Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka

Kila nikiona uzi uko bold najua tayari episode imeongezeka lkn kumbe ni drama tu za Shunie zinaendelea. moneytalk naomba tuongee tafadhali
 
SEHEMU YA 25.

Sekretari alisimama na kumwangalia Bazoka aliyekuwa amesimama, alimshangaa kwani mwanaume huyo ni kama hakuwa kwenye hali ya kawaida, alikuwa akimwangalia kwa wasiwasi mkubwa kana kwamba kulikuwa na kitu kilichokosekana humo ndani.
Dada yule akapeleka birika la kahawa mpaka mezani, hakumuona Bazoka wa pili ambaye alikuwa kwenye kiti, macho yake yalifumbwa, hakuwa na uwezo wa kuliona jini hilo ambalo lilikaa na kumwangalia tu.
“Unaonekana haupo sawa bosi,” alisema sekretari huku akimwangalia bosi wake.
“Nipo poa!”
“Kabisa?”
“Yeah! Naomba nikuone baadaye,” alimwambia huku akimtaka kutoka ndani ya chumba hicho.
Hilo halikuwa tatizo, akatoka na kuendelea na shughuli zake huku akimuacha Bazoka humo, hakujua kama kulikuwa na Bazoka wawili, huyo mmoja alikuwa kwenye kiti.
“Wewe ni nani?” aliuliza Bazoka huku akimwangalia tena jini lile.
“Acha maswali ya kitoto Bazoka, wakati umeingia nilikwambia naitwa nani! Umesahau?” alimuuliza huku akimwangalia.
“Oh! Sawa! Kwa nini umekuja kwangu?” alimuuliza.
“Hilo ndilo swali ambalo ulitakiwa kuniuliza mwanzo kabisa, badala yake umekuwa ukiuliza maswali ya kijinga sana,” alimwambia, akaanza kuinuka kwenye kiti kile, akamtaka Bazoka aende akakikalie yeye, akafanya hivyo.
“Nimekuja kwa lengo moja kubwa!” alimwambia.
“Lipi hilo!”
“Nnataka kukusimamisha wewe tu kwenye nchi hii, uwe tajiri mkubwa sana ila utatakiwa kufanya kitu kimoja,” alimwambia huku akimwangalia.
“Kitu gani?”
“Kutoa kafara ya watu wawili!”
“Kafara kwa mara nyingine? Hapana! Nimetoa kafara siku chache zilizopita, kwa nini unaniambia nitoe tena kafara?” alimuuliza.
“Bazoka! Nisikilize kwa makini kabisa.”
“Sawa!”
“Huku ulipo kunakuwa na madarasa, ulipokuwa umeingia, ulikuwa darasa la chini kabisa, baada ya kutoa kafara, sasa umeingia kwenye daraja jingine, hili utatakiwa kutoa kafara na ndipo hapo utakapofanikiwa zaidi na kuulipia huu ulinzi nitakaokupa,” alimwambia huku akimwangalia.
“Kwa nini kila siku ninatoa makafara mimi tu? Kwa nini wenzangu hawatoi mfululizo kama mimi?” aliuliza Bazoka kwa staili ya kulalamika.
“Wenzako walishindwa!”
“Akina nani?”
“Nalo hilo ni swali la kijinga sana kuniuliza,” alimwambia.
“Okay! Nishawajua. Kwa nini walishindwa?”
“Ni kwa sababu hawakutaka kuwatoa kafara marafiki na ndugu zao na ndiyo maana nimeamua kukufuata na kukwambia utoe kafara, kafara pekee utakayotakiwa kuitoa ni kuwamaliza wao,” alimwambia.
“Kuwamaliza wao?”
“Ndiyo!”
“Unamaanisha Sultani na Christopher Bonge?”
“Ndiyo haohao!”
“Inawezekana vipi? Kwa nini iwe hivyo? Hapana! Siwezi kumwaga damu, tena kwa marafiki zangu wa karibu,” alisema Bazoka huku akiliangalia jini lile.
“Wala usijali! Kazi hautoifanya wewe, kuna mtu ataifanya ila utatakiwa kuweka saini ya damu,” alimwambia huku akimwangalia.
“Saini ya damu?”
“Ndiyo!”
“Nikikataa?”
“Utakufa wewe!”
Bazoka akakaa kimya, hakukuwa na kitu alichokichukia kama kusikia kifo. Hakutaka kufa, maisha yalikuwa mazuri mno, alikuwa na utajiri mkubwa, alitamani hata kuishi milele kwa kuwa alipata kila kitu alichokihitaji.
Alimwangalia jini lile, ni kama hakuelewa vile, aliambiwa marafiki zake hao walifanya ukaidi wa kumwaga damu kwa watu wao wa karibu na ndiyo maana akafuatwa yeye na kuambiwa ni lazima afanye mauaji.
Kwake ilikuwa vigumu sana, lisingekuwa jambo jepesi hata kidogo kuwafuata watu hao na kuwamaliza. Alimkumbuka Sultani jinsi alivyomwamini na kumuingiza kwenye ulimwengu huo, kummaliza ungekuwa usaliti mkubwa sana ambao hakuwahi kuufanya maishani mwake.
Hakutaka kuona hilo likitokea na ndiyo maana alikataa, ugumu ulikuwa ni kuonana na watu hao ana kwa ana na kuwamaliza ila baada ya kuambiwa kilichohitajika kwake ni ruhusa tu, kidogo akawa na nguvu.
“Na ni nani atawamaliza?”
“Kuna mtu!”
“Yupi huyo!”
“Mfungulie mlango! Amekwishafika,” alimjibu.
Bazoka alishangaa, hakusikia hodi mlangoni lakini aliambiwa amfungulie mlango kwa kuwa tayari alifika na alikuwa mahali hapo. KWanza akataka kukataa lakini akaona si tatizo, kwa kuwa aliambiwa mtu huyo alikuwa mlangoni, akaufungua.
Macho yake yakatua kwa msichana mzuri wa sura, kwa kumwangalia mara moja ilikuwa ni rahisi kusema umekutana na msichana mrembo kuliko wote katika dunia hii.
Alikuwa na umbo namba nane, hipsi zilizochomoka ambazo watoto wa mitaani waliziita bastola. Kiuno chake kilichambulika vizuri na kifua chake kilisimama kama msichana aliyetoka kuvunja ungo.
Sura yake ilikuwa nyembamba kidogo, nyusi zake zilikolezwa kidogo na wanja alioupaka, alikuwa mweupe kiasi na mashavuni mwake kulikuwa na vishimo viwili ambavyo vilikuwa vikionekana kila alipokuwa akicheka ama kutabasamu.
Macho yake yalikuwa ya goroli, lipsi nene za kunyonya, alikuwa na meno meupe na puani mwake alikuwa na kipini huku nywele zake zikiwa ndefu kidogo.
Japokuwa alitembea sehemu nyingi na kukutana na wasichana wa kila aina lakini akakiri kuwa hakuwahi kumuona msichana mrembo kama huyo aliyesimama mbele yake.
“Ka...karibu..” alimkaribisha.
“Nashukuru,” aliitikia na kuingia ndani.
Sauti yake ilikuwa silaha nyingine kabisa, ilikuwa laini ile ya kumtoa nyoka pangoni na kumuamrisha acheze kadiri alivyoweza, sauti ile ilipenya masikioni mwa Bazoka, ilikwenda mpaka ndani kabisa na kumsisimua kupita kawaida.
Msichana huyo alikuwa ananukia, marashi yake ni kama hayakuwahi kuwepo katika dunia hii, harufu hiyo ilimfanya Bazoka kutamani kumwangalia zaidi na zaidi kwani hakuisha hamu hata kidogo.
“Naitwa Bazoka,” alijitambulisha hata kabla ya kuambiwa kufanya hivyo, akampa mkono, wakashikana na kusalimiana.
Mikono ya msichana huyo ilikuwa laini mno, ni kama ya mtoto aliyezaliwa saa chache zilizopita. Bazoka alipomshika mkono akatamani aendelee kuushikilia tu kwani ulimsisimua na kuhisi kama amepigwa shoto iliyosambaa mwilini mwake na kumfanya kusisimka kupita kawaida.
“Naitwa Shunie,” alijitambulisha msichana yule.
“Oh! Umependeza, una sauti nzuri na ngozi nzuri sana,” alisema Bazoka huku akiachia tabasamu pana.
“Nashukuru sana!”
“Na unaonek.....”
“Bazoka! Tumalizie harakaharaka. Shunie, weka mkataba mezani,” alisema jini Bazoka na msichana huyo kufanya hivyo haraka sana.
Mkataba ukawekwa mezani, alichoambiwa ni kuusaini ili kazi ya kuuliwa kwa watu hao kufanyika haraka sana. Hakutaka kubisha, akasaini na Shunie kuchukua pini, akamchoma kidoleni na kumwambia damu ile aipake kwenye mkataba ule, akaanya hivyo.
“Nashukuru sana Bazoka! Tutakurudia kazi ikikamilika!” alisema jini Bazoka.
“Lakini mb...” alisema Bazoka lakini hata kabla ya kumaliza sentensi yake, wawili hao wakapotea chumbani humo, ikabaki harufu ya Shunie tu ambayo iliendelea kumpagawisha ofisini mule.

Je, nini kitaendelea?
 
Hahahhaaa uwiiii naitwa shunie
 
He he

Nyemo bwana shunie mimi unanijua vizuri tu nilivyo na shape yangu no 1
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom