Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka

Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka

UCHAWI WA BILIONEA BAZOKA
MSIMULIAJI: HUSSEIN SANURA
IMEANDIKWA: NYEMO CHILONGANI
0718069269

Sehemu ya 07.

Alikaa kwa wiki nzima huku akiwasiliana na wenzake, Bonge na Sultani ambao walimwambia kuwa kutoa kafara halikuwa jambo gumu, katika kipindi cha kwanza kama hicho angeona kuna ugumu lakini baada ya kuzoea, kusingekuwa na ugumu wowote ule.
Walimtia moyo ili aone kile alichokuwa akienda kukifanya ni cha kawaida sana. Maneno yao yakamuingia, hofu aliyokuwanayo ikaanza kupungua na kujiaminisha kweli kile alichotakiwa kukifanya kilikuwa cha kawaida sana.
Baada ya siku mbili, akachukua kisu kile alichopewa, akakiweka ndani ya gari na kuondoka nyumbani. Siku hiyo alidhamiria kufanya mauaji aliyoambiwa kufanya. Hakutaka kujifikiria mara mbili, alilazimishwa kwa kuwa ndiyo ilikuwa njia mojawapo ya kumfanya kuwa na utajiri ule aliokuwanao.
Akaondoka na kuelekea Manzese, moyo wake ulidhamiria siku hiyo ni lazima atoe kafara ya kwanza na baada ya hiyo angezimalizia zile zilizokuwa zimebaki.
Alipofika maeneo ya Manzese Midizini akalipaki gari lake mbali kabisa na kuanza kutembea kuelekea mahali walipokuwa watoto wanacheza mpira.
Kabla ya kufanya kitu chochote kile akasimama na kuanza kuwaangalia watoto hao huku akiyasoma mazingira ya mahali hapo. Hakutaka kukurupuka, hakutaka kufanya vitu pasipo mahesabu.
Ilikuwa ni lazima auone urahisi ulikuwa mahali gani na kama angeamua kumchukua mtoto mmoja, je, kungekuwa na mtu aliyekuwa akimfuatilia au la? Alikuwa makini na kugundua mahali pale palikuwa na usalama mkubwa hivyo kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angemfuatilia.
“Kupo salama, ngoja nimfuate yule pale,” alisema na kuanza kumfuata mtoto mmoja aliyekuwa pembeni huku akiwaangalia wenzake wakicheza mpira.
Alipomfikia, akamsalimia, akaamkiwa na kusimama pembeni yake. Kwa kumwangalia mtoto yule, hakuwa na miaka zaidi ya kumi, akaanza kuongea naye stori za kitoto lakini mwisho wa siku alihitaji kutengeneza urafiki naye.
Hilo alifanikiwa, akaanza kuongea naye mfululizo huku akimuuliza maswali mengi tu ambayo mtoto huyo aliyajibu kitoto sana.
Hiyo ilikuwa mbinu ya kwanza lakini pia alihitaji kutumia pesa kwa kuamini kwa mtoto yeyote ingekuwa ni rahisi kuuteka moyo wake. Akaingiza mkono mfukoni na kutoa shilingi elfu tano.
“Unaishi na nani nyumbani?” alimuuliza huku akijitahidi kuachia tabasamu.
“Mama na baba!” alijibu mtoto yule.
“Unasoma wapi?”
“Magomeni!”
“Darasa la ngapi?”
“Darasa la nne,” alijibu mtoto yule huku naye akitabasamu, kila alipomwangalia Bazoka, akili yake ilimwambia alikuwa rafiki mzuri tu.
“Na unaitwa nani?” aliuliza.
“Hussein Madebe.”
Alizungumza naye kwa dakika kumi, wakawa marafiki wakubwa hivyo kumpa ile noti ya shilingi elfu tano na kuondoka zake. Alichohitaji ni mazoea tu, alijua fika inawezekana kabisa mtoto huyo alikuwa na rafiki yake aliyekuwa albino, alimuhitaji huyo hivyo kumpata kwa urahisi ilikuwa ni lazima kumtumia mtoto ambaye angekwenda kumwambia kuhusu yeye.
Akaondoka na kuelekea nyumbani kwake, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, mtihani aliopewa ulikuwa mkubwa lakini ilikuwa ni lazima afanikishe kwa kuwa hakuwa na jinsi.
Yalikuwa ni masharti makubwa ambayo yangeufanya utajiri wake kuchipukia na kuendelea kuwa mkubwa kila siku. Alijipa moyo kwamba kila kitu kingekuwa vizuri kabisa hivyo hakutakiwa kuwa na hofu hata kidogo.
Nyumbani hakuwa mzungumzaji sana, alimwambia mke wake kulikuwa na vitu vingi ambavyo kipindi hicho alikuwa akivishughulikia hivyo alikuwa bize sana.
Mkewe hakuwa na wasiwasi hata kidogo, ubize wake aliuona, hakuwa mtu wa kutulia hata kidogo, alipokuwa akifika nyumbani, alikaa kwa dakika kadhaa na kuondoka zake huku akionekana kuwa na haraka kupita kawaida.
Siku hiyo hakulala kwa raha kama siku nyingine, kichwa chake kilikuwa kikifikiria mtihani uliokuwa mbele yake. Siku iliyofuatia, akaamka na kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kufuatilia biashara zake.
Ziliendelea kuingiza pesa nyingi, alishangaa, mafanikio ambayo alikuwa akiyapata kipindi hicho yalikuwa makubwa mno. Aliheshimiwa, alikuwa na umri mdogo lakini kila alipopita alisalimiwa kwa heshima kama alikuwa mtu mzima.
Hilo ndilo alilokuwa akilitaka, kwake, alitamani kuona siku moja watu wakimuheshimu kama walivyokuwa wakifanya siku hiyo. Kila alipopita, aliitwa bosi na hakuchungulia mfuko wake, kila mtu ambaye alikuja kulia shida mbele yake, alimsaidia pasipo kuangalia alikuwa nani.
Wakati akiendelea kufanya hayo yote, akiheshimiwa kila alipokuwa akipita bado mguu wake uliendelea kuuma. Ulimkosesha furaha kabisa, kidonda chake kilikuwa kikubwa sana na wakati mwingine alipokuwa peke yake alikuwa akilia kwa maumivu makali.
Kidonda hicho hakikupona, kilitakiwa kuwa hivyohivyo mpaka siku ambayo alikuwa akiingia kaburini. Hakutaka kuhangaikia tena matibabu, aliamua kuachana nacho japokuwa mke wake mara kwa mara alimwambia kwamba wajaribu kwenda katika hospitali kubwa lakini hakutaka kabisa.
Ilipofika jioni ya siku hiyo, haraka sana akaingia ndani ya gari lake na kuelekea kule Manzese Midizini ambapo jana yake alijaribu kutengeneza urafiki na mtoto mmoja kwa kuzungumza naye na hata kumpa pesa.
Alipofika karibu na huko akatafuta sehemu ya kupaki gari lake, alipoipata na kufanya hivyo akaanza kuondoka kuelekea kule uwanjani. Alipofika, hakutaka kumfuata mtu yeyote, aliwaangalia watoto ambao walikuwa wakicheza mpira, akafanikiwa kumuona akiwa peke yake pembeni kabisa.
Akamfuata, alipomfikia, akaanza kuongea naye huku akijitahidi kutoa tabasamu pana. Mtoto yule alipomuona, akafurahi kwani alijua rafiki yake wa jana ambaye alimfuata na kumpa pesa alirudi tena.
Walikaa na kuzungumza mambo mengi, Bazoka alimwambia jinsi alivyofurahi kuonana naye lakini pia akamdanganya kwamba alitaka kukutana na rafiki yake mwingine ambaye alikuwa albino.
“Una rafiki yako albino?” alimuuliza.
“Ninaye! Anaitwa Yusufu! Unamtaka nikamuite?’ aliuliza Hussein.
“Hapana! Ila unaye?”
“Ndiyo!”
“Ni rafiki mzuri kwani?”
“Ni mzuri ila nyumbani kwao wanamkatazaga kutoka!”
“Kwa nini?”
“Eti watamuiba!”
“Ila wewe ukimwambia mtoke si mtatoka?”
“Eeeeh! Atakubali!”
“Basi njoo naye kesho! Halafu nitakupa hela na zawadi nyingine,” alisema Bazoka huku akiachia tabasamu kwani hakutaka kuonekana adui hata kidogo.
Alichokifanya ni kuondoka na kumwambia kesho yake aende naye pale kwani kulikuwa na sehemu alitaka kumpeleka ili wakifika huko wachukue zawadi nyingine na kurudi nyumbani.
Kwa kuwa mtoto Hussen hakuwa akielewa kilichokuwa kikiendelea, akakubaliana naye na kuondoka huku akimwambia afanye liwezekanalo wazazi wake wasijue kitu chochote kile.
Siku iliyofuata, akarudi mahali hapo na kukutana na Hussein, mtoto huyo alikuwa na mwenzake, albino ambaye alimwambia Bazoka kwamba huyo ndiye aliitwa Yusufu aliyekuwa akimuulizia na kumwambia kwamba leo aende naye mahali hapo.
Bazoka akaachia tabasamu pana kwani tayari aliona kufanikiwa kwa kile alichokitaka hivyo kazi ilikuwa kwake kuwachukua na kuwapeleka kule kulipokuwa na gari lake na kuondoka nao.
Hakutaka kwenda nao muda huo kwani kulikuwa na mwanga hivyo kama angefanya hivyo ilikuwa ni lazima kuonekana na watu wengine na hivyo kumtilia shaka. Akasubiri mpaka giza liingie ndiyo akawachukua na kuondoka nao.
Kwa sababu hakukuwa na mwanga wa kutosha, kwake ilikuwa ni afadhali kabisa kwani alifanikiwa kuwafikisha mpaka ndani ya gari na kitu cha kushangaza hakukuwa na mtu yeyote yule ambaye alishtukia kitu chochote.
Akaliwasha, kabla ya kuondoka, akamwambia Hussein akamnunulie maji dukani kwani alikuwa na kiu, kwa sababu mtoto huyo hakujua kitu chochote kilichokuwa kikiendelea akilini mwa mwanaume huyo na tayari alimuona kuwa rafiki, akakubaliana naye na kuelekea dukani.
Huku nyuma, Bazoka hakutaka kubaki, akaliwasha gari na kuondoka mahali hapo akiwa na Yusufu kuelekea njia ya Kigogo huku akimwambia mtoto huyo kwamba Hussein angekwenda kule walipokuwa wakienda wao.
“Atakuja! Huwa anakujaga pale mbele, tutamsubiri,” alisema Bazoka huku akionekana kushinda vita ya kile kilichokuwa kimempeleka mahali hapo, mtu wa kwanza ambaye alikuwa ni albino alikuwa ndani ya gari lake, kilichotakiwa kufanyika ni kumuua kama alivyoambiwa ili aendelee na mtu mwingine, bibi kizee.

Je, nini kitaendelea?
Je, Bazoka alifanikiwa kila kitu?
Tuonane siku Jumatano.
 
UCHAWI WA BILIONEA BAZOKA
MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI
0718069269

Sehemu ya 08

“Bibi mwenyewe yule pale,” alisikika mwanamke mmoja akimwambia mwenzake, sauti yake ilikuwa ni ya chini sana kama mtu ambaye hakutaka mwingine asikie.
“Kumbe ndiye yule?”
“Ndiyo! Usikaone vile, kachawi hako, kakikuangalia na macho yake tu, lazima ufe,” alisema mwanamke huyo na kutembea harakaharaka kana kwamba hawakutaka kuonwa na mtu waliyekuwa wakimzungumzia.
Kwa jina aliitwa Bi Semeni, alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na umri mkubwa waliokuwa wakiishi katika Mtaa wa Magomeni Makanya. Alikuwa mwanamke mwenye umri wa zaidi ya miaka themanini, katika maisha yake yote, hakuwahi kuwa na mume wala mtoto na tetesi nyingi zilizokuwa mtaani hapo zilisema aliwahi kuwa na mume, akamtoa kafara, si hao tu bali aliwahi kuwa na watoto lakini wote aliwatoa kafara.
Alikuwa mchawi, aliyewaroga watu usiku, aliogopwa kila kona hapo Makanya, katika nyumba aliyokuwa akiishi, hapakuwa na mtu aliyekuwa akiisogelea, japokuwa kulikuwa na vyumba vinne wazi lakini hakukuwa na mtu aliyethubutu kwenda kupanga.
Nyumba hiyo ilikuwa na mauzauza mengi, kipindi cha nyuma wakati watu wakiwa hawajui kuhusu uchawi wake, wapangaji walimiminika katika nyumba hiyo lakini kitu cha ajabu kabisa hakukuwa na mpangaji aliyekuwa akiishi zaidi ya siku tatu, nyumba ilikuwa na uchawi kwa kiwango cha juu kabisa.
Kila siku usiku wapangaji walichukuliwa na kupelekwa shambani kulima, walipoamka walichoka sana lakini ukiachana na hiyo, pia walikuwa wakiota ndoto mbaya na za kutisha, zile za kukimbizwa na majini au kupelekwa makaburini.
Kila mpangaji ambaye alisikia hayo yote yalisababishwa na Bi Semeni, hakukuwa na mwingine ambaye alitamani kuendelea kuishi hapo, akaondoka zake na kumuacha mwanamke huyo peke yake ndani ya nyumba.
Uchawi ndiyo yalikuwa maisha yake, kila siku usiku alikuwa mtu wa kwenda kuwanga akiwa uchi kabisa. Aliishi maisha ya peke yake, hakutaka kuona kukiwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akiishi ndani ya nyumba yake.
Usiku wa manane alichukua dawa zake na kuingia kwenye ulimwengu wa giza, akapanda ndani ya ungo wake na kwenda kuonana na wachawi wenzake.
Mtaani hapo kulikuwa na idadi ya watu wengi waliokuwa wakifa. Wengi walijua ni vifo vya kawaida, kulikuwa na wale waliopata ajali za kugongwa na magari au bodaboda, kulikuwa na watu waliokuwa wakiugua, wengi walirogwa na bibi huyo na kuonekana kama ulikuwa ni ugonjwa au ajali ya kawaida.
Bi. Semeni alipenda uchawi kuliko kitu chochote kile, katika maisha yake hakutaka kuona watu wakifanikiwa, wale waliokuwa wakihamia katika mtaa huo huku wakiwa na maisha mazuri, aliwaroga na kuwarudisha nyuma kabisa, zile biashara walizokuwa wamezifungua alizifunga na kufanya mambo mengine yasiyokuwa na maana.
Kwake, alijisifu, alipenda uchawi wake, aliwatisha watu wengi na wengine kumuogopa kama Mungu. Hakukuwa na aliyekuwa na thubutu ya kumwambia kitu chochote kile, hata wale waliokuwa wakimsalimia walimsalimia kwa sababu tu walimuogopa.
Siku nyingi zilipita hatimaye jirani na nyumba ya Bi. Semeni akahamia jamaa aliyeitwa Frank na mke wake aliyeitwa kwa jina la Sara.
Walikuwa wanandoa waliokuwa wakipendana mno, kila siku waliwaonyeshea watu kweli walipendana kwa mapenzi ya dhati. Wengi waliokuwa wakiwaona wakatamani mno kuwa na mapenzi kama watu hao walivyokuwa.
Kila walipokwenda, walikuwa pamoja, waliwaonyeshea watu katika dunia hii hakuna kitu ambacho kinaweza kuwatenganisha na kuachana kama walivyokuwa wanandoa wengine.
Sifa za kupendana kwao zilikuwa nyingi mitaani, zilisambazwa na hatimaye kumfikiria Bi. Semeni. Aliposikia, moyo ukamchoma, yeye kama mchawi hakutakiwa kuyafurahia maendeleo ya watu wengine, hakutakiwa kuona watu wengine wakifurahi.
Jukumu lake kubwa ni kuona watu wakikaripiana, wakigombana na hata kuwekeana visasi kwa sababu hiyo ndiyo roho aliyokuwa akiipandikiza shetani kwa watu wake.
Moyo wake ulimchoma mno, akatamani kufanya jambo, alihitaji kuwaona wakilia hivyo baada ya miezi kadhaa ikagundulika Sara alikuwa na mimba.
Hakutaka kuona watu hao wakiwa na mafanikio, wakipata watoto. Hiyo ilikuwa habari njema kwa wanandoa hao pasipo kujua katika mtaa huo waliokuwa wakiishi kulikuwa na mtu ambaye hakupenda kuwaona wakiwa na furaha, wakiishi maisha waliyokuwa wakiishi.
Alichohitaji bibi huyo ni kuwaona wakilia hivyo kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuichezea mimba hiyo. Kila siku usiku alikuwa akiondoka chumbani kwake kimazingara na kuelekea ndani ya nyumba ya Frank. Aliwakuta wamelala, alimfuata Sara na kumuweka kitako kisha kutoweka naye huku pale kitandani akiliacha gogo lililokuwa na muonekano kama wa mwanamke huyo.
Alihitaji kumchosha kwanza, alimpeleka sehemu iliyokuwa na msitu mkubwa na kumuweka katikati. Alibaki akimwangalia, uzuri wa Sara ulimkasirisha, hakumpenda mwanamke huyo hivyo kuchukua dawa fulani nyeupe iliyokuwa kama unga na kuipata tumboni mwa Sara huku akiongea maneno yasiyoeleweka.
Alipomaliza, akamchukua na kumkalisha kitako, akaanza kumchezea ngoma ambazo hazikusikika, akaanza kuimba huku akiyasugua makalio yake usoni na tumboni mwa mwanamke huyo na alipomaliza, akamchukua, wakapotea na kutokea chumbani kwake, akamuweka pembeni ya mumewe na yeye kuondoka.
Asubuhi ilipofika, Sara aliamka huku akisikia maumivu makali ya tumbo. Hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea, pale kitandani alipokuwa akaanza kupiga kelele.
Frank akaamka na kumwangalia mke wake, alimwambia alisikia tumbo lilkikata, yaani kama kulikuwa na mtu ambaye alishika wembe na kuanza kulikatakata.
“Pole sana! Amka twende hospitalini,” alisema Frank huku akimuinua Sara.
Ilikuwa ni asubuhi sana lakini kwenye jambo hilo hakutaka kupuuzia, haraka sana akamchukua na kuondoka naye kuelekea hospitalini.
Njiani, Sara alikuwa akilia, maumivu hayakupungua, aliendelea kuhisi kama utumbo wake ulikuwa ukikatwakatwa. Hawakuchukua muda mrefu, wakafika hospitalini na kumpeleka katika sehemu ya matibabu na kuanza kutibiwa.
Ulikuwa ni uchawi, hata daktari alipoangalia tatizo, hakuona kama kulikuwa na chochote kile, tumbo halikuchafuka, hata yeye alipoambiwa na Sara kwamba alikuwa na maumivu makali, alishangaa yalikuwaje na wakati tumbo lilionekana kuwa sawa, na hata mtoto ambaye alianza kutengenezwa hakuonekana kuwa chanzo cha tatizo hilo.
“Lilianza kuuma muda gani?” aliuliza daktari.
“Asubuhi ya leo, linauma sana,” alijibu Sara.
“Pole sana! Nitakupa dawa za kwenda kutumia,” alisema daktari na kumuandikia dawa ambazo alikwenda kuzichukua kwenye kidirisha kidogo na kuondoka mahali hapo.
Frank alirudi na mke wake, Sara mpaka nyumbani na kuanza kuzitumia dawa hizo. Tumbo halikuacha, liliendelea kuuma ila ilipofika majira ya jioni likaacha.
Alichokiamini dawa zilianza kufanya kazi, aliamini hivyo kwani mabadiliko hayo yalianza kutokea baada ya kuzinywa. Maisha yaliendelea, hawakujua kama kwenye kila kitu kilichokuwa kikiendelea ni Bi Semeni ndiye aliyekuwa akihusika kwa asilimia mia moja. Hawakumjua bibi huyo vizuri, kwao waliona ni jambo la kawaida tu kumbe upande wa pili kulikuwa na harakati za mwanamke huyo ambaye hakupendwa mtaa mzima kutokana na uchawi wa kuwatesa watu wengine mahali hapo.
Baada ya kupita wiki moja huku tumbo likiwa linauma na kuacha, Sara akaamua kuanza safari zake za kliniki huku akisindikizwa na mume wake aliyejitoa kwa asilimia mia moja kwa ajili yake.
Wakati siku zikiendelea kwenda mbele ndipo akapewa taarifa kwamba inawezekana kabisa mke wake alikuwa akiumwa tumbo kwa kuwa waliishi karibu na bibi aliyekuwa akisifika kwa kuroga watu.
Hilo halikuingia kichwani mwa Frank hata kidogo, hakuamini katika ushirikina, kwa sababu hakuwa amegombana na mtu yeyote yule aliamini alipendwa na wote pasipo kujua wachawi walikuwa na mchezo wa kuwachukia watu hata kama hawajafanyiwa jambo baya lolote lile.
Mifano iliyohai ipo mitaani kwetu, unaweza kumsaidia mchawi pesa kwa sababu umemuona akiishi maisha ya tabu lakini anachokifanya ni kuichukua ile pesa na kwenda kuiroga ilimradi tu usifanikiwe tena.
“Haiwezekani! Yule bibi? Hapana, nakataa,” alisema Frank huku akimwangalia mwanaume aliyempelekea taarifa kuhusu Bi. Semeni.
“Kaka! Yule bibi ni nuksi sana! Niamini,” alisema kijana huyo aliyeitwa kwa jina la Ibrahim.
Frank aliendelea kubisha, alimfikiria Bi Semeni, alikuwa mwanamke mzee, mpole ambaye hakuwa na nguvu hata ya kutembea kwa mwendo mrefu akiwa peke yake.
Kwake, kuambiwa kwamba bibi huyo ndiye alikuwa nyuma ya kila kitu alibisha na kumwambia Ibrahim kile alichokuwa akimwambia hakikuwa na ukweli hata kidogo.
Kijana huyo hakutaka kubishana naye, alichokifanya ni kuondoka na kumuacha Frank hapo alipomkuta. Hilo jambo hakutaka kulipuuzia, akamshirikisha mkewe, Sara lakini kwa staili ya kumtetea bibi huyo aliyekuwa akitisha kwa uchawi.
“Eti Sara! Kale kabibi kanaweza kuroga watu kweli?’ aliuliza Frank, kwa jinsi swali lake alilouliza, aliweka kipengele kimoja cha kuambiwa hapana.
“Mh!”
“Ndiyo nimeambiwa hivyo! Ila nimekataa! Hizi ni dhambi nyingine za kujibebea mpenzi,” alisema Frank.
Wote wawili waliamini hivyo Bi. Semeni hakuwa na uwezo wa kuroga kutokana na muonekano wake ulivyokuwa. Hawakujua kama kile walichoambiwa ndicho kilikuwa ukweli wenyewe.
Walimuamini kutokana na muonekano wake lakini hawakujua kile kilichokuwa ndani yake. Kila walipokuwa wakimuona kwao mwanamke huyo mzee alionekana kuwa mtu mstaarabu kuliko watu wengine.
Watu waliokuwa wakimfahamu Bi. Semeni hawakutaka kukaa kimya, walichoamua kilikuwa ni kumwambia Frank ukweli juu ya mwanamke huyo jinsi alivyokuwa msumbufu mtaani hapo.
Franck alipoambiwa, akabisha, kwake ilikuwa ni vigumu kuamini kama Bi. Semeni alikuwa mchawi, kwake alionekana kuwa mwanamke dhaifu ambaye asingeweza kufanya mambo ya kilozi hata kidogo.
“Tatizo unabisha sana...” alisema mwanaume aliyekuwa akimwambia Frank.
“Bibi yule awe mchawi?”
“Kwani inashindikana vipi?”
“Jamani! Yaani yule bibi awe mchawi! Hilo jambo haliwezekani!” alisema huku akiwa na sura ya kubisha kabisa.
“Labda kwa kuwa humjui! Uliza mtaani uambiwe,” alisema kijana huyo.
Mpaka wanaachana Frank hakuwa amemwamini na ndiyo kwanza akaenda kumwambia Sara. Mwanamke huyo aliposikia, hakubisha wala hakukubali, kwake moyo wake uligawanyika, upande mmoja uliamini lakini upande mwingine ulibisha.
“Eti jamani yule bibi ana uchawi gani? Yaani wanataka kuniambia kila mzee ni mchawi? Watu wana dhambi sana,” alisema Frank huku akimwangalia Sara.
“Kwani wamesemaje?”
“Eti yule bibi mchawi!”
“Bibi gani?”
“Yule tunayemuonaga pale nje anasuka ukiri!”
“Yule bibi?”
“Ndiyo! Eti mchawi!” alisema Frank.
Sara hakumwambia kitu lakini kwa kile alichoambiwa ni kama kilibadilisha kila kitu kwake, akaanza kuogopa kila alipokuwa akikutana na Bi. Semeni, kijasho kilikuwa kikimtoka na mwili kumsisimka.
Hali ilibadilika kabisa na hata usiku alipokuwa akilala alikuwa na hofu kubwa, wakati mwingine alikuwa akishtuka huku akitetwa jasho lilimfanya mume wake kushangaa.
“Kuna nini?” aliuliza Frank.
“Ndoto mbaya!”
“Ni ndoto tu mke wangu! Lala mpenzi,” alisema lakini Sara hakuwa akipata usingizi tena, moyo wake ulikuwa na hofu tele, na kila alipokuwa akishtuka usiku, mtu wa kwanza kumfikiria alikuwa Bi. Semeni.

Mbona kama umechanganya mafaili mkuu
 
Huyu jamaa Kila siku nawambieni Apimwe Mkojo Na mavi maana Haelewi kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom