Mpauko
R.I.P
- Jan 19, 2019
- 2,323
- 3,451
- Thread starter
- #41
FAILI NAMBA 25
MWANDISHI:ROBIN MIHO
***************04*****************
Code E02, Harold Mlembuka ambaye ndiye aliyekuwa na cheo kikubwa kuliko sisi wawili alilitupia faili katika meza fupi ya Vioo iliyokuwa pale sebuleni, akalifungua na kuanza kulisoma kimya kimya kwa dakika takribani tatu kisha akatugeukia.
"mtu wa kwanxa kuuawa alikuwa mfanyabiashara wa madini Remo Kyaruzi, kisha akafuatia waziri wa madini hamuoni kama kuna tatizo hapa? " alizungumza harold na kututupia macho.
"lipo, lipo naona kuna uhusiano fulani kati ya vifo hivi na madini" nilisema na kuendelea,
"je! ripoti ya awali imeonyesha aina gani ya siraha iliyotumika? "
"ni bunduki kubwa aina ya M16" alijibu Haold
"lakini majeshi yetu hayana aina hii ya bunduki" Clif alisema akaongeza,
"basi na inawezekana tukahusisha tukio hili na ujambazi, matukio mengi ya ujambazi hapa Mwanza yamehusisha bunduki hii na huingia nchini kupitia mpaka wa Burundi na Tanzania,lakini Je! Katika mauaji ya Mheshmiwa Kipingu ni siraha gani iliyotumika? "alimalizia na swali Cliff
"ni sub machine gun(SMG) " aliitikia Harold huku akilisoma faili kimya kimya.
"aisee nadhani tunahitaji kuchunguza kwanza hili suala la Mr. Kyaruzi ikumbukwe kwamba faili limesema uchnguzi mpya ufanyike bila kuzingatia uchunguzi uliokwishakufanyika" nilizungumza.
"vilevile uchungzi ukamilike ndani ya wiki mbili na usizidi wiki tatu kwa maana ya kwamba leo tarehe kumi na tano, itatulazimu kumaliza kazi hii wii ya kwanza ya mwezi wa nane wahusika wote wawe mbele ya mkono wa dola".aliongeza Harold kabla ya kulifunga faili ile na kusimama.
"tunahitaji kuonana na mlinzi aliyejeruhiwa sku ya tukio nyumbani kwa Mr. Kyaruzi, Cliff tafadhali tupeleke hospitli ya Kissesa" aliongea Harold na kufungua begi lake akatoa sweta nyeupe yenye kikofia kwa nyuma, nami sikuwa nyuma nikalitwaa sweta langu jekundu nalo likiwa na kikofia, tukainuka na kutoka nje, ilishatimu saa mbili na dakika kumi.
Tuliuacha mtaa wa Mwembechai, tukayapita majengo ya Marwa store na kuigia mtaa wa Rwegesora, dakika tatu zilitukuta tukiingia barabara ya Pamba, gari iliambaa kwa kasi tukaiacha barabara ya pamba na kuingia barabara ya Kenyatta dakika 20 baadaye zilitukuta tukiwa nje ya geti la hospitali ya Kissesa.
Haikutuwia ugumu dakika tano mbele tulikuwa ndani ya ofisi ya mzee wa makamo mrefu mwembamba mwenye upara na nywele fupi zilizotawaliwa na mvi chache,
Harold akatoa kitambulisho kabla hajatoa utambulisho wetu sote watatu, ingawaje utambulisho ule ulijawa na hila kwani tulitumia majina feki yaliyokuwa katika vitambuiho tulivyopewa na code E01.
"naitwa dokta Wilson Mlaguzi" alijitambulisha.
"tunashukuru kukufahamu bwana Wilson na kama tulivyokwisha kueleza lengo letu tunahitaji kufahamu maelezo ya kitabibu ya bwanaYusuph Kamkaze, mlinzi binafsi wa marehemu Remo Kyaruzi" alizungumza Harold,
dk. Wilson hakuzungumza kitu akafungua mtoto wa meza na kutoka na faili, akalifungua na kusoma kwa sekunde kadhaa kabla hajatugeukia,
"bwana Yusuph Kamkaze alijeruhiwa kwa risasi iliyovunja mfupa wa ubavu wa kulia na kutokeza upande wa pili, jambo la kushukuru ni kwamba haikumjeruhi sana kwani iliparaza sentimita chache kuufikia utumbo mdogo, ingekuwa hatari zaidi endapo ingeufikia utumbo" alimalizia dk. Wlson
"hakuna kingine? " nikadakia
"hakuna" alijibu dk. Wilson na kututaka twende kumtazama bwana Kamkaze, akajivika kifaa chake cha kupimia mapigo ya moyo akauendea mlango nasi tukamfuata.
tukakwea hadi katika gorofa pekee ya jengo hili, tukiwa katika korido tulipishana na pande la mtu mweupe kiasi akiwa kavalia kaunda suti nyeusi miwani ya macho yenye fremu za rangi ya fedha, aliuwa kainamisha uso wake chini akiongea na simu.
Hatimaye tuliufikia mlango wa wodi namba 21 tukiongozwana dk. Wilson tukaingia,
tulichokiona mbele yetu kilitufanya tuzubae kwa sekunde kadhaa, mwili wa bwana Kamkaze ulikuwa umelala chini katika dimbwi la damu huku kisu kikubwa kikiwa kimejikita vilivyo kifuani alikuwa akitapatapa kupigania roho yake.
"wametuwahi" aling'aka Clifford, dk. Wilson alitoa simu yake huku akijaribu kumtuliza bwana kamkaze.
"shit atakuwa yule jamaa tuliyepishana naye" nilisema huku nikiukimbilia mlango n kutoka nikitimua mbio, Clifford akiwa nyuma yangu, tulishusha ngazi kwa kasi tukiangaza huku na kule bila mafanikio.
"kaangalie upande wa vyooni" nilimwambia Clifford huku nikishika uelekeo wa getini na uzuri ni kwakba Hospitali hii ilikuwa na geti moja tu.
"samahani babu, kuna mtu yeyote aliyetoka muda huu? " nilimuuliza mzee aliyevalia sare za kampuni moja ya ulinzi iliyopewa tenda ya ulinzi katika hospitali hii.
"ndiyo wametoka watu wawili wampanda pikipiki nyeusi hizi za boksa" alijibu mzee yule huku akinishangaa, nilijikuta nikishika mikono kiunoni kabla sijamuuliza tena mlinzi yule,
"kuna aliyevaa kaunda suti nyeusi na miwani ya macho?
" ndiyo alikuwa amepakiwa katika hiyo pikpiki sikuona miwani kwani alivalia helimeti"
Nikaitoa simu yangu na kutamka "code E02, code E04 tumeshaachwa, kibanda cha mlinzi"
nikaitia simu mfukoni, simu hizi za kisasa maalumu hazikuunganishwa na mtandao wowote wa simu zikiwa na mawasiliano na watu wanne tu, hivyo ujumbe ule uliwafikia code E01, Code E02 na code E04.
Nikasimama pale kibandani na kumweeza mlinzi yule kilichotokea muda mfupi uliopita,
haikupita hata dakika moja Clff alisimamisha gari mbele yangu nikajipakia na kuyaacha majengo ya Hospitali hii huku tukiwa tumefadhaishwa na tukio lillotokea pale hospitali.
"mambo yameharibika wamekwishakushajua uwepo wetu, lakini ni nani hasa aliyewashtua kuwa tupo pale hospitali? Je! Tumekutana nao kama bahati au walifika baada ya kujulishwa kuwa sisi tupo hapa? " aliuliza Cliff
"Dk. Wilson mpuuzi yule" alisema Harold huku akiuma meno kwa hasira.
"mnakumbuka ni dakika ngapi alizitumia kutuacha mule ofisini kwake? Aliaga kuwa anakweda kuchukua faili la matibabu ya bwana Kamkaze, mlibaini nini baada ya hapo? " alimalizia kwa swali Harold.
"aliliweka mezani lakini hakulitumia hilo bali alichukua faili la bwana Kamkaze katika mtoto wa meza" niliitikia, nikatoa kitabu kidogo cha kumbukumbu nikaandiika jina la dk. Wilson na jina la Hospitali ya Kissesa.
"hakuna jinsi Dk. Wilson ni mshukiwa wetu namba moja, hakuna namna"niliongea wa hasira.
"pia bwana yule kabla hajakata roho alinitazama na kutamka neno moja tu SIKAJULA jambo baya zaidi ni kwamba dk. Wilson alisikia nilimuona akishtuka kwa mbali kuna kitu anafahamu mshenzi yule" alisema Harold
"pia sioni haja ya kurudi maskani, Cliff moja kwa moja Ilemela nyumbani kwa marehemu Remo Kyauzi" alitoa amri Harold kabla hajaendelea,
"tukilala usiku huu tunakuwa tumewapa nafasi watu hawa kuharibu ushahidi kule nyumbani kwake, ni lazima twende sasa hivi" alisisitiza Harold.
Ilikwishatimu saa nne na robo usiku
*******************************
WAPELELEZI WA SIRI WAMESHAGUNDULIKA, WAMESHAWAHIWA KWA BWANA KAMKAZE, JE! SAFARI YA ILEMELA ITAZAA MATUNDA? TUKUTANE KESHO.