Oscar Pius Blog
Member
- May 5, 2015
- 34
- 67
MTUNZI; NDUGU KAGUTA
UTANGULIZI.
Jioni ya jumatano ya tatu ya kwanza mwezi machi mwaka huu, haina tofauti na siku nyingine kwa wakazi wa jiji kubwa na maarufu nchini Tanzania.Machweo yalikaribia na kuwafanya wengi wawe katika harakati za kuachana na shughuli zao rasmi na zisizo rasmi na kuandaa milo na malazi kwa wale waliokuwa nayo ,huku wachache kama walinzi ,wauza baa, wauza miili, wauguzi na madaktari , askari na wengine wengi ambao kazi zao haziendeshwi kwa kufuata machweo ama mawio ya jua walikuwa wakijipanga kuingia kazini.
Wakati hayo yakiendelea katika hali ya kawaida kuna mengine yalikuwa yakiendelea kwa siri na hatari ndani mwake, ambayo yaliwahusisha watu mbalimbali kwa umoja wao ama utengano wao.Hili la siri lilimhusu kijana mmoja mtanashati aliyekuwa ndani ya ofisi za moja ya mitandao maarufu ya simu akirudishia namba yake ya simu ambayo ilikuwa imepotea siku mbili zilizopita.Huyu alikuwa na siri ya kweli siri iliyomhusu yeye pekee duniani na wafu wengi ambao alikuwa akiwajua hakutaka kuifanya siri yake ijulikane kwa kiumbe yeyote ambaye anaendelea kuvuta hewa na kuitoa akifurahia uhuru huu wa hali ya juu tuliopewa na Muumba.Siri hiyo ndiyo iliyomfanya airudishie namba yake hiyo ili asije kuipoteza siri yake ambayo hakutaka ulimwengu wa walio hai waijue.
Dakika kumi baadaye alitoka na kuelekea ofisini kwake ambako ni kama alikuwa kitegemea kulisikia jambo fulani ambalo kwa siku mbili alikuwa akitamani kulisikia ,Ilikuwa ni katika ofisi za kampuni moja kubwa la habari nchini ambako alikuwa akifanya kazi kama mwandishi wa habari.Hatua hamsini kutoka kwenye jengo la ofisi aliyokuwa akielekea alikiona kitu kilichomshtua na kumshangaza sana.Aliegesha gari na kutoka nje akimfuata mmoja ya wafanyakazi waliokuwa wakishangaa kile kilichokuwa kikiendelea.
‘’Kuna nini?’’
‘’Hatari’’Alijibu yule mfanyakazi ambaye alikuwa kama amechanganyikiwa.
‘’Hatari gani?’’
‘’Mwenyewe sijui’’Aliongea yule mfanyakazi ambaye alikuwa ni mlinzi wa getini pale ofisini.
‘’Sasa umejuaje kama hatari?’’Aliuliza lakini kabla ya kujibiwa simu yake iliita, baada ya kuipokea alirudi garini na kulitoa gari kwa kasi kuelekea mahali ambako alikuwa ameitwa.
*******
Vijana kumi na mbili walikuwa wakiendelea kucheza mpira kwenye bonde lililokuwa kwenye mto uliokuwa ukipita nyumba ya kiwanda cha Bakhresa ,pale kwenye daraja la reli inayopitia karibu na ofisi ya kampuni ya Mwananchi bila hofu yoyote.Hawa walikuwa ni miongoni mwa mamia ya vijana wengi waliokosa maeneo ya michezo baada ya sera na matendo ya wenye madaraka na wenye mali pamoja na uvivu wa umma katika kusimamia na kudai haki na kutimiza wajibu wao.Mioyo yao ilijawa na amani kwani walikuwa wamezoea na walishajiwekea sheria ambazo ziliwapa uhuru wa kufanya walichokitaka ili wasiuharibu mchezo.
‘’Atakayepiga mpira ukavuka reli ataufuata mwenyewe na ukipiga kwenye majani marefu unaufuata pia’’Alisisitia mmoja wa vijana wale ambaye alionekana kukerwa na mgeni mmoja ambaye tangu aje na mwenyeji wake amekuwa akiupiga mpira kwa nguvu na wenzake waliudaka kama mara tatu wakiuzuia usiende kule ambako hawakupenda uende.
‘’Samahani naomba unisaidie kaka Juma , sitopiga tena kule’’Aliongea Hafidh Mgeni ambaye alikuwa ameupiga mpira ule kwa mara ya nne sekunde kadhaa baada ya kuonywa .
‘’Ukipiga tena utaufuata mwenyewe na itabidi upumzike’’Juma alitoa onyo kwa ndugu yake mgeni kutoka Morogoro ambaye alikuwa hajamaliza hata wiki tangu aje kumtembelea mama yake mkubwa ambaye alikuwa akiupenda urafiki wa mwanaye Juma na Hafidhi kila pale walipokuwa wakienda Morogoro.
‘’Sawa sitorudia kaka’’
Yakaisha mpira ukaletwa, lakini kwa Hafidh aliona hajatimiza kile kilichomfanya aupige mpira kule ulikokuwa ukienda, akajaribu bahati yake kwa mara ya mwisho ili atimize lengo lake.Akawa anasubiri aupate mpira lakini kama vile wenzake walilijua lengo lake mpira ukawa haufiki kwake , akaendelea kuhangaika kuukaba mpira kwa akili na nguvu zake kwani hata aliokuwa nao upande mmoja wakawa hawampi mpira , akatamani kuwakaba kwani muda ulikuwa ukikimbia kuliko vile alivyokuwa akitaka.Jua lilikuwa likisogea kama vile likikimbizwa hali iliyomfanya Hafidh aendelee kuhangaika kuupata mpira ule ili aupige kule alikokuwa akitaka uende ili aipe taarifa moja jamii ambayo alikuwa na uhakika ilikuwa haina.
Baadaye akapata wazo wazo ambalo lilizaa matokeo aliyokuwa akitaka , mpira kukapigwa kuelekea kwa mwenzake aliyekuwa nusu hatua kutoka alipokuwa amesimama akaunasa na kuupasia kwa mtu mwingine , lakini hakuwa akipasia kweli kwani alimlenga yule kiongozi aliyeonekana mkali sana ambaye alikuwa akija kuunyang’anya kwa kasi kasi iliyomfanya kutane na mpira uliombabatiza na kuelekea kule alikokuwa akikutaka, naam mpira ukafika usawa ule ule alioutegemea na yule kiongozi hakuwa na cha kuongea zaidi ya kutembea kibabe akielekea kwenye nyasi ndefu zilizokuwa katikati ya bonde lile.
‘’Mamamaaaaaa!’’ sauti iliyojaa woga ilisikika kutoka upande aliokuwa ameelekea yule kiongozi wa wale vijana jambo lililowafanya wote waliokuwa eneo lile kuelekea kule sauti ilipotokea wakiwa na hofu kubwa mioyoni mwao na wale walioshindwa kuidhibiti hofu na uoga wao walibaki wameshika vichwa vyao tayari kutahayari.
Yule kiongozi alikutwa ameanguka hana fahamu , mbele yake taswira ya kuogofya iliwafanya watazamaji kushika vichwa kwa mshangao, huku wenye nyongo zenye mwitikio wa haraka wakatapika , pia kulikuwa na wale waliokuwa wameziba pua huku wakiivuta hewa ile mbaya kwa vinywa vyao ambavyo kwa wakati huo hata hawakukumbuka kama ndiyo njia ya vyakula vyao na si hewa chafu iliyozishinda pua zao ambazo ni maalum kwa kazi hiyo, isipokuwa kwenye nyakati za maalum wakiamini ule ulikuwa ni wakati maalum.
*******
Jioni ya siku iliyopita Hafidh akiwa peke yake akitoka kuzunguka zunguka baada ya kuachana na kaka yake Juma ambaye baada ya kutoka kucheza mpira pale bondeni na kufuatana na binti mmoja ambaye bila shaka walikuwa wapenzi aliona amezidiwa na sambusa alizokuwa amenunuliwa na kaka yake katika kule ‘kumzuga’ na kumchelewesha ili amsubiri.Sambusa zile zilimfanya asikie tumbo lake likiunguruma likidai kupunguza kitu kilichochafua kabisa mfumo wake, alitamani akimbie hadi nyumbani ili akajisaidie lakini hakuweza kufanya hivyo kwani mwenyeji wake alimwomba sana asije kwenda nyumbani peke yake , mama yake angemlaza nje ya nyumba kwa vipigo, na vitisho juu.
Hafidh hakutaka kumwangusha mwenzake , akaamua kuzugazuga atafute hata choo kibovu hakukipata, pori hamna , kwa kifupi hakupata faragha lakini akakumbukakale kapori kadhaifu pale bondeni alipokuwa akiwaangalia akina Juma wakicheza soka giza lile dhaifu lililopata nguvu kila sekunde iliposogea lilimpa nguvu ya kwenda huko na hofu ya chatu na wadudu wengine wakali lakini ile hali ya kuzidiwa iliyomfanya atembee kwa mwendo wa ajabu kama amechomwa kisu tumboni alifanikiwa kuzipenya nyasi huku akiwa na uhakika hakuna aliyekuwa anamwona kutokana na giza kukomaa na umeme kukatwa.
Akapata faragha aliyoitaka huku kelele za haja zikimtisha na kuhisi zingesikika mbali lakini walau tumbo likawa na adabu kidogo, hadi pale alipokamilisha dakika tano na kuvuta majani ambayo hakuwa na uhakika kama yangemtawadha kweli na kuyatumia na kutoka kwa hofu akirudi alikotoka lakini akateleza na kuanguka bahati nzuri alitanguliza mikono lakini alihisi kama hakuwa ameshika ardhi.Hakutaka kuhanagika nacho, maadam alikuwa amemaliza haja yake aliinuka na kukimbia kuelekea pale nduguye alimtaka amsubiri , lakini akajikwaa kwenye kile kitu ambacho alikuwa amekishika pale alipoteleza, safari hii alikiangukia katika kutafuta pa kushika ainuke akajikuta akikishika kile kitu na kumpa hofu akainuka tena kabla ya kufanikiwa kuondoka eneo lile na kukimbilia pale alipotakiwa awepo.
Dakika moja baadaye nduguye alifika na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza , ndiani simulizi za kussisimua za mapenzi kutoka kwa Juma zilitawala maongezi yao.
‘’Unajua yule ‘mtoto’ alinipendea soka, yaani ananipenda sana’’
‘’Kweli?’’
‘’Huniamini mdogo wangu mie naitwa , Kiluvya, Mbagala hata Bagamoyo huko kucheza mpira, huko nako warembo kibao wanaimba jina langu, yaani wananitamani lakini mie nakufa Na Maria yule motto anajielewa , halafu