Hadithi ya kusisimua: Jini mauti

Hadithi ya kusisimua: Jini mauti

duu!!! uyu dem noma ukijplipendekeza tu ni kuzimu vumbafu.
 
Demu anagawa kinoma, ukiwa siliasi unakula mzgo hata kama ni toi
 
Jini mauti 29
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Mvulana huyu aliitwa John. Alikuwa kidato cha tano, hakuwa muongeaji sana, maisha yake yalitawaliwa na upole mkubwa, hakuwa mzungumzaji sana.
Endelea…

Kwa kumwangalia John, nilitokea kumpenda, sikujua ningemwambia nini ili apate kunielewa.
Hakukuwa na mtu aliyewahi kuzungumza na John kwa zaidi ya dakika tano, alipenda kukaa peke yake lakini kitu kingine kilichowashangaza watu, huyu John alikuwa na akili sana darasani.

Kwa kumwangalia, alikuwa na mwili wa kawaida lakini kama kulikuwa na kazi ya kufanya, iwe ya kubeba vitu au kazi nyingine, John alifanya kwa nguvu zote, kitu cha kubeba watu wawili, tena kwa shida, yeye alikibeba peke yake.
Kama John akiwa mbele yako, kisha wewe ukiwa nyuma na kumuita, alivyokuwa akigeuka, hakuweza kugeuka shingo tu kukuangalia, alikuwa akigeuka mwili mzima kama roboti.

Maisha yake yalimshangaza watu wengi, wengine wakahisi kwamba alikuwa na tatizo, kumbe mbali na hilo, kulikuwa na kitu kingine kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake ambacho watu hawakuwa wakikifahamu, hata mimi pia sikukifahamu katika kipindi hicho, ila baadaye nilijua kila kitu.
“John,” nilimuita, alikuwa mbele yangu akitoka darasani, kama kawaida yake, akageuka mwili mzima.
“Niambie Davina.”
“Unakwenda wapi?”
“Nyumbani.”
“Hivi unaishi wapi?”
“Sinza Mori.”
“Nashukuru kukufahamu.”
Nilichokihitaji ni mazoea na John, hakukuwa na kitu kingine zaidi ya hicho. Nilimpenda, kiukweli niliwahi kupenda lakini kwa John nilipenda mpaka nikawa sili, sinywi wala sioni.
Nilijua kwamba kila nilipofanya mapenzi na mwanaume, ilikuwa ni lazima afe lakini kwa John, nikashindwa kujizuia kabisa, mapenzi yake yaliukimbiza moyo wangu vilivyo.
Kila nilipofika shule ilikuwa ni lazima nionane na John, nizungumze naye hata kwa dakika chache ndipo niendelee na ratiba yangu.

Kulazimisha ukaribu namna ile, mwisho wa siku nikajikuta nikiwa karibu sana na John ambaye hakuwa mzungumzaji sana.
Ukaribu ule ukasababisha mimi na yeye kuanza kutambulishana nyumbani. Kwangu, niliendelea kuwa na furaha mno, baada ya siku kadhaa ndipo nilipoona kwamba kulikuwa na jambo moja tulitakiwa kufanya, jambo hilo ni mapenzi.
“Kufanya mapenzi?” aliniuliza.
“Ndiyo!”
“Hapana! Haiwezekani, kwani sisi wapenzi?”
“John! Yaani hisia zote hizi, mambo yote tunayofanya bado unataka nikutongoze? Tena mimi msichana nikutongoze!” niliuliza na kumuonesha hisia kali za kimapenzi kupitia macho yangu.
“Hukuniambia.”
“Sawa. Basi ndiyo nakwambia kwamba ninakupenda,” nilimwambia.
“Nashukuru.”
“John! Kwa nini unanifanyia hivi?”
“Kukufanyia nini?”
“Kuniumiza! Kwani ukiniambia kwamba unanipenda pia, utaumia?”
“Hapana! Okey! Nakupenda pia.”
“Sasa inakuwaje?”
“Kuhusu nini?”
“Kuionesha dunia kwamba sisi ni wapenzi.”
“Usiwe na hofu! Tuvutevute muda kwanza,” aliniambia na kuleta stori nyingine kabisa.
Nilimpenda sana na kila nilipomwambia tufanye mapenzi, alinizungusha tu. Kuna siku alisema kwamba tutafanya kesho, ilipofika, aligeuka na kusema siku nyingine. Nilikuwa simuelewi, wakati mwingine nilidhani alishtukia kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu.
Kutokana na kuwa wapenzi, shule nzima wakalifahamu hilo, wakajua kwamba ninatoka kimapenzi na John. Kila siku ilikuwa ni lazima tuonane shuleni, nilipokuwa nikiumwa, ilikuwa ni lazima aje nyumbani kuniangalia.
Wanaume wengi walikasirika kwa kuwa walinitamani sana, walitamani kuwa na msichana aliyekuwa na umbo zuri kama langu. Hawakupata nafasi, kile walichokuwa wakikitaka hawakukipata, mwisho wa siku wakajikuta nikiangukia kwenye mikono ya John.

Kwa wasichana walinichukia sana, walimpenda John, kila mmoja alitaka kuwa naye kutokana na upole wake, uzuri wake na hata akili zake. Wengi walijigongesha kwake lakini mwisho wa siku mvulana huyo akaamua kuwa na mimi.
Kwa hiyo shuleni tukazungukwa na maadui na miongoni mwa wasichana waliokuwa wakinichukia alikuwepo mmoja aliyeitwa Asha. Alikuwa msichana mrembo ambaye pale shuleni walimpa jina la Beyonce, alipenda kupendwa, kitendo cha kuwaona wanaume wengi wakimpapatikia kilimpa raha.

Alitembea na wavulana kadhaa, hakuchuja, mwisho wa siku kabisa akataka kutembea na John.
Alianza kumtafuta kijana huyo, alijitahidi kuweka mitego ya kila aina lakini John hakuingia mkenge, alikasirika mno, baada ya siku kadhaa, akashtukia John akiwa nami.
Hilo ndilo lililomuumiza mno, hakuamini, akaniwekea kinyongo lakini sikutaka kujali. Alitangaza vita lakini hakujua alikuwa akitangaza vita na mtu wa aina gani. Aliwaambia marafiki zake kwamba alinichukia na ilikuwa ama zake ama zangu, ilikuwa ni lazima kunikomesha.

Kwa kuwa John alikuwa wangu, sikutaka kujali sana, nikamsikiliza na kukubaliana naye kwamba tulitakiwa kusubiri.
Kila siku nilishikwa na mhemko, mwili ulinisisimka kila siku, nilishindwa kabisa kuvumilia, nikajiona kwamba ule uvumilivu niliokuwa nao ulikuwa ukienda mwishoni kabisa.
Baada ya kukaa kwa kipindi cha miezi miwili ndipo aliponiambia kwamba kile nilichokuwa nikikitaka basi kilitakiwa kufanyika. Nilifurahi moyoni, sikuamini kama kweli hatimaye John alikubaliana nami.
“Kweli?”
“Ndiyo! Mbona hauamini mpenzi?” aliniuliza.
“Basi tu. Tufanyie wapi?”
“Wewe unataka wapi?”
“Popote tu.”
“Basi nitakushtua, twende Bagamoyo, kuna hoteli nzuri tu. Ila kuna kitu,” aliniambia.
“Kitu gani?” nilimuuliza, akashusha pumzi.
“Nadhani huo ndiyo utakuwa mwisho wa mimi na wewe kuonana,” aliniambia maneno yaliyonishtua.
“Kivipi?”
“Kwani haujaelewa?”
“Yaani ndiyo utakuwa mwisho wa mimi na wewe kuwa pamoja?”

Itaendelea
 
Image may contain: 1 person, shoes and text

KITABU KIPYA CHA JINI MAUTI
Ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi Nyemo Chilongani ambacho kinachomzungumzia msichana mrembo mchawi, Davina, mwenye figa iliyowachanganya wanaume kiasi cha kumtamani pasipo kujua kwamba msichana huyo alikuwa ameingiziwa JINI MAUTI mwilini mwake kwamba kila mwanaume anayelala naye ni lazima afe.
Wanaume walichanganyikiwa na kutamani kuwa naye. Mtu wa kwanza kulala na Davina alikuwa Thomas. Kijana mwenye uzuri wa sura, aliyependwa na wasichana wengi. Hakumpenda Davina lakini kwa sababu msichana huyo alimpenda Thomas, akamfanyia uchawi na kupendwa.
Uhusiano ukawa mkubwa, wakajikuta wakiwa karibu na siku ambayo walilala pamoja ndiyo siku ambayo Thomas alikufa kwa kuchukuliwa msukule. Huo haukuwa mwisho, ukawa mwanzo wa mauaji, aliua wanaume wengi lakini mwisho wa siku akakutana na mwanaume ambaye alimchanganya.
Mwanaume huyu aliitwa John. Alihisi kwamba kama angefanya naye mapenzi angekufa, wakafanya lakini kitu cha ajabu, John hakufa, akahisi kwamba alikuwa jini kitu ambacho si kweli.
Walipomaliza huku akiwa amepigwa na mshangao, John akainuka kitandani na kumwambia kwamba anaondoka, anakwenda wapi? Hajui na mwanaume huyo alipoufungua mlango na kutoka,
alipoubamiza, Davina hakumuona tena, akachanganyikiwa mno.
Hakujua mwanaume huyo alikwenda wapi, hakujua alipoteaje na wakati hakuwa mchawi kama alivyohisi. Hapo ndipo utata unapoanza, hapo ndipo uchawi unapoanza kumtesa na kumlaza kitandani huku akiugua ugonjwa usioonekana kiasi cha kukohoa damu na kuonewa huruma na kila mtu aliyemwangalia.
Unajua nini kilitokea? Unajua nini ulikuwa mwisho wa Davina na uchawi wake? Majibu yote yapo ndani ya kitabu hiki ambacho kinapatikana Dar es Salaam, kwa watu wa mikoa mingine wanaweza kuwasiliana kwa namba 0718069269.
Gharama ya kila kopi ni shilingi 5000 tu!
Kariakoo kinapatikana, namba 0755-718169.
Mwenge kinapatikana kwa namba 0718-069269.
Shunie Madame S Madame B MziziMkavu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom