MPANGAJI 03
Sele hakukaa hata kidogo aliondoka zake mara tu baada ya kumuacha Ester pale kwao,
Sasa Ester alizunguukwa na wapangaji wote waliokuwepo wakitaka awaeleze kuhusu Sele,
āhivi anaongea kabisa, halafu anacheka?ā aisha alidakia
ājamani Sele ni mwanaume mzuri tu kama walivyo wanaume wote, yaani sijui nisemeje ni binadamu kabisa!ā alisema ester sasa alishachoka kufanya mahojiano ambayo kwa uono wake yeye haukuwa na kichwa wala miguu,
āhaya tuambie mlikula nini, kawhiyo Sele pia anakula kabisa!ā aliuliza mama Mwajuma!
āhahahaha jamani mama, eti anakula, kwahiyo bado mnaamini Sele ni Zimwi, sijui jini huko..ā alisema ester akiingia ndani
āna mizigo yote hii mwanangu umemaliza mshahara wako huko!ā alisema mama mwajuma
āhapo vitu vingi kaninunulia Seleā alisema Ester sasa akiangalia hotpot lilipo ili achukue chakula
āmh makubwa haya jamani!āalisema mama Mwajuma sasa akimtafutia maji ya kunawa mwanae
Ndani ya muda mfupi Sele alizoeana kabisa na Ester na sasa unaweza kuwakuta wamekaa nyuma ya nyumba usiku wakipiga soga huku wakicheka kabisa, hata hivyo Sele alikataa kata kata kumueleza chochote kuhusu maisha yake pamoja na Ester kujinasibu kumuelezea hadithi zake za mahusiano yaliyopita na maisha ya shule kwa ujumla , Sele hakuthubutu kumueleza chochote,
Na sasa waliweza kubadilishana namba za simu na siku nyingine wangechati mpaka usiku wa manane,
Baada ya sikukuu ya Pasaka sasa Ester alipaswa kuondoka kurudi kazini kwake lindi , Tayari mkuu wake wa shule alishampigia kumkumbusha umuhimu wa kurejea mapema,
Hivyo siku hiyo Ester alitumia muda wake kwenda kariakoo kununua vitu baadhi alivyodhani vingemfaa , aliwaza na kuwazua akaona atafute zawadi ndogo kwa ajili ya Sele na hivyo akaingia duka moja la kuuza simu na kununua simu janja aina ya Tecno F2.
ābila shaka Sele atafurahi kuwa na simu hii janja, na nitakuwa namtumia picha zangu nay eye ananitumia zake nikiwa Lindiā aliwaza Ester.
Alirudi nyumbani na kuandaa mizigo yake tayari kwa safari kesho yake, baada ya kumaliza alitoka nje kwenda kumsubiri rafiki yake Sele ambaye alifika kwa wakati kabisa,
āyaani umejuaje kunisubiri hapa!ā alisema Sele akiwa na bashasha kweli kweli,
āah yaani acha tu wewe mwanaume una kismati maana hata sijui kwanini nimekuzoea hiviā alisema Ester bila kujielewa
ānisubiri basi hapa nikaweke mizigo then nitakukuta hapa nje!ā alisema Sele akiingia ndani
āmh yaani mpaka naondoka sijaingia chumbani kwako Kaka sele Jamani!ā alisema Ester akipiga hatua kumfuata Sele,
āHAPANAA!!ā alifoka Sele , mpaka mwenyewe akashangaa na kurudi nyuma kwa ester kuomba radhi,
ānisamehe Ester, kwakweli hakuna mtu ataingia chumbani kwangu , nasikitika nimekufokea nisubiri tu nakujaā alisema Sele akiingia ndani haraka
ānitaingia hiki chumba Sele, kama sio leo basi kesho!ā alijisemea Ester akimsubiri Sele atoke
Sele alitoka baada ya dakika chache tu kisha wakasogea kwenye msingi wa nyumba ambao ulikua haujaisha na kukaa kupiga Story,
āyeah kama nilivyokuambia kesho nasepa Sele nitakumisi sana!ā alisema Ester kwa uchungu kidogo
āyeah, ndio hivyo kazi ni muhimu sana Ester inabidi uende mimi mwenyewe nitakumisi ujue, wengine wananitenga mara waniite zimwi, siijui jinni.. hahahaha!ā alisema sele akimalizia na kicheko
āhahaha yaani nakuambia kabla hatujaonana nilikua naambiwa sana habari zako , ila kumbe mtu mwenyewe wala hata hauko hivyo,ā alisema Ester akilala kwenye mabega ya Sele
āhahaha mawazo yao tu, sema unajua maisha ya Dar kila mtu na hamsini zake kwahiyo nadhani watu wako bize sana kutafuta riziki ndio maana wananifikiria vibaya!ā alisema Sele
ākaka Sele nimekuletea Zawadi hiiā alisema akitoa ile simu kwenye box lake na kumkabidhi Sele,
āloh asante sana Ester kwa smartphone hiiā alisema Sele akiichukua
āooh asante kwa kushukuru, ndio sasa nikiwa Lindi nitakuwa nakupigia video call, nakutumia picha na video zangu Sele!ā alisema Ester kwa furaha
āsikiliza ester mimi situmii mtandao wowote wa kijamiiā alisema Sele kwa upole huku mkono mmoja akiwa ameuweka begani kwa Ester
āsele unasema kweli?ā Ester alihamaki akimtazama Sele machoni hakuamini kabisa maneno haya yanatoka kwa kijana mwenye umri wa miaka 30-33 hivi
āyaani hutumii facebook, insta, whatsapp?ā aliuliza Ester na Sele aliatingisha kichwa tu kuashiria anakubaliana nae..
ābasi ni kweli kuna tatizo Sele!ā alisema Ester sasa akitoa kitambaa chake kwenye suruali aliyokua amevaa akifuta machozi na kisha akasimama na kuondoka kurudi ndani
ārudi esterā Sele alijaribu kumuita lakini tayari Esta alishawahi kulifikia geti kurudi ndani
ānilijua tu atachemka, mimi ni Zimwi kweli!ā alijisemea Sele akipiga ngumi kwenye mchanga kwa hasira alijisikia vibaya sana kuagana na esta katika hali ile esta alirudi ndani na kukimbilia Chumbani kwake alijikuta akilia bila sababu mpaka yeye mwenyewe akawa anajishangaa
āTriiiiiaā simu yake ilitingishika kuashiria ujumbe mfupi uliingia
Aliufungua na kusoma ulitoka kwa sele
āNINA ZAWADI YAKO PIA TAFADHALI UJE UICHUKUEā
Esta aliwaza kama aende ama abaki lakini baadae alijiona mpumbavu kulia mbele ya mtu ambaye hata hakuwa na mahusiano yoyote
Alijikaza kisabuni na kutoka nje na kumkuta sele akiwa ameshikilia begi dogo hivi la wastani
āhii zawadi yako Estaā alisema akimkabidhi kisha akageuka kurudi chumbani kwake!
āna hili begi, mbona kama kuna uzito humu?ā aliuliza esta,
ābhana ni zawadi yako vyote pamoja na begiā alisema Sele akitabasamu kisha akaendelea na hatua zake kadhaa kuingia kwake,
Esta bado alikua na shauku ya kujua ndani ya begi kulikua na nini, hivyo aliangalia huko na huko kuhakikisha hakuna mtu pale nje kisha akaingia ndani na kufungua lile begi..
Ndani kulikua na komputa mpakato mpya kabisa aina ya apple ikiwa katika makaratasi yake
āwhaaatā Esta aliweka ile komputa kitandani huku akiwa haamini, hakujua kama afurahi ama la, haraka alichukua Simu yake ana kuingia mtandaoni na kwenda kwenye google kisha akatafuta āapple sx400 min series priceā bila hiyana google wakamletea $1,100 , alijaribu kubadili pesa hizo na kuweka kwenye pesa ya Tanzania na kukuta ni zaidi ya million mbili!
āyaani huyu Sele ananinulia mimi zawadi ya million mbili?, sele huyu katika nyumba ya kupanga ya kawaida tu?ā Sasa akili yake ilimwambia huyu āseleā sio mtu wa kawaida kama alivyokuwa anamchukulia,
Aliwaza na kuwazua kisha akaona ngoja acheze huu mchezo
Alichuchukua simu yake na kuandika ujumbe mfupi kwa sele
āasante sana kwa zawadi dear ila nina ombi mojaā
Kisha akutuma kwa sele , baada ya muda mfupi yake simu yake ilitoa ishara kuwa ujumbe ule umepokelewa na hivyo akasubiri jibu
āyap karibuā sele alijibu
ānaomba sana kesho unisindikize hadi ubungo tafadhali sana, naomba sana kesho usiende kabisa kaziniā aliutuma ujumbe huo kwa sele
āEsta nilishapanga hilo nisingekuacha uende mwenyewe bestā alijibu sele kisha wakaagana
Kila mmoja aliwaza kuhusu mwenzake
Badala ya furaha Sele alijikuta machozi yakimtoka, alienda kwenye sanduku lake ambalo alikuwa ameliweka kwenye kabati ya nguo,
Alitoa bahasha kadhaa kisha akatoa picha mbili aliziangalia muda mrefu huku machozi yakimtoka
ānipe Baraka zako , nipe Baraka zako!ā alisema huku machozi yakimtoka akiwa ameshikilia zile picha,
Sele sasa hakuweza kutazama zile picha zaidi alizirudisha na na kisha akaenda bafuni alifungulia maji tu yakimwagikia mwilini na mwishowe akagundua kuwa alikuwa hajavua nguo zake kumbe