Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-30-

ILIPOISHIA:
"Zile sauti za kutisha zilizidi kunisogelea nikaona kama nitazubaa basi nitakufa. Nilijilazimisha kukimbia huku nimeshika mkono kwenye mbavu. Nilikwenda hivyo kwa kuchechemea mpaka nilipotokea kwenye mti mkubwa.
SASA ENDELEA...


"Kwa vile nilikuwa nimechoka sana, nilijiegemeza kwenye mti mkubwa pembeni ya barabara, pamoja na alfajiri ile kuwa na baridi kali lakini usingizi ulinichukua.
"Mpaka nilipoamshwa na wanakijiji, sikuamini waliponiambia pale ni Kongwa Dodoma na muda ule ni saa nane mchana, kingine kilichonishangaza kuelezwa siku ile ni Jumapili wakati niliondoka nyumbani Jumatatu.

"Yani bado siamini kutembea kwa mguu kwa wiki nzima, kibaya zaidi nakumbuka nilitembea usiku mmoja lakini imeonekana nilitembea wiki nzima. Kama nilitembea wiki nzima, mbona sikuuona mchana zaidi ya usiku tu?" Sara alihoji huku machozi ya uchungu yakimtoka.
"Dada hiki ni kituko yani lazima uende kanisani ukaombewe, lazima watakuwa ni wachawi tu walikuchukua."

"Na..na..kwe...," Sara alisita kuzungumza baada ya kumuona nguruwe amekaa kwenye kiti alichokaa Happy, alipiga kelele za uoga.
"Mamaa nakufa nguruwe."
"Sara nguruwe yupo wapi?" Happy alimshangaa rafiki yake.
"Si..si...," alituliza macho na kushangaa kumuona aliyekaa mbele yake ni Happy na si nguruwe kama alivyoona..

"Sara upo sawa?" Happy aliamini rafiki yake hayupo sawa.
"Ni..ni..hapana..hapana," Sara alituliza macho yake baada ya kumuona tena nguruwe kwenye kochi hakupiga kelele, alitulia na kufikicha macho ili kupata uhakika kama kweli kilichopo mbele yake ni nguruwe au anaona maruweruwe. Baada ya macho kutulia alimuona tena shoga yake Happy wala si nguruwe.
"Happy naomba nipumzike, siko vizuri sijielewi kabisa."

"Sawa dada lakini kwanza nenda ukaoge ili kuufanya mwili upumue."
"Sawa," Sara alisema huku akivua nguo alizokuja nazo na kuchukua taulo ili aende bafuni.
Alichukua sabuni na mswaki kisha alitoka nje na kumuacha shoga yake akimfanya usafi wa chumba. Sara alielekea nje alipofika mlangoni alisita kutoka baada ya kuona nguruwe wamejaa uani. Alizidi kushangaa na kumwita Happy kwa sauti.
"Happy njoo."
Happy aliacha kufanya usafi na kusogea mlangoni.
‘Vipi?"
"Eti nje unaona nini?"
"Kawaida, kwani umeona nini?"
"Nguruwe."
"Nguruwe?" Happy alishtuka.

"Hebu ngoja," Sara alisema huku akipekecha macho na kuona wapo wapangaji wenzake na si nguruwe.
"Mmh! Mbona mwaka huu wangu."
"Shoga kuna umuhimu twende kanisani ukaombewe."
"Ngoja nikaoge."
Sara alikwenda hadi bafuni na kuoga kisha alirudi ndani bila hali ile kumtokea tena. Kwa vile alikuwa amechoka sana, alipanda kitandani na usingizi mzito ulimchukua.
****
Siku ya pili Sara alidamka mapema na kuoga kisha alitoka kwenda kazini kwa kumuaga shoga yake Happy. Happy alimuuliza alivyolala.
"Vipi umelala salama?"
"Namshukuru Mungu nimelala salama, wacha niwahi kazini japo sijui bosi wangu kama atanielewa."
"Atakuelewa tu kwani kilichotokea si cha kawaida."
"Mmh! Ngoja niwahi."
"Mi nilikuwa na wazo."
"Wazo gani?"
"Nilikuwa na wazo la kwenda kwanza kanisani ukaombewe pepo mchafu."
"Wazo zuri lakini lazima nifike kwanza ofisini nijue hatima yangu ndipo twende huko kanisani."
"Basi ukirudi jioni tutapanga."
"Sawa."
Sara aliagana na shoga yake na kuwahi kazini kama kawaida kwa kuwahi ili afanye usafi kabla bosi wake hajafika.


Je, nini kitatokea? Kesho wakati kama huu itaendelea....
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-29-

ILIPOISHIA:
Pamoja na kuamini alikuwa ndani ya basi, bado hakuamini kama tukio lililomtokea lilikuwa la kweli. Kwake aliamini ile ni ndoto iliyomchanganya na akiamka asubuhi atajikuta yupo kitandani amelala. Basi liliwasili jijini Dar majira ya saa sita na nusu mchana, bado Sara hakuamini ndipo aliteremka.
SASA ENDELEA...


Baada ya kuteremka aliangalia pesa yake ya nauli aliyokuwa amefunga kwenye khanga chakavu.
Alifungua na kuikuta elfu moja iliyochafuka kwa udongo wa kijijini, chini alikuwa amevaa ndala rangi mbili moja nyekundu na nyingine bluu. Nywele zake zilikuwa timutimu.

Sara alionekana kweli mwana kijiji kutokana na jinsi alivyokuwa, muda wote hakujiona kwani kama angejijua alivyo asingeweza hata kutembea kutokana na jinsi anavyojipenda. Hata alipotaka kupanda daladala konda alimuona wa kuja na kumsemesha maneno ya kejeri.
Sara hakujali aliingia ndani ya daladala hadi Kinondoni Kanisani anapokaa. Baada ya daladala kusimama aliteremka na kuelekea kwake. Alipokaribia alishangaa kuona mlango wa chumba chake ukiwa wazi. Shoga yake Happy aliyekuwa amekaa nje alikuwa wa kwanza kumuona na kushtuka kufuatia rafiki yake huyo kuwa katika mavazi ya ajabu, gauni lililochanika mabegani khanga iliyopauka na kandambili rangi mbili.
“Sara!” Happy alimwita kwa sauti ya juu.
Sauti ile ilikuwa kama kitu kilichomzindua toka usingizini na kujikuta naye akijishangaa.
“Shoga ulikuwa wapi? Jamani mbona umevaa nguo za ajabu?”
Kauli ile ilimfanya ajichunguze na kujikuta akijishangaa mavazi aliyovaa na kujikuta akiangua kilio huku akisema.

“Mungu wangu! Kumbe kweli nilidhani ndoto.”
“Kumbe kweli nini jamani?” Happy alitaka kujua.
Sara hakusema kitu alikimbilia ndani na kujitupa kitandani na kuanza kulia kilio cha sauti na kuwafanya majirani wakusanyike nje ya chumba chake. Happy ndiye aliyeingia ndani kutaka kujua shoga yake alikumbana na nini, kitu kilichofanya atoweke nyumbani kwa wiki nzima na kurudi akiwa kama mwana kijiji.

“Sara umepatwa na nini?” Happy alitaka kujua.
“Mmh! Hata simamini nitembee usiku kucha mchana kutwa kwa siku sita bila kupumzika mpaka Dodoma?”
“Dodoma?” Happy alishtuka.

“Ndiyo dada hata siamini hizi nguo nimepewa na wasamaria wema wa Kongwa walioniokota nikiwa nimelala barabarani.”
“Wewee!” Sara alishtuka.
“Yaani kama nisingepanda Hiace toka Kongwa kisha basi la Shabiby ningebisha na tiketi yake ni hii,” Sara alimuonesha Happy tiketi ya basi ambayo ilionesha ilikuwa ya siku ile.

Baada ya Sara kuisoma akili yake bado haikuamini shoga yake kwenda Dodoma kwa miguu aliona kama mchezo wa kuingiza.
“Sara, siku ile si ulisema unakwenda kununua nyama ya nguruwe na ndizi?”
“Ndiyo shoga yangu, nimetoka vizuri mpaka karibu kwa Macha Kitimoto. Ghafla nilijishangaa kujikuta katikati ya pori hata sijui ni pori gani.”

“Wewee!” Happy alizidi kushtuka.
“Yaani niliogopa mpaka haja ndogo ikanitoka, kibaya zaidi nyuma yangu kulikuwa na milio ya ajabu ya kutisha na kunifanya nikimbie kwenda mbele japosikujua ni wapi nilipokuwa nakimbilia. Kila nilivyokuwa nikikimbia ndivyo sauti za kutisha zilivyokuwa zikinisogelea na kunifanya nizidi kukimbia.

“Nakumbuka upande wa khanga wa juu ulinidondoka lakini sikuujali zaidi ya kuyaokoa maisha yangu ambayo niliyaona yapo hatarini. Kandambili nilizokuwa nimevaa zilinidondoka na kujikuta nakimbia pekupeku huku nikikatiza kwenye vichaka na kukanyaga miba.
“Kutokana na kutokewa na vitu vile vya kutisha ambavyo sikudhania kukutana navyo hata siku moja, nilijua ile ni ndoto tu wala si kweli. Baada ya kukimbia kwa muda mrefu bila kupumzika, nilianza kusikia vichomi kwenye mbavu na kunifanya nishindwe kutembea.
“Zile sauti za kutisha zilizidi kunisogelea nikaona kama nitazubaa basi nitakufa. Nilijilazimisha kukimbia huku nimeshika mkono kwenye mbavu. Nilikwenda hivyo kwa kuchechemea mpaka nilipotokea kwenye mti mkubwa.


Je, nini kitatokea? Kesho wakati kama huu itaendelea....

Ndugu mzizimkavu umerudia hii sehemu...cross check tena kwenye server yako!!!
 
Huyo nijini kafiri kama ww hakuna jini hanayependa zina na kama jini mbona hamesahau kumwambia mustafa mbona hujampaka mkeo mafuta kingine hunatuzallilisha SS waislam. Hinamahana sie tunapenda sana majini na zinaa. majina yako mengi John, Sam, Daniel,jack ,rose nk ya makafiri .chonde chonde husipende kutumia majina ya upande mmoja katka hadithi zako za kijinga

we jamaa ni kumazan
 
Hadithi ya kusisimuwa: Mimba ya jini-31-


ILIPOISHIA:
"Wazo zuri lakini lazima nifike kwanza ofisini nijue hatima yangu ndipo twende huko kanisani."
"Basi ukirudi jioni tutapanga."
"Sawa."
Sara aliagana na shoga yake na kuwahi kazini kama kawaida ili afanye usafi kabla bosi wake hajafika.
SASA ENDELEA...

Mlinzi alimpa ufunguo kama kawaida, alifungua ofisi na kushtuka kuikuta safi imeisha safishwa. Hali ile ilimshtua na kumfanya atoke nje mpaka kwa mlinzi na kumuuliza;

"Eti nani kafanya usafi?"
"Wapi?"
"Ndani ya ofisi?"
"Wewe ndo wa kwanza kuja sijamuona mtu yeyote."

"Kwa...kwa niiii toka nilipoondoka nani alikuwa akifanya usafi?"
"Kwani da Sara ulienda wapi?"
"John si muhimu kujua, nijibu swali langu."

"Toka uondoke sijawahi kumuona mtu akifanya usafi, nakumbuka siku ambayo wewe hukuja bila taarifa nilitaka kwenda kufanya usafi lakini bosi alinikataza, tokea siku hiyo sijamuona mtu akifanya usafi."
"Ina maana toka niondoke hakuna mtu uliyemuona anafanya usafi?"
"Sijawahi kumuona."

"Mbona ofisi inaonesha imefanyiwa usafi muda si mrefu tena wa hali ya juu?"
"Basi majini ndiyo yamefanya usafi," mlinzi alisema kwa utani.
"John na wewe umeligundua hilo?"
"Lipi?"

"La kuwepo na jini ofisini?"
"Mi nimesema tu, hilo jini lifanye usafi kwa ajili gani?"
"Kama mimi nilikuwa sifanyi usafi, basi nani amefanya?"
"Mmh! Labda bosi."

"Nataka kukuambia hapa kuna mchezo, unamjua yule mwanamke?"
"Mwanamke gani?"
"Yule mrembo anayekujaga ofisini."
"Ndiyo."

"Yule nina wasiwasi siyo mtu wa kawaida."
"Una maanisha nini?"
"Mimi simwelewi huenda ni jini!"
"Jini? We acha mambo ya ajabu angekuwa jini tungemuona?"
"Nakwambia ipo siku utakubaliana na mimi."

"Kwa hiyo bosi wateja wake wengine ni majini?"
"Hebu kwanza nikuulize?"
"Uliza."
"Tangu niondoke yule mwanamke kaja mara ngapi?"
"Kwa kweli sijamuona."

"Muongo!"
"Kweli."
"Basi we subiri kama ni yeye nitakomeshana...na...na,"Sara alinyamaza baada ya kuliona gari la bosi wake likisimama getini.

Hakutaka kuongeza neno alichepua mwendo kuwahi ofisini, alijisikia vibaya bosi wake kumkuta eneo lile badala ya ofisini. Lakini alipanga kujitetea alikuwa akimuuliza kitu mlinzi.
Mustafa toka akiwa ndani ya gari alishtuka kumuona Sara, baada ya kupaki gari alielekea ofisini na kupokewa na Sara kama ilivyokuwa kawaida na kupeleka vitu ndani.

Wakati wa kupokelewa alitaka kukataa lakini hakuona sababu ya kukataa, alimuacha apokee lakini alitaka maelezo ya kina atakapomuuliza ili aendelee na kazi lakini kinyume na hapo alipanga kumfukuza kazi kwani tangu aondoke hakukuwa na pengo lolote.
Baada ya kutulia kwa muda Sara aliingia ofisini kwa bosi wake akiwa hajiamini na kufika kusimama mbele ya bosi wake. Mustafa aliacha kusoma gazeti la siku ile na kunyanyua uso wake kumtazama.
"Shikamoo," Sara alimuamkia kwa kupiga magoti.

Ilikuwa mara ya kwanza Sara kumuamkia kwa heshima vile jambo ambalo hakuwahi kulifanya siku za nyuma. Mustafa alijikuta akimshangaa Sara kwa kitendo kile, wakati huo Sara alishtuka kuona aliyekaa mbele yake si bosi bali nguruwe. Alituliza macho ili kupata uhakika.
Hakukuwa na mabadiliko zaidi ya kuona nguruwe amesimama kwenye kiti cha bosi wake akichezesha pua. Alikaza macho kuangalia kama alichokiona ni kweli au maruweruwe. Bado hali ilibakia ileile ya kumuona nguruwe mbele yake, alipekecha macho ili kuikataa hali ile kwa kuamini yale yalikuwa maruweruwe kama yaliyomtokea jana yake.

Itaendelea kesho wakati kama huu....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom