Hadithi; The girls in island-05

chiqutitta

JF-Expert Member
Nov 13, 2015
1,160
3,124
SEHEMU YA TANO
THE GIRLS IN ISLAND 05





“swali zuri sana,… ninapoongelea wanawake ni tofauti sana na wanawake hawa wa duniani. Kwanza hamshangai kuwa wanaishi jinsia moja katika hicho kisiwa na hakuna mwanaume. Vipi wanazaliana na kuwa na rika kuanzia watoto mpaka vijana. Tofauti yao nyingine na sisi ni kwamba hawazeki. Narudi kwenye swali nililoulizwa, watu wanashidwa kuwaridhisha wasichana hao kutokana na muda wa kufanya mapenzi kwa viumbe hao. Hutumia masaa tisa kwa uchache mpaka kufika kileleni. Sasa unafikiri binaadamu wa kawaida unawezaje kumudu kukaa juu ya kifua cha msichana kwa masaa yote hao bila kupumzika?” aliongea Hija na kuwafanya waandishi wa habari wagune.

Songa nayo:



“najua mtakua na maswali mengi ya kuniuliza kama sitawaeleza kinaga ubaga juu ya safari yangu ya kisiwa hicho. Nakumbuka ilikua…………



******************



Ni siku nzuri iliyokua na kila kitu kilichonifanya niite kuwa siku hiyo ni nzuri baada ya kuamka bila ochovu. Pia nilikua na mzuka sana wa kufanya kazi siku hiyo.

Sikuona uvivu wa kwenda kijiweni kwetu feri kwa ajili ya kwenda kuangalia mitego yetu baada ya siku mnbili nyuma tulipoenda kutega samaki wakubwa kwenye kina kirefu baharini.

Nilipofika tu feri, nilikutana na marafiki zangu na kila mmoja alikua na tabasamu baada tu ya kuniona.

“inakuaje mwanangu.. naona leo umetokelezea.” Aliongea rafiki yangu mmoja anayeitwa BOKKER.

“acha utani bwana, kwa mchomoko gani huu mpaka uniambie kuwa nimetokelezea… waliotokelezea huwaoni bwana.” Niliongea na kumuonyeshea rafiki yangu mwengine ambaye alishavua nguo zake na kuvaa nguo za kazi ambazo zilikua chafu.



“ahsante kwa matusi Hija.” Aliongea yule rafiki yangu na wote tukacheka.

Kwakua wote tulikua hatujapata kiamsha kinywa, tukaona ndio muda muafaka wa kwenda kunywa chai kwa mama Chaddy.



“mama chaddy… leo ndio utachagua ni nani mwanaume wako wa kweli, maana timu imetimia leo hii.” Aliongea rafiki yangu mwengine anayeitwa AMANI.

“Mwanaume wangu wa kweli ni pesa tu, mwanye nazo huyo ndio mwanaume wangu wa ukweli.” Alijibu mama Chaddy huku akiendelea kutu miminia chai.

“mimi nipe Suzy tu nikutunzie.” Nilimtania mama Chaddy huku Suzy akiwa ananipimia maharage.



“niachieni mwanangu, bado anasoma huyu.” Aliongea mama Chaddy na kunipatia chapati zangu kwenye sahani ya bati.

“sasa mama chaddy,mimi ndio bosi wa oda yote hii. Inakuaje unaniwekea kwenye sahani ya bati?.. lete sahani ya udongo.” Niliongea huku nikijitanua ilimradi tu wenzangu wapate kucheka.



“haya bosi mkuu.” Aliibu mama Chaddy na kwenda kuniletea hiyo sahani ya udongo.

Tulikunywa chai na mimi nikalipa oda yote hiyo iliyonigharimu kama shilingi elfu saba na mia tano kwa watu wote watano tuliokunywa chai pale kwa mama Chaddy.



Baada ya kushiba, tulikwenda kwenye boti yetu yenye hadhi kidogo kuliko boti zote za pale kijiweni kwetu. Japokua boti nyingi zilikua na injini, lakini yetu tulifunga injini mbili kutokana na ukubwa wa boti yetu.



Tulianza safari huku nahodha nikiwa mimi mwenyewe tayari kwa kwenda kuchukua kilichopatikana baharini.

Safari ilianza taratibu huku kila mmoja akiwa ananipigisha stori zake. Wengine walikua wananipigia story za mademu zao ilimradi tu kusogeza muda ili tufike safari yetu ambayo ilitumia masaa mengi kufika huko.



Tulikata maji kwa spidi ya ajabu na kufika eneo tulilokua tumetega nyavu zetu. Cha ajabu hatukuziona zile nyavu. Hata baada ya kuhangaika kwa muda mrefu hatukufanikiwa kuziona.

Tulisogea mbele zaidi lakini pia tuliambulia patupu. Kwa mbali tulikiona kisiwa kidogo kikiwa kina miti mingi ya rangi ya kijani.



“kuna uwezekano waliotuibia nyavu na samaki wetu wanatoka kwenye kile kisiwa.” Aliongea SAIDI

“labda, ila mbona huwa tunafika hapa kila siku na huwa hatukioni hiki kisiwa?.. au nyangumi yule amelala pale?” aliongea Bokker na kutufanya wote tuliokuwa pale kumcheka.

“nyangumi gani anakuwa na miti?.... acha ushamba bokker” nilimchana live Bokker na wote tukaendelea kumcheka.



“sasa tunafanyaje?... maana tumechoma mafuta mpaka huku.” Aliongea PHILIPO.

“Itabidi twende tu kwenye kile kisiwa. Ili mradi ijulikane tu tumekuja kutalii maeneo haya.” Alongea Amani na kuungwa mkono na watu wote tuliokua pale.



Tuliwasha chombo chetu na kwenda mpka kwenye kile kisiwa na kupaki boti yetu. Lakini kwe mbele kidogo tulioana boti zipatizo sita zikiwa zimepaki maeneo mbali mbali.

Kila mmoja alikua anashangaa jinsi miti hiyo ilivyokuwa mirefu. Tulizama kwenye huo msitu taratibu huku tukifuata nyayo zilizokuwa pale chini. Tulitembea kwa mwendo wa dakika ishirini hivi, tukaona watu mbele yetu wakiwa wanahangaika kulisukuma jiwe kubwa la dhahabu ambalo lilkua limeziba mlango wa pango.

Watu walikua wengi tena kutoka mataifa mbali mbali. Ila tulishangaa kuona walikua ni jinsia moja tu. Wote tulikua wanaume. Hapo ndipo nikakumbuka kua tulikua tumefika kwenye kisiwa cha wanawake ambacho nilihadithiwa tu na babu yangu kuwa hicho kisiwa ni cha ajabu na hakuna aliyekwenda akarudi zaidi ya mtu mmoja tu. Tena mwana sayansi wa siku nyingi aliyegundua madini ya Rubbi.

Tulifika pale na kuwasalimia kwa luhga ya Kiswahili na wao wakatupa ishara tu ya mikono kuashiria kuwa walikua hawaelewi tuongeacho.



Tuliamua kuungana nao kulisikuma lile jiwe lakini halikufunguka. Mpaka kiza kikatufikia pale pale tukiwa tunahangaika kulisikuma lile jiwe ambalo lilikua limeziba njia na ndani yake kulikua na watu waliokua wanalia kuomba msaada.



“tuondokeni jamani.” Niliwaambia wenzangu kwa Kiswahili na kunielewa wachache tu kwakua wengi walikua wachina na wazungu.

“poa” waaliitikia na wote tukageuza na kurudi tulipotoka. Tulipofika kwenye fukwe za

Bahari ya kisiwa hicho, lakini cha ajabu zaidi hatukuona boti yoyote iliyokuwepo pale. Tulichanganyikiwa sana na hatukujua ni vipi tutaondoka kwenye ksiwa hicho.



“tatafanyaje jamani na usuki huu?” niliwauliza wenzangu ambao nao walionekana wamechoka kama mimi.

“turudini tu tuungane na wenzetu, maana hatujui nani aliyezichukua boti zetu.” Aliongea Bokker na wote tukaungana nae bila hata kujiuliza mara mbili wala kujadiliana.



Tulirudi tena msituni huku safari hii kila mmoja akiwa amejawa na uoga usioelezeka.

Tulipfika pale wenzetu walipokuwepo, hatukuwaona tena na lile jiwe lilikua pembeni huku pamgo likiwa linaonekana kuwa na mwanga ndani.

“si bure, kutakua na majini eneo hili.” Aliongea Amani na kutuangalia kwa zamu.

“jamani msiwataje hao viumbe, maana hawatajwi maeneo kama haya.” Aliongea Phalipo aliyeonekana kuwa muoga kuliko sisi wote tuliokuwepo pale.



“tufanyeje sasa, maana mimi naona kama kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha kama tukiendelea kuwa hapa.” Niliwaambia wenzangu ambao wote walisisimka nilipogusia swala la kufa.

“mi nashauri tuingie tu kwenye hili pango.” Aliongea Amani.

“yaani kati ya wajinga wewe unaongoza kwa ujinga. Wewe si uliona kuwa watu walioingia humu walikua wanaomba msaada wa kutoka humu.” Aliongea Bokker.

“sasa wale watu waliokuwa wanahangaika kufungua hili jiwe unafikiri wameenda wapi?” aliuliza Philipo.

“wameingia humu baada ya kufanikiwa kuisukuma hili jiwe… au kuna mtu ana mawazo mengine tofauti na mimi?” nilijibu hilo swali la Philipo kwa kujiamini kidogo ili mawazo ya kifo yaondoke moyoni mwangu.



Kila mtu alikubaliana na mimi ingawaje nilijua kuwa kila mtu atakua na mawazo yake tofauti kichwani mwake. Tulingia kwenye lile pamgo huku kila mmoja akimuomba Mungu wake amjaalie usalama wa safari yake ambayo hata hakuijua mwisho wake.

Tuliingia kwenye lile jiwe huku tukiwa makini huku kila mmoja akiwa na uoga wa kushika chochote japokua tuliyaona madini mengi yakiwa yanawaka mle ndani. Tufanikiwa kutokea upande wa pili wa lile pango na kukuta kumekucha tayari. Tulishangaa sana kwakua tulijua kuwa tumetumia masaa matatu tu mule ndani.

Lakini tulishikuru pia kwakua mahala hapo palikua panatisha sana usiku.

Urefu wa miti iliyokuwepo upande wa pili, ulinifanya nikumbuke maelezo ya mwanasayansi Mac Donald kwenye kitabu chake nilichowahi kusoma zamani nilipo kwenda maktaba ya taifa wakati nasoma shule ya msingi. Kitabu hiko kilielezea kuanzia fukwe hizo zilivyo,lile jiwe la dhahabu na pango. Pia miti hiyo ambayo imeelezewa ilikua inafanana kabisa na niliyokua naiona mbele yangu.

Hapo ndipo nikaamini kuwa tulikua kwenye kisiwa cha wanawake kilichokuwa kinaelezewa kwenye kitabu cha THE GIRLS IN ISLAND.



Hapo hata mimi nikaanza kuogopa upya kwakua kisiwa hicho kilikua na wasichana waliokuwa na hamu muda wote wa kufanya mapenzi. Pia walikua wanatumia muda mrefu kufika kileleni. Hapo mawazo ya kufaulu mtihani huo yalinifanya nishikwe na kitete huku nikipunguza hatua zangu za miguu nilizokua napiga kuelekea mbele.



“vipi Hija?” aliuliza Booker baada ya kugeuka nyuma na kugundua kuwa walikua wameniacha umbali mrefu kidogo.

“hamna kitu.” Nilificha na kuongeza hatua za miguu yangu na kuwakuta baada ya wote kusimama na kunisubiria maeneo hayo.



“vipi kamanda, mbona unatutisha?” aliuliza Bokker baada ya kuwafaikia walipo.

“hamna kitu,.. ni mawazo tu ya hapa na pale katika kutafuta njia ya kutoka kwenye kisiwa hiki.” Niliongea na kuendelea mbele ilimradi tu safari iendelee kwakua walishaweka kituo pale.

Mbali na kukaa muda mrefu, lakini hakuna aliyelalamika njaa. Tuliendela kukata pori hilo huku tukiomba Mungu tusikutane na wanyama wakali.



Baada ya mwendo mrefu, tuliona mwisho wa msitu huo na mbele yake kulikua na majani mafupi kama yaliyolimwa. Tukakazana mpaka tukafika eneo hilo. Hatukuamini macho yetu baada ya kufika eneo hilo. Tulizisikia kelele za watu na baada ya kusogea eneo hilo tuliona viumbe wa ajabu wakiwa uchi huku maziwa na nyeti zao ziikionyesha kuwa walikua jinsia ya kike.

Walikua wanawavua nguo watu waliowakamata na kuwarusha kwenye sufuria kubwa sana lilikua na uwezo wa kuigia hata watu kumi na tano. Lilikua na maji ya moto yaliyochemka vibaya huku viumbe wengine wakiendelea kukoka moto kwa miti mikavu.



Hapo kila mmojaa alibaki ametoa macho huku mioyo yetu ikidunda kuliko kawaida. Bila hiyari yangu, nikajikuta mwili mzima umetokwa na vipele vya baridi na macho yangu yakiwa yanatoka machozi kutokana na mpasuko wa moyo niliokuwa nao baada ya kuona mtu akipikwa huku akiwa hai.
 
Duu nzuriiiii enhee mkuu ikawaje
Mkuu ungezionganisha hiZi hadithi ktk uzi moja ingekua poa sanaa
Wapenda story tupo lete mambo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom