Inaendelea
Kama nilivyotangulia kusema kuwa kwenye hyo nyumba tuliyokua tumehamia walitaka tuhame.Mzee mwenye mji alikua amecharuka vby mno, alikua anadai kuwa Mzee wangu anatembea na mkewe japo me niliona hayanihusu hayo mambo lakin nilijua pengine huyo mzee tuhuma zake zina ukweli ndani yake.Mzee wangu namfahamu tabia zake ko ckua na mashaka na hilo sema utafanyaje sasa.
Kipindi hicho alikua kachukua likizo ya kustaafu ko muda mwingi alikua home mambo mengine nilisimamia me na bro wangu.
Ila mtu kuwa na Nyba yako ni raha yani unaepuka mambo mengi sana.Mngekua mnamuona Mzee wangu wakat huo alikua ni wakuonewa huruma.
Mzee alimaliza likizo ya kustafu akawa kastafu rasmi alisota kiaina.
Muda wa kuhama ulifika ilikua tarh 30 mwez wa nane siku ya alhamis Mzee mwenye nyumba alikuja na mwanae mapema asubui kusimamia show ya kuhama.Me ckuwepo home maana nilikua silali sana home kuna sehem nilkua nalala.
Hapo ikumbukwe mzee wangu alikua hata nyumba hajatafuta ko ilibid aanze kutafuta siku ile ile.Aisee ilikua ni kazi sana, wakat me na mzee tunafuta Nyumba ya kuhamia Bro na madogo wenye walibaki kukusanya vitu ( na tulikua na Vitu vingi


)...Siku hyo tulikosa nyumba ko Mwenye nyumba alisema kesho ijumaa atakuja kufunga mji wake.
Kwa vile huyo mzee alikuja kishari basi nilisema lazima ni mkomeshe kivyovyote vile.Ijumaa ilifika kama zali nyumba zilipatikana mbili Kubwa sana afu geti kali zote,ko tulizikagua tukapenda moja nzuri sana geti kali afu ina vyumba vinne viwili Masters.Gari lilikuja la kubeba vitu na huyo Mzee alikuepo anahakikisha tumehama.
Kama nilivyosema lazima ni mpige tukio huyo mzee chochote chake hata roho itulie kwa ajili ya kumdhalilisha Mzee wangu.
Alikua kakaa kwenye sofa za sebuleni kwetu ( tulikua bado hatuja yatoa nje ) kawaida ya Wazee wakikaa lazima usingizi uwashike.Nilimpa chai na mkate afanye kunywa lakin yule mtoto wake alisema kashiba akatoka nje.
Mzee alikua anasimu yake kaiweka kwenye mfuko wa shati sasa niliikuwa na plan nitaichukuaje ( yaan mpk nilisema eeh...Mungu nisaidie


)...uzur ni kwamba yule Mzee alimaliza kunywa chai akatoka nje kwenye gari lake ( walikua na gari ).
Mchana ilifika Mzee na mwanae nikaona wanaondoka na gari lao nikajua mission failed.Lakin mida ya jioni sasa alirud tena akiwa mwenyewe alikuta gari la mizigo ndo ilinaanza kupakia mizigo.Kipindi anatoka kwenye gar na akufunga mlango wa gari.
Kipindi tunapakia vitu kwenye gari kwenye gar niliona ile simu na ubaya nilikua na jamaa wa gari namsaidia kubeba vitu.
Nilimwambia huyo jamaa ngoja niongee na mzee wangu kwenye simu anipe maelekezo ( Mzee wangu yeye alitangulia na mdogo wangu wa kike kwenye hyo nyumba )...nilitoa simu nikazuga kama napiga.huku namcheki yule mzee.Alikua ndani, nilifungua mlango wa gar chapu nikachukua simu ilikua kiti cha pembeni mwa dereva nikaenda mbali kidogo nikaizima kisha nikarud nikaificha kwenye Sanduku la nguo za Mama angu ( aliacha nguo zake ).kama vile sio mimi nikarud kuendelea na kazi ya kupakia vitu.
Nilipakia lile sanduku kabisa litangulie ili kupoteza ushahidi.Gari lilivyorud round ya mwisho nilipanda nikasepa nikimuona yule mzee anafunga mlango wa nyumba yake hana hata habari.
Tulifika kwenye hayo makazi mapya tukapanga vitu fresh kwa ajili ya kuanza maisha mapya.nilichukua kale ka simu nikatoa laini nikazichoma moto,Simu mpk leo ipo sema haitamaniki.
Kesho yake ndo sikuamin macho yangu ilikua zamu yangu kuumia na mimi.
Nilipigiwa simu na yule jamaa wa Ps akanambia kuwa Ps,Tv,pad na viti vimeibiwa...Roho iliniuma sana nikaenda kushuhudia tukio nilikuta ni kweli.
Nilicheka kicheko cha uchungu.tukaenda police kutoa taarifa.Nilishawai kuleta thread humu ya hili tukio.Kuna masai mmoja nae jamaa alimleta eti ana dawa ya kuwakamata wezi "* hii dawa ukitumia siku tatuu mwisi analeta vitu mwenyewe*"...hayo ni maneno ya huyo masai.
Nilimpa 5k maana ndo alisema hyo dawa ndo bei yake.Huyo masai alikua ni mlinzi wa Complex, siku tatu ziliisha nikaona mwizi ajaja nilimfuata Yero anipe hela yangu.Alidai hana hela nilimpiga ngumi moja jinsi alivyoanguka mpk nikaamua nimuachie hyo hela tu.
Niliamua tu nipoteze hilo tukio maana nilijua pengine Mungu kanipa onyo.Uzur ni kwamba nilikua na Xbox

home ko nilikua najipanga upya nianze tena hyo biashara.
Nitarejea tena.