Hadithi: Gamboshi

Hadithi: Gamboshi

twasafi

Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
53
Reaction score
67
UTANGULIZI

Ni hadithi inayohusu kijiji kilichopo mkoa wa simiyu wilaya ya bariad ambacho kiko umbali wa takribani kilometa 12 za mlaba kutoka simiyu mjini, kama hili jina litakuwa geni kwako na hujawahi kuliskia kabisa basi ngoja nikufamishe kidogo.

Gamboshi ni kijiji kinachofahamika kwa uchawi nchi Tanzania kikifahamika ni makao makao makuu ya wachawi ukiachana na mkoa wa sumbawanga basi kwa lugha nyingine unaambiwa ni kitovu cha wachawi yani mizimu yote inapatikana huko, ndo kijiji pekee unaambiwa mchana giza usiku ulaya.

Julai mwaka 1999 serikali ilichukua maamuzi ya kukitenga kijiji hicho baada ya vifo vya zaidi ya watu hamsini [50] vilivoketea ndani ya siku moja ikiaminika ilikuwa na uhusiano na mambo ya kishirikina basi watu waliambiwa kuhamaka makazi na kutafuta sehemu zingine za kuishi.

Kwa muda wa takribani miaka ishirini [20] hamna ambae amekuwa na taarifa zozote kuhusu eneo hilo basi ndo mda serikali kutoka kwenye ofisi ya rais, ilitumwa barua kwa mkuu wa mkoa wa simiyu barau ya agizo la kukifungua kijiji hicho kwa upya ikiwezekana atume maaskari mara moja na kufunguliwe kituo kidogo cha polisi nae mkuu wa mkoa wa simiyu alitii maagizo yaliyo kuwa yametoka kwa rais na kuitisha kikao cha maaskari wa jeshi la polisi, kutoka wilaya zote za simiyu.

Mkuu wa mkoa kwa kutambua kuwa askari wengi wangekuwa na uonga wa kufanya kazi kijiji kule lakini bado ilikuwa inamlazimu kuchagua sababu pia alikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo, basi alifanya maamuzi na kumchagua Mwita Choma na Baraka Kulwa kama maaskari teule kwenda kijijini gamboshi.
Lakini bila kufaham wamejiigiza kwenye shida kubwa nao walikuba kazi ile kwa mikono yote.

SEHEMU YA KWANZA

Tarehe 13 mwezi wa sita mwaka 2019 saa kumi na mbili afajiri [06:00am] akiwa amelala kwake kengele ya mezani [ Alarm] ilikuwa ikipiga kelele kumanisha mda wa kuamka umefika nae taratibu akijinyoosha kutoa uchovu wa usiku, akamudu kufungua macho huku akiwa anatazama aliona mtu akija ghafla kurukia kitandani kama kwa kishindo alishutka sana maana alikuwa na wenge la usingizi lakini hakuwa mwingine bali mke wake Mwita choma

“Habari za asubuhi, mme wangu”. alikuwa ni mke wake mwita akitoa salam huku akilukia kwa kitanda alipo mume wake
“ unajua umenishutua” mwita alimuliza mke na kueka kituo bila kujibu salam yake
“ kumbe umeogopa, basi pole mume wangu”anaomba radhi huku sura yake ikiwa inatabasamu kama anataka kucheka .
“ Umeamkaje kipenzi changu” bado aliuzua huku sura yake ikiwa na tabasamu lilelile
“ salama tu mke wangu.” alijibu salam ya mke wake akaambatanisha na swali,
“mbona umeamka mapema sana leo”
“ kuna kitu konki nimekuandalia kabla ya hujaondoka” alimjibu swali la mume akimtazama kwa ukalibu
“Aah konki” mwita alianza kumtenkenya mke wake huku akirudia neno “konki”
Konki! konk, konki! konki! Mwita aliendelea kumtenkenya huku mke wake akicheka na kumwomba aache anahisi atajikojolea!
Mwita aliacha huku mke wake akiwa ameweka sura ya kununua nae alijirudi na kumwambia
“ kumbe umeumia, basi pole mke wangu” huku sura yake ikiwa inatabasamu kama anataka kucheka

Wakiwa bado wapo kitandani mke wake hakujibu chochote bali alisogeza uso wake karibu na kushika kidevu cha mume wake na kumpiga busu la wakika, na kulikatisha haraka huku akishuka kitandani na kumwambia mume wake amfate bafuni. Nae Mwita alishuka kitandani haraka akiwa na boxer tu na kuelekea bafuni, basi huko kilikuwa ni kitendo cha kuendelea kudumisha ndoa yao ambayo imeishi kwa muda wa miaka mitano sasa wakiwa bado hawajafanikiwa kupata mtoto.

Mwita choma ni kijana wa miaka therathini [30] kabila mkulya urefu wake nin wastani, akiwa na miaka 25 alibahatika kupata mke aitwae ni Janeth. akiwa na miaka 27 aliteuliwa kuwa ofisa msimamizi wa kituo kidogo kilichopo wilaya ya bariadi mkoani simiyu alifanya kazi kwa waminifu huku sifa zikimndondokea kama kijana jasiri. Badaa ya kutumikia jeshi la polisi kwa kipindi wa muda mrefu akiwa ofisa msimamizi alipewa kazi ya kwenda kuwa mkuu wa kituo kijijini gamboshi kama ilivotoka kwa ofisi ya raisi kuwa wateuliewe askari wawili waende wakafanye kazi kijijini huko.

Na ndo ilikuwa siku yenyewe akiwa ameamka salama akiwa nyumbani kwake na mke wakiwa bafuni wanamlizia kuoga. Akiwa amejifunga taulo kiunoni alisikia sauti ya simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita aliishika na kuangalia jina lilikuwa ni rafiki yake Baraka kulwa alikuwa anapiga alikuwa amemsave [ Partern in crime] alipokea na kuongea nae

“Kaka, habari yako” ndo kitu cha kwanza aliskia alipo pokea simu ilikuwa ni salam kutoka kwa rafiki yake
“ salama kaka, kwema?”
“uko wapi”
alijibu salam huku akikaa kitandani. Akaongezea swali jingine
“Kwema! Niko nyumbani napata breakfast” baada ya kujibu swali mwita alicheka na kuuliza
“Haha haha”
“Hivi mdogo wangu huna mpango wa kuoa kabisa!”
“Maana kila siku ujipikie mwenyewe ufue kwa nini usioe?”
Aliuliza na kubaki kusubiri atasema nini
“Mimi ntaoa tu kaka ata usijali ni mipango tu”
“Sawa, wahi kituo sababu tutakuwa tunaondoka mapema si unalewa sehemu tunayoenda unaambiwa usiku ni ulaya” alikubali kisha kumpa taarifa nyingine
“Haha haha, sawa kaka” alicheka kidogo kwa taarifa mwita aliyompa kisha akakubali na kukata simu maongezi yakawa yameishia hapo
Mwita akaweka simu kitandani iliavae nguo za jeshi la polisi ambazo zilikuwa zinamkaa vizuri sana sababu pia ya mwili wake uliokuwa umekaa kimtindo wenye mpangilio na kwenda kupata chai ambayo mke alikuwa kamwandalia, alikuta janeth akiwa anamsubiri seblen akiwa tayari kashaweka chai mezan alikuwa kavaa kitenge tu.
“Karibu chai mme wangu” alimkaribisha chai mme wake kwa tabasamu nzuri kabisa huku akimtengenezea kiti aweze kuketi
“Ahsante mke wangu” alishukuru na kuketi kwenye kiti huku mke wake akiwa ubavu wake wa kushoto
Hakika kilikuwa chakula kitamu ambacho hata mwita alishambulia kama hana akili timamu
“wewe umeshakula mke wangu” aliuliza huku akiendelea kula
“ hapana babo ntakula baadae kidogo, saivi nataka nikae karibu na wewe” alimjibu mme wake na kuongezea shida yake kwa huo mda
Mwita alitambua kwa nini mke wake alisema maneno yale na alikuwa hana jinsi zaid ya kumfariji
“ usijali mama angu, mimi ni wako siku zote “ alimwambia maneno mazuri akiwa anambembeleza kwa kumshika shavu akitumia mkono wake wa kushoto
Janeth alisimama na kumwambia mme wake asuburi na kuelekea chumbani alipo rudi alikuwa na kiboski kidogo ambacho kilikuwa kimefungwa vizuri
“ Kwa ajili yako mme wangu” alimpatia kwa mikono miwili likiabatinishwa na taabasam kama ilivyo kawaida yake kutabasamu
“Ahsante mke wangu” mwita alifurahi alionesha kabisa kashukuru alisamama na kumpatia busu mke wake, alipo jaribu kufungua mke wake alikataa na kumwambia utaifungua baadae
“kuna nini kwani “ akaongezea na swali
“ utaona tu, lakini usikifungue hapa” alimwambia akiwa anamtazama machoni bila kupepesa
“ sawa” mwita alikubali lakini alibaki na maswali kutakuwa na nini kwenye boski maana kilikuwa kidogo sana chenye urefu wa 5 na upata wa 3
tayari kamaliza kupata chai alichukua begi lake la mgongoni lilokuwa mezani na kuelekea nje akiwa anatoka alimgeukia mke wake na kumwambia
“ usisahau kufunga milango mda wa kulala na ukiwa unatoka”
“ na ukiwa na shida yoyote nipigie mimi kwanza”akaongezea huku akiwa anafungua mlango
“sawa , mme wangu” alikubali huku akimtazama mme wake akielekea kupanda gari la jeshi la polisi aina ya toyota landa cruiser ikiwa inafahamika kama [ Defender ]
Mwita aliwasha injini ya gari na kushusha vioo huku mke wake akiwa bado anasubiri aondeke
“ kwaheri, ubaki salama” alimwaga akiwa anamtazama kwa mbali
“ sawa, safari njema mme wangu” alimjibu na kuingia ndani
Mwita alipandisha vioo na kuondoa gari kuelekea kituoni.
 
SEHEMU YA PILI

Aliwasiri kituoni mida ya saa mbili kamili, shughuli zilikikuwa zinaendelea kama kawaida aliegesha gari lake la jeshi alilokabidhiwa kama kuwa usafiri wake. Alipo shuka aliekea moja kwa moja mpka ndani ya kituoni alipishana na afande kadhaa na kusalimia
“Afande, Habari yako”. Akaongezea
“umeamkaje “
“Salama tu, ,Mwita!” alikuwa ni Afande mwana dada anaitwa veronica ni afande alikuwa ni lazima umpate mapokezi kujituma kwake kwenye kazi basi walikuwa marafiki wazuri sana na Afande mwita
“Habari za Nyumbani” veronica aliongezea swali huku akimtzama mwita
“Nzuri kabisa! Afande Baraka kashafika”. Alimjibu salama yake kuongezea na swali
“ Ndio, nilimuona akiwa na Afande mgosi wakiwa wamekaa area tatu” Afande veronica alijibu na kujmwlezea wapi anaweza kumpta Afande baraka.
“Poa, Ahsante!” Alimshukuru na kuelekea area tatu
Area tatu ilikuwa ni jina wanatumia jeshi la polisi palikuwa ni kwenye pembe ya kushoto ya kituo cha polisi. Sababu palikuwa ni hapo hapo kituon basi alitembea na kumkuta Afande Baraka na Afande Mgosi wakiwa wanabadilisha mawazo wakishushia na kahawa wakiwa wamekete kwenye viti
“Habarini za Asubuhi Afande” aliwasalimia huku akiwapatia mikono.
“Nzuri mkuu” alikuwa ni Afande Baraka anajibu salama ile, huku mgosi akiwa kimya anatazama kwa makini. Akaongezea.
“ Aisee mkuu unabanwa! Mpka saiz sa tatu ulikuwa bado upo nyumbani.
“ Majukumu tu Afande, We si umekataa kuoa. Alimjibu huku Akiwa analekibisha mkanda wa kiunoni
“ Hapana ni mipango tu kaka” huku akijibu alikuwa anasimama ili kuendelea kufanya maongezi.
“Sasa fanya hivi” alikuwa ni mwita anakitu anataka kumwambia Afande baraka akiwa kamshika bega aliendelea
“ Nenda kwa veronica mwambie akupatie files zote za ufunguzi ofisi pia niwakute wewe na yeye kwenye gari” Afande baraka aliachiwa maagizo hayo na afande Mwita na kuondoka kuendelea na shughuli zingine za kufutilia vitu wanavohitaji kwenda navyo gamboshi kutokana na mazingira yatakuwa mageni na hamna mtu anajua panafananaje walikuwa wanahitaji kufika mapema kablab ya jua halijazama. Mwita akiwa pale hakuzungumza kitu na mgosi sababu walikuwa hamna mawasiliano mazuri baina yao, kipindi cha nyuma walikosana sababu ya kila mmoja kutaka madaraka.
Kipindi cha nyuma inasemekana mgosi alishajaribu kumua Afande mwita kwa kumwekea sumu kwenye chakula, lakini hamana aliekuwa na ushahidi kuhusu ilo kwahiyo waliacha lipite.
Hivi karibuni Afande Mwita alifaham kuwa Mama mzazi wa Afande veronica alishawahi kuishi gamboshi kipindi cha nyuma basi aliongea na veronica na mama yake alitoa msaada wa mtu ambae ataenda kuwapokea watapofika gamboshi. Siku iyo alikuwa anahitaji amkute afande baraka na afande veronica wakiwa wanamsubiri kwenye gari yake kama alivomwachia maelekezo afande baraka wakiwa na mafaili na kila kitu wanachohitaji ili kuianza safari mapema, ikiwa ni mida ya saa sita mchana lakini cha kushangaza alimkuta afande baraka peke yake akiwa kakaa ndani ya gari.
“Vipi afande “
“ ah mkuu, safi tu”
”Yuko wapi veronica” ilikuwa ni salam ya afande mwita akimsalim Afande na kuambatanisha na swali
“ alipata dharura akanambia atarudi”
“Dhararu gani”Afande mwita aliuliza swali tena baada ya kujibiwa, na kubaki ameshika kiuno. Akiwa kasimama nje ya gari upande wa dereva anajaribu kutafakari anampata wapi veronica , mpka anajikuta kashika kiuno huku anamatazama na afande baraka . Afande baraka kufunja ukimya alitaka kujua nini kinaendelea.
“ Kwani kuna tatizo mkuu? Hatuwezi kuondoka”
“Ndio, veronica anakwamisha mambo
“ ki vipi? Kama ni faili zote ninazo nini kingine tunahitaji”
“ Tunahitaji kuondoka na veronica”
“Tunaenda na veronica!!?” Afande baraka alishangaa badaa ya kupewa taarifa iyo sababu yeye alikuwa afaham kama wanaenda na Afande veronica kijijini.
Afande mwita aliamua kupanda kwenye gari na kufunga mlango waweze kuzungumza vizuri na afande mwenzake baada ya kuona kama kumuuzi kwa kuumpa taarifra kwa wakati huo
“ Wiki mbili zilizopita niligundua kwamba mama yake veronica alishawahi kuishi kwenye hicho kijiji
Kwahiyo nilimwomba veronica anisadie nafasi niongee na mama yake baadhi ya vitu, alikubali na tukaenda mpka kwao nikaongea na mama yake na moja ya vitu vikubwa alivo nisaidia ni kunipa namba ya mwenyeji ambae atatupokea tukifika.
Afande mwita aliendelea kujielezea.
Ndo nikaona tunaweza kumwitaji veronica nikatuma barau ya kuomba tuongozane nae kwenye kikosi barua ilirudi wamekubali na veronica alikubali pia.
Afande mwita aliweka kituo na kumwacha Afande baraka azungumzie
“ Ukafanya mambo yote hayo ukashindwa kunihisha “
“ Nilikuwa nimepanga nikwambie”
“Lini!?”
“Ndo nipo kukuambia saivi”
“Mimi ni patern wako kwa nini na pia ni rafiki yako ” Afande mwita alishindwa kujibi maswali ya afande baraka vizuri akabaki amekaa kimya japo waswahili wanasema ukimya nao ni jibu. Zilipita sekunde wakiwa wote wako kimya ndipo Afande kuangalia saa yake ya mkononi na kugundua mda umeenda sana.
“Verinoca alikwambia dharura yake inahusu nini”? Mwita alimuuliza Afande baraka taarifa yoyote ambayo inaweza kusaidia kujua veronica kaelekea wapi, akiwa anatoa simu yake mfukoni baraka alitoa jibu.
“Hapana, lakini kipindi nashika simu yake nimpatie niliona inatoka hospitalini”afande baraka alimjibu huku akikumbuka kutokana na uzoefu wake code alizoona kwenye simu ya Afande veronica zilikuwa zinatoka hospitalini.
Afande mwita baada ya kutoa simu yake mfukoni alipiga namba ya afande veronica akakuta haipatikani akaamua kupiga tena majibu yakarudi vilevile kuwa simu haipatikani bado tena akahisi anahitaji kujaribu kwa mara nyingine ya tatu akapiga lakini bado majibu yalirudi namba unayopiga haipatikani jaribu tena baadae. Afande aliishiwa nguvu kabisa akizatama saa ya mkononin inaonesha mida ya saba na robo [13:15] alihisi kuchanganyikiwa, lakini ghafla alipata wazo na kupiga namba moja kwenye simu iliita na kupokewa
“ Halo mama shikamoo”
“ Halo nani”
“Veronica?” Afande mwita alishangaa baada kupiga namba ya mama yake veronica ikapokelewa na binti yake . akaongezea
“uko wapi, na kwa nini umezima simu” Afande mwita aliongea ni kama analalamika
“ nipo hostipitalini mama kazidiwa ghafla, simu yangu imezima chaji na sielewi nafanya nini” alikuwa ni afande veronica akiongea kwenye simu upande wa huku akiongea alikuwa analia.
Hakika afande mwita alijiskia vibaya baada ya kuskia afande anaempenda analia kwenye alibaki kakaa kimya nakuuliza.
“uko hospitali gani”
“ Ya rufaa”
“ Hodi na chumba namba ngapi”
“ Hodi ni A2 chumba namba 13
“ Sawa, nakuja hapo” ilo ndo lilikuwa swali la afande mwita baada ya hapo alikataa simu na kuelekea hospitalini kama alivomwahidi kwenye simu kwamba “nakuja hapo”
Aliwasiri hospitali mida ya saa saba na nusu [13:30] walishuka wote kwenye gari yeye na afande baraka na kuelekea mapokezi, walionesha vitambulisho vyao na afande mwita kuuliza hodi na chumba flani viko uapande gani, walielekezwa na kufika chumbani hapo alipokuwa kalazwa mama wa veronica.
Afande mwita alichokikuta hakukitegemea, alikuta afande ambae anajua ni jasiri na anajiamini alimkuta kanywea kwa kiasi kikubwa sana hata yeye ilimfunja moyo kuona vile.
“Pole”
“ Ahsante”alikuwa ni mwita akitoa pole zake kwa afande veronica
“ Pole shem” ilikuwa ni pole kutoka kwa afande baraka ambayo ilifanya wote wageuke na kumwangalia, Afande veronica alitabasamu kwa mbali huku mwita akiwa haelewi kinachoendelea
afande alikuwa ni mtu wa masiala sana kwahiyo walimpotezea
“ Anaendeleleaje” afande mwita aliuliza kufaham hali ya mama
“Daktari ndo kamaliza kumpima kasema nimwache apumzike” alimjibu mwita akiwa yuko pembene yake akifarijiwa,Baraka akiwa kwa nyuma yao alikuwa akisatababasamu tu kichini chini
Afande Mwita aliendelea kumfariji na kumuuliza kama angekupenda kula nini basi amuagize kiukweli Afande mwita alionesha kumjali sana afande veronica kupita maelezeo na veronica alikuwa ni binti mmoja mrembo sana ilikuwa ni lazima kama wanaume ufutike tu, baadae alipo tazama saa hata afande veronica alitambua mda umeenda na wanasafari inawasubiri
“Itabidi mwende” afande veronica alimwambia huku akimtzama machoni afande mwita
“Unawakika utakuwa sawa ukibaki peke yako”
“Ndio!” alijibu kwa kujiamini
“Sawa” Basi Afande mwita alikuwa hana jinsi baada ya jibu la veronica alinyanyuka alipokuwa amekaa na kumwaga
“ ukihitaji chochote usisite kunipigia simu” Afande mwita aliongea huku akiwa anaelekea mlango wa kutoka
“Sawa” ilikuwa ni jibu la Afande Mwita huku akibaki na sura ya upekwe ulijionesha kabisa
Afande Baraka na Afande mwita waliekea mpka kwenye gari waliokuja nalo aina ya toyota ikifahamika kama [ Defender] waliingia ndani ilikuwa ni majira ya saa nane kamili [14:00] na wanahitaji kufika gamboshi kabla jua halijazama na ni safari isoyo pungua masaa matatu afande mwita aliwasha injini na kuondoa gari kwa kasi kubwa.
 
Je unadhani watafika gamboshi kabla ya jua kuzama nipe maoni yako nishushe sehemu ya tatu
 
SEHEMU YA TATU

Wakiwa wanaendelea na safari afande baraka alikuwa akiendelea kupitia baadhi ya mafaili huku akiangalia huku na kule ndani ya gari ndipo alipo fungua kwenye dashboard na kitu cha kwanza alichoona kwa haraka kilikuwa ni kiboski kidogo kilicho fungwa na matilio ya kung’aa alitaka kujua ni basi alitoa na kuuliza
“Nini hiki”
“Au ndo ulikuwa unataka kumpa veronica hii” aliongezea kabla hata hajajibiwa
“ Iyo ni zawadi nimepewa na mke wang” alimjibu akiwa anamtazama
“alf kwa nini uwaze na nataka kumpa veronica” akaongezea
“Kwani mimi sina macho, mkubwa anaambiwi tazama”
“We unachofikilia hakipo, me mwaminifu”
“ Sawa lakini, macho nayo yanaongea ”
“Chunga usiruhusu watu wakakusoma kilahisi”
“ unamanisha nini.” Afande mwita aliweka kituo na kuuliza baada ya kupewa fumbo ambalo hakulielewa
“ We angalia mbele bana”
“Usije kuniingiza machakani” akaongezea kisha akarudisha zawadi ile pahari alipo ikuta lakini bado alikuwa haamini kama inatoka kwa mke wake na alikuwa anataka sana kujua ina nini ndani.
Afande mwita baada ya kuachwa kwenye fumbo kubwa alikuwa hana budi ya kuendelea kuendesha gari huku waki wapo robo ya safari yao.
Walitembea kilometa nyingi bila kusimama ikafika pahari Afande mwita alikuwa anahitaji kutulia na kutoa haja ndogo pia mda huo afande baraka alikuwa kapitiwa na usingizi, alishuka kwenye gari na kwenda kichaka kilichokuwa pembene ya barabara. Kipindi anatoka kujisaidia aliona watu wakiwa kwenye msululu wakiwa wanavuka barabara aliwatazama kwa mbali na alielekea kwenye gari, aliingia na kuwasha injini na kuondoa gari lakini baada ya kuendesha akiwa kwenye kasi ghafla watu aliona wanavuka barabara kwa mbali walitokea kwa mbele ndipo alipo minya bleki kwa kasi kubwa nusra awagonge mpka afande baraka shituka usingizi
“Mungu wangu nakufa!” alikuwa ni afande baraka baada ya kushituka kwenye usingizi mzito
Afande mwita alikuwa bado katahamaki haelewi nini kimetokea,mikono ikiwa ipo kwenye ushukani akiwa hata haskii afande baraka akimsemesha
“oya kaka” afande mwita alimshutua afande mwita kwa kupiga makofi kumtoa kwenye kitu kama msongo wa mawazo
“Naam”
“kaka utaniua na presha”
“ unajua kuendesha familia, gari inataka kukushinda” akaongezea
Afande mwita hakujibu chochote alichukua chupa ya maji na kunywa alijisahau na kuiweka pembene huku akiwa ajaifunga na kuwasha injini ndipo kichupa kilidondoka na kumwaga maji
“ Ah kaka nini tena”
“ uko sawa kweli?” afande baraka alipata wasiwasi
“ Ndio kaka” aliwasha injini kwa mara nyingine baada ya gari kuwa limezima na kuendelea na safari.
Baada ya kutembea robo tatu ya safari walipita kibao kimoja kilichopo pembene upande wa kulia wa barabrara ambacho kilikuwa na kutu lakini kinaonekana kinasomeka “Gamboshi Kilometa 12”
Walikipita baada ya kama dakika kumi na tano gari lao lilizima injini ndipo walipaki pembene
“Shida nini tena “ Afande mwita alijiuliza
“ Hii gari imeshachoka” Afande baraka alimjibu akiwa anashuka kwenye mwita nae alifwata na kwenda kufungua boneti ya gari kutazama kuna shida gani
Alitazama kwa sekund lakini sababu yeye hakuwa mtaalamu wa magari alirudishia boneti kwanza na kuchukua simu yake mfukoni alipo washa alikuta mnara wa mtandao umebaki mmoja kwenye ndipo alikumbuka alipewa namba za mwenyeji atakae wapokea, aliwahi na kufungua mlango wa gari lakini mda anaangaza aliona karatasi ndogo imeloana na majI
“Aaaah baraka!”
“Nini hiki” akaongezea huku akiwa kaishika karatasi ndo iliyokuwa na namba za simu za mtu atakae wapokea watakapo fika
“We ndo ulimwaga maji” alijibiwa na afande baraka
“ Sa tunafanyaje” aliuliza tena
“Kwani ulikuwa hujasave kwenye simu” Afande baraka aliuliza
“Hapana” Alijibu huku akipitia phonebook yake
“ Tuko karne ya 20 na unashindwa kusave kitu cha msingi kwenye simu unaacha kwenye karatasi”
“Sasa unanambia au unafoka” Afande mwita aliuliza huku akimtazama
“ Hapa cha kufanya ni kutafuta plan b” akaongezea
“Kuna plan b” Afande baraka akauliza
“Haipo ndo naifikiria”
“ Tupo katikati ya poli wewe upo kufikiria plan b”
“Sasa unataka nifanye nini”
“Wewe unawazo gani” Afande mwita aliuliza
“Sina!” Afande baraka alimjibu huku akiendelea kumtazama
Afande mwita aliangaza huku na kule na kweli walikuwa katikati ya poli na mda unaenda hajui afanye, alichukua maamuzi ya kushuka kwenye kichaka kilicho pembene yao na kumwacha afande akiwa kasimama mbele ya gari
“Plan b yako ni kunitelekeza hapa!?” Afande baraka aliuliza huku akimtazama afande mwita akiishiria kwenye machaka, alibaki peke yake akiangalia huku na kule lakini kulikuwa hakuna dalili ya kupata msadaa.
Afande akiwa kichaka alikuwa akitembea bila kujua anaelekea wapi alitembea kwa mwendo wa dakika kumi ndipo alisikia sauti ikitokea nyuma yake na kumwita “Mwita choma Maige” aligeuka kwa kasi na kutoa buduku yake aina ya pisto iliyokuwa kwenye pembene ya kiuno chake. Aliinyoosha kwa mtu huyo alikuwa ni mzee sio chini ya miaka 40 afande mwita alimtazama na kuuliza
“We nani?”
“Weka bunduki chini” mzee huyo alimwambia bila wasiwasi
“Naongea kwa mara ya mwisho sitarudia”
“We nani?” alimwambia huku akiweka bunduki yake tayari kwa kupiga
Mzee huyo aliuliza swali moja ambalo lilimfanya afande baraka arudishe bunduki yake ilipokuwa
“Yuko wapi Veronica”
“ Nimeamwacha hosipitali” alijikuta hakijibu bila kutaka huku akilegeza mikono yake
“Na wewe ni nani yake”
“Mme wake” akaongezea
“Hapana, Boss wake” alijibu akiwa anamtazama kwa makin sana
“Haya basi twende kijijini” Mzee alimwambia huku akimwosha njia kwa mkono
“Kuna askari mwenzangu nilimwacha kwenye gari “
“Naomba tumwende” akaongezea
“Kuna mtu mwingine tofauti na veronica?” mzee aliuliza kwa mshangao ambayo hata Afande mwita hakuelewa. Afande mwita aliongoza njia kwenda kumrudia alipo mwacha afande baraka lakini wakitembea walikutana nae njia kabla hata hawajafika mbali
“Mkuu”
“Ulikuwa umeenda wapi?”afande baraka aliuliza
“Na huyo ni nani”Akaongezea
“Mwenyeji wetu”
“Umempataje”
“Ilo sio swali” Afande mwita alimjibu na kumgeukia yule mzee na kumwambia tunaweza kwenda
Mzee aligeuka kulia kwake na kuongoza njia huku afande mwita na baraka wakifwata.
Ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja jioni walitembea kufikia mpaka afande baraka kuhitaji maji ya kunywa aliona maji yakitililika na kuamua kusogea pale alipotaka kutafuta namna aweze kunywa maji mzee alimkataza na kusogea karibu yake alichukua jani dogo na kuchukua tone ya maji yaliyokuwa yakitililika akamwambia ageuke mkono wake afande baraka alifanya ivo alimwekea yale maji juu ya mkono wake ndipo afande baraka alihisi kama kuna moto umedondoka kwenye mkono wake alishutka na kurusha mkono juu, Yule mzee hakuongea mengi aliendelea kuwa ongoza walitembea kwa mda wa masaa mawili walifika gamboshi mida ya saa moja jion cha kushangaza palikuwa kimya hamna kelele wala mtu hata mmoja afande mwita ndoa alikuwa haelewi
“Ndo hapa?” aliuliza akiwa hana wakika na swali lake
“Ndio” mzee alimjibu bila kumtazama huku akiendelea kutembea
“Wanasema huku usiku huwa ni ulaya mbona buza pazuri sasa” Afande baraka alijuliza mwenyewe bila kupata jibu
Walikuwa kitembea huku kila hatua waliyokuwa wakitembea ilikuwa ikisikika, mpaka walipofika kwenye nyumba ndogo pia napo kulikuwa kimya kabisa mzee aliwafungulia mlango palikuwa giza akawaambia waingie walianaglia na kuingia kishingo upande aliwafungia mlango na kuwasha taa kwa nje akawaogaza kwa kuwaambia pumzikeni afande baraka alipo jaribu komeo palikuwa pamefungwa kwa nje
“Huyu mzee vipi”
“Kafunga kwa njee” alijiuliza mwenye huku akimtazama afande mwita akiwa tayari kashasinzia sababu ya uchovu wa kutembea na kuendesha gari na yeye alibakiwa hana njisi na kujilaza na kupumzika kama walivoambiwa na mzee yule nae alielekea kitandani na kupumzika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom