Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka

Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka

Huyu jamaa Kila siku nawambieni Apimwe Mkojo Na mavi maana Haelewiki kabisa
 
NYEMO CHILONGANI
UCHAWI WA BILIONEA BAZOKA
0718069269

SEHEMU YA 09.

Bazoka aliegesha gari pembezoni mwa Daraja la Manzese huku kichwa chake kikiwa na mawazo tele. Mtoto yule albino aliyekuwa amemchukua alikuwa ndani ya gari lake, alijiona kuwa mshindi zaidi ya watu wote ndani ya dunia hii.
Ilikuwa ni lazima amuue na kwenye kufanya hilo isingekuwa muda huo, ilikuwa ni jioni, alitakiwa kusubiri mpaka usiku ndipo afanye mauaji hayo na kutokomea zake.
Hakujua baada ya hapo ingekuwaje, alijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu na mwisho wa siku kuamua kumpigia simu Sultani kwa lengo la kumuuliza maswali mawili matatu.
“Imekuwaje?” alisikika Sultani akiuliza.
“Mzigo ninao hapa!” alimjibu.
“Mzigo gani sasa?”
“Huu wa mtoto, hivi nikifanya ile kazi natakiwa nipeleke chochote ama?” aliuliza.
“Hapana! Wewe fanya kazi na uondoke, yaani upande wa pili kila kitu kitakuwa kimekamilika. Kumbuka kila unapokwenda majini yanakufuatilia,” alisema Sultani.
“Sawa haina shida.”
“Kuna kingine!”
“Kipi?”
“Unakumbuka yale maneno ambayo unatakiwa kuongea kabla ya kutoa sadaka ya damu?” aliuliza.
“Nayakumbuka!”
“Basi usisahau kuyatamka!” alisema Sultani na kukata simu.
Mtoto yule albino alikuwa kimya ndani ya gari, hakuuliza swali lolote lile, alikuwa akifuatilia safari ile kana kwamba alikuwa akimfahamu Bazoka aliyeonekana kuwa makini sana.
Watu waliokuwa nje hawakuwaona, gari lile lilikuwa na vioo ambavyo havikumuwezesha mtu aliyekuwa nje kuona lililokuwa likiendelea ndani.
Pale Manzese alipolisimamisha gari lile watu walikuwa wakipita na kuendelea na safari yao lakini hapakuwa na yeyote aliyekuwa akifahamu hasa kilichokuwa kikiendelea.
“Msitu wa Pande,” alijisemea, hakutaka kuendelea kusubiri hapo, haraka sana akaliwasha gari lake na kuondoka hapo.
Alikuwa na kisu chake, alijiandaa kwa kile alichokuwa akihitaji, ilikuwa ni lazima afanikishe hilo kwani bado utajiri ulikuwa mtamu na ilikuwa ni lazima afanye juu chini kuhakikisha anaendelea kuwa na utajiri aliokuwanao.
Safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida, kutoka hapo Manzese mpaka ulipokuwa msitu wa Pande alichukua saa mbili kutokana na foleni, akafika huko huku tayari ikiwa ni majira ya saa moja usiku.
Barabarani hapakuwa na magari mengi, alipata nafasi ya kuendesha taratibu na kuingia ndani ya msitu huo. Mpaka muda huo mtoto yule alikuwa kimya kabisa, hakuzungumza lolote lile, ni kama aliwekewa madawa ya kishirikina asiweze kuzungumza lolote lile.
“Hapa panafaa!” alisema baada ya kufika mahali fulani ambapo kulikuwa na miti mingi, kichaka na gari lake lilikuwa la kwanza kabisa kuingia ndani ya eneo hilo.
Akateremka na kuanza kuangalia huku na kule, alihitaji kuona kama kulikuwa na usalama, alipaona panafaa hivyo kumteremsha mtoto Yusufu ambaye alikuwa kama zezeta, yaani hakuzungumza lolote lile wala kulia.
Ni kama Bazoka alibadilika, alikuwa mtu mwenye huruma tele lakini kitu cha ajabu baada ya kumchukua Yusufu na kwenda naye huko msituni huruma yote ikamtoka na kuwa na roho ya kinyama.
Hakutaka kuuliza hili wala lile, akamlaza chini na kuanza kumchinja huku akitamka maneno aliyokumbushwa na Sultani. Damu zikaanza kutoka shingoni mwa Yusufu, alitamani kupiga kelele lakini alishindwa kwani kisu kilikata koromeo lake na kulitoa kabisa.
Ulikuwa ni unyama mkubwa lakini kwa Bazoka mambo yalionekana kuwa kawaida kabisa, aliifanya kazi hiyo kwa uhakika wa asilimia mia moja, baada ya hapo akaifuta mahali pote alipopagusa na kuondoka zake huku akiiacha maiti msituni hapo.
***
Amina, mwanamke mzuri wa sura, aliyejaaliwa kuwa na umbo zuri alikuwa ndani ya kituo cha polisi cha Mburahati huku akionekana kuchanganyikiwa, alikuwa akilia kama mtoto, alimlilia mtoto wake ambaye mpaka muda huo, majira ya saa moja usiku hakuwa amerudi nyumbani.
Polisi walimwangalia, walimuonea huruma, walitamani kusikiliza kila kitu kilichotokea kwake lakini hakuwa akizungumza vizuri kwa sababu maneno na kilio vyote kwa pamoja vilikuwa vikitoka kwa pamoja.
Alijisikia uchungu, mtoto wake, Yusufu alikuwa mwanaye wa pekee, aliyekuwa akimpenda kuliko kitu chochote kile, leo hii hakuwa amerudi nyumbani, kwa taarifa za chini zilisema alikwenda kucheza na watoto wenzake, cha ajabu watoto wote walirudi majumbani kwao isipokuwa Yusufu tu.
Alikuwa akimfikiria mume wake, hakujua ni kwa namna gani angeweza kumwambia baada ya kutoka kazini, yaani aufumbue mdomo wake na kumwambia Yusufu alipotea, angeanzaje na wakati kila siku alionywa kutokumuacha nje hasa nyakati za jioni.
Polisi walichukua maelezo yake na hatimaye kuanza kumtafuta mtoto huyo, kila kona hakuwa ameonekana jambo lililowafanya kujiuliza zaidi juu ya mahali mtoto huyo alipokuwa.
“Au ametolewa kafara?” aliuliza polisi mmoja.
Mitaani hali ilikuwa mbaya, kupotea kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kulishamiri kila kona, watoto wengi wa hivyo walipotea na walipokuwa wakipatikana hawakuwa na baadhi ya viungo miilini mwao.
Hali ilikuwa mbaya kila kona na polisi walimshangaa sana Amina kwamba ilikuwaje amuache mtoto wake nje, yeye aendelee na mambo yake ndani na wakati watoto wa aina hiyo walikuwa dili kila kona?
Alionekana kuwa mzembe mno ila kwa kipindi kama hicho hakikuwa cha kumlaumu, ilikuwa ni lazima wampe moyo na kumwambia mtoto wake angepatikana, kama ni lawama, wampe baada ya kumpata na si kipidi hicho.
Mumewe aliporudi, akaitwa kituo cha polisi na kuambiwa kilichotokea, kwanza akakaa kimya, moyo wake ulimchoma na hasira kuwaka moyoni mwake. Hakuamini kama mkewe alifanya ujinga uleule ambao kila siku alikuwa akimwambia na kumuonya sana.
Alihisi kudharaulika, leo mtoto alipotea na haikujulikana mahali alipokuwa, moyo wake ulimchoka kupita kawaida.
“Yaani ilikuwaje?” aliuliza Iddi huku akimwangalia polisi.
“Taarifa zinasema alitekwa!”
“Na nani?”
“Watu wanasema kuna mtu alikwenda na gari, akamchukua na kuondoka naye!” alijibu polisi.
“Gari gani?”
“Ndiyo tunalifanyia uchunguzi! Tutakuja na majibu!” alijibu.
Iddi hakutaka kuongea na mkewe, na kwa siku kama hiyo hakutaka kabisa kurudi nyumbani, hasa baada ya kutoka kituo cha polisi. Moyo wake ulijeruhiwa, aliamini endapo angerudi nyumbani basi angemuua mke wake.
Akaelekea kwa rafiki yake, akamuhadithia kila kitu na kumwambia dhahiri hakutaka kurudi nyumbani kwa kuwa mkewe alimkasirisha, angeweza kumuua kwa uzembe alioufanya.
Upande wa pili polisi wakaanza upelelezi wao, mtu ambaye alichaguliwa kulifuatilia suala hilo alikuwa mpelelezi mashuhuri, Ashrafu Maganza. Ilikuwa ni lazima alifuatilie kwa undani mpaka kugundua kile kilichokuwa kimetokea,
Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kwenda mpaka Manzese, huko angechukua maelezo ya kutosha, kwenye hayo maelezo yote aliamini kungekuwa na kitu ambacho kingempa picha nzuri ya kuendelea na upelelezi huo.
***
Ni usiku wa manane, Frank alikuwa amelala na mke wake, Sara aliyekuwa na ujauzito. Hali ilikuwa ni ya ukimya kabisa, hapakuwa na kelele zozote zilizokuwa zikisikika kwa usiku kama huo.
Huku ukimya ukiendelea, ghafla Sara akaanza kupiga kelele za maumivu makali. Haraka sana Frank akaamka na kumwangalia mke wake, kwa siku hiyo ilikuwa ni tofauti, alipiga kelele kubwa na kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumwangalia vizuri.
Chini ya kitovu chake kulikuwa na damu na majimaji machafu, yalikuwa yakitoka mfululizo kitu kilichomfanya Frank kuogopa na kuona kama asingefanya juhudi za kumpeleka mkewe hospitalini basi kungekuwa na balaa.
Akamuinua na kumtoa nje, akaelekea sehemu ya Bajaj, akachukua moja, ikambeba yeye na mkewe na kuelekea hospitalini huku akiendelea kumpoza mke wake.
Kwa kelele zile alizokuwa akipiga Sara zilionyesha kabisa alikuwa kwenye maumivu makali, dereva alijitahidi kuendesha kwa kasi kubwa awahi hospitalini kwani alihisi endapo angechelewa basi mwanamke huyo angepata tatizo zaidi.
“Anataka kujifungua nini?” aliuliza dereva huku akionekana kuwa na hofu.
“Hii mimba ina miezi saba!” alijibu Frank.
“Miezi saba?”
“Ndiyo!”
“Mh! Basi kutakuwa na tatizo! Acha tuwahi,” alisema derva.
Baada ya dakika kadhaa wakafika katika Hospitali ya Mwananyamala, wakamteremsha na kumuweka kwenye machela iliyokuwa hapo na kuisukuma kuelekea ndani kabisa.
Huko manesi wakampokea na haraka sana kumpeleka katika chumba maalumu na kuanza kumfanyia uchunguzi kujua tatizo lilikuwa nini. Frank alikaa nje na dereva Bajaj ambaye hakutaka kuondoka mpaka kuona ni kitu gani kingeendelea mahali hapo.
Baada ya kama nusu saa dokta akatoka ndani ya chumba kile na kuwasogelea kule walipokuwa, alionekana kuwa na jambo zito alihitaji kuzungumza na Frank kabla ya kuendelea na mambo mengine.
“Mkeo alikuwa na tatizo gani hapo kabla?” aliuliza dokta huku akimwangalia, swali lake lilimfanya kila mmoja kushangaa kwani kwa kumwangalia tu alionekana kuwa na mimba.
“Hakuwahi kuwa na tatizo!” alijibu.
“Kabisa?”
“Ndiyo!”
“Na alianza kuvimba tumbo lini?” aliuliza dokta, swali jingine lililomshangaza kila mtu.
“Sijakuelewa dokta!”
“Nazungumzia tumbo!”
“Mke wangu ana mimba, ina miezi saba!” alijibu.
“Mkeo ana mimba?”
“Ndiyo! Si unamuona!”
“Hapana! Mkeo hana mimba!” alijibu dokta.
“Hana mimba?”
“Ndiyo! Hana mimba! Ni tumbo tu limevimba na ndiyo maana nilikuuliza mkeo alikuwa na tatizo gani hapo kabla!” alijibu daktari, jibu hilo likamfanya Frank kushtuka, hakuamini kuyasikia maneno hayo, ilikuwaje mkewe asiwe na mimba na wakati hapo kabla walikwenda kwenye hospitali mbalimbali na kuambiwa alikuwa na mimba, ilikuwaje leo aambiwe ni tumbo tu lilivimba? Hakika ilimshangaza.

Je, nini kitaendelea?
 
Mzee baba hii ni ya 8 au ya 9?
 
NYEMO CHILONGANI
UCHAWI WA BILIONEA BAZOKA
0718069269

Sehemu ya 10.

“Lakini daktari! Nilikwenda hospitalini na mke wangu, wakaniambia ana mimba, tena tulimpima, nilionyeshwa mpaka vipimo, mpaka mtoto kwa jinsi alivyokaa, na wakanitolea picha, nikamuona, sasa inakuwaje unaniambia mke wangu amevimba tumbo tu?” aliuliza Frank huku akionekana kushangaa.
“Una hizo picha ngumu?”
“Ndiyo! Zipo nyumbani!” alimjibu.
“Nenda kazichukue nizione,” alisema daktari.
Frank hakutaka kubaki hospitalini hapo, haraka sana yeye na dereva Bajaj wakatoka na kurudi nyumbani, njiani alikuwa na mawazo tele, alikuwa kimya huku akionekana kushangazwa na kile kilichokuwa kimetokea.
Ilikuwaje daktari amwambie mke wake alivimba tumbo na wakati alijua alikuwa na mimba? Tena si kwa kuambiwa tu, aliona mpaka vipo na picha ngumu ilitolewa ambayo ilionyesha jinsi mtoto alivyokaa tumboni.
Dereva Bajaj alitulia, hakuwa na cha kusema zaidi ya kushangaa, kile alichokisikia kwa daktari na kwa Frank kilimchanganya na hakujua nani alikuwa mkweli na nani hakuwa mkweli.
Safari iliendelea mpaka walipofika nyumbani ambapo moja kwa moja Frank akateremka na kuelekea ndani, chumbani kwake na kuchukua karatasi hiyo ngumu na kurudi ndani ya Bajaj.
“Si unaona...picha ilipigwa, mtoto huyu hapa,” alisema Frank huku akimuonyesha dereva ambaye naye alibaki akishangaa, alipomaliza kuangalia, akazichukua na kuziweka ndani ya bahasha na kuondoka mahali hapo.
Hawakuchukua dakika nyingi, wakafika hospitalini hapo, akaambiwa daktari alikuwa na kazi ya kumwangalia mgonjwa mwingine hivyo aliatkiwa kusubiri kwenye benchi, hilo wala halikuwa tatizo, akasubiri na dereva huyo.
Ni ndani ya robo saa tu akatoka na wote kwenda kumuona ndani ya ofisi yake, walipofika, wakakaa kwenye kiti na kuanza kuzungumza naye, kitu pekee alichotaka ni kujihakikishia kwa kile kilichotokea, alihitaji kupewa hiyo karatasi.
Halikuwa na tatizo, Frank akampa bahasha iliyokuwa na karatasi ile. Daktari akaichukua na kuanza kuifungua kwa ndani, akaitoa hiyo karatasi na kuanza kuingalia, aliiangalia kwa makini kabisa, akayarudisha macho kwa Frank.
“Sasa mbona sioni picha ya mtoto?” aliuliza daktari.
“Huoni picha ya mtoto?” aliuliza Frank huku akionekana kushtuka.
“Ndiyo! Iko wapi?” aliuliza huku akimpa karatasi ile.
Ni kweli! Frank na dereva walipigwa na mshangao, walipoiangalia karatasi ile ili kumuona mtoto aliyekuwa tumboni, hakuwa akionekana, yaani karatasi ilikuwa nyeusi tii.
“Inawezekana vipi?” aliuliza dereva, yaani hapo akagundua kulikuwa na mauzauza mengi.
“Picha ilikuwepo!” alisema Frank, alichanganyikiwa mno.
“Iko wapi?”
“Ilikuwa hapa!”
“Sasa mbona haionekani?”
“Sijui! Yaani....dereva, hata wewe si uliiona?” aliuliza Frank huku akimwangalia dereva ambaye naye alibaki kimya huku akiwa amepigwa butwaa.
Duniani kulikuwa na maajabu mengi, yaliyoshangaza lakini kwa hilo lililokuwa limetokea usiku wa siku hiyo ilikuwa ni balaa. Liliwaaminisha kuwa uchawi ulikuwepo kwani kupotea kwa picha ya mtoto aliyekuwa tumboni, halikuwa jambo la kawaida hata kidogo.
.Daktari hakutaka kuwaamini, jambo hilo hakuwahi kulisikia hata siku moja kwamba kulikuwa na taswira kwenye karatasi ngumu hospitalini halafu eti ghafla tu picha haikuwa ikionekana.
Alihisi kudanganywa, aliwauliza mara kwa mara kama kweli walikuwa na uhakika kwa kile walichomwambia, walisisitiza kwamba kweli hiyo picha ilikuwepo.
“Sasa iko wapi?” aliuliza kwa mara nyingine.
“Hata sisi hatujui!” walisema.
Daktari hakutaka kujali sana, hakuwaamini watu hao, alichokifanya ni kuendelea kufanya mambo yake, hasa kumuhudumia Sara aliyekuwa katika chumba cha mapumziko.
Baada ya kukaa kwa dakika kadhaa, akamruhusu kwenda kumuona mke wake, yeye na dereva wakaingia ndani na kumwangalia mwanamke huyo aliyekuwa kitandani.
Alimwangalia mke wake, alisikia maumivu makali moyoni mwake, hakujua mke wake angesemaje mara baada ya kumwambia tumbo lake halikuwa na mtoto bali lilijaa upepo tu.
Ni kama alimuona mke wake akilia kwa uchungu, hakuwa tayari kuona hilo likitokea, ilikuwa ni lazima kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mke wake anapata kile alichostahili kupata, kama alirogwa basi aliamini kulikuwa na watu waliokuwa hatari katika mambo hayo, hivyo naye alitakiwa kujipanga.
“Ni lazima nifanye kitu!” alisema huku akimwangalia dereva.
“Kitu gani?”
“Hivi unahisi kitu gani kimetokea?” alimuuliza.
“Yaani hata mimi nashangaa! Kwanza imekuwaje? Si pale tuliiona ile picha ya mtoto?”
“Ndiyo!”
“Sasa imekuwaje hospitalini haionekani?”
“Yaani ni mauzauza tu!” alisema.
Dereva alimwangalia Frank, kwa jinsi mwanaume huyo alivyokuwa alionekana kuhitaji sana msaada, alichomwambia ni kwamba asubuhi walitakiwa kwenda Chamazi kwa mtaalamu kwa ajili ya kuangalia tatizo lilikuwa nini.
Mara ya kwanza Frank alikataa kwani alimwamini Mungu lakini dereva alimwambia kama binadamu alitakiwa kujipanga, kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakipambana naye hivyo alitakiwa kujilinda kama wengine.
“Hivi unahisi watu wanakaa huru kwa sababu tu Mungu ameamua iwe hivyo? Watu wanawindwa sana,” alisema Frank.
“Najua!”
“Sasa kama unajua, unataka kujua kilichotokea kwa mke wako, basi huna budi kufanya nilichokwambia! Yaani ni lazima twende kwa mtaalamu kucheki!” alisema dereva.
Frank alikataa lakini mwisho wa siku akakubaliana na dereva huyo kwamba walitakiwa kwenda sehemu kucheki.
Asubuhi ilipofika hata kabla ya kwenda hospitali, dereva akampitia na kumwambia ampeleke huko Chamazi kulipokuwa na mtaalamu wake, hakutakiwa kuhusu mke wake, alimwambia hata kama angekwenda huko asubuhi hiyo bado angeambiwa tumbo lilivimba na hamukuwa na mtoto yeyote yule.
Akakubaliana naye na kuelekea huko, njiani Frank alikuwa na mawazo tele, alizaliwa huku akimwamini Mungu, hakuamini kwenye utalaamu wa kienyeji lakini hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kwenda huko.
Baada ya saa kama moja na nusu, hatimaye wakafika hapo Chamazi ambapo walianza kuelekea mahali nyumba ya mwanaume huyo ilipokuwa.
Walipofika, nje walikutana na watu wachache, wanaume kwa wanawake waliokuwa na matatizo yao binafsi. Walikaa kwenye moja ya mikeka iliyokuwa mahali hapo na kusubiri wengine wasubiri.
Kwa Frank hakuwa akiamini mambo hayo, hakujua kama kungekuwa na mtu ambaye angeweza kumroga mke wake na wakati hakuwa na uadui na mtu yeyote yule.
Mahali hapo watu walikuwa wakiitwa kwa zamu, ilipofika zamu yao, wakaitwa na kuingia ndani. Wakapitiliza na kukaa chini huku wakimwangalia mzee aliyekuwa mbele yao, alikuwa akiwaangalia kwa zamu.
Hakuzungumza nao kitu, alichukua karatasi nyeupe na kuandika maneno fulani ya Kiarabu kwa kutumia unyoya wa kuku uliolowanishwa na damu ya ndege huyo iliyokuwa kwenye kifuu kidogo pembeni.
“Unapitia kipindi kigumu sana Frank!” alisema mwanaume huyo baada ya kuyasoma maneno yale kwa dakika kama mbili hivi.
Frank akashtuka, hakuamini alichokisikia, hakuwahi kumuona mzee huyo, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona, kitu cha ajabu kabisa eti alikuwa akimfahamu jina lake!
Alilijuaje na wakati hiyo ilikuwa siku ya kwanza. Mzee huyo alibaki akitabasamu, alimwangalia Frank na kuona ni kweli alishtuka kwa kile alichokisema.
“Sara amechezewa! Yule bibi unayesikia ni mchawi ndiye anayefanya haya yote,” alisema mzee huyo, Frank akazidi kushangaa.
“Bibi gani?” aliuliza, alifanya hivyo kwa kuwa alitaka kuona kama mzee huyo angemfahamu.
“Bi. Semeni!”
“Daah!” alisema kwa masikitiko, huyo mzee alikuwa hatari sana.
Kila kitu alichokuwa akikisema mganga yule kilimshangaza, aliyajuaje yote hayo, ni afadhali angemwambia hapo kabla labda angesema kweli aliyafahamu kwa kuwa aliambiwa lakini kitendo cha kuambiwa na wakati hakuwa amemwambia kabla, tayari mzee huyo alionekana kuwa mtaalamu wa kweli.
Akamwambia matatizo mengi, alichomuhakikishia ni kwamba mimba ya mke wake ingerudi tena, ni ndani ya saa chache tu ila alitakiwa pia kupeleka dawa na kuifukia mbele ya nyumba ya bibi huyo, na kama si mbele, basi nyuma ama pembeni, yaani afukie mahali karibu na nyumba hiyo.
Akapewa dawa hiyo na kuruhusiwa kuondoka, alichomwambia mganga ni kwamba angefanya malipo mara baada ya kuona yale aliyomwambia yamefanikiwa.
“Utalipia baadaye ukishafanikiwa!” alisema mganga.
“Na hii dawa ni ya nini?”
“Hiyo ya kufukia?”
“Ndiyo!”
“Hiyo itakusaidia kutokuonekana kwenu mbele ya macho ya huyo bibi!” alimjibu.
“Sawa. Nashukuru!”
Hawakuendelea kubaki, wakainuka na kuondoka. Moyoni mwake alikuwa na imani kubwa, walipofika maeneo ya Kwa Azizi Ally simu yake ikaanza kuita, haraka akaichukua kutoka mfukoni, namba ilikuwa mpya na alipoanza kuzungumza, akaanza kuisikia sauti ya daktari, akaipokea.
“Niambie dokta!” alisema.
“Aisee kumbe kweli!” alisema daktari.
“Kweli nini?”
“Mkeo ana mimba! Ndiyo nimeiona hapa! Yaani sijui ilikuwaje! Upo wapi?” alisema na kuuliza.
“Njiani kuja huko!”
“Basi wahi, mkeo anakuulizia!” alisema na kukata simu.
Kwa mara ya kwanza ndani ya siku hiyo tabasamu likaonekana usoni mwa Frank hakuamini kile alichoambiwa. Akamwambia dereva, hata mwanaume huyo naye hakuamini, yule mganga alionekana kuwa kiboko ya matatizo yote.
Bajaj ikaendeshwa kwa mwendo wa kasi na baada ya dakika nyingi ikafika hospitalini. Frank akateremka na kuelekea ndani ya hospitali hiyo huku akimwacha dereva akiipaki Bajaj yake mahali salama.
Hatua zake zilikuwa haraka haraka mpaka ofisini kwa daktari na kuanza kuzungumza naye. Akaonyeshwa karatasi ngumu jinsi mtoto wake alivyokuwa tumboni mwa mkewe.
Machozi yakaanza kumtoka, hakuamini kama mimba ile ingeonekana tena, ila kubwa zaidi daktari akamwambia ili kuwe na usalama zaidi ilikuwa ni lazima mkewe afanyiwe upasuaji, mtoto atolewe.
“Kwa hiyo atakuwa njiti?” aliuliza.
“Ndiyo! Ila atakuwa salama!” alisema daktari na Frank kukubaliana naye.
Siku hiyo Sara alitakiwa kubaki hospitalini hapo akipatiwa matibabu. Alizungumza na mume wake ambaye muda wote alionekana kuwa na furaha tele. Walizungumza mengi na ilipofika usiku Frank akaondoka kuelekea nyumbani.
Kichwa chake kilikuwa kikifikiria ile dawa aliyopewa na mganga ambayo alitakiwa kwenda kuifukia karibu na nyumba ya Bi. Semeni. Hakutaka kuwa na presha, kwa kuwa ilikuwa majira ya saa mbili aliamini kulikuwa na watu wengi ambao wangemuona.
Alisubiri mpaka ilipofika majira ya saa sita ndipo akatoka huku akiwa na dawa yake. Aliangalia huku na kule, mtaa ulikuwa kimya kabisa, alitembea mpaka mahali kulipokuwa na nyumba ya mwanamke yule.
Alipofika, alipigwa na butwaa, hakuamini macho yake, aliangalia mahali aliposimama, nyumba haikuwepo, kulikuwa na uwanja mkubwa uliokuwa na makaburi kila kona.
Ilimuogopesha, kila siku alipokuwa akipita mahali hapo alikuwa akiiona nyumba ya Bi. Semeni, eti siku hiyo, tena muda wa kwenda kuifukia ile dawa, nyumba haikuwepo, kulikuwa na makaburi tu na miti ya mibuyu miwili mikubwa, hata nazo nyumba za majirani zilizokuwa mbele yake nazo hazikuonekana zaidi ya makaburi.
“Mh! Mbona kuna makaburi? Haya makaburi yametoka wapi?” alijiuliza huku akiweweseka, kile kilichokuwa kikionekana mbele yake, hakika kilimsisimua.

Je, nini kitaendelea?
 
Siwezi kuposti hadithi kila siku...na siwezi kuposti hadithi kila baada ya siku mbili. Apart from kuposti hadithi bado kuna mambo mengine ya maisha ya kuniingizia pesa inabidi yafanyike.
Nyemo utajibu kila mtu vingine potezea we weka story tu ukipata mda huwezi mridhisha kila mtu humu
 
Mkuu Nyemo nimefurahi kukuona uku mara nyingi inabid niingie fb kusoma simulizi zako nadhan kwa sasa nitakuwa mubashara...
Ombi langu ni moja fanya mpango account yako iwe verified na uwe na uzi maalumu wa story zako wafuatiliaji wengi huku...
Japo na wajuaji wapo pia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom