HADITHI YA PENZI LA NYOKA MTU

Mwalimu Truth

Member
Feb 15, 2015
57
62
PENZI LA NYOKA MTU
MTUNZI:HAKIKA JONATHAN
WHATSAP:0629905923
*SEHEMU YA KWANZA**
Msitu wa Ukijani ulikuwa kimya sana,ukimya uliopelekea sauti za ndege kusikika kila pembe ya msitu huo.Ndege walipokezana kuimba kwa furaha kufurahia mwanga hafifu wa jua uliopenya kwenye miti mirefu ya msitu huo iliyonawili na kupendezeshwa na matawi ya kijani yaliyonawili haswaa!.
Ilikuwa yapata majira ya saa tisa arasili,Boka mkono wa shoka kama alivyojulikana na wengi alikuwa ameketi kando ya barabara nyembamba ya kuingilia na kutokea msituni.Jasho jembamba lilimchuruzika mwilini,nguo zake ngumu zilizotengenezwa kwa ngozi ya ng’ombe zililowa na kuwa tepetepe.Alikuwa amechoka sana,pilikapilika za hapa na pale msituni,kurusha mikuki huku na kule hazikuzaa matunda siku hiyo.Alijitazama chini hadi juu,alijidharau,kwa mara ya kwanza akaudharau mwili wake mkubwa ulioheshimika na kuogopwa na kila mtu katika kijiji cha Mwasonge.
“Haiwezekani!!Haiwezekani mimi Boka nikose hata Sungura!Wazazi wangu watakula nini leo???”Alijisemea.
Akatazama kulia,akatazama kushoto,akatazama juu tena,shingo yake alikuwa akiizungusha kama mtu aliyehisi kitu.Alipojiridhisha hakukuwa na kitu wala hatari yoyote,alisimama na kuchuma matawi kadhaa ya miti.Jambo ambalo ilikuwa rahisi sana kutokana na mwili mrefu aliokuwa nao,waliompachika jina la mkono wa shoka hawakukosea.Jina hilo lilimfaa haswaa!Ilikuwa kawaida kwake kumchana chana simba kwa mikono yake,simba yoyote yule aliyetoroka msituni na kuvamia kijiji.Boka alipambana naye bila woga huku askari wa mtemi wakikimbia na kujificha,Boka alipambana na kushinda.Mtemi alimpenda sana Boka,alimwomba Boka kujiunga na jeshi lake lakini Boka alikataa,alimwomba Boka amuoe binti yake lakini Boka alikataa.Jambo ambalo lilimshangaza sana mtemi,wazazi wa Boka pamoja na wanakijiji wote wa Mwasonge.
Boka baada ya kukata magome ya miti,alitandika vizuri na kujilaza kusubili jua lizame ili ajisogeze mtoni kujaribu bahati yake,alikuwa na uhakika atakuta wanyama wengi wakinywa maji baada ya kula Na kushiba.Dakika moja ilipita,tatu zikapita,tano zikapita,Boka alianza kukoroma.Alikuwa amepitiwa na usingizi mzito na mtamu.
“Puuuuu!”Kishindo kilisikika,kama upepo alirukia upande wa pili na kuutwaa mkuki wake tayari kwa ajili ya kumkabili adui yake aliyedondoka kutoka juu,kama asingekuwa shapu na mwepesi basi angedondokewa na kitu hicho kichwani.Alimtazama adui yake,hakuamini macho yake.Hakuwa adui wa kumdhuru,bali alikuwa Bata mzinga,mkubwa,aliyenawili na kupendeza.Alikuwa amejeruhiwa sehemu za kwenye mabawa yake,hivyo hakuwa na uwezo wa kuruka.Boka alitazama juu mtini,mahali ambapo Bata yule alitokea.Macho yalimtoka Boka kama mjusi.Nyoka mzuri mwenye rangi za kuvutia alikuwa mtini huku akiuchezesha mkia wake kwa staili ya kutoa ujumbe fulani,laki Boka hakuweza kuelewa chochote kile.Alikuwa bize akitafakari imekuwaje leo hii anakutana na nyoka huyu mara tatu mfululizo tena katika mazingira tofauti tofauti.Mara ya kwanza Boka alimkuta nyoka yule majira ya asubuhi,akiwa juu ya jiwe kandokando ya barabara ya msituni akiota jua.Baada ya Nyoka yule kumuona Boka aliuchezesha mkia kwa staili ile ile na kisha kuingia vichakani kujificha.Mara ya pili Boka alimkuta Nyoka yule akiwa amezungukwa na kundi la simba waliotaka kumjeruhi na kujipatia kitoweo,Boka aliingiwa na moyo wa huruma kutokana na nyoka huyo kuonekana mpole tofauti na nyoka wengine ambao Boka aliwahi kukutana nao.Nyoka yule alikuwa ametulia tuli bila hata kujitetea akisubili kutafunwa na simba,Simba walipojaribu tu kumsogelea basi walikipata cha mtema kuni.Huyu alipigwa mkuki wa shingo,yule akapigwa teke la tumboni,huyu akapigwa kifuti cha mbavu,yani vurugu tupu!.Ndani ya sekunde tano tu,simba wote wane walikuwa wamelala chali kifo cha mende.Nafsi zao zilikuwa zimeacha mwili..
Baada ya Boka kumsaidia Nyoka yule,alianza kumshangaa kuanzia kwenye mkia,alipofika kwenye kiwiliwili,ndipo alipojiridhisha kile alichokifikiria mwanzoni.
“Huyu si ndiye yule nyoka eboo!!,nyali nyali mtima kunde kama ni mkosi ukae mbali na mimi mjukuu wa Boka Mwatogole.Boka alipiga kelele baada ya kushuhudia vichwa vitano vya nyoka yule,alimkumbuka vizuri nyoka huyu,mara ya kwanza alimkuta akiota juu juu ya jiwe alimpuuzia na kuona kama maajabu ya kawaida tu.Lakini sasa halikuwa jambop la kawaida,lilikuwa jambo la kushangaza na kuogopesha.Nyoka yule alichezesha mkia wake,vichwa vyake vikainama na kuinuka chini kama vile Nyoka aina ya Kobra,akainuka na kuinama kisha akaondoka zake kuelekea vichakani.Nyoka yule aliinama na kusujudia kama ishara ya kumshukuru Boka kwa kumnusuru kuliwa na Simba wenye njaa kali.
“Nyali nyali mtima kunde!,eee Mungu wangu,mizimu ya Babu yangu mninusuru na balaa hili”Boka alipiga kelele huku akimtazama nyoka yule juu ya mti,nyoka wa ajabu aliyekutana naye mara ya tatu sasa.Aliamini kabisa nyoka yule ulikuwa ni mkosi kwake,huku roho nyingine ikipingana naye kutokana na matendo ya upole na ukarimu yaliyoonyeshwa nyoka yule.
“Puuuuh!Puuuuu!’Vishindo vingine vilisikika,maua mazuri yenye rangi nyekundu yalidondoshwa na nyoka yule kutoka juu mtini,nyoka yule alikata maua yale kutoka kwenye mti ule kwa kutumia mkia wake.Akauchezesha mkia wake,akainama na kusujudia kisha akaondoka zake na kupanda juu kabisa ya mti,akapotea,Boka aliangaza huku na kule,hakumuona tena.Giza lililosababishwa na jua la machweo lilimfanya akate tamaa ya kuendelea kuangaza mtini,mwanga ulikuwa hafifu sana.
“Ngru ngru ngruuu!”tumbo lake liliunguruma kudai chakula kwa sauti kubwa mithili ya mtu aliyepumua kwa kutumia tundu lililo katikati ya makalio,kumbe sivyo!Njaa ilikuwa imemkaba,tangu asubuhi alikuwa hajatia chochote kile mdomoni.Akageuka nyuma,alimkumbuka yule bata mzinga,bata mzinga alikuwa vile vile,alikuwa amejikunyata kwa huruma.Hakuwa na nguvu za kutoka mahali pale.Boka akatabasamu,alielewa kuwa nyoka yule alitambua tatizo la Boka siku hiyo,alikuwa amewinda siku nzima bila kubahatisha chochote.Bata huyo ilikuwa ni zawadi yake,nyoka yule alilipa fadhira kwa wema aliokuwa ametendewa.Boka alichukua maua yale mazuri,akamchukua na Bata yule kisha akaanza safari ya kurudi kijijini huku mawazo yake yakiwa mbali sana.Alikuwa akimtafakari nyoka yule mwenye akili na vitendo vya ajabu kama binadamu…Nyoka alijua kuomba msamaha,nyoka alijua kulipa fadhira,nyoka asiyeng’ata wala kuonesha ukali wowote kwa adui yake.
“Huyu ni nyoka wa aina gani?”Boka aliwaza,akawazua,hakupata majibu ya kutosheleza maswali yake.
***
JIPATIE HADITHI HII MWANZO MPAKA MWISHO KWA SH 2000 TU,MALIPO YAFANYIKE MPESA 0763338857,HALOPESA 0629905923.JINA HAKIKA BUCHA.
*****
NENDA FACEBOOK KALIKE PAGE YANGU UFURAHIE HADITHI MBALIMBALI,UNACHELEWA NINI?.PAGE YANGU INAFAHAMIKA KWA JINA LA Mwalimu Hakika.
IMG-20191124-WA0000.jpeg
 
Back
Top Bottom