blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,096
- 7,471
- Thread starter
- #301
Mwishowe, akaanza kusema, na sauti yake ilikuwa ya unyenyekevu, wala si kama yake ya desturi, akasema, ‘’Sijawahi kufikiri ya kuwa ipo siku nita fundishwa wajibu wangu na Mzulu lakini mambo yaonyesha namna tunavyoweza kushawishiwa.
Labda mtaweza kufahamu jinsi ninavyoona aibu, tena nimestahili kuaibika. Kweli ilikuwa wajibu wangu kumshika Sorais na kumweka katika mikono ya askari wa zamu, lakini sikuweza, basi.
Nilimwacha aende zake, nikaahidi sitaitoa nje habari hiyo, ndiyo aibu yangu, Aliniambia ya kuwa nikijipanga upande wake atakubali nimwooe na kunifanya mfalme wa nchi hii, lakini nashukuru ya kuwa nilikataa hata alipoahidi nimwoe, nikasema kuwa siwezi kuwahaini rafiki zangu,Basi,ndugu zangu mnaweza kufanya mnayotaka kunifanyia, nimeyastahili yote.
Nitasema haya nawaomba nanyi mjilinde msipende mwanamke kwa moyo wenu wote na kujaribiwa naye kama mimi nilivyojaribiwa,’’ akageuka ili aende.
Sir Henry akasema, ‘’Mwenzangu, ngoja kwanza. Mimi nina hadithi ninayotaka kusimulia.’’
Akamsimulia habari ya mambo yale yaliyotokea jana baina ya yeye na Sorais. Basi, habari za mambo yale zilimvunja moyo zaidi maskini Good. Akasema, ‘’Nadhani habari hizi zimekwisha niponya,’’ akageuka akaenda zake, nami nilimsikitikia sana.
Siku ile ilikuwa siku ya baraza ambayo Malkia walizoea kukaa katika sebule kubwa na kusikiliza haja za watu, na kufanya mashauri mengineyo ya sheria na fedha, na mambo kadha wa kadha, basi baadaye kidogo tulikwenda sebuleni, na Bwana Good akafuatana nasi.
Tulipofika tulimkuta Nyleptha amekwisha kaa kitini pake, na mambo yanaendelea kama kawaida, amezungukwa na washauri, wakuu, wana sheria, makuhani, na jeshi kubwa kidogo la askari.
Lakini ilikuwa dhahiri kwa nyuso za watu na kwa namna watu walivyoongeaongea, ya kuwa hawaangalii mambo ya kawaida ila wanatazamia mengine, maana habari zimekwisha enea kuwa vita vya kindanindani vi karibu.
Basi, tukamwamkia Nyleptha, tukakaa katika mahali petu pa siku zote, pia muda mambo yaliendelea kama kawaida, mara tarumbeta zilianza kupigwa nje ya jumba, na mlio mkubwa uliwatoka umati wa watu waliokuwa wamehudhuria nje kutazama mambo yatakayotokea:
‘’Sorais! Sorais! Ndipo mingurumo ya magurudumu ya magari iliposikika na halafu pazia kubwa mwisho wa sebule lilivutwa upande, na Sorais ‘’Bibi wa Usiku’’ aliingia, wala hakuja peke yake.
Agon kuhani mkuu alimtangulia amevalia mavazi yake yaliyo bora, na kila upande wake makuhani walishindamana.
Sababu ya kuwako makuhani ilikuwa dhahiri, maana kwa kuwa amefuatana nao, hawezi kuzuiliwa, kwa kuwa kuwazuia makuhani ni kufanya mambo ya kufuru. Nyuma yake walikuwako wakuu wengine na kundi la askari waliochaguliwa.
Kumtazama tu ikawa dhahiri kuwa Sorais hakuwa na amani, maana badala ya mavazi yake ya siku zote amevaa mavazi namna ya kiaskari, tena alikuwa amechukua mkuki mdogo wa fedha mkononi mwake.
Basi, alipita katikati ya sebule na watu walijitenga wampishe njia, na alipofika karibu na mwamba mtakatifu alisimama, akaweka mkono wake juu yake, akasema kwa sauti kubwa. ‘’Salamu, Ee Malkia!’’
Na Nyleptha akajibu ‘’Salamu dada yangu! Karibu usiogope hutadhurika.’’
Sorais hakusema neno, akapita mpaka akasimama mbele ya viti vya kifalme, kisha akasema, ‘’Nina haja Ee Malkia!’’
Nyleptha akajibu, ‘’Sema, dada yangu, kuna kitu gani zaidi ninachoweza kukupa nawe unao nusu ya ufalme wote.’’
Akajibu, ‘’Unaweza kuniambia mimi na watu wote wa Zuvendi habari za kweli. Utamtwaa Yule mgeni mbwa mwitu kuwa mume wako ama sivyo?’’
Akamwelekezea mkuki wake mdogo Sir Henry.
Sir Henry akaukunja uso wake, akageuka akamwambia Sorais kwa sauti ndogo, ‘’Nakumbuka ya kuwa jana ulikuwa na majina mengine ya kuniita wala si mbwa mwitu, Ee Malkia.’’
Basi, hapo Nyleptha aliona mambo hayawezi kifichika tena, akaondoka, akashuka katika kiti chake, akaenda mpaka pale Sir Henry alipokuwepo, akasimama pale pamoja naye.
Akaiondoa bangili ya dhahabu mfano wa nyoka katika mkono wake, akamwambia Sir Henry apige magoti, akapiga goti moja, kisha, akaitwaa bangili ile ya dhahabu akaikunjua akaiweka shingoni mwa Sir Henry, akambusu pajini, akamwita ‘’Bwana mpenzi.’’
Kisha akasema, ‘’Waona, nimeiweka bangili yangu katika shingo ya mbwa mwitu, na tazama! Atakuwa mbwa wa kunilinda, ndilo jibu langu kwako wewe Malkia Sorais dada yangu, na kwa watu waliyofuatana nawe.’’
Kisha, akageuka akawaambia wote waliopo kwa sauti thabiti, ‘’Ndiyo, Bibi wa Usiku, na wakuu, na makuhani na watu wote mliopo , hii ndiyo dalili mbele yenu nyote, ya kuwa nimemtwaa mgeni huyu awe mume wangu.’’ Akamshika mkono wake akawatazama watu wote kwa ujasiri.
Tendo alilolitenda lilikuwa la uhodari, na Wazuvendi, kama watu wote walivyo, hupenda ujarisi, basi walipaza sauti zao kwa shangwe.
Lakini Sorais alisimama akitazama chini, maana hakuweza kustahimili kuiona furaha ya dada yake, na jinsi alivyomwibia mwanaume aliyetumaini kumpata, akatetemeka kwa hasira ya wivu aliouona.
Kisha, aliuinua uso wake, akaunyosha juu mkuki wake mdogo, akautikisa, akasema.
‘’Na wewe Nyleptha, unafikiri kuwa mimi Sorais, Malkia wa Zuvendi nitakubali mgeni huyo akikaliye kiti cha kifalme cha baba yangu? Hasha! Hasha! Kifua changu kingali na uzima ndani yake, na watu wangalipo wa kunifuata na mkuki upo wa kupigia, sitakubali! Nani, nani watakaonifuata mimi?
Sasa Nyleptha, mtoe mgeni mbwa mwitu na wale waliokuja pamoja naye wauawe kwa moto, maana sio hawa waliyofanya dhambi ya kufisha juu ya Jua kama sivyo, basi nitapigana vita! Vita vya damu! Nakuambia Nyleptha nitakubandua katika kiti chako, nawe utatupwa, utatupwa toka juu ya ngazi kuu mpaka chini yake, kwa sababu umetia aibu nyumba ya kifalme.
Na ninyi wageni, nawaambieni nyote isipokuwa Bougwan, ambaye kwa kuwa alinitumikia nitamwokoa akiwaacha wenzake, (na Bwana Good alikitikisa kichwa chake sana kukataa) nitawafunika kwa mabati ya dhahabu na kuwafungia minyororo mngali hai katika ncha za panda za sanamu zile nchani mwa dari, iliiwe dalili na maonyo kwa watu wote.
Na wewe Inkubu, wewe utakufa kwa namna nyingine ambayo sitakuambia sasa.’’
Basi, akanyamazana akitweta, maana ghadhabu yake ilimtikisa kama tufani, na mnong’ono wa nusu hofu na nusu kumsifu, ulivuma katika sebule.
Kisha, Nyleptha akajibu kwa madaha na utulivu, akasema, ‘’Dada yangu, heshima yangu ingevunjika kabisa kama ningesema maneno kama hayo uliyoyasema, na kuogofya kama wewe ulivyoogofya.
Lakini ukifanya vita, basi, mimi nitajaribu kupigana nawe, maana ingawa mikono yangu huonekana kuwa nyororo, lakini itakuwa kama chuma cha kukaba koo za jeshi lako. Sorais, sikuogopi!
Nahuzunika kwa mambo utakayoyaleta juu ya watu wetu na juu yako mwenyewe, lakini kwangu mimi, nasema, sikuogopi. Na wewe jana tu ulijaribu kumvuta Bwana wangu awe mpenzi wako na Bwana wako, ambaye leo unamwita mgeni mbwa mwitu.
Tena, usiku huu huu ulininyemelea kama nyoka mpaka katika chumba changu cha kulala kwa njia ya siri, nawe ulijaribu kuniua, mimi dada yako, katika usingizi wangu’’
Sauti ya Agon na watu wapatao ishirini wengine zililia, ‘’Uwongo! Uwongo!’’
Basi, hapo nilisimama mbele, na huku ninakiinua kile kipande cha kisu, nikasema, ‘’Si uwongo, je, kipini cha kisu hiki ki wapi Ee Sorais?’’
Na Bwana Good akajitokeza ili authibitishe uaminifu wake tena, akasema, ‘’Si uwongo. Nilimshika ‘Bibi wa Usiku’ pale kitandani pa Malkia Nyleptha, na kisu chake kilivunjikia kifuani pangu.’’
Basi Sorais aliona kuwa mioyo ya watu inageuka upande mwingine, akautikisa mkuki wake, akasema, ‘’Nani wako upande wangu? Je, Bougwan?’’ Hivi akageuka kumuuliza kwa sauti ndogo, kisha akaendelea.
‘’Wewe mwoga, kama ungalinifuata mimi ungeweza kuwa mfalme wangu na mume wangu’’
Akalia, ‘’Vita! Vita! Vita! Hapa nimesimama na mkono wangu juu ya mwamba mtakatifu utakaodumu mpaka Wazuvendi watakapojiinamisha chini ya mgeni. Nani watamfuata Sorais katika kushinda na kujipatia heshima.’’
Mara umati wa watu ulianza kufumukana kwa ghasia. Wengi waliokuwapo walijipanga upande wa Sorais, lakini wengine walitoka upande wake wakajipanga upande wetu. Katika hao waliotutoka, kiongozi mmoja wa askari wa Nyleptha aliyegeuka alijaribu kukimbia mlangoni walimopita watu wa Sorais.
Lakini Umslopogaas alikuwapo anatazama, akamshika, maana aliona kuwa akitoka, basi wengine watamfuata. Basi, Yule askari aliufuta upanga wake akajaribu kumpiga Umslopogaas.
Hapo, Mslopogaas alirudi nyuma kwa mlio mkali akauepuka upanga, akalizungusha shoka lake, akampiga, na Yule askari akaanguka chini amekufa.
Basi, hii ilikuwa damu ya kwanza kumwagika katika vita. Nikalia, ‘’Fungeni milango’’ nikifikiri kuwa labda tutaweza kumzuia Sorais, na kwa namna hii kuzuia matata.
Lakini tulichelewa; basi yeye na askari zake walikuwa katika kupita, na mara walikuwa wakienda mbio katika njia zao, zikajaa sauti za farasi na mingurumo ya magurudumu ya magari yake.
Basi, Sorais, akapita akivuta nusu ya watu nyuma yake kama chamchela katika mji, akashika njia yake kuiendea Marstuna iliyo ngome kadiri ya maili mia moja na thelathini upande wa kaskazini wa Milosis.
Baada ya hayo, mji ulijaa sauti za vishindo vya vikosi na matengenezo ya vita, Mzee Umslopogaas alianza tena kukaa katika jua na kuyanoa makali ya Inkosikazi.