Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

ya daraja la salenda niliikuta kwenye wall ya post mbali mbali kama ujuavyo mtu akisoma post hata ya miaka miwili nyuma aka like au ku comment lazima ule uzi utaonekana upya but nataka kujua jinsi ya kusoma post individual user ili niweze kutafuta hadithi ambazo zimeshaisha nizisome nikisubiria hii ifike mwisho
 
hizi hadithi ni za global publisher au za shigongo maana kama umsomaji wa magazeti pendwa kama risasi utazikuta zinaendelea juma kwa juma mzizi anazitoa kwenye hizo link kama tungekua tunazijua hizo link nirahisi kuzifuatilia but mimi sizijui hizo link so nafuatilia kwa mzizimkavu lkn pia mzizi hajaanza leo kuzitupia humu so kuna hadithi nyingi alishawahi zitupia nataka kujua jinsi ya kuingia kwenye wall ya mzizi na kuanza kusoma post zake naamini nita zikuta nyingi zilizo kwisha kufika mwisho hope umenielewa japo kiduchu

tafuta thread imeandikwa 'story za mzizimkavu'
 
ya daraja la salenda niliikuta kwenye wall ya post mbali mbali kama ujuavyo mtu akisoma post hata ya miaka miwili nyuma aka like au ku comment lazima ule uzi utaonekana upya but nataka kujua jinsi ya kusoma post individual user ili niweze kutafuta hadithi ambazo zimeshaisha nizisome nikisubiria hii ifike mwisho

waoh nimeshaziona tayari duuuuh zipo nyingiiiii mpaka sijui pa kuanzia kusoma
Habari yako ndugu? Pitia hapa bonyeza Nusu siku ndani ya jeneza

Hadithi ya kusisimuwa: Mimba ya jini

Jini wa daraja la Salendar...

Utajiri wa damu

Godoro La Mtumba

Majangaaa Mbona Majangaaa!

Wakala wa Shetani

SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini...

Macho ya Bundi

Mama yangu adui yangu
 
Hadithi ya kusisimuwa: Mimba ya jini-34-

ILIPOISHIA:
“Sara umefika salama?” sauti haikuwa ngeni lakini hakuwa na uhakika nayo ilibidi aulize.
“Nani?”
“Mi shogayo Shehna.”
“Aah! Dada nimefika salama.”
“Ile hali haijatokea?”
“Ndi..ndiyo.”
“Mbona kama una wasiwasi?”
“Ni kweli kuna sauti naisika kwa mara ya pili lakini siielewi.”
“Inasemaje?”
SASA ENDELEA...


“Inasema niache kufuatilia mambo yasiyonihusu la sivyo nitageuzwa nguruwe kabisa.”

“Kwani unafuatilia nini?” Shehna alijifanya kuuliza.
Swali lile lilikuwa gumu kwa vile asingeweza kumueleza anamfuatilia yeye, alibidi adanganye kwa kusema:
“Dada wee nimfuatilie nani?”
“Haiwezekani sauti hiyo kutokea mara ya pili, kama kuna kitu unakifuatilia achana nacho kwa vile kila kitu cha ajabu kikikutokea kina sababu.”
“Nimekusikia dada yangu.”
“Hebu acha kufuatilia hicho ulichotaka kukifuatilia tuone nini kitatokea.”
“Sawa dada.”
“Basi mdogo wangu oga kisha kunywa maji ya baridi ulale.”
“Nitafanya hivyo dada.”
Sara alikwenda kuoga kisha alikunywa maji ya baridi na kujikuta akipitiwa na usingizi mzito.
***
Sara aliamka siku ya pili bila kutokewa na mauzauza yoyote, alikwenda hadi kazini kama kawaida na kukuta ofisi haijafanyiwa usafi. Aliingia katika kazi ya kufanya usafi kama kawaida yake na kusubiri muda wa bosi wake kufika. Baada ya muda Mustafa aliwasilili na kupokewa na Sara.
Kama kawaida alichukua vitu vya bosi na kwenda kuviweka ofisini, Mustafa alipoingia ofisini alishangaa kukuta ofisi chafu. Hata hali ya hewa haikuwa kama ile aliyoizoea wakati wa Shehna akifanya usafi. Alitoka hadi kwa Sara na kumuita.
“Sara njoo mara moja.”
Sara alinyanyuka na kwenda kwa bosi wake kumsikiliza alijua anaitiwa kazi ya siku ile. Alipofika alikutana na swali lililomshtua.
“Sara kazi imekushinda?”
“Kwa nini bosi?”
“Mbona ofisi inanuka kama zizi la ng’ombe.”
“Bosi mbona mi sisikii harufu yoyote mbaya?”
“Ina maana husikii harufu mbaya ya ofisi?”
“Bosi kipi kimeongozeka, nimefagia na kufuta kama siku zote sasa hiyo harufu kama zizi imetoka wapi?”
“Sara kazi imekushinda heri usingerudi ofisi yangu ikaendelea kusafishwa na Shehna, unakuwa kama upo bustanini lakini kurudi kwako hakuna ulichokifanya zaidi ya kuongeza uchafu.”
“Bosi mbona sikuelewi hiyo harufu kama beberu ipo wapi?”
Ghafla ndani ya ofisi ilisikia harufu nzuri ya manukato aliyoizoea, alimwambia Sara aondoke.
“Sara kaendelee na kazi.”
“Asante bosi.”
Sara alitoka na kwenda kuendelea na kazi, wakati akifanya kazi alijikuta mtu mwenye mawazo mengi juu ya tukio la muda mfupi uliopita la bosi wake kumgeuka kuwa hajafanya usafi na kusema ofisi inanuka kama zizi. Kilichomshangaza kingine kilikuwa harufu nzuri ya manukato iliyoingia ghafla ofisini ambayo hakujua yametoka wapi.
Hakutaka kusema kitu aliendelea na kazi na kupanga akitoka kazini jioni lazima aende kwa mganga wake ili amuangalizie kinachomtokea ni nini kwa vile haikuwa hali ya kawaida kwa mtukio yote.
Wakati akiwaza vile alishtuliwa na sauti ya Shehna.
“Shoga za kazi?”
“Ooh! Dada karibu,” alisema huku akionesha kushtuka.
Shehna alikuwa amevaa dela zuri lililonakshiwa na nyuzi za hariri, alikuwa amenawiri na kupendeza alionekana mwanamke mrembo zaidi ya siku zote.
“Asante.”
“Da Shehna hongera umependeza sana.”
“Nashukuru.”
“Karibu dada a’ngu.”


Itaendelea Jumamosi ijayo......
 
Hadithi ya kusisimuwa: Mimba ya jini-35-

ILIPOISHIA:
Shehna alikuwa amevaa dela zuri lililonakshiwa na nyuzi za hariri, alikuwa amenawiri na kupendeza, alionekana mwanamke mrembo zaidi ya siku zote.
"Asante."

"Da Shehna hongera umependeza sana."
"Nashukuru."
"Karibu dada a'ngu."
SASA ENDELEA...



"Nimekaribia, vipi umeamkaje?"
"Namshukuru Mungu leo nimeamka salama."
"Vipi ile hali ilitokea tena?"
"Kwa kweli mpaka nakuja kazini nashukuru hali ile wala sauti haijanitokea tena."
"Kama nilivyokueleza, zingatia uliyoambiwa na ile sauti yana sababu, utashangaa mambo yako yatakwenda vizuri."

"Asante dada kwa msaada wako pia nitazingatia ushauri wako."
"Vipi bosi yupo?"
"Yupo pita."
"Hapana muulize kwanza."
Sara alinyanyua simu na kumpigia Mustafa aliyemwambia amruhusu aingie.
"Dada pita."

"Asante."
Shehna aliingia ndani ya ofisi alikutanisha macho na Mustafa aliyekuwa akiangalia mlangoni.
"Wawooo mpenzi."
Mustafa alijikuta akitoka kwenye kiti chake na kwenda kumpokea kwa kumkumbatia kisha alimchumu.
"Asante mpenzi," Shehna alishukuru baada ya kubusiwa kwenye shavu.

Waliachana kwa kila mmoja kukaa sehemu yake, Shehna alionekana mwenye furaha usoni mwake tofauti na siku zote. Alimuangalia Mustafa usoni alitaka kusema neno lakini aliishia kutabasamu na kufanya uzuri wake uongezeke.
"Vipi mpenzi?" Mustafa alimuuliza huku naye akijenga tabasamu mwanana lililokuwa likimpa uhuru Shehna kuzungumza.

"Mmh! Mustafa nashukuru sana."
"Kwa kipi?"
‘Kwa vyote, lakini kimoja ndicho nimefurahi sana tena sana sipati kusema."
"Vipi hivyo na kipi kimekufurahisha sana?"
"Nikwambie?" Shehna alimuuliza Mustafa huku akimtazama kwa jicho la aibu.

"Niambie mpenzi," alitoa tabasamu la kumruhusu aseme kilichokuwa moyoni mwake.
"Kwanza nashukuru kwa kunipa nafasi moyoni mwako, pili kunivumilia kwa usumbufu wangu, tatu kunipa penzi ambalo sijawahi kupata katika maisha yangu yote na kubwa zaidi nimekuja kukueleza sasa hivi mimi ni mjamzito."
"Wewe!" Mustafa alishtuka.

"Kweli kabisa, unakumbuka jana ilikuwa siku ya ngapi mimi kulala kwako?"
"Mmh! Hata sikumbuki."
"Muone!" Shehna alisema huku akimshika kidevu Mustafa.
"Jana mpenzi ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kukutana kimwili, mpaka juzi bado sikuona mabadiliko. Nilichanganyikiwa mtoto wa kike, lakini penzi ulilonipa jana lilikuwa tamu ajabu kidogo nife kwa raha kumbe watoto walikuwa wanaingia."

"Kweli?"
"Kweli kabisa nami si muda mrefu nitaitwa mama."
"Hongera!" Mustafa alisema huku akizunguka meza na kumkumbatia.
"Hongera wewe kunipatia nilichokitafuta kwa muda mrefu."
"Basi tuongere wote."

"Mustafa mpenzi, kuanzia leo hatutaonana mchana kwa vile sipendi kutembea na tumbo."
"Mbona bado sana?"
"Siwezi kutembea, familia yetu ikibeba ujauzito husumbuka sana."
"Sawa mpenzi, lakini nyumbani si utakuja?"
"Hapana ila nitawatuma watu wakufuate usiku siku mojamoja na alfajiri watakurudisha."
"Hakuna tatizo."

"Ila mpenzi kwa mwezi mzima hatutaonana nakwenda nyumbani mara moja kufanya mambo ya kimila baada ya kupata ujauzito."
"Mmh! Mpenzi nitateseka, nimekuzoea sana."

"Usiwe na wasiwasi nitakuwa nawe karibu muda wote."
"Tutakuwa pamoja kivipi wakati hautakuwepo kwa mwezi mzima?"
"Kila siku nitakuwa katika ndoto zako na ukiamka wala hutakuwa na majonzi, usiku utakuwa kama mchana tena upo na mimi."



Itaendelea leo usiku.
 
Hadithi ya kusisimuwa: Mimba ya jini-35-

ILIPOISHIA:
Shehna alikuwa amevaa dela zuri lililonakshiwa na nyuzi za hariri, alikuwa amenawiri na kupendeza, alionekana mwanamke mrembo zaidi ya siku zote.
“Asante.”

“Da Shehna hongera umependeza sana.”
“Nashukuru.”
“Karibu dada a’ngu.”
SASA ENDELEA...



“Nimekaribia, vipi umeamkaje?”
“Namshukuru Mungu leo nimeamka salama.”
“Vipi ile hali ilitokea tena?”
“Kwa kweli mpaka nakuja kazini nashukuru hali ile wala sauti haijanitokea tena.”
“Kama nilivyokueleza, zingatia uliyoambiwa na ile sauti yana sababu, utashangaa mambo yako yatakwenda vizuri.”

“Asante dada kwa msaada wako pia nitazingatia ushauri wako.”
“Vipi bosi yupo?”
“Yupo pita.”
“Hapana muulize kwanza.”
Sara alinyanyua simu na kumpigia Mustafa aliyemwambia amruhusu aingie.
“Dada pita.”

“Asante.”
Shehna aliingia ndani ya ofisi alikutanisha macho na Mustafa aliyekuwa akiangalia mlangoni.
“Wawooo mpenzi.”
Mustafa alijikuta akitoka kwenye kiti chake na kwenda kumpokea kwa kumkumbatia kisha alimchumu.
“Asante mpenzi,” Shehna alishukuru baada ya kubusiwa kwenye shavu.

Waliachana kwa kila mmoja kukaa sehemu yake, Shehna alionekana mwenye furaha usoni mwake tofauti na siku zote. Alimuangalia Mustafa usoni alitaka kusema neno lakini aliishia kutabasamu na kufanya uzuri wake uongezeke.
“Vipi mpenzi?” Mustafa alimuuliza huku naye akijenga tabasamu mwanana lililokuwa likimpa uhuru Shehna kuzungumza.

“Mmh! Mustafa nashukuru sana.”
“Kwa kipi?”
‘Kwa vyote, lakini kimoja ndicho nimefurahi sana tena sana sipati kusema.”
“Vipi hivyo na kipi kimekufurahisha sana?”
“Nikwambie?” Shehna alimuuliza Mustafa huku akimtazama kwa jicho la aibu.

“Niambie mpenzi,” alitoa tabasamu la kumruhusu aseme kilichokuwa moyoni mwake.
“Kwanza nashukuru kwa kunipa nafasi moyoni mwako, pili kunivumilia kwa usumbufu wangu, tatu kunipa penzi ambalo sijawahi kupata katika maisha yangu yote na kubwa zaidi nimekuja kukueleza sasa hivi mimi ni mjamzito.”
“Wewe!” Mustafa alishtuka.

“Kweli kabisa, unakumbuka jana ilikuwa siku ya ngapi mimi kulala kwako?”
“Mmh! Hata sikumbuki.”
“Muone!” Shehna alisema huku akimshika kidevu Mustafa.
“Jana mpenzi ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kukutana kimwili, mpaka juzi bado sikuona mabadiliko. Nilichanganyikiwa mtoto wa kike, lakini penzi ulilonipa jana lilikuwa tamu ajabu kidogo nife kwa raha kumbe watoto walikuwa wanaingia.”

“Kweli?”
“Kweli kabisa nami si muda mrefu nitaitwa mama.”
“Hongera!” Mustafa alisema huku akizunguka meza na kumkumbatia.
“Hongera wewe kunipatia nilichokitafuta kwa muda mrefu.”
“Basi tuongere wote.”

“Mustafa mpenzi, kuanzia leo hatutaonana mchana kwa vile sipendi kutembea na tumbo.”
“Mbona bado sana?”
“Siwezi kutembea, familia yetu ikibeba ujauzito husumbuka sana.”
“Sawa mpenzi, lakini nyumbani si utakuja?”
“Hapana ila nitawatuma watu wakufuate usiku siku mojamoja na alfajiri watakurudisha.”
“Hakuna tatizo.”

“Ila mpenzi kwa mwezi mzima hatutaonana nakwenda nyumbani mara moja kufanya mambo ya kimila baada ya kupata ujauzito.”
“Mmh! Mpenzi nitateseka, nimekuzoea sana.”

“Usiwe na wasiwasi nitakuwa nawe karibu muda wote.”
“Tutakuwa pamoja kivipi wakati hautakuwepo kwa mwezi mzima?”
“Kila siku nitakuwa katika ndoto zako na ukiamka wala hutakuwa na majonzi, usiku utakuwa kama mchana tena upo na mimi.”



Itaendelea leo usiku.

lete stor MZIZI MKAVU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom