani kuunganisha sehemu mbalimbali za wenyeji chini ya serikali yenye nguvu, na kuzipunguza sana nguvu za makuhani.

Na baadaye, Mungu akinijalia, natumaini kuweka tayari njia ya kuiondoa dini isiyo ya akili ya kuliabudu jua na kuingiza dini ya kweli ya Kikristo.

Kwa heri,

HENRY CURTIS.

Nilisahau kusema ya kuwa zamani za miezi sita, Nyleptha alijifungua mtoto mwanaume mzuri sana nadhani atakuwa mrithi wangu.

HC.

MAELEZOYA BWANA GEORGE CURTIS

Hati ya maandiko hayo yenye anwani yangu iliyoandikwa kwa mkono wa ndugu yangu mpenzi Henry Curtis ambaye nilifikiri kuwa amekwisha kufa, iliniwasili salama. Ilichukua muda wa miaka miwili kinifikia.

Nimeyasoma kwa ushangao, na ingawa sasa nimefarijika kujua kuwa yeye na Bwana Good wako hai, lakini kwa jinsi wanavyokaa katika nchi ile ya mbali naona ni kama kwamba wamekwisha kufa.

Wamejitenga na Uingereza na rafiki na jamaa zao milele.
Namna hati hii ilivyopata kunifikia sijui, lakini naona kwamba Yule tarishi aliyetumwa alimkabidhi bwana mmojawapo aliyeitia katika posta. Barua zile alizozitaja ndugu yangu hazikuniwasilia, na kwa hivi naona zimepotea njiani.

GEORGE CUTTIS.

MWISHO.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom