Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka

Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka


Waja wa jf hawana shukrani jamani
Mtu kajitolea kuleta story zake bure tu tusome

Kama una roho nyepesi unasusa kabisa kuleta story na ninavyomjua nyemo mzee wa kupanick soon anasusa nipo hapa
 

Waja wa jf hawana shukrani jamani
Mtu kajitolea kuleta story zake bure tu tusome

Kama una roho nyepesi unasusa kabisa kuleta story na ninavyomjua nyemo mzee wa kupanick soon anasusa nipo hapa
aache
 
  • Thanks
Reactions: T11
ᛕꪖꪑꪖ ꪜ꠸ρ꠸ ꪖꪖꪀƺ꠸ᦓꫝꫀ ᥴꫝꪖꪀꪀꫀꪶ ꪻꫀꪶꫀᧁ᥅ꪖꪑ ꪻꪊꪑᠻꪊꪖꪻꫀ ᛕꪖꪑꪖ ꪗꪊꪶꫀ ꪑ᭙꠸ꪀᧁ꠸ꪀꫀ😂😂
 

Waja wa jf hawana shukrani jamani
Mtu kajitolea kuleta story zake bure tu tusome

Kama una roho nyepesi unasusa kabisa kuleta story na ninavyomjua nyemo mzee wa kupanick soon anasusa nipo hapa
Aende huko
 
Mnawatetea utafikiri wanafanya hisani

Kuna wanachopata
 

Waja wa jf hawana shukrani jamani
Mtu kajitolea kuleta story zake bure tu tusome

Kama una roho nyepesi unasusa kabisa kuleta story na ninavyomjua nyemo mzee wa kupanick soon anasusa nipo hapa
Hawanijui hawangoja niwavutie kasi.
 
NYEMO CHILONGANI
UCHAWI WA BILIONEA BAZOKA
SEHEMU YA 15

Mpelelezi Maganza aliona kama kudanganywa, aliambiwa gari moja lilisimama pembeni ya uwanja wa mpira ambalo alikuwa na uhakika kumchukua Yusufu na kuondoka naye lakini kitu cha ajabu kabisa, eti hilo gari halikuwa likionekana.
Alihisi kudanganywa, hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka kuelekea ndani ya gari lake na kuondoka mahali hapo. Kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, alikuwa na maswali ambayo hayakuwa na majibu hata kidogo.
Kwenye suala hilo akahisi kabisa kulikuwa na nguvu za kishetani zilizokuwa zikitokea na kwa sababu aliamua kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu, basi hapakuwa na budi kujiandaa vilivyo.
Akarudi ofisini kwake, akatulia, aliendelea na kazi kidogo tu na kuondoka kurudi nyumbani kwake. Mkewe alimwangalia, alimzoea kumuona mume wake akiwa mtu wa mawazo tele, yaani ilikuwa ni sehemu ya kazi zake, alivurugwa kila siku na alipokuwa akimuona kwenye hali hiyo, hakutaka kumsumbua kabisa.
Akamuandalia chakula, akala na kuanza kuzungumza. Alimwambia kilichokuwa kimetokea, jinsi alivyoambiwa gari lilionekana kwenye ile picha ya mnato iliyorekodiwa na alipofika yeye, gari halikuonekana tena.
Mkewe alishangaa mno na kumuonya mume wake kwamba hilo suala limekaa kishirikina sana, kama alikuwa na uwezo wa kuachana nalo basi alitakiwa kufanya hivyo.
“Haiwezekani! Halafu sisi polisi kama serikali huwa hatuamini uchawi,” alisema Maganza huku akimwangalia mke wake.
“Lakini mume wangu, kama gari lilikuwepo, unafika wewe na kuonyeshwa hiyo video, gari halionekani, unahisi ni sawa hivyo?” aliuliza mke wake.
“Nisikiliza mke wangu! Ishu ni kwamba serikali haiamini kwenye uchawi,” alimwambia.
“Kwa hiyo?”
“Nitaendelea kufuatilia!”
Maganza alikuwa mbishi, hakutaka kukubali kushindwa, kulikuwa na kesi nyingi alizokuwa amezifuatilia, tena ambazo aliambiwa kuachana nazo kwa kuwa zilikuwa za kishirikina lakini alizishinda zote hizo.
Kwake, ushirikina haukuwa na nafasi yoyote ile na ndiyo maana aliona ni lazima apambane kuhakikisha anafanikiwa kumfahamu muuaji wa mtoto Yusufu ambaye mpaka muda huo hata mwili wake hawakuwa wameupata.
Muda wa kulala ulipofika, akalala zake, usingizi mzito ukampitia.
Maganza alijikuta amesimama mbele ya makaburi mengi yaliyokuwa kwenye eneo lililokuwa na barii kali, kwenye makaburi hayo ya Kiislamu na Kikristo kulikuwa na watu wanne, wanaume waliokuwa na miili mikubwa wakiwa wamesimama huku wakiwa uchi kama walivyozaliwa.
Pamoja na ukomavu wake, umwamba lakini Maganza akaonekana kuogopa mno, alikuwa akitetemeka huku kijasho chembamba kikimtoka, aliwaangalia wanaume wale, walisimama vilivyo huku wakimwangalia.
Kwa pembeni kidogo kulikuwa na jeneza, walionekana kuwa mahali hapo tayari kwa kuzika. Jeneza halikuwa limefungwa, lilikuwa wazi, na kwa jinsi walivyosimama ni kama walikuwa wakiaga sura ya mwisho.
Akatamani kuondoka mahali hapo lakini akashindwa, alibaki akitetemeka, hakujua kama kwa sababu ya hofu ama baridi lililokuwa likimpiga mahali hapo, miguu yake haikuwa ikinyanyuka, yaani ni kama kulikuwa na mtu aliyeishika na kutotakiwa kuondoka mahali hapo.
Huku akiwa anajiuliza ni kwa namna gani alifika mahali hapo, akasikia muungurumo fulani wa kutisha ukitoka ndani ya jeneza lile, ulikuwa muungurumo fulani uliokuwa ukitisha sana, akazidi kuogopa, ghafla maiti iliyokuwa ndani ya jeneza lile ikaanza kutoka.
Ilikuwa ni ya mtoto, albino, ilikuwa na pamba puani na mdomoni mwake, ilifumba macho lakini ghafla tu, ikafumbua macho na kumwangalia usoni.
Akaogopa, hakutarajia kukutana na kitu kama hicho, moyo wake ukashikwa na hofu zaidi, akatamani kukimbia, akashindwa, kijasho chembamba kilichokuwa kikimtoka kikaongezeka.
Ilikuwa ni maiti ambayo ilitoka na kuanza kumfuata kule alipokuwa, hatua zake hazikuwa za kawaida, wakati mwingine aliona kama miguu yake haikuwa ikikanyaga chini, alimsogelea, alipomfikia, akanyoosha mkono na kumpa kikaratasi cheupe kilichokuwa na maandishi mekundu.
Hakutaka kukichukua lakini kitu cha ajabu kabisa akauona mkono wake ukiinuka na kuunyoosha kwa ile maiti na kukichukua kile kikaratasi huku wale wanaume wanne wakiwa wamegeuka na kuanza kumwangalia.
Alipokishika tu akahisi kama akipigwa na kitu fulani mwilini mwake, mfano wa shoti ya umeme, ghafla, hapohapo akashtuka kutoka kwenye usingizi mzito.
“Mamaaaa...” alipiga kelele na kuyafumbua macho yake.
Alikurupuka kutoka kwenye usingizi mzito, akayafumbua macho yake na kuangalia huku na kule, pembeni alikuwepo mke wake, kitu cha ajabu kabisa, pamoja na kukurupuka huku akiwa amepiga kelele mkewe hakuweza kushtuka.
Alimwangalia, alilala fofofo, akampuuzia lakini alipojiangalia mkononi mwake, moyo wake ukapiga paaaa! Alikuwa na kipande cha karatasi mkononi mwake, kilikuwa kilekile alichopewa kwenye njozi kaburini.
“Mungu wangu!” alisema kwa mshtuko, hakuamini alichokiona.
Akakifungua na kuanza kukiangalia, kiliandikwa maneno machache tu yaliyosomeka Alkabuaz Taarib. Hakuelewa yalimaanisha nini, aliyashangaa, macho yalimtoka na hakuamini kama kile kilichokuwa kikitokea kilimtokea yeye.
“Imekuwaje? Nani ameni...” alijiuliza lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, akasikia sauti moja kubwa ikiliita jina lake kutoka nje.
“Maganzaaaaaa.....” akapigiwa na mshtuko zaidi, saa ya ukutani ilionyesha ni saa nane na nusu usiku.
***
Bi. Semeni alijua huyu mpangaji aliyempangisha kipindi hiki hakuwa mpangaji kama wapangaji wengine, inawezekana huyu alikuwa na jambo lake. Kilichomshangaza ni namna alivyokuwa kule uani, halikuwa jambo la kawaida tena kwa wakati huo lakini alipomuuliza, alimwambia alikuwa chooni.
Alikwenda chooni kuona labda kweli alikuwa huko, hakukuta maji yoyote yakiwa yamemwagwa, akahisi kabisa kulikuwa na kitu alichokuwa akikihitaji.
“Au mwizi?” alijiuliza.
Akataka kufanya uchunguzi wake, ilikuwa ni lazima ajue mpangaji wake huyo alikuwa mtu wa namna gani kwa kuwa haikuwa rahisi kufanya yale aliyokuwa ameyafanya.
Aliwahi kumuwangia mara moja, hakuonekana kuwa na ubishi wowote ule, yaani kwa kifupi hakuwa na ulinzi hata kidogo, kwenye suala la kuhisi kwamba inawezekana alikuwa mchawi, likaondoka kichwani mwake, akahisi sasa inawezekana huyu mpangaji alikuwa mtu mwingine kabisa.
Hakutaka kumwambia kitu chochote kile, huku Bazoka akiwa chumbani kwake, Bi. Semeni akaenda mpaka mlangoni kwa nje, akasimama na kuanza kusikilizia humo ndani kuona kama kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, kulikuwa na ukimya mkubwa.
Alijiamini, alikuwa mchawi tena mwenye nguvu lakini kwa hali aliyoionyesha mpangaji wake tayari ilianza kumpa hofu, tena iliyomuingia mpaka moyoni mwake.
“Sasa naogopa nini?” alijiuliza.
Aliona ni ujinga mkubwa mno kwa mtu kama yeye kumuogopa mtu ambaye hakuwa mchawi hata kidogo, alikuwa na nguvu kubwa, aliamini endapo angemchukua na kumuwangia, kusingekuwa na ugumu wowote ule, sasa kwa nini awe na hofu?
Akasubiri mpaka ilipoingia usiku, akala, akaweka vifaa vyake, siku hiyo kitu alichotaka ni kuhakikisha anamchukua Bazoka na kuondoka naye, ampeleke kwenye shamba lake lililokuwa huko Bagamoyo, amlimishe ekari kama nne na kumrudisha, alitaka kufanya hivyo kama adhabu kwa kile alichokifanya.
Baada ya usiku mwingi kuingia huku Bazoka akiwa amelala, akajiandaa, kama kawaida yake akawa mtupu kabisa, alikuwa na hirizi kubwa kiunoni mwake, uso wake ulikuwa na masizi, akafungua dari lake, fisi mkubwa akatoka, akampanda na kuongea maneno fulani, akaanza kuondoka mahali hapo.
Wakatokea chumbani kwa Bazoka, alimuona amelala, akamsogelea, akammwagia unga fulani, akamchukua, akampakiza juu ya fisi na kuanza kuondoka naye kama alivyokuwa akifanya siku nyingine.
Hakujua ni kitu gani kilitokea, kitu kama radi kikamulika na kumpiga fisi, akaanza kwenda huku na kule, wala hawakufika mbali, wote watatu wakaanguka, waliangukia msituni, sehemu iliyokuwa na miti mingi, kulitisha kupita kawaida.
Huku akiwa chini na hajui ni kitu gani kimetokea, ghafla akaanza kusikia vicheko kutoka vichakani, vilikuwa vya watu ambao hakuwafahamu lakini kwa jinsi vicheko vile vilivyosikika, alijua kabisa vilijaa dhihaka tele.
“Nipo wapi?” alijiuliza, alipoangalia pembeni, Bazoka alikuwa amelala vilevile. Hofu ikaujaza moyo wake.

Je, nini kitaendelea?

Kwa wanaoona hadithi inachelewa, waje Mwanza watuwekee minara mingi ya Halotel kuwe na network yenye kasi kwa internet.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom