Hadithi: Kalamu Yenye Siri Ya Damu

Hadithi: Kalamu Yenye Siri Ya Damu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,662
Image may contain: one or more people, hat and text

Mwandishi/Mtunzi: NYEMO CHILONGANI.
..................................................
-KIONJO-

Kuna mwandishi mmoja wa vitabu vya simulizi, alianzia kazi zake kwenye Facebook kitambo hicho. Alipata jina, akawa na watu wengi waliokuwa wakifuatilia kazi zake.

Akaanza kuingiza vijisenti, baadaye akakutana na washikaji wakamshauri atoe vitabu ili auze na kupata pesa. Jamaa akafanya hivyo, akaandika vitabu, akaanza kujulikana, yaani ukimtaja mwandishi wa mitandaoni, jina lake lilikuwa la kwanza.

Baada ya kufanikiwa, jamaa akakutana na mshikaji mwingine, akamwambia aandike kitabu kizuri na akiweke kwenye mtandao wa Amazon.

Akafanya hivyo, akaandika kitabu na kukiweka huko, kilikuwa cha Kiingereza, kiliuza kidogo, aliingia pesa ila hakuridhika. Mshikaji akamwambia aandike kitabu kingine, yeye akaandika kitabu kiitwacho There Is No God At All' yaani Hakuna Mungu Kabisa.

Kitabu hicho kilishtua watu, ni kitabu kilichofunua mambo mengi. Watu walikinunua huko Amazon ili kuona jamaa aliandika nini mpaka aseme hakuna Mungu.

Ni ndani ya wiki moja, kitabu kiliuza kopi milioni moja, akatengeneza pesa nyingi na kiliendelea kufanya mauzo makubwa.

Baadaye, maofisa wa CIA wakaamua kukinunua na kukisoma kwani humo ndani kulikuwa na mambo mengi yaliyofichwa, ambayo yalikuwa mafumbo yao kwa muda mrefu na humo yalikuwemo majibu ambayo yangewafanya kutokuwa na maswali mengi.

Humo kulikuwa na majibu juu ya mpigaji halisi wa majengo ya biashara ya WTC, kulikuwa na majibu juu ya chanzo cha gaidi wa kimataifa Hemed Al HAssan kuamua kuzishambulia nchi za Magharibi lakini pia kulikuwa na majibu ya kwa nini watu wengi waliamua kuzikimbia nchi zao masikini na kwenda kuishi nchini MArekani.

Kwa kifupi kitabu hicho kilikuwa na mambo mengi. Kitu kilichowafanya maofisa wa CIA kuhisi kwamba mwandishi huyo alikuwa akifahamu mambo mengi kuhusu matukio mengi yaliyokuwa yakiendelea, kitu cha muhimu kabisa, walihitaji kumjua alikuwa nani, na alikuwa nchi gani.

Walianza kumfuatilia. Kwa msaada mkubwa wa watu wa Facebook, waliwaambia kwamba jamaa alikuwa akiitumia akaunti yake kutoka nchini Nigeria, wakaelekea huko, walimtafuta sana, wakapigiwa simu na kuambiwa kwamba jamaa alikuwa akitumia akaunti yake nchini Misri, wakaenda huko.

CIA walikuwa wakimtafuta mwandishi wa kitabu hicho, alijificha kwa kuwa alijua kupitia kitabu hicho alikuwa akitafutwa kila kona, hakuwa mhalifu ila alijificha kwa kuwa alihitaji tu kuwasumbua hao maofisa wa CIA.

HAwakuwa na picha yake kwani hata kwenye vitabu vyake vyote, hakukuwa na picha zake. Walifuatilia mpaka namba za simu zilizokuwa kwenye akaunti zake, hakuwa akipatikana na walipoulizia kwenye makampuni ya simu waliambiwa kuwa hakuna mtu ambaye alikuwa akitumia namba hizo, sasa huyo mwandishi alizotoa wapi? Na alizitumiaje?
......................................

ILI KUPATA UHONDO HUU na mwingine kibao, wasiliana na Mwandishi@Chilojnr
 
Asante sana kaka mkuu kwa sapoti
 
Kupitia mgongo wa mwandishi nanyi mnataka kutugeuza Amazon?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom