Hadithi tamu: Hisia zangu

duhhhhhhhhhhhhhhh..kazi kwelikweli.......mpaka lin tena..???
 
Miaka miwili si mchezo!!!!!!


Jamaa watabandua kizibo tu..........
 
duhhhhhhhhhhhhhhh..kazi kwelikweli.......mpaka lin tena..???
Nitajitahidi niwe naiwweka Jumapili maana Ijumaa na Jumamosi nimepata kazi inayoniweka bize sana, samahani sana kwa wote niliowakera.
 
Njoo endelea bac na hii kitu bac maana naona unatuacha na genye muda mrefu sana..








 
[MENTION]
Mommadou Keita[/MENTION]

Mbona hivyo tena kimya kinatisha!!!!!!!!


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Achana na huyu wewe twende tukamalizie kule kwa kina cecy na colin


[MENTION]
Mommadou Keita[/MENTION]

Mbona hivyo tena kimya kinatisha!!!!!!!!


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Achana na huyu wewe twende tukamalizie kule kwa kina cecy na colin


Sawa Mkuu;

Nilikuwa namfuatilia huyu nijue kijana EDO amefikia wapi;


Kwa kweli mtu kuahidiwa miaka miwili ni ngumu sana kumuamini kulinda penzi.
 
Edo, pole yako ungekomaa ukakata seal mwenyewe, ningekuwa mimi ningelia mpaka nikaikata. ona sasa!
 
Inaonekana itakuwa nzuri,hebu ngoja nianze kuifatilia
 
daaah! kiukwe hadithi hizi zinanifanya nipoteze mawazo kabisa
 
ILIPOISHIA...
Hello,
Edo. Najua umefika salama mpenzi wangu. Pole na safari baba. Napenda kukuhakikishia kuwa, moyoni mwangu umejaa wewe pekee na hakuna nafasi ya mwingine zaidi yako. Nakupenda sana.
Ukipata ujumbe wangu, tafadhali unijibu.
Lilian.
Edo akavuta pumzi ndefu sana kisha akazishusha taratibu kabisa. Akatulia kwa muda. Baadaye kidogo akafungua ujumbe unaoufuata.
Ujumbe huo ndiyo uliomshtua sana moyo wake. Aliuma meno kwa nguvu, akarudi kuangalia jina na anwani ya mtu aliyemtumia ili ajiridhishe kuwa Lilian ndiye aliyemtumia.
Ni kweli alikuwa ni Lilian!
Akazidi kuchanganyikiwa!
SASA ENDELEA...

ALITEMBEA kwa maringo yaliyoonekana wazi. Hayakuwa ya kutafuta. Lucy alijua alivyo mrembo, hivyo kuonyesha maringo ilikuwa kichagizo cha jinsi alivyo.
Wanafunzi wengine walikuwa wakimkodolea macho wakati akitembea taratibu akionekana asivyo na haraka na alipokuwa akielekea. Ni kweli hakuwa na haraka maana safari yake ilikuwa inaishia hosteli.
Pamoja na uzuri wa umbo lake, pia mavazi yake yalimshawishi kila mwanaume aliyekamilika kumwangalia kwa uchu wa mahaba mazito.
Kwa mwanaume mkamilifu, ingekuwa vigumu sana kwa Lucy kupita mbele yake bila kukata shingo kumwangalia. Lucy alizawadiwa urembo wa kutosha!
Alitembea hadi alipofika kwenye barabara kubwa ya lami, akasimama kupisha magari yapite kisha akavuka na kupanda kijimlima kidogo kuelekea hosteli.
Alipofika chumbani kwake, alijitupa kitandani, kisha akajilaza kwa mgongo na kuyarusha mcho yake juu ya dari na kuanza kuwaza...
“Siwezi kushindwa kumshawishi Lilian. Ni mtoto mdogo sana. Mimi namuweza. Hanishindi kwa lolote,” akawaza.
“Lazima aingie kingi,” akajisemea kwa sauti.
“Huyu mtoto mdogo tu kwangu, anajifanya ana msimamo. Itakuwa yeye...hapa Bongo akili kichwani.”
Lucy alikuwa kwenye lindi zito la mawazo. Kikubwa kilichokuwa akilini mwake ni milioni tano alizoahidiwa na mzee mwenye fedha zake, mfanyabiashara mkubwa jijini Dar es Salaam, Pamseck Kinga.
Kinga hujulikana zaidi kwa jina la Pam. Kazi aliyopewa na Pam ni kuhakikisha anamuingiza Lilian kwenye himaya yake. Kwa kuanzia Pam alimpa shilingi milioni moja kwenye bahasha ili ampelekee Lilian.
Fedha kwake ilikuwa siyo shida, tatizo kubwa lilikuwa matumizi tu!
Lucy akiwa bado yupo mawazoni, akifikiria mbinu nyingine mpya ya kumnasa Lilian kiulaini, simu yake iliita. Alipoangalia kwenye kioo akakutana na jina la Pam. Haraka akapokea.
“Nategemea kusikia kitu kizuri kutoka kwako, haya niambie,” sauti ya Pam iliunguruma simuni.
“Mh! Pam mbona una haraka sana baba?”
“Lazima niwe na haraka. Namtamani sana huyo mtoto. Niambie umefikia wapi?”
“Hatua nzuri.”
“Hatua nzuri siyo?”
“Kabisa.”
“Nataka kujua kitu kimoja kwanza; amechukua huo mzigo?”
“Ndiyo lakini kwa kumlazimisha sana.”
“Anajua ulipotoka?”
“Hapana, lakini lazima atakuwa anahisi, kwani yeye mtoto? Kuna pesa inaweza kujipeleka yenyewe?”
“Kweli lakini, dalili unazionaje?”
“Pam usiwe na wasiwasi, niachie mimi hii shoo nitaisimamia mpaka mwisho.”
“Nakuamini Lucy, ni mtihani wako mdogo sana. Ukiufaulu milioni moja itakuwa halali yako.”
“Sema.”
“Nataka wikiendi hii uje naye club, utaweza?”
“Milioni ipo?”
“Kumbuka mimi ndiyo nimekuahidi.”
“Sawa, niachie mimi.”
“Nakutumia laki tano baadaye kidogo, ukifanikiwa kuja naye, laki tano yako nitakumalizia. Kumbuka matumizi mengine yote ambayo utakayotumia wewe na rafiki zako kutokana na ujio wenu nitalipia mimi.
“Hapo namaanisha kuanzia mambo ya salon na mengineyo nitarudisha. Kazi yako ni moja tu; kuhakikisha Lilian unakuja naye disko. Mambo mengine niachie mimi.”
“Kazi ndogo, tuma pesa hiyo kwa namba zangu za simu.”
“Robo saa ijayo fedha itakuwa tayari imeshakufikia.”
“Poa Pam.”
“Usiniangushe Lucy.”
“Umenisahau mara hii?” akasema Lucy huku akisindikiza na kicheko cha nguvu.
“Sawa.”
Pam akakata simu.
Lucy aliendelea kuisikiliza simu yake. Alipogundua ilikuwa imekatwa, akaitoa sikioni.
“Nitajua cha kufanya,” akasema.
Palepale akamtumia meseji Latifa iliyosomeka: “Shoga, Pam amenipa dili lingine, amesema kama nikifanikiwa kwenda na Lilian club wikiendi hii, atanipa milioni moja.
“Sasa nakupa dili, na wewe hapa nakushirikisha, utakula laki mbili. Naomba uanze kulianzisha.”
“Poa shoga yangu, miye tena? Huku huku naanza mambo,” akajibu Latifa.
***
Wiki moja bila Edo nchini Tanzania ilikuwa ngumu kwa Lilian. Chuo kilianza kuwa na ugumu kidogo. Kwa namna alivyojizoesha matumizi makubwa, bila Edo ilikuwa ni wakati mgumu sana kwake.
Pamoja na fedha wanayopewa wanafunzi wote kwa ajili ya matumizi, bado haikuweza kukidhi mahitaji yake ipasavyo. Umuhimu wa milioni aliyopewa na Lucy akiwa hajui ilipotokea ulionekana dhahiri.
Kwa kutumia hila na maneno laghai, Latifa na Lucy walifanikiwa kuwateka mawazo Leila na Lilian na kukubali kwenda disko, kichwani wakiamini walikuwa wanakwenda kwenye berthday.
Walipofika Masaki, kibao kikageuka. Wakaambiwa wanakwenda Klabu Maisha. Lilian aligoma, kwa ushawishi wa Lucy na Latifa, Leila akajikuta akiunga mkono, Lilian akajikuta akikubali kuingia. Lucy aliwalipia wote.
Disko lilikuwa limechangamka sana. Lilian alionekana kuwa mpole, akiwa amekaa kwenye kiti muda wote akinywa juisi. Latifa na Lucy walikuwa wamekolea kilevi, wakicheza kwa madaha muziki uliokuwa ukirindima.
Leila alijikuta akifuata mkumbo na kwenda kucheza na wenzake. Muziki ulipokolea, Lucy alikwenda kumvuta Lilian na kuelekea naye kwenye sehemu maalumu ya kuchezea muziki.
Kwa shingo upande, Lilian alijikuta akienda. Hakujua kuwa alikuwa akienda kukutana na Pam!
***
Edo aliendelea kusoma ujumbe ule zaidi ya mara tatu; maneno yalikuwa yaleyale. Safari hii aliamua kusoma kwa sauti:
Edo
Nilijua lazima hili lingetokea. Ni wiki tu tangu umeondoka, lakini tayari hisia za usaliti zimeanza kunukia. Nakuomba baada ya kusoma ujumbe huu, tafadhali endelea na maisha yako, nami niache na maisha yangu.
Siwezi kuendelea kulazimisha mapenzi mahali nisipopendwa. Kwa taarifa yako kwa sasa natafuta mwanaume mwingine ambaye ataweza kunithamini na kujua umuhimu wangu.
Kutokea muda utakaosoma ujumbe huu, ondoa kichwani mwako kuwa una mwanamke Tanzania anayeitwa Lilian.
Lilian.
Edo akaamua kujiridhisha tena kujua kama aliyetuma alikuwa ni Lilian. Ni kweli ulikuwa ujumbe kutoka kwa Lilian. Hilo alijihakikishia kwa asimilia mia moja!
Itaendelea.
 
af mbona haditj ya wakil hutoi mizambwa tunakuda epusode km tano iv tuwekee bas cz hadith zako ni nzur mno hongera
 
Last edited by a moderator:
Nani ameingilia account ya Lilian jamani, Lily hawezi kuandika hivyo kwa edo, haiwezekani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…