jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,830
- 10,091
asante
,🤣🤣🤣🤣Madamu s mwanangu sana
asaantee, nashukuru Allah nimeuona, msijali akiweka na mm nawekaMadame S heri ya mwaka mpya,endelea kuangusha mnara hivyo hivyo
,🤣🤣😂😂😂😂 hamuwez teseka na arosto na wakat nipo
asanteeeMadam umetisha sanah
Mama wakumaliza utata
Hujakaripiwa kweli?,hamuwez teseka na arosto na wakat nipo

nambieeMama wakumaliza utata
walaaHujakaripiwa kweli?![]()
Ongeza basi madamwalaa
hajashusha kule kaishia hapohapoOngeza basi madam
Asante kwa kunisaidia...nakuwa bize mno na huku network inazingua kishenzi. Nikiweka na endapo nikajisahau kuweka huku naomba unisaidieNYEMO CHILONGANI
UCHAWI WA BILIONEA BAZOKA
0718069269
SEHEMU YA 20
Wale fisi waliendelea kumsogelea Bazoka hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya mahali hapo, alikuwa akiogopa lakini ghafla huku akiwa hajui ni kitu gani kimetokea, mwanga kama wa radi ukapiga, fisi mmoja akapigwa na kubabuliwa, akaanguka chini, akafa.
Akashangaa kuhusu radi hilo, likapiga jingine, hapohapo likatokea jitu kubwa mfano wa nguzo ya umeme, lilikuwa na mwili mkubwa, mikono yake ilikuwa mikubwa huku akiwa na makucha marefu.
Mwili wake ulikuwa na manyoya, alitisha na sura yake ilikuwa kama ya Mbweha, meno yalitokeza kwa nje, wale fisi badala ya kumsogelea Bazoka, sasa wakageuka na kuliangalia hilo dudu lililosimama pembeni yao.
Kwa kutumia mikono yake mirefu, hapohapo akaanza kupambana na hao fisi, kwake wala haikuwa kazi kubwa hata kidogo, aliwashambulia mara moja tu, fisi wawili walipigwa na kufa na mmoja alikwanguliwa ubavuni na makucha ya jitu lile, akaanguka chini, akaugulia maumivu na kukimbia mahali hapo kuelekea porini.
Bazoka alibaki akitetemeka, hakuamini kile alichokuwa akikiona mahali hapo, alihisi kama alikuwa kwenye njozi moja ya kutisha sana, iliyomfanya kusisimka mwili wake wote. Sasa akawa anaangaliana na jitu lile, alitamani kukimbia lakini miguu ilikosa nguvu kabisa.
Halikuzungumza, likageuka na kuondoka zake huku akimwacha Bazoka akimwangalia. Hakujua nini kilitokea lakini ghafla akajikuta akiwa ndani ya chumba cha Bi. Semeni, mwanamke huyo alikuwa palepale kitandani, alikuwa akitoka damu nyingi ubavuni mwake, hapo akili ya Bazoka ikamwambia kwamba ndiye yule fisi aliyekuwa amekimbia.
“Siwezi kukucha,” alisema Bazoka, haraka sana akamsogelea, akamchoma kisu tumboni, mara mbili, akakichomoa, akaufungua mlango na kuondoka nyumbani hapo kupitia kulekule ukutani uani.
Damu zilikuwa zimetapakaa kitandani, Bi. Semeni aliuawa vibaya, japokuwa alikuwa mchawi wa kutisha lakini alikutana na mtu aliyekuwa na nguvu zaidi yake.
Watu hawakujua kilichokuwa kimetokea, ilikuwa ni usiku na kubwa zaidi waliogopa kuingia ndani ya nyumba hiyo. Siku iliyofuata kulikuwa na misiba mitatu mtaani, kulikuwa na wanaume wawili na mwanamke mmoja walikufa wakiwa kitandani.
Kila mmoja alishangaa, vilikuwa ni vifo vya ghafla ila kilichowashangaza wengi ni kufa kwa siku moja, tena wote walikufa wakiwa usingizi, watu hao ndiyo walikuwa wale fisi waliofika kwa ajili ya kumsaidia Bi. Semeni.
Mwanamke huyo hakuonekana, watu walikuwa wakijiuliza sababu zilizofanya kutokuonekana lakini hapakuwa na yeyote aliyejua chochote kile. Walizoea kumuona akiwa nje akisuka ukili lakini hakuwa akionekana tena.
Baada ya siku ya tatu kuingia ndipo wakaanza kusikia harufu kali ya mzoga ikitokea ndani ya nyumba ile. Kila mmoja alishangaa, hawakujua ulikuwa mzoga wa nini, ilikuwa ni rahisi kusema wa paka ama panya lakini kila walipokuwa wakiijadili harufu ile, haikuwa ya kawaida.
Kuingia ndani ya nyumba hiyo waliogopa, halikuwa jambo la kawaida kuingia kichwa kichwa ndani ya nyumba ya mwanamke mchawi kama Bi. Semeni, ulitakiwa kujipanga vilivyo.
Watu hao wakatoa taarifa katika ofisi ya serikali ya mtaa ambao hao ndiyo waliofika mahali hapo na kuingia ndani kuona kulikuwa na nini. Nje ya nyumba hiyo kulikuwa na watu zaidi ya mia moja, kila mmoja alitaka kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea ndani.
Wengi walisema kulikuwa na maiti, inawezekana Bi. Semeni aliamua kumuua mtu na mwili huo kuuacha humo. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa alipoingia na watu wake mpaka chumbani mule, hawakuamini walichokiona.
Mwili wa Bi. Semeni ulikuwa kitandani, kulikuwa na damu zilizoganda, mwili uliharibika na nzi walikuwa wakiuzingira tu. Hawakuugusa wala kugusa chochote kile, wakapiga simu polisi ambao walifika hapo baada ya dakika kadhaa.
Wakaingia ndani, wakaupiga picha, wakafanya mambo yao na kuuchukua. Watu waliposikia kwamba ni Bi. Semeni ndiye aliyekuwa amekufa ndani ya chumba chake, kila mmoja alishangilia kwa furaha, hapakuwa na mtu aliyeamini kama mwanamke huyo alifariki dunia.
Hawakuwa wakimpenda, aliwafanya kutokuwa na amani hata kidogo, kila mtu alitamani kuona siku moja anakufa, na siku hiyo ndiyo iliwadia, hatimaye yule mchawi aliyekuwa akiwatesa alikufa, inasemekana mwili wake ulichomwa kisu.
Kila mmoja alibaki akiwa na mshangao, hawakujua ni nani alimchoma kisu, wengine walisema inawezekana alijichoma mwenyewe kama kujimaliza lakini hilo likatoka vichwani mwao kwa sababu kisu hakikuwepo.
“Huyu ameuliwa!” alisema jamaa mmoja.
“Na nani? Kuna mtu anaweza kumuua? Atakuwa amejimaliza mwenyewe,” alisema mwanaume mwingine.
“Hapana! Angekuwa amejichoma kisu na kujiua, kisu kingeonekana,” alimwambia.
“Ila kweli!”
“Itakuwa mtu aliingia, akamuua na kutokomea zake!” alisema mwanaume huyo.
“Sasa atakuwa nani? Yaani uingie kwa Bi. Semeni, umuue na yeye anakuangalia tu!” alisema jamaa huyo.
“Sijajua! Ngoja tusikilize polisi watasemaje,” alisema.
Kamanda Masumbuko akapelekewa taarifa ya mauaji hayo, alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani hasa kilichotokea mpaka mtu aingie ndani ya nyumba ya mwanamke huyo na kumuua.
Ripoti aliyopelekewa mezani kwake aliambiwa pia kwamba mwanamke huyo alikuwa mchawi mkubwa, hakupendwa na kifo chake kiliwafanya watu wengi kushangilia, inawezekana kulikuwa na mtu aliyejitoa na kumuua.
Kichwa cha Kamanda Masumbuko kikamkumbuka mtu mmoja tu, Maganza, akampigia simu na kutaka kuonana naye ofisini kwake, hilo halikuwa tatizo, baada ya dakika kadhaa, mwanaume huyo alikuwa humo.
“Kuna taarifa nimeletewa!” alisema huku akimwangalia.
“Taarifa ipi mkuu?”
“Kuna mwanamke ameuawa hapo Magomeni!”
“Mwanamke gani?”
“Sijajua ni yupi ila kwa taarifa hizo zinasema alikuwa akichukiwa na mtaa mzima!” alimwambia.
“Kwa sababu gani?”
“Ulozi! Nasikia alikuwa anapaa usiku!”
“Na ndiyo sababu iliyopelekea watu washangilie?”
“Kabisa. Sasa ninahitaji ulifuatilie hili suala!” alimwambia.
“Haina shida. Na mwili upo wapi?”
“Hospitali ya Mwananyamala!”
“Sawa. Acha nikauone kwanza,” alisema.
Maganza hakutaka kupoteza muda, haraka sana akaondoka na kuelekea huko hospitalini. Kichwani mwake kulikuwa na mambo mengi, hakuwa amemalizana na suala la mtoto Yusufu, tayari mezani kwake kulipelekwa kiesi nyingine kabisa.
Kwa maelezo ya bosi wake alimwambia kifo cha mwanamke huyo kiliibua furaha sana mtaani kwa sababu alikuwa mchawi, kwa maana hiyo inawezekana kabisa kulikuwa na mtu aliyeingia ndani ya nyumba hiyo na kumuua kwa makusudi kabisa kwa sababu hakupendwa.
Alichukua dakika kadhaa akafika huko hospitalini, akateremka na kumfuata mkunga mkuu na kumwambia kilichompeleka hapo, akachukuliwa na kupelekwa mpaka mochwari na kuonyeshwa mwili wa Bi. Semeni.
Aliuangalia, aliangalia jeraha la kisu kwa umakini, lilikuwa kubwa, hilo lilimuonyesha hakuwa amechomwa mara moja, hapakuwa na kisu kilichokuwa na uwezo wa kuchoma na kuacha tundu kubwa namna hiyo.
“Huyu alichomwa mara kadhaa,” alisema huku akimwangalia daktari.
“Kwa sababu gani?”
“Angalia tundu! Na mtu aliyemchoma anatumia mkono wa kulia,” alisema.
“Umejuaje?”
“Kama angekuwa antumia mkono wa kushoto, angemchoma upande huu wa kulia, ukiona mtu amechomwa tumboni, upande kidogo wa kushoto, jua muuaji anatumia mkono wa kulia,” alimwambia, daktari akashangaa.
“Ila pia ana jeraha ubavuni!” aliambiwa.
“Jeraha? Hebu tulione,” alimwambia, daktari akafungua zaidi shuka, ni kweli mwili wa Bi. Semeni ulikuwa na majeraha kama ya kucha mbili kubwa zilizopita ubavuni mwake.
“Kwa jinsi ninavyoona ni kama kucha!” alisema daktari.
“Kucha? Kuna kucha zinazoweza kujeruhi pakubwa kama hivi?” aliuliza huku tayari akiwa na majibu kwamba hazikuwa kucha.
“Sasa tutasemaje? Ama alichanwa na kisu pia?”
“Hapana! Hizi si alama za kuchanwa na kisu! Hebu subiri niende kwake, naweza kupata majibu,” alisema na kuondoka mahali hapo.
Sasa akachanganyikiwa! Hakujua kilichokuwa kimetokea, kuhusu jeraha la kuchomwa na kisu ilikuwa ni rahisi sana kujua kilichotokea lakini yale majeraha ya ubavuni yalimuweka kwenye wakati mgumu sana.
Akaondoka na kuelekea Magomeni, alipofika, haraka sana akateremka na kuifuata nyumba hiyo. Majirani walikuwa wakimwangalia, kwa jinsi alivyokuwa akitembea, kila mmoja alijua alikuwa polisi.
Akaingia mpaka ndani, akaanza kuangalia huku na kule, alikuwa makini kabisa. Akaingia mpaka ndani ya chumba alichouawa Bi. Semeni na kuanza kuangalia huku na kule, kulikuwa na harufu kali ya dawa iliyopulizwa na polisi kuondoa harufu mbaya ya mzoga.
“Alichomwa kisu akiwa kitandani,” alijisemea huku akiendelea kuangalia chumbani mule.
“Ile mikwaruzo ubavuni aiipatia wapi?” alijiuliza huku akiendelea kukikodolea macho chumba kile.
Aliporidhika, akatoka na kusimama ukumbini. Sasa akaanza kujiuliza ni kwa namna gani muuaji huyo aliingia chumbani humo. Kuingia kwa mlango wa mbele, alikataa hilo, mara nyingi wauaji wanaokwenda sehemu fulani kufanya mauaji huwa hawapitii mlango wa mbele kwa sababu hawakutaka kuonekana.
“Labda alipitia mlango wa nyuma,” alijisemea na kuelekea uani.
Akaanza kuangalia huku na kule, kwa jinsi mazingira yalivyokuwa alikuwa na uhakika hapakuwa na mtu yeyote aliyeingia lakini kwenye kuangalia akauona ukuta ukiwa na alama fulani nyeusi, ilikuwa kubwa.
“Muuaji alipitia ukutani! Hii ni alama ya kiatu alipokuwa akiuparamia ukuta huu,” alijisemea huku akiwa ameusogelea ukuta na kuiangalia alama ile.
Je, nini kitaendelea

Kweli mkuu una shida ya network, nikajua kama wale wengineAsante kwa kunisaidia...nakuwa bize mno na huku network inazingua kishenzi. Nikiweka na endapo nikajisahau kuweka huku naomba unisaidie![]()
Mkuu inaonekana muoga kweli wa buku buku ...😁Kweli mkuu una shida ya network, nikajua kama wale wengine
Shukrani
usijali tupo pamojaAsante kwa kunisaidia...nakuwa bize mno na huku network inazingua kishenzi. Nikiweka na endapo nikajisahau kuweka huku naomba unisaidie![]()
Sikuwa na uoga huo mpaka nilipotapeliwaMkuu inaonekana muoga kweli wa buku buku ...![]()
Huko wapi? PoleHuku ni hatari...halotel sometimes mnara unazima kabisa