Mbeky
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 672
- 520
Story kufuruuu!
Kwa lugha nyingine tunasema story kuntu
Story kufuruuu!
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-24-
ILIPOISHIA JANA :
Alifungua na kuingia ndani ambako ilikuwa ofisi imejaa vumbi na uchafu kutokana na kutofanyiwa usafi.
SASA ENDELEA
Alijiuliza Sara amepatwa na nini mpaka muda ule hajafika ofisini, aliingia ofisini na kuweka vitu vyake kisha alitoa simu na kumpigia, simu iliyopokelewa na mwanamke upande wa pili.
Haloo.
Haloo, nazungumza na nani?
Maria.
Sara yupo wapi?
Alitoka jana kufuata chakula lakini ajabu mpaka kunakucha hatujamuona.
Sasa kaenda wapi?
Hata sisi tunashangaa kibaya hata simu hakuchukua.
Mmh! Sawa.
Mustafa alikata simu na kujikuta akichoka na kukaa kwenye kochi lake huku akijawa na mawazo ya kujiuliza Sara atakuwa amekwenda wapi. Akiwa katikati ya mawazo alisikia mlango wa ofisi ukigongwa alijua Sara ndiyo anafika.
Ingia, alisema kwa sauti.
Mlango ulifunguliwa na kutanguliwa na harufu nzuri ya manukato aliyoyazoea ya Shehna, mara aliingia shehna katika vazi la gauni refu la kitambaa cha kitenge na kiremba chake alionekana mwanamke mzuri kuliko siku zilizopita.
Mustafa kuzungumza alishindwa alibaki kamtumbulia macho kama siku yake ya kwanza kumuona.
Mustafa kushangaa gani huko kama ndiyo leo siku yako ya kwanza kuniona? alimuuliza huku akimsogelea alipokuwa amekaa.
Shehna lazima nimsifu Mungu kwa utundu aliofanya kukuumba, Shehna wewe ni mwanamke mzuri wa wazuri, uzuri wako kama nyoka anayejibadili mwili wake, kila siku uzuri wako unaongezeka, wa leo unashinda wa jana pia naamini wa kesho utauzidi wa leo.
Mmh! Kawaida sema bado hutatuliza macho kwangu unaniangalia kwa wasiwasi, kama ungekuwa hunitazami kwa wasiwasi wala usingenishangaa. Nilichokibadili asubuhi hii ni nguo tu, mimi ni yuleyule wa jana wa leo na kesho vilevile.
Wewe unaweza kusema hivyo, najuta kuchelewa kukujua mapema.
Ulinifahamu mapema lakini hukunitilia maanani, nilikuja kwako kila wakati lakini labda uliniona mwanamke malaya.
Ha..ha..pana, sijakufikiria hivyo!
Sasa tatizo lako nini?
Nina wasiwasi wenye fedha zaidi yangu wataninyanganya.
Kwani nipo wapi siku zote wasikunyanganye wakunyanganye leo? Shehna alimuuliza huku akimuangalia jicho tata lililozidi kumchanganya Mustafa na kutamani heri angekuwa mkewe wa ndoa. Lakini bado aliona maisha ya Shehna asingeyaweza kwani kila alipokutana naye alikuwa na nguo na vito vya thamani ambavyo aliamini hawezi kuvinunua.
Shehna aligundua alichokuwa akikiwaza Mustafa baada ya kukaa kimya kwa muda. Alimshtua kwa kumwita jina lake.
Mustafa.
Naam.
Kwa nini unajibebesha mawazo mazito ambayo sivyo unavyonifikiria?
Umejuaje?
Si kujuaje, bali nataka kukuthibitishia maisha yangu na wewe ni tofauti unavyonifikiria, kila kitu juu ya mustakabali wetu niachie mimi.
Sawa nimekuelewa.
Na..na mbona ofisi chafu?
Nashangaa mpaka muda huu msaidizi wangu sijamuona, ha..halafu nasikia toka jana usiku hajarudi.
Kauli ile ilimfanya Shehna acheke kicheko cha umbea kilichomfanya Mustafa ashtuke na kuhoji.
Vipi mbona unacheka kama unajua kinachoendelea.
Walaa, nimecheka tu.
Yaani hapa nimechanganyikiwa ngoja nimwite mlinzi ufanye usafi.
Walaa, kazi hiyo nitaifanya miye.
Hapana Shehna, acha ataifanya mlinzi.
Kwani mimi kufanya kuna nini?
Utajichafua bure wakati watu wa kuifanya kazi hii wapo.
Basi leo nitaifanya mimi, naomba unipishe mara moja.
Sawa, basi nipo nje kwa mlinzi.
Hakuna tatizo.
Mustafa alitoka nje na kumuacha Shehna ofisini, kabla ya kufanya kitu aliangua kicheko cha mfululizo kufurahia alichomfanyia Sara mwanamke aliyemuona asidi aliyetaka kushindana naye. Kisha alijishika kwenye paji la uso na kutulia kwa muda, mara vijakazi na watwana toka ujinini walipiga magoti mbele yake na kumuuliza.
Mwana wa Mfalme wa jini la bahari ya dhahabu una shida gani unayotaka tukufanyie?
Nataka baada ya muda mfupi ofisi yote uwe safi kuliko siku zote.
Hewala mwana wa mfalme.
Vijakazi na watwana waliingia katika kazi ya usafi iliyochukua dakika tano kila kitu kilikuwa safi ndani. Kilibadilishwa kila kitu na kuwekwa pazia nzuri la halili na kuifanya ofisi ipendeze mara dufu. Baada ya kufanya usafi walipiga magoti mbele ya Shehna na kusema....
Itaendelea siku ya kesho wakati kama huu.....
Habari yako ndugu? Stori na Hadithi zangu Pitia hapa bonyeza Nusu siku ndani ya jeneza
Hadithi ya kusisimuwa: Mimba ya jini
Jini wa daraja la Salendar...
Utajiri wa damu
Godoro La Mtumba
Majangaaa Mbona Majangaaa!
Wakala wa Shetani
SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini...
Macho ya Bundi
Mama yangu adui yangu
Mkuu.@mcmalck
hili zal noma!
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-25-
ILIPOISHIAJANA :
Vijakazi na watwana waliingia katika kazi ya usafi iliyochukua dakika tano kila kitu kilikuwa safi ndani. Kilibadilishwa kila kitu na kuwekwa pazia nzuri la halili na kuifanya ofisi ipendeze mara dufu. Baada ya kufanya usafi walipiga magoti mbele ya Shehna na kusema.
SASA ENDELEA
Mtukufu mwana wa Mfalme wa jini la bahari ya dhahabu tumemaliza kazi, kama kuna kasoro tupo tayari kwa adhabu yoyote kutoka kwako.
Hapana nawamini.
Asante mwana wa mfalme.
Shehna hakuwa na shida ya kukagua kwa kuamini majini walikuwa wakijua usafi kuliko mwanadamu.
Nimefurahi kwa yenu nzuri, mnaweza kuondoka.
Kufumba na kufumbua vijakazi na watwana walitoweka na kumuacha Shehna alifurahia hali nzuri ya kupendeza ya ofisi. Alitoka nje na kumwita Mustafa aliyekuwa akizungumza na mlinzi. Alikwenda ndani na kuishangaa ofisi ilivyopendeza tofauti na siku zote.
Duh! Kazi hii imeifanya peke yako?
Umemuona nani akinisaidia?
Hongera sana.
Asante, ila kama Sara hatatokea na kesho funguo iache mlangoni, nitakuwa nawahi mapema kufanya usafi kabla hujafika mpaka atakaporudi kazini .
Nitafanya hivyo.
Mustafa mimi si mkaaji ilikuja kukushukuru wa mapenzi yako matamu, hakika leo nimefaidi usichana wangu kwa kupata penzi lililokamilika. Nakuahidi baada ya kushika ujauzito nitakupatia zawadi kubwa sana.
Wala usihofu, lakini nina wasiwasi wa kuharibu masharti yako.
Wala usiwe na wasiwasi, asubuhi umenilaisishia kufanya mambo yetu bila mkeo kukusumbua. La muhimu kufanya yote kama niliyokuelekeza.
Nitafanya hivyo.
Basi nikuache uendelee na kazi.
Nashukuru.
Walikumbatiana kisha Shehna aliondoka na kumuacha Mustafa alimsindiza kwa macho.
***
Wiki nzima ilikatika bila kuonekana kwa Sara huku Shehna akiendelea kufanya usafi kila siku na kuifanya ofisi izidi kupendeza. Kwa hali ile ilifikia hatua ya Mustafa kuomba Sara isirudi tena kutokana na usafi uliokuwa ukifanywa na Shehna uliifanya ofisi yake isifikiwe kwa kila aliyeingia na kutaka kupatiwa mtu mwenye uwezo wa kufanya usafi kama wa ofisini kwake.
Wakati wote huo kila siku Shehna alikwenda nyumbani kwa Mustafa na kufanya naye mapenzi kitandani kwake huku mkewe akiwa amepitiwa usingizi. Siku zote alifuata masharti aliyopewa kuyafanya kabla ya kulala. Zoezi kubwa kwake lilikuwa kumpaka mafuta mkewe ambayo humfanya alale mpaka asubuhi bila kugeuka na kuacha wafanye mambo yao bila yeye kujua kinachoendelea.
Mustafa alifanya vitu vyake siku zote kwa umakini mkubwa kwa vile mkewe hakuweza kukutana naye tena kimwili baada ya kuelezwa na Shehna ili aweze kupata mtoto huku akiendelea kutumia dawa alizopewa. Hata kulala sehemu ya ukutani hakulazimishwa kwa vile lilikuwa moja ya masharti ya dawa.
Siku zote alifanya kama alivyoelekezwa, lakini siku moja alirudi nyumbani akiwa amechoka sana na kusahau kumpaka mafuta mkewe kwa kuamini aliisha mpaka. Usiku kama kawaida Shehna aliingia ndani na kunyanyua Mustafa na kwenda naye bafuni kuoga baada ya kuoga alirudi kitandani na kuanza kuandaana kisha waliingia kwenye tendo.
Hatua ya awali iliisha kila mmoja alifurahia penzi la mwenzake kisha walipumzika kwa muda ili kujiandaa kwa hatua nyingine. Shehna kama kawaida alimpa Mustafa maji ya kunywa yaliyomrudishia nguvu na kurudi tena bafuni kuoga na kuingia hatua ya pili. Mapenzi yalipopamba moto Shehna aligugumia kimapenzi kwa kuusifia uwezo wa Mustafa kimapenzi.
Kwa vile mke wa Mustafa hakupakwa mafuta ya kumlaza, sauti ya kulalamika kimapenzi ilimshtuka usingizini.
Itaendelea Kesho Wakati kama huu
Hadithi yako hinahu binafsi. Kwa nn washiliki wote ni waislam hina mahana sie ndio tuna majini na tunapenda zinaa hacha ukafiri wataje makafiri wezio .pili hakuna jini hayependa zinaa huyo hatakuwa jini kafiri kama ww
Huyo nijini kafiri kama ww hakuna jini hanayependa zina na kama jini mbona hamesahau kumwambia mustafa mbona hujampaka mkeo mafuta kingine hunatuzallilisha SS waislam. Hinamahana sie tunapenda sana majini na zinaa. majina yako mengi John, Sam, Daniel,jack ,rose nk ya makafiri .chonde chonde husipende kutumia majina ya upande mmoja katka hadithi zako za kijinga
Hadithi yako hinahu binafsi. Kwa nn washiliki wote ni waislam hina mahana sie ndio tuna majini na tunapenda zinaa hacha ukafiri wataje makafiri wezio .pili hakuna jini hayependa zinaa huyo hatakuwa jini kafiri kama ww
Huyo nijini kafiri kama ww hakuna jini hanayependa zina na kama jini mbona hamesahau kumwambia mustafa mbona hujampaka mkeo mafuta kingine hunatuzallilisha SS waislam. Hinamahana sie tunapenda sana majini na zinaa. majina yako mengi John, Sam, Daniel,jack ,rose nk ya makafiri .chonde chonde husipende kutumia majina ya upande mmoja katka hadithi zako za kijinga