HADITHI: Damu, mabusu na machozi

HADITHI: Damu, mabusu na machozi

SEHEMU YA 09


Mzee Katobe alipofikishwa kituoni alitoa maelezo yake huku akitetemeka na kubabaika na kuwafanya askari wawe na wasiwasi zaidi juu ya tukio hilo, ilibidi atupwe mahabusu na polisi wakamchukua mke wake kwenda nyumbani kufanya upekuzi! Njia nzima mama huyo alikuwa akilia lakini upande mwingine wa moyo wake aliamini nyumbani wasingepata kitu chochote cha kuwasaidia polisi, kama ni bunduki mzee Katobe alikuwa akiimiliki kihalali. Wasiwasi wake ulikuwa ni damu iliyokuwa imetapakaa sakafuni.
“Kama wataikuta ile damu kwa kweli lazima baba Nancy atakuwa kwenye matatizo, sikumbuki tuliporudi nyumbani kama niliangalia vizuri sebuleni!” Aliwaza mama Nancy akijaribu kukumbuka.
Walipofika mama yake Nancy alifungua mlango macho yake yakiwa sakafuni, hakuna hata tone la damu! Mzee Katobe alisafisha wakiwa hospitali, furaha ikamjaa moyoni mwake na maaskari zaidi ya watano wakamiminika ndani ya nyumba na kuanza shughuli ya kupekua wakimulika tochi kila mahali, bunduki ilipatikana chumbani walipoomba kitabu cha kumiliki, mama alikifuata mahali kilipokuwa na kuwakabidhi.
“Ilitumika mara ya mwisho lini?”
“Mimi sifahamu! Sijaona ikitumika!”
“Una uhakika?”
“Ndiyo!”
Upekuzi uliendelea sebuleni, makochi yalinyanyuliwa na uhamishwa sehemu yalipokuwa! Kwa dakika kumi na nzima maaskari walikuwa sebuleni, wakikaribia kuondoka baada ya kutokupata kitu chochote cha kuwasaidia! Askari mmoja alipiga kelele wote wakageuka na kumwangalia.
“Vipi?”
“ Ganda la risasi!” Alisema askari huyo na wote wakamkimbilia!
“Wee mama unatudanganya?”
“Ah! Unajua….. Unajua!….!” Mama Nancy alikosa cha kuwaeleza!
“Sema ukweli?”
“Kwa kweli sifahamu haya mambo labda muulize mwenyewe!” Aliongea Mama Nancy na baadaye akaanza kulia machozi.
Ganda la risasi lililopatikana lilitosha kabisa kuunganisha na maelezo ya Danny ili kumtia mzee Katobe hatiani, walirudi kituoni na kutoa taarifa kwa mkuu wa kituo! Hawakuwa na shida tena na mama Nancy hivyo walimwachia aondoke zake, hakukuwa na dhamana yoyote kwa mzee Katobe.
****
Ilikuwa tayari saa sita ya usiku wakati mama Nancy anaondoka kituoni, hakutaka kwenda nyumbani tena wakati huo bali wodini ambako aliamini mtoto wake Nancy alikuwepo na pia alitaka kufahamu hali ya Danny kwa wakati huo, ni yeye peke yake aliyekuwa tegemeo katika tatizo lililokuwa linamkabili mzee Katobe! Kama angesema kweli alipigwa risasi na mzee Katobe basi mume wake angefia jela na huo ndio ungekuwa mwisho wa kila kitu lakini kama angekanusha, ni wazi hata kama polisi wangefanya kitu gani wasingekuwa na uwezo wa kumtia mume wake hatiani lazima mzee Katobe angeachiwa huru.
Wodini kama alivyokuwa amefikiria alimkuta Nancy akiwa amekaa pembeni mwa kitanda cha Danny, alikuwa akilia machozi.
“Vipi mwanangu?”
“Hamna tatizo mama!”
“Mbona sasa unalia?”
“Danny amebadilika!”
“Amebadilika!”
“Ndiyo!”
“Kwanini?”
“Anasema kama siwezi kukubali kufanya naye ngono na mwisho kuwa mke wake, atasema ukweli kuwa baba ndiye alimpiga risasi!” Aliongea Nancy kwa uchungu akijifuta machozi.
Neno ngono lilikuwa marufuku katika maisha yake, kiapo alichokula kwa mganga bado alikikumbuka! Hakuwa na ruhusa ya kufanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine yeyote isipokuwa Tony! Kama angediriki kufanya hivyo lazima angepata madhara na madhara yenyewe aliyakumbuka, ni kufa au kuwa mwendawazimu.
Ni kweli alimpenda baba yake lakini asingediriki kumvulia Danny nguo yake ya ndani na kufanya naye mapenzi, alikuwa katika wakati mgumu kupita kiasi kufanya maamuzi! Aidha afanye ngono awe mwendawazimu au agome kufanya ngono Danny aseme ukweli juu ya kilichotokea na baba yake, ngome yake na kila kitu kwake apatikane na hatia na kufia jela! Nancy alimwaga machozi mbele ya mama yake.
“Unasema kweli?”
“Kweli kabisa mama! Ndivyo alivyoniambia!”
Mama yake Nancy alimgeukia Danny na kumwangalia kwa macho ya huruma kisha kuanza kumuuliza kama yaliyosemwa na Nancy yalikuwa na ukweli wowote, Danny alikiri na kumwambia mama yake Nancy juu ya mapenzi aliyokuwa nayo kwa mtoto wake na hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee ya kumpata.
“Baba! Baba! Baba! Nakubembeleza tafadhali, usifanye hivyo!”
“Kwanini mama? Kwani kuna tatizo gani mimi kuwa na mwanao? Hivi nyinyi hamuoni kama mmeniumiza? Kwa kweli kama Nancy hatakubali kufanya hivyo nitasema ukweli, sidanganyi!” Alimaliza Danny na kugeukia ukutani.
Nancy aliinamisha kichwa chake chini, alijuta ni kwanini alikula yamini kwa mganga! Alitamani kubadilisha mambo, awe huru na kukubali kufanya ngono na Danny ili kumwokoa baba yake, maisha ya baba yake yalikuwa mikononi mwake!
“Kesho nitakwenda Mlingotini nikamtafute huyo mganga, nimweleze yote yaliyotokea na kama kuna namna yoyote ya kuniondolea Yamini hii ili niokoe maisha ya baba yangu basi ifanyike kwa gharama yoyote ile!”
Saa tisa na nusu ya usiku aliondoka hospitalini na kwenda hadi nyumbani, Nancy hakulala! Saa kumi na mbili ya asubuhi bila kumuaga mama yake aliondoka nyumbani akitembea kwa miguu kwenda Mlingotini, bado alikumbuka mahali nyumba ilipokuwa! Jua lilipochomoza tayari alikuwa kijijini Mlingotini, alishangazwa na hali aliyoikuta nyumbani kwa mganga. Nyumba ilikuwa imeanguka na hapakuwa na dalili ya mtu yeyote kuendesha maisha katika eneo hilo.
Hakuelewa nini cha kufanya, alianguka chini na kulia kwa uchungu! Dunia ilikuwa imembadilikia, kila kitu katika maisha yake kilikuwa kimejisokota kuanzia kwa Tony hadi kwa Danny na baba yake mzazi!
Akiwa amelala chini aliweza kuona makaburi mawili pembeni yake, akawa na uhakika kuwa pengine mganga wa kienyeji alifariki dunia!
“Nitafanya nini mimi?”
Nancy aliendelea kulia akiwa amelala ardhini, mawazo yalimjaa kichwani na alishindwa kuelewa angefanya kitu gani kama mganga aliyemlisha yamini asingepatikana! Alitamani kufa na kuiacha dunia lakini alipofikiria sana aliona hilo halikuwa jibu sahihi la kutatua matatizo yake ukizingatia tayari baba yake mzazi alikuwa mahabusu na alitakiwa kufanya lolote ili atoke.
“Inavyoonekana Danny hatanii na sijui ni kwanini baba naye alimpiga risasi? Amedhamiria nifanye naye ngono, lakini mimi siwezi mpaka niondolewe yamini!” Aliendelea kuwaza huku akilia.
Mara ghafla alisikia sauti za wanawake wakiongea nyuma yake, akanyanyuka na kukaa kitako, wanawake watatu walisimama njiani wakiwa na ndoo mikononi mwao jambo lililoashiria walikuwa wakienda kisimani kuteka maji. Walisimama hapo kwa muda bila kusema chochote na Nancy wakiendelea kunong’ona wao kwa wao kwa sauti za chini.
Baadaye aliwashuhudia wakikatisha njia na kutembea kwenda mahali alipokuwa amekaa.
“Vipi binti?” Walimuuliza baada ya salamu.
“Nina shida na mzee aliyekuwa akiishi katika nyumba hii!”
“Yule mganga?”
“Ndiyo! Jina lake nimelisahau kidogo!”
“Mzee Mwinyimkuu!”
“Ndiyo!”
“Mbona hayupo muda mrefu!” Aliongea mwanamke mmoja, taarifa hiyo ilimpa matumaini Nancy aliyehisi mganga alishafariki dunia.
“Kwa hiyo kumbe hajafariki?”
“Haya makaburi unayoyaona ni ya mke na mtoto wake, walifariki ghafla yeye akadai wachawi wa Bagamoyo wanamchezea akaamua kuhama!”
“Alihamia wapi?”
“Tabora!”
“Mjini?”
“Hapana! Kijiji kimoja kinaitwa Kisanga!”
“Una uhakika?”Aliuliza Nancy
“Uhakika ninao si alikuwa jirani yetu na alituaga wakati wa kuondoka! Kwani una shida gani naye?”
“Matatizo ndugu yangu!”
“Matatizo gani?”
Badala ya kujibu Nancy aliangua kilio tena jambo lililowafanya akinamama hao watamani kudadisi zaidi na zaidi ili kuelewa kilichokuwa kinamsumbua, mara ya kwanza alisita kueleza lakini baadaye alijikuta akilazimika kufungua mdomo wake na kusema ukweli! Wote walishika mikono vichwani mwao na kumsikitikia.
“Pole sana shoga! Kwanini ulikubali kufanya hivyo?”
“Mapenzi! Nilimpenda sana mpenzi wangu”
“Yuko wapi kwa sasa?”
Nancy akaangua kilio kwa mara nyingine tena, swali hilo lilimkumbusha Tonny mwanaume katili asiye na shukurani aliyemfanyia unyama mkubwa kuliko mwingine wowote katika maisha yake! Maumivu makali yaliuchoma moyo wake. Wanawake wale walizidi kumbana wakitaka kufahamu.
“Aliniacha! Sababu ya mwanamke mwingine ndiyo maana nahangaika kuiondoa hii yamini ili niweze kupata mchumba mwingine na kuolewa”
“Shoga! Acha nikupe ushauri, usijaribu kufanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine kabla hujaiondoa yamini! Nimeshaona wengi sana hapa Bagamoyo na hata Dar es Salaam wakiokota makopo sababu ya kukiuka kiapo!”
“Sasa mimi nifanye nini jamani?” Aliuliza Nancy!
“Nakushauri uende Tabora ukamtafute mganga wako, uongee naye ili akuondolee! Narudia tena usijaribu kufanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine tofauti na yule wa mwanzo!”
“Wa mwanzo hanitaki kabisa!”
“Basi nenda kamtafute mganga wako, tena simama upesi uondoke usifanye mchezo!” Alimaliza mwanamke mwingine.
“Unaitwa nani dada?” Nancy aliuliza wakati akisimama.
“Naitwa Mwamtumu! Wewe je?”
“Naitwa Nancy!”
“Unaishi Dar es Salaam?”
“Ndiyo!” Aliitikia tu ingawa alijua si jibu la swali alilokuwa ameulizwa.
Nancy hakuwa na la kufanya, mwili wake wote ulikuwa umelegea na akili yake yote kuchanganyikiwa! Alihisi hakuna msaada kutoka mahali popote zaidi ya mganga wa kienyeji aliyepandikiza yamini mwilini mwake, huyo ndiye mtu pekee ambaye angeweza kutatua matatizo yake kwa wakati huo.
Je nini kitaendelea?
Je Nancy atampata mganga huyo?
 
SEHEMU YA 10


Alitamani kumshirikisha mama yake katika tatizo alilokuwa nalo lakini alishindwa angeanza vipi! Alihisi angeonekana mjinga. Alitembea kwa unyonge kichwa chake kikiwa kimejaa mawazo mengi, mbele kidogo alitengana na akina mama aliokuwa nao na yeye kuendelea na safari hadi nyumbani kwao.
Hakumkuta mama yake lakini mlango ulikuwa wazi, alifungua na kuingia, mezani alikuta kipande cha karatasi na kukichukua, juu yake kiliandikwa jina lake, ilikuwa ni barua kutoka kwa mama yake! Aliisoma mwanzo mpaka mwisho, hayakuwa maneno mengi zaidi ya taarifa kuwa mama yake aliondoka kwenda kituo cha polisi kama yeye Nancy angeweza basi amfuate huko.
“.....lazima niondoke kwenda Tabora sasa hivi! Tena imekuwa vizuri sijamkuta mama!” Aliwaza Nancy akikimbia kwenda chumbani kwake ambako alianza kupanga nguo katika begi, kutoka hapo alikimbia tena chumbani kwa wazazi wake, alielewa mahali pesa zilipohifadhiwa! Hivyo alichofanya ni kufungua kabati na kutoa shilingi milioni moja katika pesa zilizokuwepo.
“Mama atanisamehe sana! Nafanya hivi kumsaidia baba, ninachotakiwa kufanya sasa hivi ni kuwahi Tabora haraka iwezekanavyo na kama nitamkuta huyo mganga na akaniondolee balaa nililonalo mwilini nitarejea haraka iwezekanavyo nikiwa tayari kufanya lolote na Danny!” Aliwaza Nancy.
Alitoka ndani ya nyumba yake na kukimbia mbio hadi stendi ya basi ambako alipanda daladala lililomchukua moja kwa moja hadi katikati ya jiji la Dar es Salaam ikiwa tayari ni saa tano na nusu mchana, hakutaka kwenda mahali kokote zaidi ya stesheni ya treni na kukata tiketi ya daraja la tatu.
“Nitakwenda hivyo hivyo kwa taabu ili mradi nimpate huyo mganga!” Aliwaza baada ya kukata tiketi yake.
Alibaki stesheni hadi saa 11 jioni muda wa kuingia katika mabehewa ulipofika na saa kumi na mbili treni ya abiria kwenda Kigoma na Mwanza iliondoka Nancy akiwa mmoja wa abiria. Moyoni alijawa na huzuni isiyo na kipimo, maisha yake yalikuwa yamecheza tikitaka na kujikuta akiwa kichwa chini miguu juu, furaha yote aliyowahi kuwa nayo ilikuwa imepotea na aliamini yote hayo yalisababishwa na Tonny! Alimchukia mwanaume huyo kuliko kitu kingine chochote.
“Sitamsahau Tonny! Na sitampenda mwanaume na kama ikitokea nikafanya tendo la ndoa na Danny, nitakuwa nimefanya kwa sababu nataka kumsaidia baba yangu! Vinginevyo nisingediriki kufanya hivyo!” Aliwaza Nancy wakati treni ikizidi kukata mbuga kuelekea Morogoro, hakulala usiku mzima akiwaza na wakati mwingine alilia machozi, mawazo juu ya baba yake aliyekuwa akiteseka mahabusu hayakumwacha.
Kulipokucha asubuhi walikuwa Dodoma, kulikuwa bado kilometa nyingi sana mbele yake kabla ya kufika Tabora, alitamani kupaa na kufika Tabora dakika hiyo hiyo.
Kutwa nzima alikuwa ndani ya treni akisafiri bila kula wala kunywa chochote! Mdomo wake ulikuwa mchungu kupita kiasi, hakutamani kula chochote alichohitaji wakati huo ni kukutana na mganga tu basi hakuna kingine hapo ndipo angeweza kula chakula kwa furaha.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kusafiri kwa usafiri huo na hata kuwa nje ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani! Ilikuwa ni safari iliyompeleka mbali na alikokulia, mahali asikomfahamu mtu yeyote, bila wazazi wake kuelewa kwamba alikuwa amesafiri! Kwake huo ulikuwa ni uamuzi mkubwa kupita kiasi.
*****
Saa tatu usiku treni liliingia Tabora na watu kuanza kuteremka, tangu Dar es Salaam hadi anashuka behewani alikuwa bado hajafungua mdomo wake kuongea na mtu! Lakini alipokanyaga ardhi ya Tabora alilazimika kuuliza kwani hakuelewa hata hicho kijiji cha Kisanga kilikuwa umbali gani kutoka mjini Tabora.
“Dada habari yako?” Alimwita dada mmoja aliyekuwa akipita mbele yake huku akiwa na begi mkononi pamoja na mtoto mdogo mgongoni, alimwamini mama huyo kwa namna alivyoonekana! Tabora ilitisha kwa vibaka katika kipindi hicho, asingeweza kumuuliza mtu yeyote aliyemwona.
“Nzuri tu!”
“Naomba nikuulize!”
“Uliza tu!”
“Unakifahamu kijiji cha Kisanga?”
“Ndiyo ninakokwenda!”
“Kweli?”
“Kwanini unauliza kwa mshangao?”
“Kweli Mungu ni mkubwa! Hata mimi nakwenda huko huko na ni mgeni kabisa, hata hapa Tabora ni mara ya kwanza kufika!”
“Unakwenda kwa nani Kisanga?”
“Mzee Mwinyimkuu!”
“Mwinyimkuu gani?”
“Ni mganga wa kienyeji!”
“Ahaa! Huyo namfahamu!”
Moyo wa Nancy ulijaa furaha isiyo kifani, bila kutegemea alijikuta akishangilia na kumfanya mwanamke aliyekuwa mbele yake ashangae na kutaka kufahamu ni kwanini alifurahia kiasi hicho.
“Ni babu yangu sijamwona muda mrefu sana, nilikuwa nje ya nchi nikisoma na niliporudi nikakuta alihamia Kisanga!”
“Wewe ni mwenyeji wa Bagamoyo? Maana nasikia huko ndiko alitokea”
“Ndiyo!”
“Basi umefika!”
Nancy hakuwa tayari kuyaamini masikio yake kutokana na kauli alizozipata kutoka kwa mwanamke aliyekuwa mbele yake, hakutegemea kama ingekuwa rahisi kiasi hicho kumpata mzee Mwinyimkuu na hapohapo alianza kumshawishi mwanamke huyo waondoke mara moja kwenda Kisanga.
“Kisanga saa hizi?”
“Ndiyo!”
“Hakuna magari mpaka kesho!”
“Kwani hakuna gari la kukodi?”
“Kama pesa unazo litapatikana!”
“Unafikiri inaweza kuwa shilingi ngapi?”
“Sielewi labda twende stendi tukaulize!”
“Nafurahi sana kukutana na wewe dada! Umekuwa msaada mkubwa sana kwangu!” Alisema Nancy wakati wakiingia kwenye teksi.
“Dereva unapafahamu Kisanga?”
“Ndiyo!”
“Tunaweza kupata gari la kutupeleka huko?”
“Kama pesa ipo hata mimi naweza!”
“Shilingi ngapi?”
“Ipo sitini elfu?”
“Nikikupa hamsini huendi?”
“Poa!”
“Basi nyoosha moja kwa moja!”
Mambo yalizidi kumshangaza Nancy kwa jinsi yalivyokuwa yakienda bila mkwamo wa aina yoyote, alipata picha kuwa alikokuwa akielekea pia yangekwenda hivyo hivyo na ikiwa mganga angefanya kazi ya kumwondolea yamini usiku huo basi siku iliyofuata angerejea Tabora na kupanda tena treni au basi kurejea Dar es Salaam, hiyo ndiyo mipango iliyoendelea kichwani mwake wakati gari likipita katika mabonde kuelekea Sikonge.
Waliingia wilayani Sikonge saa saba usiku, Nancy akiwa amechoka taabani sababu ya ubovu wa barabara na safari ya siku mbili, hawakutaka kusimama walinyoosha moja kwa moja wakipita katika barabara mbovu katikati ya mashamba ya watu.
“Mh! Huku mbunge wenu nani?”
“Ah! bwana wee, sisi tulishajizoelea, nyie watu wa mjini ndio mnateseka!”
“Kwa kweli mna shida!”
“Lakini tumekaribia, kutoka hapa hadi Kisanga ni kama kilometa mbili!”
“Afadhali!”
Nusu saa baadaye sababu ya ubovu wa barabara waliingia kijijini Kisanga, kila sehemu ilikuwa giza na nyumba zilionekana kwa taabu sana chini ya miembe mikubwa! Haikuwa rahisi kwa Nancy aliyezaliwa na kukulia mjini kuamini kuwa binadamu waliishi eneo hilo. Palionekana porini zaidi kuliko makazi ya watu.
“Twende kwanza nikupeleke wewe, ndio mimi nitakwenda nyumbani!”
“Nashukuru sana kwa kipaumbele ulichonipa!” Nancy aliongea.
Alikuwa amefurahi mno kufika kijijini Kisanga na hatimaye angekutana na mzee Mwinyimkuu mkombozi wa maisha yake kwa wakati huo, alipomuuliza mwanamke aliyekuwa naye ndani ya gari ambaye tayari alishamfahamu kwa jina la Mariam juu ya ni lini alimwona mzee Mwinyimkuu kwa mara ya mwisho.
“Miezi miwili iliyopita kabla sijaondoka kwenda Morogoro alikuwepo!”
“Kwa hiyo bado yupo?”
“Lazima, atakwenda wapi? Dereva simama hapo!” Mariam alimwamuru dereva wa gari na akakanyaga breki na kuegesha pembeni.
“Nancy umefika twende nikusindikize!” Aliongea mwanamke huyo wakishuka garini, giza lilikuwa kila upande! Nancy alizidi kutishika.
Begi lake likiwa mkononi walianza kutembea pamoja wakielekea bondeni, mwendo wao ulikuwa wa taratibu sababu hawakuwa na tochi! Ghafla Mariam alisimama.
“Mh!” Aliguna.
“Vipi?”
“Mbona pako hivi?”
“Pakoje?”
“Hapa ndio nyumbani kwa mzee Mwinyimkuu lakini pananishangaza, sikupaacha hivi!”
Ingawa ilikuwa katikati ya usiku, pamoja na giza kutanda kila upande, bado Nancy na Mariam walikuwa na uwezo wa kuona nyumba zote zikiwa zimeteketezwa kwa moto! Mariam alishika mikono kichwani mwake, akiwa haelewi nini kilitokea wakati akiwa hayupo! Aliogopa kuonekana mwongo na kuwa amemsumbua Nancy kumtoa mjini Tabora hadi Kijijini Kisanga bila sababu yoyote.
“Hakyanani kabisa dada, mzee Mwinyimkuu alikuwa hapa sijui kitu gani kimetokea wakati mimi nikiwa Morogoro!” Aliongea mwanamke huyo akiwa na mtoto wake mgongoni.
Nancy alikuwa kimya, mwili wake wote ukitetemeka, furaha yote aliyokuwa nayo iliyeyuka akagundua safari ya kumtafuta mzee Mwinyimkuu ilikuwa haijafika mwisho na hakufahamu angeimaliza lini na vipi! Ilikuwa ni lazima aendelee kumtafuta mganga huyo hadi ampate na kumwondolea Yamini aliyomwekea mwilini mwake.
“Laiti ningejua nisingefanya kitendo hiki, nilimwamini mwanaume ambaye baadaye alikuja kunisaliti! Mapenzi, mapenzi ni kitu kibaya sana!” Aliongea kwa sauti Nancy.
“Kwani kuna nini mdogo wangu?” Mariam aliuliza Nancy akiwa amekaa chini akilia, alikuwa akimfikiria mama yake na baba yake aliyekuwa mahabusu kwa kosa la kumpiga risasi Danny!
Maisha yalikuwa yamemgeuka, kila kitu kilionekana kuwa adui yake, alishindwa kuelewa ni kwanini alikuwa katika hali hiyo, imani yake kwa Mungu ilianza kupungua! Isingewezekana kama kweli Mungu angekuwepo amwache yeye ateseke kiasi hicho.
“Kwani kuna nini mdogo wangu? Unaumwa? Bahati mbaya hujanieleza nini tatizo lako, hivi kweli huyu mzee ni babu yako tu au kuna kitu kingine?” Mariam aliuliza maswali mfululizo baada ya kuona Nancy hajajibu swali lake la mwanzo na kuendelea kulia.
Picha hiyo ilimwonyesha Mariam wazi kwamba kulikuwa na tatizo katika akili ya Nancy na si tatizo dogo pengine yeye angekuwa wa msaada kwake katika kipindi hicho ukizingatia Nancy hakuwa na ndugu yeyote Kijijini Kisanga.
“Sio babu yangu!” Nancy aliamua kueleza ukweli.
“Sasa tatizo ni nini? Na kwanini unamtafuta?”
“Niliwahi kufanya makosa Fulani katika maisha yangu!”
“Makosa gani?”
Badala ya kujibu Nancy aliangua kilio tena, ikabidi Mariam akae naye kwenye nyasi na kuanza kumbembeleza ili aeleze ukweli, kwikwi ya kulia ilipomwachia Nancy alijikaza akafungua mdomo wake na kuanza kueleza kilichotokea, Mariam alisikitika kupita kiasi.
“Sikulaumu Nancy! Hata mimi ningeweza kufanya hivyo, ni wazi ulimpenda sana Tonny lakini alikusaliti, Mungu anajua jinsi ya kukufariji! Furaha yako inakusubiri mbele, hata hivyo nisingekushauri ufanye tendo la ndoa na mwanaume mwingine kabla hujampata mzee Mwinyimkuu, ni hatari! Haya mambo si ya kufanyia mchezo, rafiki yangu mmoja naye alifanya mchezo huu huu, sikutishi hivi ninavyoongea na wewe ni marehemu, yeye na mwanaume waliyetembea naye waling’ang’aniana hadi kifo!” Mariam aliongea na kuzidi kumtia hofu Nancy.
“Sasa nifanye nini dada? Nitampata wapi huyu mzee ili aniondolee hii balaa mwilini mwangu? Haya ni mateso na si mshauri mwanamke mwingine afanye kitendo hiki! Hata kama anampenda mwanaume kiasi gani!”
“Twende nyumbani tukalale, kesho tukiamka tutaulizia vizuri hapa kijijini nini kilitokea nyumbani kwa mzee Mwinyimkuu, si ajabu yupo hapahapa kijijini lakini amehamia sehemu nyingine!” Aliongea Mariam na kumpa matumaini Nancy, moyoni aliamini lazima mzee Mwinyimkuu alikuwa sehemu fulani kijijini na siku iliyofuata wangempata.
Je nini kitaendelea?
Je Nancy na Mariamu wataweza kumpata Mwinyimkuu?
 
SEHEMU YA 11


Walitembea hadi barabarani ambako wote waliingia tena ndani ya teksi waliyotoka nayo Tabora na kuendelea na safari yao kwenye majengo mawili makubwa ya bati, Mariam akamwamuru dereva asimame.
“Simama hapo pembeni ya hizo nyumba!”
“Hapa ndio nyumbani kwenu?”
“Ndiyo! Baba yangu ni mganga katika hii hospitali!”
“Wewe ni mtoto wa Mabula na mke wake Elizabeth?” Dereva aliuliza
“Ndiyo! Unawafahamu?” Aliitikia Mariam
“Mimi ni mtu wa Sikonge na hakuna mtu asiyewafahamu watu hawa katika wilaya yetu! Tiba zao zimewasaidia wengi sana!”
“Basi hao ndio wazazi wangu na mimi naishi nao hapa nyumbani ila nilikuwa nimekwenda kumtembelea mjomba wangu Mikumi huko Morogoro, karibu sana!” Aliongea Mariam akisaidia kushusha mizigo kwenye gari.
Wakati wakiongea hayo Nancy alikuwa kimya, kichwa chake kilijaa tani kadhaa za mawazo, alishindwa kuielewa hati yake kama asingempata mzee Mwinyimkuu, alitamani kufa badala ya kuendelea na maisha ya mateso. Kumbukumbu za wazazi wake zilizidi kumchanganya na kuna wakati Tonny aliingilia kati, alimtupia kila aina ya lawama kama mtu aliyeharibu maisha yake yote.
“Tonny! Sijui kama naweza kumsamehe!” Aliwaza Nancy wakati akishuka na wote wakaagana na dereva wa teksi na kuongoza kwenda mbele ya nyumba iliyokuwa pembeni, Mariam akagonga kwa muda wa karibu dakika kumi ndipo mlango ukafunguliwa.
“Wawooooo! Karibu tulimo mkaya!”(Haooooo! Karibuni ndani!) Mama yake Mariam alisema wakati akiwapokea mizigo yao na kuwakaribisha ndani ambako salamu ziliendelea.
Baba yake Mariam baadaye aliungana nao ikawa ni furaha kubwa katikati ya usiku, kama ilivyo kawaida ya Wanyamwezi mama yake Mariam alinyanyuka akitaka kwenda jikoni kuandaa chakula lakini mwanae akamzuia akidai ulikuwa ni usiku mkubwa mno wangeweza kuvumilia.
“Sasa wewe unaongea, je kama mgeni ana njaa?” Mama yake Mariam aliongea huku akitabasamu.
“Hapana mama, sijisikii kula kabisa!” Nancy aliingilia kati ni kweli kwa mawazo aliyokuwa nayo kichwani mwake asingeweza kutia kitu chochote mdomoni, alichohitaji wakati huo hakikuwa chakula, kinywaji au kitu chochote cha kupitia mdomoni! Alichohitaji ni mzee Mwinyimkuu, bila yeye aliamini maisha yake yasingekuwepo tena hivyo hapakuwa na haja ya kula chakula.
Hawakuongea kitu chochote zaidi, kilichofanyika ni kuwaandalia mahali pa kulala na wote wakaingia chumbani bila hata kuoga na kujitupa vitandani mwao.
Mariam akilala na mtoto wake na Nancy peke yake, hakupata hata lepe la usingizi hadi asubuhi, kazi yake ilikuwa ni kuhesabu mabati huku akiwafikiria wazazi wake na maisha yake mara milioni na zaidi, alitamani kuche haraka ili aulizie mahali alipohamia mzee Mwinyimkuu lakini masaa yalikwenda kwa mwendo wa kinyonga.
Mpaka asubuhi, Nancy alikuwa bado akilia na alikuwa mtu wa kwanza kunyanyuka kitandani na kuketi na nusu saa baadaye Mariam alifuatia baada ya mtoto wake kuanza kulia.
“Hujalala kabisa Nancy!”
“Hata kidogo! Mawazo yangu yote yako kwa huyu mzee, lazima nimpate kama si hapa mahali pengine popote lakini namwomba Mungu sana ili asaidie nimpate hapahapa kijijini, tofauti na hapo nitahangaika kwa sababu siko tayari kurudi nyumbani kabla ya kumwona!”
“Nimeshakuelewa ila acha baba na mama waamke tutawauliza, mimi bado naamini mzee Mwinyimkuu yuko hapa hapa kijijini hawezi kwenda popote!”
“Hivi ni Mnyamwezi yule?”
“Hapana si Mnyamwezi ni mtu wa Kigoma lakini wengine huwa wanasema ni mtu wa Zaire aliyekuja hapa nchini miaka mingi kutibu watu na dawa zake za asili, sina uhakika sana!”
****
Nancy alikuwa amechakaa na afya yake kuporomoka, mawazo aliyokuwa nayo yalitosha kumkondesha! Kama ungejaliwa kukutana naye usingeamini kuwa msichana huyo alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu, ngozi yake ilikuwa imepauka kwa sababu ya kutokuoga, alijichukia mwenyewe lakini hakujali! Haikuwa rahisi kugundua aliwahi kuwa ni msichana mzuri siku za nyuma.
Alikaa kitandani akiwa amejishika shavu, akisubiri wazazi wa Mariam waamke! Alikuwa na hamu kubwa ya wakati huo, jibu la wazazi wa Mariam ndilo lingemwezesha kuelewa kama angekaa Kisanga zaidi au angesonga mbele kumtafuta mzee Mwinyimkuu.
Muda mfupi baadaye akiwa katika mawazo hayo, mlango wa chumbani kwao uligongwa na sauti ya mama yake na Mariam ilisikika akiwasalimia.
“Mwangaluka Mariam!”
“Mwangaluka!”
“Mwalala mpola?”
“Mpola duhu!” Walisalimiana kwa Kinyamwezi Nancy akiwasikiliza, ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kuwasikia Wanyamwezi wakisalimiana kwa karibu, kabila yao ilimvutia hasa walivyovuta maneno na kupandisha sauti na kushusha, ulikuwa ni kama muziki na alitamani waendelee kuongea zaidi. Zamu yake kusalimiwa ilipofika kiswahili kilitumika, ilifanyika hivyohivyo hata kwa baba yake Mariam.
Dakika chache baadaye wote walitoka chumbani na kwenda kuungana na wazazi wa Mariam waliokuwa sebuleni, moyo wa Nancy ulikuwa ukienda kwa kasi kubwa! Alitamani sana kusikilia ambacho angeambiwa, aliamini kwa vyovyote wazee hao walikuwa wanaelewa kilichompata mzee Mwinyimkuu na wapo alikokuwa kwa wakati huo.
“Baba na mama!” Mariam aliita kwa heshima.
“Naam!” Wakaitika wote kwa pamoja.
“Huyu ni rafiki yangu anaitwa Nancy! Tulikutana naye Tabora lakini yeye amekuja hapa kijijini kumtafuta mzee Mwinyimkuu, nafikiri mnamfahamu yule mganga wa pale kwenye kona ya kwenda Sikonge!”
“Ndiyo tunamfahamu! Hebu njoo kwanza hapa tutete kidogo mwanangu!” Mama yake Mariam alinyanyuka na kumchukua Mariam hadi pembeni ambako alianza kuongea kwa sauti ya chini, hiyo pekee ilitosha kumshtua Nancy na kumfanya aelekeze masikio yake yote walipokuwa wamesimama!
“Kwani huyu binti ni nani yake? Maana yaliyompata mzee Mwinyimkuu ni ya kusikitisha sana!” Mama yake Mariam aliuliza akifikiri Nancy asingesikia bila kuelewa kuwa maneno yote yalikuwa yakiingia masikioni mwa Nancy na kati hali ya kushangaza alimwona Nancy akinyanyuka mahali alipokuwa amekaa na kuwafuata tena akilia machozi.
“NIAMBIENI TU! NINI KIMEMPATA? AU KAFA? TAFADHALI NIELEZENI NIJUE MOJA! HAKUNA HAJA YA KUONGELEA PEMBENI MIMI NI MTU MZIMA!” Aliongea Nancy kwa sauti ya huzuni.
Je nini kitaendelea?
Je ni kweli mzee Mwinyimkuu amefariki?
 
SEHEMU YA 12

Hali ilikuwa mbaya mjini Bagamoyo, baba yake Nancy alikuwa bado akishikiliwa na polisi kwa kosa la kumshambulia Danny kwa risasi, alishahojiwa tayari na hata mke wake pia na wote katika maelezo yao walikanusha kutokea kwa tukio hilo! Maelezo pekee ambayo yalikuwa bado hayajachukuliwa yalikuwa ni ya Danny aliyekuwa hospitali akiuguza mguu wake uliovunjika, aliwazungusha maaskari kwa makusudi.
Kama ilivyokuwa kwa mama yake Nancy, ndivyo ilivyokuwa kwa Danny! Wote hawakuelewa ni wapi alipokuwa Nancy kwa siku zote alizokuwa amepotea, mama alichanganyikiwa! Kuna wakati alihisi mwanae alichukua uamuzi wa kwenda kujiua, baada ya kutafuta kwa siku kadhaa bila mafanikio hatimaye aliamua kutoa taarifa polisi ambao waliendesha msako katika magofu yote mjini Bagamoyo na hata ufukweni mwa bahari ya Hindi lakini hakuna aliyefanikiwa kumwona Nancy.
Hakuna aliyeelewa binti huyo alikuwa wapi, mahojiano kati ya Danny na polisi yaliahirishwa kila siku kutokana na Danny mwenyewe kugoma kuongea, alitaka kwanza akutane na Nancy waongee na kupanga namna ya kufanya! Alielewa wazi katika hatua tatizo la baba yake lilipokuwa Nancy asingekuwa na chaguo jingine isipokuwa kukubali kuwa mpenzi wake tu! Kitendo chake cha kupotea katika mazingira ya kutatanisha kilimfanya Danny avute subira.
Wazazi wa Danny tayari walisharejea nchini kutoka Uswis ambako wote walifanya kazi Benki ya Dunia na kwenda Bagamoyo ambako waliendelea kumuuguza mtoto wao pekee wa kiume Danny! Alikuwa kipenzi chao.
Hakuweza kuwaficha wazazi wake ukweli juu ya tukio lililotokea, kila kitu alikiweka wazi, walichukia kupita kiasi na walitaka mzee Katobe apewe adhabu kubwa na ikibidi kufungwa miaka mingi afie gerezani au aonyongwe.
Kwa nguvu ya ushawishi aliyokuwa nayo baba yake Danny, mzee George Kasoma katika serikali na hata mahakama ingawa hakuna mtu aliye juu ya sheria, lazima mzee Katobe angefungwa, hicho ndicho walichotaka kitokee na kila siku walimshawishi mtoto wao atoe maelezo kwa polisi kueleza kila kitu kilichotokea mpaka kupigwa risasi.
Mara kadhaa mama yake Nancy aliwafuata wazazi wa Danny na kuwaomba msamaha ili mtoto wao asifungue mdomo na kusema ukweli lakini kila alipokwenda alifukuzwa, hawakutaka hata kumwona na walimhakikishia lazima mzee Katobe angefia jela!
Alipoona imeshindikana kwa wazazi wa Danny alirudisha matumaini yake kwa mtoto, kila siku alimbembeleza Danny asimwingize matatani mume wake kwani alikuwa na uwezo wa kumwepusha na kifungo.
“Ilikuwa ni hasira tu! Hata baba Nancy anajuta, amenituma nije kwako kukuomba umsaidie!”
“Mama siwezi kukudanganya, kama Nancy akipatikana na akakubali kuwa mke wangu nitafanya kesi hii isiwepo kwa sababu mimi ndiye mwenye kauli, wazazi wangu kila siku wananishinikiza nitoe maelezo ya kumgandamiza mzee Katobe lakini nasita kwa sababu sijaonana na Nancy na kusikia msimamo wake, nakushauri uendelee kumtafuta bila kuchoka!”
“Nimejitahidi sana! Lakini mafanikio ni kidogo, sijui mwanangu atakuwa amekwenda wapi? Nina wasiwasi atakuwa amekufa! Ina maana asipopatikana Nancy huwezi kumsaidia baba yake?”
“Kwa kweli haiwezekani! Na ninasema wazi kuwa, nitawazungusha polisi kwa wiki tatu mfululizo, baada ya hapo nitalazimika kusema ukweli kwa hiyo ongeza juhudi za kutafuta mama!” Alimaliza Danny, walikuwa wawili tu ndani ya chumba alicholazwa, wazazi wa Danny walikuwa hawajafika kutoka hoteli ya Badeco walikofikia.
Mama yake Nancy aliondoka wodini akiwa amenyong’onyea kupita kiasi, maneno yaliyosemwa na Danny siku hiyo yalitisha, aligundua hapakuwa na utani na ilikuwa ni lazima afanye kila kinachowezekana ili mtoto wake apatikane. Hilo ndio lingeweza kumwokoa mume wake na kifungo, hakuwa na chaguo lolote zaidi ya kuridhia mwanae aolewe na Danny kama kwa kufanya hivyo kungemfanya kijana huyo afiche siri yake ya risasi.
“Hata hivyo sio mbaya! Sijui kwanini Nancy hamtaki wakati wazazi wake wana uwezo na ni wasomi wazuri tu! Ni familia nzuri ambayo kama Nancy akiolewa kwayo itakuwa ni furaha tu, ni lazima apatikane kama yuko hai! Nitafanya kila kinachowezekana, nitatumia kila kilichopo katika muda wa wiki mbili atakuwa amepatikana!” Aliongea peke yake mama Nancy akitembea kutoka wodini hadi nje ambako alipanda gari lake na kwenda hadi gerezani ambako mume wake aliwekwa mahabusu.
Alimweleza kila kitu kilichoongelewa na hata mzee Katobe mwenyewe alikubali Nancy aolewe na Danny, hakuna mtu kati yao aliyeielewa siri ya Yamini aliyokula kwa mganga wa kienyeji, mzee Mwinyimkuu ndio maana walikuwa tayari hata kutumia nguvu ili mradi Nancy aolewe na Danny na hatimaye mzee Katobe kuachiwa huru.
“Sasa sijui tutampata wapi?”
“Peleka matangazo redioni na kwenye televisheni pia!”
“Nitafanya hivyo!”
“Na utangaze zawadi nzuri kwa mtu yeyote ambaye atasaidia kupatikana kwa Nancy, kama yupo hai lazima tutampata! Lakini kama amekufa basi tena!”
“Lakini mimi nina wasiwasi huyu mtoto anaweza kuwa amerudi tena China! Tatizo anampenda sana Tonny, pamoja na mabaya yote aliyofanyiwa yupo tayari kurudiana naye!”
“Basi nenda Wizara ya mambo ya nchi za nje wanaweza kukuelekeza jinsi ya kuwasiliana na ubalozi wa nchi yetu nchini China ili watusaidie kumtafuta!Kwanini umefikiria hivyo?”
“Nilikuta zile pesa ulizoziweka kabatini hazipo!”
“Basi kaondoka! Wala tusihangaike kufikiri eti amekufa! Ila sijui tutamrudishaje ili aje aongee na Danny wakubaliane na mimi nitolewe mahabusu!”
“Wazo lako la mambo ya nchi za nje nimelipenda, ninakwenda sasa hivi!”
Alipotoka mahabusu mama Nancy alinyoosha moja kwa moja kuelekea Dar es Salaam, saa moja na nusu baadaye alikuwa jijini na kwenda moja kwa moja redio one na ITV ambako alilipia matangazo ya kutafutwa kwa Nancy, kutoka hapo alinyoosha moja kwa moja wizara ya mambo ya nchi za nje na kueleza tatizo lake kwa msaidizi wa waziri aliyeamua kupiga simu kwenye ubalozi wa Tanzania nchini China na kuahidiwa kuwa Nancy angetafutwa kwa udi na uvumba, wafanyakazi wengi wa ubalozi walimkumbuka kutokana na vurugu alizozifanya nchini humo.
Matangazo yalianza kuruka hewani karibu kila siku lakini hakukuwa na mafanikio yoyote, siku zilizidi kukatika hatimaye wiki ya kwanza, ya pili na kuingia ya tatu! Danny bado aliendelea kusisitiza nia yake ya kueleza ukweli kama Nancy asingepatikana ndani ya wiki tatu, polisi bado walimtembelea wakitaka kuchukua maelezo yake.
“Wiki ijayo ndio nitakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutoa maelezo! Kwa sasa hivi hapana!” Alizidi kuvuta muda ili wiki tatu zikamilike hatimaye ikawa imebaki siku moja bila Nancy kupatikana wala habari za yeye kuonekana mahali popote kusikika! Mama yake alizidi kuchanganyikiwa naye alikata tamaa kabisa ya kumwokoa mume wake na kifungo! Alijihesabu duniani alikuwa amebaki peke yake baada ya mume wake kufungwa maisha na mwanae kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Siku ya mwisho alidamka asubuhi na mapema na kuwahi wodini akiwa bado amekata tamaa, alitaka kuongea na Danny kwa mara nyingine na kumwomba aongeze muda zaidi, aliwakuta wazazi wake wamekwishafika hivyo akashindwa kuongea na kubana nje ya wodi hadi walipoondoka ndipo naye akaingia na kumkuta Danny amejilaza kitandani.
“Mama nafikiri imeshindikana, ulichokifanya ninakijua! Uliamua kumficha Nancy makusudi ili nisimuoe, sasa shauri yako!” Aliongea Danny kabla hata ya salamu.
“Mwanangu salamu kwanza basi!”
“Sitaki salamu, nilikupa wiki tatu umeshindwa kuzitumia sasa nawasubiri maaskari niwaeleze ukweli!”
Muda mfupi baadaye mlango ulifunguliwa wakaingia wanaume wawili, mama yake Nancy aliwaelewa mara moja kwani ndio waliochukua maelezo yake kituo cha polisi, walikuja kuchukua maelezo ya Danny ili kukamilisha upelelezi ndio kesi ya mzee Katobe ipelekwe mahakamani, maelezo ya Danny yalikuwa ni muhimu sana katika kesi hiyo, maisha ya mzee Katobe yalikuwa mikononi mwake, kama angesema hakupigwa risasi na mzee huyo basi angeachiwa huru lakini kufungua kwake mdomo na kusema ni mzee Katobe aliyempiga risasi kungemaanisha kifungo cha maisha jela.
“Karibuni wazee! Nawasubiri sana leo nimepania kueleza ukweli juu ya tukio hili, kwa muda mrefu sana mmehangaika kutaka niongee nanyi lakini sikuweza, afya yangu haikuwa nzuri! Namshukuru Mungu leo naweza kuongea”
“Vizuri sana! Na huyu mama?” Aliuliza askari akiwa amemwangalia mama Nancy.
“Ni rafiki wa familia yetu!”
“Huyu si ni mke wa mzee Katobe?”
“Ndiyo!”
“Hatuwezi kuchukua maelezo akiwa hapa! Mama toka nje”
“Sawa!” Alijibu mama Nancy akitembea na kufunga mlango nyuma yake, alishindwa kujizuia na kuanza kulia hadi alipolifikia gari na kuingia ndani kisha kuondoka kuelekea nyumbani, hakutaka kuelewa nini alichokiongea Danny! Dakika tano tu baadaye alikuwa nyumbani kwake, ambako aliingia na kujitupa kwenye kochi sebuleni akaendelea kumlilia mume wake tangu siku hiyo aliamini asingeishi naye tena milele na milele.
Akiwa katika mawazo mengi mara mlango wa chumba chake uligongwa na akanyanyuka na kuusogelea kisha kufungua na kuchungulia nje, kijana mdogo alisimama mbele ya mlango akiwa na bahasha mkononi mwake na kumkabidhi baada ya salamu.
“Zimetoka wapi?”
“Baba alikuja nazo!”
“Kutoka wapi?”
Je nini kitaendelea?
Je hizo bahasha zimetoka wapi?
 
SEHEMU YA 16
Uchungu mkubwa ulimkamata moyoni, alitamani mambo yawe tofauti lakini hakuwa na jinsi ya kufanya ili kuubadilisha ukweli wa hali iliyokuwepo! Kifo cha mama yake kilikuwa kimefika na sasa chake kilikuwa kinafuata, mawazo hayo yalimfanya Nancy apoteza matumaini kabisa na hapo hapo akaona giza nene likiyafunika macho yake, mbingu zikafunguka na kuwa wazi, hakuwa na fahamu tena juu ya ulimwengu wa kawaida.
Kwa mbali alimuona mnyama mkubwa mwenye mbawa na manyoya mengi akija kwa kasi kutoka mbinguni, mikono yake ilikuwa mikubwa mithili ya shina la mti wa mbuyu, kulikuwa na kucha ndefu na nene mwisho wa mikono ya mnyama huyo.
Cha kushangaza zaidi alikuwa na jicho moja tu, alipofungua mdomo wake meno makubwa zaidi ya mamba yalionekana mnyama huyo alitisha kabisa, kadri alivyodi kumkaribia ndivyo mdomo wake ulivyozidi kufunguka ikiwa ni ishara kwamba alitaka kumla. Nancy hakuhitaji kuelezwa na mtu kuwa mnyama huyo mwenye mkia mrefu alikuwa nani, alielewa mara moja alikuwa shetani akija kuichukua roho yake!
Hakuwa tayari kwa jambo hilo bado alitaka kuishi duniani alikuwa mtoto mdogo mno kufa kabla hajapata digrii yake ya chuo kikuu, alihitaji nafasi zaidi aendelee kumtafuta mganga wa kienyeji mzee Mwinyimkuu ili amwondolee kiapo alichokiweka moyoni mwake kwamba hatafanya ngono na mwanaume mwingine yoyote yule maishani mwake isipokuwa Tonny ambaye kwa wakati huo hakuwa mpenzi wake tena alishamwacha na kumchukua mwanamke mwingine! Ni kiapo tu alichokula ndicho kiliharibu maisha yake, alitaka kiondolewe, kisha amsahau Tonny na asimpende mwanaume mwingine tena baada ya hapo maisha yake yangekuwa safi.
“Ee Mungu nisaidie nipe nafasi nyingine! Bado nataka kuishi, niongezee siku utakazo wewe!” Alipiga kelele Nancy mnyama yule alipozidi kumkaribia.
***
Polisi waliridhishwa na maelezo ya Danny juu ya mtu aliyempiga risasi ingawa walihisi kulikuwa na jambo aliloficha juu ya mzee Katobe bado walishindwa kumlazimisha akubali walichokitaka na kwa maelezo hayo walijikuta wakikosa kesi na kumwachia huru! Shukrani ya mzee Katobe kwa kijana huyo hazikuwa na maneno ya kutosha kuieleza, alipotoka tu mahabusu alinyoosha moja kwa moja hadi hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na kuingia hadi chumba alicholazwa Danny.
“Nakushukuru sana, najua umeamua kunisaidia ili kuniepusha na kufungo, hakuna wema unaoweza kulingana na ulionifanyia niko tayari kufanya lolote kama shukrani, ni mimi niliokukosea!”
“Hujanikosea kitu baba!”
“Nilikupiga risasi lakini umeamua kuficha siri!”
“Nafahamu lakini usijali, nimefanya hivyo kwa sababu nampenda Nancy!’
“Sema chochote unachotaka kutoka kwa Nancy nani nitakusaidia!”
“Nampenda nataka awe mke wangu!”
“Umekwisha kumpat! Sema kingine!”
“Sina zaidi!”
“Mama amemfuatilia, hivi sasa yuko Kigoma na ninafikiri katika muda wa wiki moja atakuwa amekwisharejea!”Aliongea mzee katobe bila kuelewa mambo yaliyokuwa yakitokea upande wa pili, katika ziwa Tanganyika ambako Nancy na mama yake walikuwa wakihangaikia roho zao, angejua wala asingetamka maneno yaliyokuwa yakimtoka mdomoni.
“Kwa hiyo akirudi na mimi nikiruhusiwa kutoka hospitali tutaoana?”
“Mimi ni baba yake, nikisema neno hakuna mtu wa kupinga! Hesabu wewe na Nancy ni mtu na mkewe, unasikia Danny? Hiyo ndiyo shukrani yangu kwako!”
“Ahsante baba!”
Mzee Katobe alishinda hospitali hadi usiku ulipoingia akimsaidia Danny katika mahitaji yote, hakuwa na mtu wa kumpa msaada tangu wazazi wake wasuse na kuondoka baada ya yeye kushindwa kueleza ukweli juu ya mtu aliyempiga risasi, walikerwa na kitendo cha Danny kuuficha ukweli, waliona mtoto wao amewavunjia heshima, kwa sababu hiyo mzee Katobe aliona wajibu wa maisha yote ya Danny ulikuwa juu yake, alikuwa na kila sababu ya kumsadia na kwa sababu alikuwa ametoka mahabusu aliahidi kufanya bila kilichohitajika kwa gharama yake.
Danny aliendelea kupata matibabu hospitali, mfupa wake ukiendelea kuunga taratibu, mawazo yake yote yalikuwa kwa Nancy alitamani arudi, wafunge ndoa na baada ya hapo warejee chuoni na kuendelea na masomo hadi mwisho, wamaliza na kupata digrii zao za sheria! Mambo yake yasingekuwa sawa wala furaha yake maishani isingekuwa kamili bila Nancy! Hivyo ndivyo alivyoelewa, ndiyo maana alikuwa tayari kuwasaliti wazazi wake kwa sababu ya mwanamke aliyempenda, penzi alilokuwa nalo kwa Nancy halikuwa la kawaida.Ilikuwa rahisi mtu kuhisi labda alinyweshwa mti dawa ya mapenzi ya kuwapumbaza wanaume jambo ambalo kwa hakika halikuwa kweli.
Siku zilizidi kukatika hatimaye wiki ikaisha tangu mzee Katobe aachiwe kutoka mahabusu, bila Nancy pamoja na mama yake kurejea! Wasiwasi ulianza kuingia moyoni mwa Danny na mzee Katobe, hisia kwamba kulikuwa na tatizo lililowapata huko Kigoma zilitawala mawazo yao, hata hivyo hawakutaka tamaa kabisa walizidi kuongeza siku lakini bado hakurejea mpaka wiki ya pili ikakatika na wasiwasi ukazidi kuongezeka.
“Labda hawajaonana, anaendelea kumtafuta!” Danny alisema.
“Inawezekana kabisa! Bahati mbaya hata namba ya simu sina na huko alikokwenda sina mwenyeji ambaye ningemwomba anisaidie kumtafuta, nafikiri hakuna tatizo, tuchukulie bado anamtafuta!”Mzee Katobe aliongea.
“Ikipita wiki itabidi kuwafuatilia, lazima watakuwa kwenye matatizo!”Danny alishauri.
“Itabidi iwe hivyo!”
“Kama nitakuwa nimeruhusiwa itabidi tuongozane kama tu pesa itakuwepo, nisingependa kuona unahangaika peke yako!”
“Unategemea kuruhusiwa hivi karibuni!”
“Daktari alikuja juzi akasema hali yangu siyo mbaya naweza kuondoka mfupa wangu umeunga vizuri! Kama sikosei kesho naweza kupewa ruhusa!”
Kama alivyosema Danny kweli siku iliyofuata, aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya X-ray yake kuonyesha mfupa ulishaunga vizuri, ilikuwa furaha kubwa mno kwake kutoka hospitali na hakuwa na mahali pengine pa kwenda isipokuwa nyumbani kwa mzee Katobe ambako wote wawili waliendelea kusubiri nancy na mama yake warejee ili mipango ya ndoa ifanyike, Danny ajipatie mke! Mpaka wakati huo hakuwa mtu aliyekuwa ameelewa kitu chochote juu ya matatizo ya upande wa pili wa shilingi.
“Hatuna njia lililopo ni kusafiri hadi Kigoma kuwafuatilia, nafikiri watakuwa kwenye matatizo!”Mzee Katobe alimwambia Danny wote wawili wakiwa mezani, chakula kilikuwepo lakini hakuna mtu aliyetamani kula! Fikra juu ya Nancy na mama yake zilichukua hamu yao ya chakula.
“niko tayari wakati wowote ukitaka tusafiri!”
“Kesho unaonaje? Mguu wako hauwezi kukusumbua?”
“Mimi ni mzima kabisa! Lolote utakalotaka hivi sasa naweza nikifanya!”
“Basi kesho tunaondoka!”
“Sawa!”
Waliagana na kila mmoja kuingia chumbani kwake kulala, kilikuwa chumba kizuri chenye kila kitu kuanzia sofa, televisheni, kiyoyozi, choo na bafu ya ndani, kilitosha kumpa binadamu yoyote raha na usingizi mara moja aingiapo chumbani, lakini ilikuwa tofauti kwa Danny, mawazo juu ya Nancy yaliendelea kumsumbua kichwani mwake mpaka saa tisa usiku alikuwa bado hajapata hata lepe la usingizi.
Masaa kumi, kumi na moja ya alfajiri hakuyaona, yalipita bila taarifa! Danny alikuwa kanisani ambako padri na kitabu chake cheusi kiitwacho Biblia alisimama mbele yake! Pembeni mwake akiwepo Nancy ndani ya shela nyeupe iliyompendeza vizuri kwa hakika wote wawili walivutia, watu wengi walijaa kanisani, mama yake Nancy alikuwepo, watu pekee ambao hakuwaona walikuwa ni wazazi na ndugu zake lakini pamoja na kutokuwepo kwao bado alikuwa na furaha kwa sababu alikuwa amemuoa Nancy, mwanamke aliyemhangaisha kwa muda mrefu.
“Danny uko tayari kumuoa Nancy?” Padri aliuliza.
“Ndiyo!”
“Unakubali kuwa naye katika shida na raha mpaka Mungu atakapowatenganisha?”
“Ndiyo padri!”
“Unaweza kuwe sahihi kwenye fomu iliyoko mbele yako!”
Danny aliinama mbele ya meza ambayo juu yake kulikuwa na fomu nyeupe pamoja na kalamu, akaichukua kalamu na kuweka saini yake, baadaye padri alimgeukia Nancy na kumuuliza maswali hayo hayo lakini badala ya kujibu alibaki kimya machozi yakimbubujika! Padri alimuuliza zaidi ya mara mbili, hakufungua mdomo wake kuseme kitu chochote, watu wote kanisani walishindwa kuelewa ni nini kilikuwa kinatokea, kanisa lilibaki kimya, furaha ilianza kuyeyuka.
“Siwezi!Siwezi!Padri siko tayari kuolewa, simpende Danny badi nampenda yule pale!” Nancy aliongea akisonta kidole chake kwenye kona katikati ya watu waliohudhuria kanisani kushuhudia ndoa ikifungwa, watu wote walielekeza macho yao mahali kidole cha Nancy kilikoelekezwa na kumwona kijana mrefu akinyanyuka na kusimama wima. ALIKUWA NI TONNY! Na alianza kutembea kuelekea altareni na kwenda kumkumbatia Nancy mbele ya Danny , wazazi pamoja na padri.
Danny alishindwa kuvimilia na kumsogelea Tonny hasira kali ilikuwa imempanda, alikunja ngumi yake ya mkono wa kushoto na kuitupa kuelekea usoni kwa Tonny, ilikuwa nzito iliyompelekea Tonny sakafuni, huku damu nyingi zikimtoka puani, kanisa lilianza kupiga kelele watu wakikimbia kwenda nje na wengine kwenda mbele kushuhudia kilichotokea.
“harusi imevunjika! Harusi imevunjika!”Maneno hayo yalisikika kila sehemu kanisani.
Padri wazazi pamoja na wazee waliokuwepo kanisani walimzunguka Tonny aliyekuwa amelala cini akiwa ametulia kabisa, baadhi walikuwa wakimshika kifuani upande wa moyo kuona kama ulikuwa unapiga na wengine wakimshika mishipa ya mikononi lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyekutana na pigo la moyo wala mshipa.
“Amekufa!”
“Kweli? Haiwezekani, mbona nimempiga kidogo tu!”Danny aliongea akijilaumu, alijutia tendo alilofanya! Hapo hapo alikalishwa chini na kuzungukwa na baadhi ya waumini kanisani, hawakutaka aondoke sababu alishafanya mauaji! simi ilipigwa polisi na muda mfupi baadaye maaskari waliingia na kumpiga pingu, wakaanza kumsukuma kwenda nje huku akilia machozi, hakuna mtu aliyemwonea huruma.
“Nancy!Nancy! Kwanini umenifanyia ukatili huu nikukosea.....!:Hakuimalizia sentensi yake alikuwa akitingishwa kwa nguvu!
“Danny!Danny!Danny! Amka tuondoke tayari saa kumi na mbili na nusu, tuwahi mabasi ya kwanza kwenda Dar ili jioni tuondoke na treni!” Ilikuwa sauti ya mzee Katobe, alimkatisha Danny ndoto yake, alinyanyuka huku akilia machozi na kumshangaza mzee Katobe.
“Vipi mbona unalia?”
“Ndoto! Nimeota ndoto mbaya sana!”
“Ndoto gani?”
“Ndoto tu, ila ni ya kutisha! Nashukuru ni ndoto vinginevyo nilikuwa na kwenda jela!”
“Achana na ndoto mwanangu, mara nyingi ni matokeo ya fikra unazokuwa nazo, tafadhali oga, kisha vaa tuondoke!”

Je nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 17
Danny hakusema kitu tena alichofanya ni kuingia bafuni ambako hakuchukua dakika tano akawa ametoka na kuvaa nguo zake vizuri na wote wakaondoka hadi stendi ambako walipanda basi liitwalo Bagamoyo Tours lililowafikisha jijini Dar es Salaam masaa matatu baadaye, kwa sababu ya ubovu wa barabara. Hakuna kazi nyingine waliyokuwa nayo jijini zaidi ya kutafuta tiketi za ndege, hawakufanikiwa kupata baada ya kuambiwa hapakuwa na ndege ya kwenda Kigoma kwa wiki nzima. Chaguo la pili ilikuwa ni treni hilo halikuwahangaisha sana, walipata tiketi daraja la kwanza na siku hiyohiyo kuondoka wakitegemea kuingia Kigoma siku mbili baadaye.
“Tutafika tu! Hata kama itachukua siku ngapi?” Aliongea mzee Katobe.
“Lazima tuwapate, nitafurahi sana kumwona Nancy ingawa ndoto yangu ya leo imenikatisha tamaa sana!”
“Hivi ni ndoto gani?”
Danny alieleza kila kitu juu ya ndoto yake na mzee Katobe akamwondolea wasiwasi na kumhakikishia kila kitu walichopanga kingekwenda sawa sawa, aliongea bila kuelewa nini kiliwapata Nancy na mama yake majini.
Safari kutoka Dar Es Salaam hadi Kigoma kwa treni ilikuwa ni ya kuchosha, ilikuwa safari ndefu kuliko zote ambazo Danny aliwahi kusafiri katika maisha yake ! Waliingia Kigoma siku mbili baadaye akiwa hoi bin taaban, na kuchukua vyumba katika hoteli iliyoitwa Lubumbashi, moja ya hoteli maarufu na za gharama mjini Kigoma.
Vichwani mwao hakuna kitu walichokuwa wakifikiria zaidi ya Nancy na mama yake, mioyo yao isingetulia mpaka wawapate watu hao ! Muda walioingia Kigoma ulikuwa mbaya, wasingeweza kufanya jambo lolote kwa kuwa tayari ilikuwa ni usiku, walilazimika kulala mpaka siku iliyofuata.
Kama ilivyo kwa siku nyingine zote, hapakuwa na usingizi kwa wote wawili ! Walikesha wakiongea na kuchanga mawazo juu ya tatizo lililokuwa limewapata, lilikuwa tatizo lao wote wawili na walikuwa na wajibu wa kulitatua.

“ Nitatumia kila kitu nilicho nacho mpaka mke wangu na mwanangu wapatikane!” Alisema mzee Katobe. “ Hata mimi pia nitatumia nguvu zangu zote kuhakikisha wanapatikana, hata kama ni kupamabana mipo tayari kupoteza maisha yangu kwa ajili ya Nancy na mama !”

Hayo ndiyo yalikuwa maneno yao, mwanzoni yalionekana ya kawaida lakini baadaye yalibadilika na kuwa kiapo ! Waliapa kuwapata Nancy na mama yake kwa udi na uvumba.
Asubuhi kulipokucha kila mmoja aliingia bafuni na kuoga, wakapata kifungua kinywa na kuondoka kuingia mitaaani ambako walianza msako kuwatafuta Nancy na mama yake, mzee Katobe akiwa na picha zao mkononi na kumwonyesha kila mtu aliyemsimamisha kumuuliza.
Kutwa nzima ya siku hiyo bila kupumzika waliuzunguka mji wa Kigoma na kuugeuza chini juu bila mafanikio ya kuwapata wala kusikia habari zao, waliporudi hotelini saa 3 usiku walikuwa wamechoka hawakuwa na kitu kingine cha kufanya zaidi ya kuoga, kula kisha kujitupa kitandani na kulala.
Huo uligeuka na kuwa utaratibu wao wa kila siku kwa wiki moja na nusu lakini bado hawakufanikiwa kuwapata Nancy na mama yake, walifika Bandarini kwenye ofisi za meli zilizofanya safari kati ya Kigoma na Zaire kuuliza kama walisafiri na vyombo hivyo, majina yao hayakuwepo ! Walichanganyikiwa na kushindwa wafanye nini, akili zao zilionekana kufikia kikomo cha kufikiri.
“ Nina wazo!”
“ Wazo gani mwanangu?” mzee Katobe aliuliza
“ Kwanini tusitumie hizo picha zao kutengeneza matangazo tuyabandike mitaani, nina uhakika lazima kuna watu waliishawahi kuwaona, kama si Nancy basi mama au wote pamoja !”
“Ni wazo zuri lakini si zitakuwa picha zisizo na rangi, watawatambuaje?”
“Siku hizi utalaamu umeongezeka sana, uwezekano upo wa kutengeneza matangazo kwa rangi ili mradi tuwe na pesa!“
“Nimekwisha sema niko tayari kutumia kiasi chochote cha pesa lakini mwanagu na mama yake wapatikane! Pesa haina tena thamani tena kwangu, maisha yangu yamekwishaharibika ! Ninachohitaji hivi sasa ni furaha na hiyo haiwezi kupatikana bila Nancy na mama yake kupatikana” Aliongea mzee Katobe kwa sauti ya kuhuzunika, ni wazi aliyoyasema yalitoka moyoni mwake. Basi niachie hiyo kazi, mimi nitaifanya ! “ Aliongea Danny.
Siku iliyofuata asubuhi Danny alikuwa wa kwanza kuondoka hotelini na kuingia mitaani ambako alifanya kazi ya kutafuta kiwanda cha uchapishaji, haikuwa kazi ngumu sana kwani saa mbili baadaye tayari alishakipata kimoja na alikuwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi wake, picha za Nancy na mama yake zikiwa mezani.
“ Nataka yawe na ukubwa wa karatasi moja ya A4, picha ziwe za rangi na ziwe kubwa!” “Juu yake kutakuwa na maneno gani?”
“Wanatafutwa na ndugu zao!”
“Kuna zawadi?”
Mkurugenzi wa kampuni hiyo bwana David Msanii aliuliza.
“Duh ! Nimesahau kuuliza, naweza kutumia simu yako?”
“Bila matatizo!”
Danny alinyanyua mkono wa simu na kubonyeza namba za hoteli ya Lubumbashi na kuomba aunganishiwe chumbani mwa mzee Katobe, sekunde kadhaa tu baadaye mzee Katobe alikuwa kwenye laini,
“Nani?”
“Ni mimi Danny!”
“Vipi umefanikiwa?”
“Ndiyo! ila kuna kitu kimoja nilisahau kukuuliza ! ”
“kitu gani?”
“Kuna zawadi yoyote tunayotoa?”
“Ndiyo! Utawezaje kuwatangazia watu wamtamfute mtu kusiwe na zawadi?”
“Sawa ni zawadi gani?”
“Millioni mbili kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa mwanangu na mama yake?”
“Ahsante sana!”
Baada ya maongezi hayo Danny alimgeukia bwana David Msanii, aliyekuwa ameketi kitini akisubiri kupewa jibu, alikuwa akichora kwenye karatasi nyeupe namna ambavyo tangazo hilo lingeonekana.
“Ni milioni mbili!” Alisema Danny. “Sawa ! Kwa hiyo hii ‘Milioni mbili’ itakaa chini yakiwa ni maandishi makubwa na ‘anatafutwa na ndugu zao’ itakaa juu, halafu hapa katikati nitaweka maandishi madogo yanayosema ‘zawadi ni’!” Aliongea bwana Msanii.
Kwa maelezo yaliyotolewa Danny alielewa tangazo lingekuwa la kuvutia sana hasa kama picha zingetoka jinsi zilivyoonekana. “Picha zitatoka hivyo hivyo?” “Ndiyo, kuna kitu kingine mngependa kuongeza?”
“Andika namba ya simu ya bosi wangu na uwaeleze kuwa anapatikana hoteli ya Lubumbashi! Baada ya siku ngapi nitegemee kupata matangazo haya?”
“Ninaanza kazi leo, nipe siku tatu!”
“Gharama yake itakuwa kiasi gani?”
“Bahati mbaya sijaelewa idadi ya nakala ninazohitaji”
“Ili kila mtu kati mji wa Kigoma ayaone matangazo haya tunaweza kuchapa kiasi gani?
Pesa sio tatizo kinachohitajika ni matangazo yawafikie watu!”
“Labda nakala elfu tano!”
“Zitagharimu kiasi gani?”
“Shilingi laki tano!”
“Hilo sio tatizo, nipe simu tena nimweleze mzee.”
“Hakuna shida.”
Danny alimweleza mzee Katobe kila kitu na akakubaliana na bei, mchana wa siku hiyo walimletea asilimia hamsini ya malipo kama utangulizi na kazi ikaanza! Siku tatu baadaye kazi ikakamilika, mzee Katobe akaajiri vijana wa matangazo, yakabandikwa katika kuta nyingi mjini Kigoma. Hapakuwahi kuwa na matangazo yaliyotapakaa namna hiyo katika mji wa Kigoma, habari ya Nancy na mama yake ikawa gumzo, watu wakawa wanaiita Bingo huku kila mtu akimpeleleza mwenzake ili apate angalau fununu ambazo zingemwezesha kuny’akuwa donge hilo.

Je nini kitaendelea?
Je Danny na mzee KAtobe watafanikiwa kuwapata Nancy na mama yake?
 
SEEMU YA 18
Watu wengi walifurika nje ya hoteli ya Lubumbashi asubuhi ya siku iliyofuata, kila mtu akizihitaji milioni mbili zilizotangazwa, kwa kuwaangalia tu watu waliofika bila hata kuuliza ungejua walikuwa ni wavuvi na walizidi kuongezeka kadri saa zilivyozidi kusogea.
“Mnataka kumwona nani?” Mtu wa mapokezi aliwauliza.
“Yule aliyetangaza kutafutiwa ndugu zake!”
“Subirini” Aliwajibu kisha kunyenyua simu na kupiga namba ya chumbani kwa mzee Katobe, dakika mbili tu baadaye mzee Katobe alikuwa mapokezi na kuomba chumba kimoja afanye maongezi na watu waliojitokeza, alipewa chumba kimoja na Danny aliungana naye dakika chache baadaye.
Katika muda wa masaa mawili alishawasikiliza watu wote lakini ni wawili tu kati yao walioonekana kuwa na maelezo ya kusaidia, yote yalikuwa ya kusikitisha yaliyomfanya Danny alie machozi.
“Kwanza alikuja huyu msichana!” Aliongea kijana mmoja akionyesha kidole chake kwenye picha.
“Endelea!”
“Alikuwa amekonda sana na alionekana kuwa na mawazo mengi. Alinikuta mimi na wenzangu ufukweni tukitengeneza nyavu zetu akatuuliza habari za usafiri kwenda Zaire, bahati mbaya hapakuwa na meli likapatikana jahazi akapanda na kuondoka zake! Siku iliyofuata akaja huyu mama akimuulizia naye alinikuta mimi ilikuwa kama bahati nikamwambia kila kitu, akataka kusafiri kumfuatilia!”
“Alikueleza ni kwa nini?”
“Hakuniambia”
“Alisafiri kwa usafiri gani”
“Nilimpeleka kwa wale Waarabu wenye boti za kukodi!”
“Akakodisha moja na kuondoka”
“Unaweza kutupeleka kwa hao Waarabu?”
“Hakika, labda tu wagome kusema ukweli”
Hawakutaka kupoteza muda maelezo waliopewa yalitosheleza kabisa. Ni kweli kijana huyo aliwaona Nancy na mama yake, walichofanya ni kuondoka pamoja na kijana huyo kwenda ofisini kwa wakodishaji wa vyombo vya majini, huko walikutana na nahodha aliyemsafirisha mama Nancy hadi katikati ya ziwa Tanganyika.
“Ziwa lilikuwa chafu mno wakati nawaacha ilikuwa mara ya kwanza mimi kukutana na hali ya namna hiyo katika ziwa Tanganyika ! Sikutegemea kurudi hapa salama, nilipofika tu nchi kavu nilisikia katika vyombo vya habari kuwa jahazi alilopanda lilizama na watu wote wakafa maji !”
Mzee Katobe na Danny waliangua kilio. Watu waliokuwepo wakaanza kuwabembeleza na kuwafariji, haikusaidia ilibidi wakodishe gari hadi hotelini ambako waliendelea kulia. Pamoja na kushindwa kuwapata watu waliokuwa wakiwatafuta wakiwa hai, mzee Katobe aliwalipa kijana aliyewapa habari mara ya kwanza pamoja na nahodha shilingi milioni moja kila mmoja wao.
“Sikubali, lazima walizikwa mahali fulani, nitazitafuta maiti zao mpaka nizipate nikawazike Bagamoyo kwa heshima zote!” Alisema mzee Katobe akilia, yeye na Danny walikuwa wamekumbatiana! Pigo walilopata lilikuwa kubwa mno kuvumilia.
“Itabidi tukodishe boti kwenye ile kampuni tuzunguke fukwe zote lazima tutafika mahali ambapo maiti zilionekana na zikazikwa!”
“Sawa!” Danny aliitikia. Walikesha wakilia na hicho ndicho kilifanyika siku iliyofuata, walirudi kwenye kampuni ya boti na kukodisha boti kubwa yenye uwezo wa kwenda kwa kasi kubwa zaidi na kuanza kuzunguka fukwe za ziwa Tanganyika wakianzia upande wa Kigoma kisha kwenda upande wa pili wa Zaire lakini hawakufanikiwa kupata taarifa za miili hiyo.
“Tutafanyaje sasa!” Aliuliza mzee Katobe baada ya wiki tatu za kutafuta, pesa nyingi zilitumika katika operasheni hiyo.
“Labda tujaribu katika visiwa!” Nahodha aliyejulikana kwa jina la Costa aliwashauri. “Sawa niko tayari kwa lolote, zoezi hili halitakoma mpaka nifanikiwe kupata miili ya mke na mtoto wangu hata kama itachukua mwaka mzima” Aliongea mzee Katobe, walikuwa na uhakika asilimia mia moja Nancy na mama yake walishafariki dunia.
****
Kelele alizozipiga Nancy baada ya kumwona mnyama wa kutisha aliyeamini ni shetani aliyekuja kuchukua roho yake ndizo zilikuwa za mwisho, alipoteza fahamu kabisa baada ya hapo! Hakuelewa kitu chochote kilichoendelea.
Alizinduka baadaye akiwa amelala ndani ya kibanda kidogo cha nyasi, kilichokuwa na giza nene.
Hakuelewa alikuwa wapi na alikuwa akifanya nini, mahali alipolala palikuwa pa baridi na hapakuwa na godoro wala shuka, alipofumbua macho yake taratibu na kuangalia ingawa kwa pembeni alimwona mzee mwenye mwili mkubwa na ndevu nyingi akiwa amepiga magoti pembeni mwake akitikisa kitu kama kibuyu.
Alishindwa kuelewa mzee huyo aliyetisha alikuwa nani, hakuwa na kumbukumbu zozote kichwani juu ya kilichotokea. Wakati akihangaika kuvuta kumbukumbu zake alisikia kipande kirefu cha mti kikipenya mdomoni na sekunde chache baadaye alistukia kitu kichungu kikimwingia mdomoni kupitia katika kipande hicho cha mti.
“Meza! Meza dawa, imekusaidia, bila hii ungekufa !” Aliongea mzee huyo kwa sauti ya kukwaruza.
Nancy alitii sauti na kumeza majimaji yaliokuwa mdomoni mwake, yalikuwa kama shubiri, yalipomwingia tumboni michango iliunguruma akasikia nguvu kidogo zikirejea na kumbukumbu zake zikamiminika kama filamu, alijiona yu katikati ya maji akihangaika kisha akashuhudia mama yake akiachia mkungu wa ndizi na kuzama.
“Mamaaaa ! Mama yanguuuu !” Nancy alilia.
“Usilie mama yako yupo.”
Alinyanyuka na kuketi kitako katika hali ya kutoamini, mzee huyo aliendelea kumhakikishia kuwa mama yake alikuwa hai! Nancy hakuamini alitaka kumwona mama yake kwa macho, halikuwa jambo rahisi kukubali.
“Subiri kwanza !”
“Wewe ni nani?”
“Naitwa babu Ayubu!”
“Ilikuwaje nikafika hapa?”
“Siku mlipotaka kuzama, mimi na mwenzangu tulikuwa jirani na eneo hilo, tukawawahi na kuwaokoa tukaja nanyi hapa kisiwani leo ni siku ya tano!”
“Unasema ukweli? mama yangu yuko hai?”
“Hakika!tena yeye amewahi kupata nguvu mapema kuliko wewe! ndiye aliyetupikia chakula leo mchana”
“Babu Ayubu unanitania!”
“Sina sababu ya kukueleza uongo”
“Yuko wapi ?”
“Kwenye kibanda cha mwenzangu! Tulipowaokoa tulifurahi sana, kwani leo ni miaka kumi na tano tangu tufike hapa kisiwani, hatujawahi kukutana na mwanamke kimwili!” Ndiyo maana tumejitahidi sana kuwaokoa maisha yenu kwa sababu mtakuwa wake zetu! mwenzangu amekwisha kumuoa mama yako, mimi nilikuwa nakusubiri !”
“Unasema nini? nahisi umechanganyikiwa, ni heri ungeniacha nikafa majini kuliko kuniokoa halafu unifanyie unachotaka kukifanya!”
“Utakubali tu! mbona hata mama yako alikataa, mateso aliyoyapata hatayasahau, kwa mdomo wake mwenyewe alijikuta akisema ndiyo!” Aliongea babu Ayubu, hasira ilisikika katika sauti yake.
“Ninasema haiwezekani, niliishakula kiapo cha kutofanya map....!”
“Weweee! kiapo chako huko huko hapa ni serikali nyingine na hakuna kituo cha polisi, ulishawahi kuona kisiwa kikubwa kama Zanzibar wanaishi watu wawili? basi ndiyo hapa!”

Je nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 19
Nancy alimwangalia baby Ayoub kwa macho ya chuki, hakuwa tayari kufanya kitendo alichokuwa akiambia hata kama angewekewa kisu shingoni, kiapo alichokula kwa mganga bado kilimsumbua kichwani mwake! Alielewa wazi kufanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine tofauti na Tonny kabla hajakutana na mzee Mwinyimkuu na kukiondoa kiapo chake, kungemletea madhara makubwa. Alikuwa tayari kuchagua kifo lakini si kumvulia babu Ayoub nguo yake ya ndani.
“Umeielewa!”
“Wewe hivisasa ni mke wangu, siamini kama kweli nimekutana na mwanamke baada ya miaka kumi na zaidi! Ungekufa ningesikitika sana ndio maana nilikuwa najitahidi kadir ya uwezo wangu wote ili upone nami nianza kula uhondo kama mwenzangu mzee kiwembe!”
“Kama ni kuniua niue lakini kitu unachosema hakiwezi kufanyika!”
“Haya subiri usiku utaona!”
“tafadhali nionyesha mahali mama yangu alipo!” Alisema Nancy.
Babu Ayoub alimsaidia Nnacy kunyanyuka kutoka mahali alipokuwa amelala na kumwongoza hadi kwenye kibanda cha nyasi kilichojengwa jirani tu na mahali kibanda cha babu Ayoub kilipokuwa, mlango ulikuwa wazi na wote wawili waliingia ndani, macho ya Nancy yaligota kwenye mgongo wa mama aliyekuwa jikoni akipika chakula! Ingawa hakumwona usoni mgongo huo ulitosha kuonyesha kuwa mwanamke huyo alikuwa mama yake, aliruka na kumkumbatia, wote wawili wakaanguka chini na kuanza kugalagala.
“Jamani mwanangu!”
“Mama!Ni wewe?”
“Ni mimi mwanangu, siamini kama uko hai tena! Umepoteza fahamu kwa karibu wiki nzima, nilishapoteza matumaini ya wewe kupona!”
“Nimenusurika mama!”
Waliendelea kukumbatiana kwa karibu dakika kumi wakilia kwa furaha, hakuna aliyekuwa tayari kuamini walikuwa salama! Wazee wawili walisimama pembeni mwao wakiwaangalia,hawakuvaa nguo yoyote mwilini mwao zaidi ya majani yaliyowafunika sehemu ya mbele! Walitisha kwa muonekano lakini wao ndio waliookoa maisha ya Nancy na mama yake.
“Mama hapa tuko wapi?” Nancy alimuuliza mama yake walipoachiana na kuketi wakiwa wameegemea ukuta.
“Ni kisiwa kinaitwa Galu!”
“Na hawa?”Nancy aliendelea kuuliza.
“Hawa wazee ndio wametuokoa! Lakini....!” Alipofika hapo mama yake Nancy alishikwa na kigugumizi, palionekana kuwa na kitu alichoshindwa kukiongea kwa wakati huo, Nancy alihisi tatizo.
“Nini mama?”
“Tutaongea baadaye!” Mama yake alinong’ona.
Mama alimwita babu Ayoub na kuanza kutambulisha kwa Nancy akisema ni binti pekee aliyejaaliwa kuwa naye katika maisha, alimshukuru kwa kuweza kumwokoa! Wakati wakiongea mama Nancy machozi yalimtoka, alikuwa na dukuduku moyoni ambalo mwanae alitamani sana kulifahamu.
“Nimemwona! Kwa hiyo wewe sasa hivi ni mama mkwe!”Aliongea babu Ayoub akitabasamu.
Mama Nancy hakujibu kitu zaidi ya kumwaga machozi zaidi ingawa babu Ayoub pamoja na mzee mwenzake waliendelea kucheka, kwao ilikuwa ni furaha kubwa mno kupata wanawake baada ya kuishi kisiwani peke yao kwa muda mrefu bila kujamiana.
“Lakini binti huyu ni binti yangu, siwezi kukuruhusu umfanyie mambo ambayo mwenzako ananifanyia mimi! Haitawezekana!”
“Ataweza tu!”Mzee Mwingine mfupi na mwenye misuli mingi mwilini aliongea huku akicheka.
Baadaye Nancy na mama yake walipewa nafasi ya kuongea peke yao, mama alisimulia habari ya kusikitisha juu ya mateso aliyoyapata mwanae akiwa usingizini! Kuna mambo alishindwa hata kuyasema kwa sababu yalikuwa aibua kwa yeye kufungua mdogo wake na kuongea mbele ya binti yake, Nancy alielewa kwa sababu tayari alishamsikia babu Ayoub akiongea.
Nancy alimweleza mama yake kuwa asingeweza kufanya kitendo cha namna hiyo sababu ya kiapo alichokula mama yake alimuunga mkono na kuahidi kumsaidia kadri alivyoweza.
“Mama suala la msingi ni kwamba tutaondokaje hapa?”
“Hata mimi sielewi, kila siku nafikiri juu ya jambo hilo lakini ni lazima tuondoke!”
“Hakuna mtumbwi?”
“Wana mtumbwi mmoja tu mdogo na huo ndio wanaoutumia kwenda kutega samaki, sidhani kama unaweza kutufikisha ng’ambo!”
“Sasa tutafanyaje?”
“Hakuna kitu kingine zaidi ya kujifanya tumekubaliana na wanachokisema ili watuzoee na kutuamini, wakati huohuo nitakuwa najifunza kupiga kasia na kuutumia mtumbwi wao ili kama nikifanikiwa kuuelewa tutajaribu kutoroka siku moja usiku!’
“Sawa mama!Lakini kumbuka mimi sitaweza kufanya tendo la ndoa na babu Ayoub!’
“Hapo sijui tutafanya kitu gani, maana mimi pia nilikataa lakini kipigo nilichopata nilijikuta nalainika na kukubali namwomba Mungu usikutane na mateso kama niliyoyapata mimi!” Aliongea mama yake Nancy na kuzidi kumtisha.
Waliporudi ndani Nancy aliketi chini na kuendelea kumshuhudia mama yake akitayarisha chakula, hapakuwa na chakula kingine kisiwani zaidi ya samaki hivyo muda mfupi tu baadaye chakula kilikuwa tayari na wote wanne walitengeneza mduara na kuanza kula, wakati wanamaliza zoezi hilo tayari ilikuwa saa kumi na mbili ya jioni.
“Twende!”Mzee Ayoub alimwamrisha Nancy.
“Wapi?”
“Nyumbani kwetu!”
“Mimi siondoki hapa! Sitaki kutengana na mama yangu!”
“Wewe unafanya utani sio?”
“Sio utani namaanisha ninachokisema, nimekwishakueleza kwamba sipo tayari kufanya tendo la ndoa kwa sababu nilishakula kiapo lakini husikii?”
“Mzee Kiwembe hebu lete ile nahiii! Tumekupa muda wa kuongea na mama yako ina maana hajakueleza yaliyompata?”
“Kanieleza lakini siwezi ni bora kufa!”
“Haya sasa, acha tuone nani atakuwa mshindi!”Aliongea babu Ayoub baada ya kukabidhiwa fimbo nyembamba iliyokatwa kutoka kwa mnyama wa majini aitwaye Kiboko!
“Nyanyuka!”
“Sinyanyuki!”
“Chaaaaaa!Chaaaa!”Fimbo hiyo nyembamba ilipita mgongoni mwa Nancy, akalia na kujikunjakunja na nyingine zaidi zikazidi kumiminika wakati mzee Kiwembe akimfunga Nancy mguu kwa kamba.
“Mamaaa! Mamaaa, tafadhali nisaidie!”Aliendelea kulia kadri fimbo zilivyoendelea kupasua mgongo wake, mama yake aliumia moyoni na kujikuta akinyanyuka mahali alipokuwa akitaka kumvamia babu Ayoub lakini kabla hajamfikia alipigwa ngumi usoni na mzee kiwembe akaanguka chini.
hakika walikuwa katika mateso na hawakujua jinsi ya kujiokoa, akiwa amelala chini mama alishuhudia mwanae akibebwa juujuu na wazee hao wawili kupelekwa kwenye kibanda cha babu Ayoub, huko alimsikia akiendelea kulia na kuomba msaada, alitamani kumsaidia lakini hakuwa na uwezo huo, maisha aliyokuwa akiyapitia Nancy ndiyo aliyoyapitia yeye karibu kila siku mpaka alipokubali kufanywa mke wa mzee Kiwembe.
Masaa matatu baadaye mzee Kiwembe akiwa amesharejea kwenye kibanda chake na kuendelea kumfanyia mama Nancy mambo yasiyostahili, kibandani kwa babu Ayoub nako kukawa kimya!Mama Nancy alielewa walishamchosha mtoto wake kwa kipigo na kujikuta akiwa tayari kwa lolote alilotaka kufanyiwa.
“Najua anamwingilia na sijui kitakachotokea ni nini?” Alijiuliza mama Nancy akilini mwake akifikiria kiapo.

Je nini kitaendelea?
Je Nancy na mama yake wataweza kutoka ndani ya kisiwa hicho?
 
SEHEMU YA 20
Hakusinzia mpaka asubuhi na kitu cha kwanza alichokifanya baada ya kuamka ni kwenda kwenye kibanda cha babu Ayoub kumwangalia mtoto wake, hapakuwa na mtu yeyote ndani ya kibanda! Alirudi haraka hadi ndani na kumuuliza mzee Kiwembe kama alikuwa na taarifa juu ya walikokuwa wameelekea.
“Labda wako ufukweni wanaoga?”
“Acha nikawaangalie!”
Alikimbia kwenda ufukweni, alikuwa na hamu ya kufahamu kama kuna madhara yoyote yaliyompata Nancy kutokana na kitendo alichofanyiwa usiku! Kabla hajafika ufukweni alikutana nao wakikimbizana, Nancy alikimbia akiwa uchi wa mnyama na kuimba nyimbo nyingi zisizoeleweka, akitaja na kuliita jina la Tonny kila baada ya maneno machache.
“Nancy!Nancy!Nancy!”Mama yake alimwita alipowafikia lakini mwanae hakumjali wala kumwitikia.
“TOKAAAA!TOKAAA MBELE YANGU MCHAWI MKUBWA WEEE!” Nancy alimwambia mama yake huku akimmwagia mchanga, maumivu yaliyompata mama Nancy moyoni mwake hayakuwa na maelezo! Machozi yalimiminika kama chemchem, lawama nyingi alizitupa kwa babu Ayoub.
“Mnaona sasa mlivyomfanya mwanangu, tulijitahidi kuwaelewesha juu ya kiapo alichokula lakini hamkutaka kuamini, tutafanya kitu gani sasa? Tayari ameshakuwa mwendawazimu!’
“Aa wapi! Hizi ni mbwembwe zake tu ili asishiriki tendo la ndoa, atake asitake huyu ni mke wangu lazima atafanya tu ! ”
“Lakini umemsababishia matatizo mtoto wangu! ”
“Hilo mimi sijali ! ”
“Nguo zake ziko wapi? ”Aliuliza mama Nancy.
“Amezitupa sehemu fulani huko ufukweni alikokuwa akikimbia ovyo!”Sehemu gani? ” Sifahamu ! Amenisumbua sana na bila kumshika angekufa maji kwa sababu alikuwa anataka kudumbukia majini ili afe ! Nancy ! Nancy ! Nancy ! Mama alimwita binti yake, badala ya kuitika Nancy aliendelea kukimbia huku akicheka na kuongea maneno yasiyoeleweka, tayari alikuwa mwendawazimu ! Kiapo alichokula kwa mganga kilikuwa kimemdhuru.
“Hahaaaa ! I don’t care ! I don’t mix milk and sugar ! I don’t go ! Here and there, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere is my hero. I love Saddam Hussein ! Haaaaa ! Haaaaa ! Haaaaa ! ” Nancy aliendelea kuongea mambo yasiyoeleweka na kuzidi kuumiza moyo wa mama yake aliyekuwa akilia huku akimfuata kwa nyuma .
Kila alipomkaribia Nancy alizidi kukimbia kwenda mbele zaidi mpaka alipokamatwa na mzee Kiwembe na kubebwa juu hadi kwenye kibanda cha babu Ayubu
“ Anajifanya mjanja ! Atatulia tu, hapa ni kisiwani bwana mambo ya hapa ni ya kijeshi-jeshi na ni lazima azae” Alijitapa babu Ayubu.
Mama yake alisikitika mno na hakuelewa ni kwa namna gani angeweza kuondoka kisiwani na mtu ambaye hakutaka hata kumkaribia, mipango yote ya kutoroka aliyoiongea na Nancy kabla hajapatwa na wendawazimu ilionekana kuwa migumu, kulikuwa na dalili kwamba maisha yao yangekuwa hapo kisiwani siku zote kama asingepatikana mtu wa kuwaokoa.
“ Na huyo mtu ataambiwa na nani kwamba tuko hapa ? Na sijui hivi sasa mzee Katobe anafikiria nini kuhusu mimi, nafikiri haelewi matatizo yanayonipata ! Nitakufa hapa bila kumwona” Aliwaza mama Nancy akimwangalia mwanae akifungwa miguu na mikono na kuunganishwa kwenye nguzo iliyokuwa katikati ya kibanda.

****
Hayo ndiyo yakawa maisha yao, Nancy akawa ni mtu wa kukaa kwenye kamba mchana na usiku, pamoja na kuwa mwehu hakuipenda hali hiyo, mara kwa mara alijaribu kujiondoa kwenye kamba lakini alishindwa.
Nyama za mikono na miguu yake zililiwa na kamba zilizomkaza na kumsababishia vidonda ! Mama yake alijitahidi kumwosha kila siku lakini alijichafua na kusababisha ngozi yake ibadilike na kuwa nyeusi. Nywele zake hazikutamanika, kwa kumwangalia mara moja tu hukuhitaji ufafanuzi kugundua hali yake ya akili.
Pamoja na hali hiyo, babu Ayubu hakukoma kumwingilia Nancy kimwili, suala la wendawazimu halikusumbua ubongo wake, alimfanyia kila aina ya ukatili akiwa kwenye kamba kama mateka, hakuyajali matatizo yake hata kidogo, kitu cha maana kwake ilikuwa kujistarehesha.
Miezi mitatu baadaye walikuwa wangali kisiwani wakipata mateso, mama yake Nancy aliishakata tamaa ya kuokolewa na kuamini hapakuwa na njia ya wao kuondoka tena kisiwani, hayo yaliishakuwa maisha yao na waliishakubaliana nayo.
Afya ya mtoto wake iliharibika kupita kiasi kwa sababu ya kugoma kula, mara nyingi alikuwa mgonjwa na alipoteza uzito mkubwa wa mwili wake ! Kwa sababu ya kutokuwepo kwa tiba yoyote pale kisiwani, matumaini kuwa siku moja mama Nancy angeondoka na mwanae akiwa salama yalipotea.
Bado hapakuwa na maongezi kati yao, Nancy hakuongea kitu na mama yake ! kila alipomsogelea alilia, maneno pekee ambayo mama huyu alikumbuka kuongea na mwanae ni yale aliyosema wakati anamsimulia juu ya mateso aliyoyapata kisiwani akilazimishwa kufanya ngono, hali hiyo ilimuumiza sana mama Nancy, mara kwa mara alitamani kuongea na mtoto wake lakini haikuwezekana ! Akili yake iliishaharibika.
“ Yote haya ni kwa sababu ya Tonny na sijui ni kwanini alimpeleka mwanangu kwa mganga kula kiapo ? ” Aliwaza mama Nancy. Mama Nancy alikuwa kama mke wa ndoa wa mzee Kiwembe, hakuyapenda maisha hayo na hakumpenda mzee huyo lakini hakuwa na chaguo jingine, alielewa wazi kuwa kumkataa kungemaanisha kifo chake na pengine cha mwanae ! Akiyafanya yote aliyotakiwa kufanya ili maisha yao yawe salama akitegemea labda siku moja wangeokolewa kutoka mikononi mwa wauaji.
Tumbo lake halikuwa la kawaida, lilikuwa kubwa kuashiria tayari alikuwa mjamzito ! Mimba ya mzee Kiwembe, jambo hilo lilimuumiza sana, mchana na usiku alilia lakini hakuweza kuubadilisha ukweli kuwa tayari alikuwa na mimba ya mtu ambaye hakuwa na mapenzi naye hata chembe.
Hakuwa na jibu la kumpa mume wake kama ingetokea siku moja akatoroka na kurudi nyumbani, alishindwa kuelewa ni maneno gani angesema ili mume wake amwelewe kwamba yote yaliyotokea hayakuwa mapenzi yake bali alilazimishwa ! Kwa hasira za mzee Katobe lazima angeuawa baada ya kuonekana msaliti.
“ Mungu atanisamehe sikuwa na chaguo haya si mapenzi yangu ! Na namwomba Mungu asaidie Nancy pia asije akapewa mimba maana babu Ayubu anamwingilia kila siku bila huruma” Aliendelea kuwaza huku akitayarisha chakula jikoni huku mzee Kiwembe akiwa amejilaza kwenye jamvi walilolitumia kama kitanda.
Afya ya mtoto wake ilizidi kumtisha alizidi kukonda kadiri siku zilivyokwenda ! Maisha yake yalikuwa hatarini, kila siku alimlilia mzee Kiwembe ili wampeleke aidha hospitali Kigoma au popote karibu lakini hakusikilizwa, alizidi kunyweshwa mizizi ya miti isiyoeleweka kila siku “ Kama Nancy atakufa, mimi pia sitakuwa na sababu ya kuendelea kuishi, nitajinyonga na kufa mara moja !” Aliwaza mama Nancy akiwa amekaa chini na kumwangalia mtoto wake aliyelala chini mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwenye nguzo.

Je nini kitaendelea?U YA 20
 
SEHEMU YA 21
Baada ya kuzimaliza fukwe zote bila mafanikio, mzee Katobe na Danny walianza kutembelea kisiwa kimoja baada ya kingine katika ziwa Tanganyika, wakianzia Kigoma kwenda chini hadi mpakani mwa Zambia na Tanzania, kisha kupandisha tena kuelekea Kigoma wakiwauliza watu wote waliokutana nao kama waliwahi kusikia mahali popote walipozikwa watu waliozama maji siku za karibuni, hawakufanikiwa kupata fununu zozote.
“ Hakuna tunachoweza kufanya ! lililopo ni kumshukuru Mungu, turudi nyumbani tuendelee na maisha ! Hakuna kitu kilichoumiza moyo wangu tangu nizaliwe mpaka leo hii kama tukio hili ”
“ Pole sana mzee Katobe lakini haya ndiyo mambo ya dunia !” Nahodha waliyezunguka naye alimfariji.
Mzee Katobe akawa amenyoosha mikono yake juu na kusema “ Haiwezikani tena !” Kilichofanyika baada ya uamuzi huo ni kufanya Ibada ziwani tena kwa masikitiko makubwa kuwaombea marehemu walale mahali pema peponi, waliamini walikuwa wamejitahidi kwa uwezo wao wote kuzitafuta maiti za wapendwa wao lakini hawakufanikiwa na hapakuwa na kitu ambacho wangeweza kukifanya tena.
“ Inatosha, inabidi tukubaliane na ukweli” Alisema mzee Katobe.
“ Nasikitika Nancy amekufa kabla sijamuoa, ameniachia mapenzi mazito moyoni, nilimpenda Nancy kwa moyo wangu wote na nitaendelea kumpenda mpaka nitakapokutana naye ahera, naamini hatatokea msichana mwingine nitakayempenda kiasi hicho” Aliongea Danny akiwa ndani ya boti, kila alipoyaangalia maji ya ziwa Tanganyika moyo wake ulizidi kuuma, aliamini ndiyo yaliyochukua uhai wa mwanamke aliyempenda .
“ Nimepoteza mke na mtoto roho inaniuma sana, hata hivyo nina wewe Danny siku zote nitakuchukulia kama mtoto wangu ingawa una wazazi wako, jisikie huru kuwa na mimi nitakusaidia kwa kila kitu utakachohitaji!”
“ Hata mimi nitakuwa pamoja na wewe ukizingatia wazazi wangu wamekasirika!” Alijibu Danny. “ Lakini ni lazima ufanye kila kinachowezekana kurejesha uhusiano mzuri na wazazi, huwezi kuishi bila maelewano mazuri na wao !”
“ Nitajitahidi !
Masaa ishirini baadaye waliingia Kigoma wakiwa wamechoka taaban na akili zao zikiwa zilijawa na hisia za msiba, pamoja na juhudi za miezi kadhaa za kutafuta maiti za watu waliowapenda walikuwa wamerudi nchi kavu wakiwa mikono mitupu na kulikuwa na deni la Sh. milioni saba ambazo mzee Katobe alitakiwa kuwalipa wenye boti aliyoikodi hakuwa na la kufanya zaidi ya kulipa.
“Tulipe nusu tu, nyingine ni msaada! Mkurugenzi wa kampuni ya kukodisha vyombo vya majini alimwambia mzee Katobe, kila mtu alimwonea huruma.
“Nitalipa” Hilo ndilo lilikuwa jibu lake na siku hiyo hiyo alikwenda benki akachukua kiasi cha fedha alichodaiwa na kulipa deni lote kisha yeye na Danny wakaondoka kwa ndege ya Shirika la ndege Tanzania kurejea Dar es Salaam, hawakukaa jijini, bali walipitiliza hadi Bagamoyo kupeleka msiba.
Wananchi wa Bagamoyo waliomfahamu mama Nancy walilia na kuomboleza kupita kiasi, ulikuwa msiba mkubwa sana mjini humo. Kwa muda mrefu walikuwa hawaoni mtu katika nyumba ya mzee Katobe, na walishindwa kuelewa yeye, mke wake na mtoto wao walikwenda wapi.
Taarifa kuwa mama Nancy na mwanae walikuwa marehemu zilimsikitisha kila mtu aliyesikia, mamia ya watu walifurika nyumbani kwa mzee Katobe kuomboleza, hapakuwa na kitu cha kuzika, hivyo hata kaburi halikuchimbwa. Yaliwekwa matanga ya siku tatu kisha majirani wakasambaa na kubaki ndugu wa karibu.
****
Mwezi mmoja baada ya msiba huo mzee Katobe na Danny walilazimika kurudi katika maisha yao ya kawaida, dunia ilikuwa bado ikiendelea hata kama mama Nancy na mwanae hawakuwa duniani ! Walikuwa ni watu wa karibu mno, mzee Katobe kama alivyoahidi alimchukulia Danny kama mwanae.
Danny alirejea chuoni kuomba kuendelea na masomo yake, ilikuwa ni bahati nzuri kwake mwaka mwingine wa masomo ndio ulikuwa unaanza, akajiunga na wanafunzi wapya na kurudia mwaka wa pili. Mazingira ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam yalimkumbusha mengi kuhusu Nancy mara nyingi alilia hasa alipowaona au kukaa mahali alipowahi kukaa na Nancy.
“Maisha yangu hayatakuwa sawa tena !” Alijisemea maneno hayo karibu kila siku.
Mzee Katobe naye hakuwa na la kufanya zaidi ya kukubaliana na ukweli na kurudi kwenye shughuli zake za biashara ingawa kwake pia maisha hayakuwa sawa na zamani, kila siku aliwafikiria mke na mtoto wake. Pengo lao lilionekana wazi, walikuwa watu muhimu sana katika maisha yake.
“Siwezi kuishi peke yangu, huzuni inazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda, ni lazima nioe mwanamke mwingine maana niliyepewa na Mungu amekwishakufa !” Siamini kama nitapata mwanamke atakayefanana na mama Nancy kwa kila kitu ” Aliwaza mzee Katobe bila kuelewa kuwa mke na mtoto wake walikuwa bado hai wakiteseka katika kisiwa cha Galu katikati ya ziwa Tanganyika .
****
“Aa wapi! Hizi ni mbwembwe zake tu ili asishiriki tendo la ndoa, atake asitake huyu ni mke wangu lazima atafanya tu ! ” “ Lakini umemsababishia matatizo mtoto wangu! ”
“Hilo mimi sijali ! ” “ Nguo zake ziko wapi? ”Aliuliza mama Nancy.
“Amezitupa sehemu fulani huko ufukweni alikokuwa akikimbia ovyo ! ” Sehemu gani? ” Sifahamu ! Amenisumbua sana na bila kumshika angekufa maji kwa sababu alikuwa anataka kudumbukia majini ili afe ! Nancy ! Nancy ! Nancy ! Mama alimwita binti yake, badala ya kuitika Nancy aliendelea kukimbia huku akicheka na kuongea maneno yasiyoeleweka, tayari alikuwa mwendawazimu ! Kiapo alichokula kwa mganga kilikuwa kimemdhuru.
“Hahaaaa ! I don’t care ! I don’t mix milk and sugar ! I don’t go ! Here and there, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere is my hero. I love Saddam Hussein ! Haaaaa ! Haaaaa ! Haaaaa ! ” Nancy aliendelea kuongea mambo yasiyoeleweka na kuzidi kuumiza moyo wa mama yake aliyekuwa akilia huku akimfuata kwa nyuma .
Kila alipomkaribia Nancy alizidi kukimbia kwenda mbele zaidi mpaka alipokamatwa na mzee Kiwembe na kubebwa juu hadi kwenye kibanda cha babu Ayubu
“Anajifanya mjanja ! Atatulia tu, hapa ni kisiwani bwana mambo ya hapa ni ya kijeshi-jeshi na ni lazima azae” Alijitapa babu Ayubu.
Mama yake alisikitika mno na hakuelewa ni kwa namna gani angeweza kuondoka kisiwani na mtu ambaye hakutaka hata kumkaribia, mipango yote ya kutoroka aliyoiongea na Nancy kabla hajapatwa na wendawazimu ilionekana kuwa migumu, kulikuwa na dalili kwamba maisha yao yangekuwa hapo kisiwani siku zote kama asingepatikana mtu wa kuwaokoa.
“Na huyo mtu ataambiwa na nani kwamba tuko hapa ? Na sijui hivi sasa mzee Katobe anafikiria nini kuhusu mimi, nafikiri haelewi matatizo yanayonipata ! Nitakufa hapa bila kumwona” Aliwaza mama Nancy akimwangalia mwanae akifungwa miguu na mikono na kuunganishwa kwenye nguzo iliyokuwa katikati ya kibanda.
*****
Hayo ndiyo yakawa maisha yao, Nancy akawa ni mtu wa kukaa kwenye kamba mchana na usiku, pamoja na kuwa mwehu hakuipenda hali hiyo, mara kwa mara alijaribu kujiondoa kwenye kamba lakini alishindwa.
Nyama za mikono na miguu yake zililiwa na kamba zilizomkaza na kumsababishia vidonda ! Mama yake alijitahidi kumwosha kila siku lakini alijichafua na kusababisha ngozi yake ibadilike na kuwa nyeusi. Nywele zake hazikutamanika, kwa kumwangalia mara moja tu hukuhitaji ufafanuzi kugundua hali yake ya akili.
Pamoja na hali hiyo, babu Ayubu hakukoma kumwingilia Nancy kimwili, suala la wendawazimu halikusumbua ubongo wake, alimfanyia kila aina ya ukatili akiwa kwenye kamba kama mateka, hakuyajali matatizo yake hata kidogo, kitu cha maana kwake ilikuwa kujistarehesha.
Miezi mitatu baadaye walikuwa wangali kisiwani wakipata mateso, mama yake Nancy aliishakata tamaa ya kuokolewa na kuamini hapakuwa na njia ya wao kuondoka tena kisiwani, hayo yaliishakuwa maisha yao na waliishakubaliana nayo.
Afya ya mtoto wake iliharibika kupita kiasi kwa sababu ya kugoma kula, mara nyingi alikuwa mgonjwa na alipoteza uzito mkubwa wa mwili wake ! Kwa sababu ya kutokuwepo kwa tiba yoyote pale kisiwani, matumaini kuwa siku moja mama Nancy angeondoka na mwanae akiwa salama yalipotea.
Bado hapakuwa na maongezi kati yao, Nancy hakuongea kitu na mama yake ! kila alipomsogelea alilia, maneno pekee ambayo mama huyu alikumbuka kuongea na mwanae ni yale aliyosema wakati anamsimulia juu ya mateso aliyoyapata kisiwani akilazimishwa kufanya ngono, hali hiyo ilimuumiza sana mama Nancy, mara kwa mara alitamani kuongea na mtoto wake lakini haikuwezekana ! Akili yake iliishaharibika.
“ Yote haya ni kwa sababu ya Tonny na sijui ni kwanini alimpeleka mwanangu kwa mganga kula kiapo ? ” Aliwaza mama Nancy. Mama Nancy alikuwa kama mke wa ndoa wa mzee Kiwembe, hakuyapenda maisha hayo na hakumpenda mzee huyo lakini hakuwa na chaguo jingine, alielewa wazi kuwa kumkataa kungemaanisha kifo chake na pengine cha mwanae ! Akiyafanya yote aliyotakiwa kufanya ili maisha yao yawe salama akitegemea labda siku moja wangeokolewa kutoka mikononi mwa wauaji.
Tumbo lake halikuwa la kawaida, lilikuwa kubwa kuashiria tayari alikuwa mjamzito ! Mimba ya mzee Kiwembe, jambo hilo lilimuumiza sana, mchana na usiku alilia lakini hakuweza kuubadilisha ukweli kuwa tayari alikuwa na mimba ya mtu ambaye hakuwa na mapenzi naye hata chembe.
Hakuwa na jibu la kumpa mume wake kama ingetokea siku moja akatoroka na kurudi nyumbani, alishindwa kuelewa ni maneno gani angesema ili mume wake amwelewe kwamba yote yaliyotokea hayakuwa mapenzi yake bali alilazimishwa ! Kwa hasira za mzee Katobe lazima angeuawa baada ya kuonekana msaliti.
“Mungu atanisamehe sikuwa na chaguo haya si mapenzi yangu! Na namwomba Mungu asaidie Nancy pia asije akapewa mimba maana babu Ayubu anamwingilia kila siku bila huruma” Aliendelea kuwaza huku akitayarisha chakula jikoni huku mzee Kiwembe akiwa amejilaza kwenye jamvi walilolitumia kama kitanda.
Afya ya mtoto wake ilizidi kumtisha alizidi kukonda kadiri siku zilivyokwenda ! Maisha yake yalikuwa hatarini, kila siku alimlilia mzee Kiwembe ili wampeleke aidha hospitali Kigoma au popote karibu lakini hakusikilizwa, alizidi kunyweshwa mizizi ya miti isiyoeleweka kila siku “ Kama Nancy atakufa, mimi pia sitakuwa na sababu ya kuendelea kuishi, nitajinyonga na kufa mara moja !” Aliwaza mama Nancy akiwa amekaa chini na kumwangalia mtoto wake aliyelala chini mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwenye nguzo.
*****
Baada ya kuzimaliza fukwe zote bila mafanikio, mzee Katobe na Danny walianza kutembelea kisiwa kimoja baada ya kingine katika ziwa Tanganyika, wakianzia Kigoma kwenda chini hadi mpakani mwa Zambia na Tanzania, kisha kupandisha tena kuelekea Kigoma wakiwauliza watu wote waliokutana nao kama waliwahi kusikia mahali popote walipozikwa watu waliozama maji siku za karibuni, hawakufanikiwa kupata fununu zozote.
“Hakuna tunachoweza kufanya ! lililopo ni kumshukuru Mungu, turudi nyumbani tuendelee na maisha ! Hakuna kitu kilichoumiza moyo wangu tangu nizaliwe mpaka leo hii kama tukio hili ”
“Pole sana mzee Katobe lakini haya ndiyo mambo ya dunia !” Nahodha waliyezunguka naye alimfariji.
Mzee Katobe akawa amenyoosha mikono yake juu na kusema “ Haiwezikani tena !” Kilichofanyika baada ya uamuzi huo ni kufanya Ibada ziwani tena kwa masikitiko makubwa kuwaombea marehemu walale mahali pema peponi, waliamini walikuwa wamejitahidi kwa uwezo wao wote kuzitafuta maiti za wapendwa wao lakini hawakufanikiwa na hapakuwa na kitu ambacho wangeweza kukifanya tena.
“Inatosha, inabidi tukubaliane na ukweli” Alisema mzee Katobe.
“ Nasikitika Nancy amekufa kabla sijamuoa, ameniachia mapenzi mazito moyoni, nilimpenda Nancy kwa moyo wangu wote na nitaendelea kumpenda mpaka nitakapokutana naye ahera, naamini hatatokea msichana mwingine nitakayempenda kiasi hicho” Aliongea Danny akiwa ndani ya boti, kila alipoyaangalia maji ya ziwa Tanganyika moyo wake ulizidi kuuma, aliamini ndiyo yaliyochukua uhai wa mwanamke aliyempenda .
“ Nimepoteza mke na mtoto roho inaniuma sana, hata hivyo nina wewe Danny siku zote nitakuchukulia kama mtoto wangu ingawa una wazazi wako, jisikie huru kuwa na mimi nitakusaidia kwa kila kitu utakachohitaji!”
“Hata mimi nitakuwa pamoja na wewe ukizingatia wazazi wangu wamekasirika!” Alijibu Danny. “ Lakini ni lazima ufanye kila kinachowezekana kurejesha uhusiano mzuri na wazazi, huwezi kuishi bila maelewano mazuri na wao !”
“Nitajitahidi !
Masaa ishirini baadaye waliingia Kigoma wakiwa wamechoka taaban na akili zao zikiwa zilijawa na hisia za msiba, pamoja na juhudi za miezi kadhaa za kutafuta maiti za watu waliowapenda walikuwa wamerudi nchi kavu wakiwa mikono mitupu na kulikuwa na deni la Sh. milioni saba ambazo mzee Katobe alitakiwa kuwalipa wenye boti aliyoikodi hakuwa na la kufanya zaidi ya kulipa.
“Tulipe nusu tu, nyingine ni msaada ! Mkurugenzi wa kampuni ya kukodisha vyombo vya majini alimwambia mzee Katobe, kila mtu alimwonea huruma.
“Nitalipa” Hilo ndilo lilikuwa jibu lake na siku hiyo hiyo alikwenda benki akachukua kiasi cha fedha alichodaiwa na kulipa deni lote kisha yeye na Danny wakaondoka kwa ndege ya Shirika la ndege Tanzania kurejea Dar Es Salaam, hawakukaa jijini, bali walipitiliza hadi Bagamoyo kupeleka msiba.
Wananchi wa Bagamoyo waliomfahamu mama Nancy walilia na kuomboleza kupita kiasi, ulikuwa msiba mkubwa sana mjini humo. Kwa muda mrefu walikuwa hawaoni mtu katika nyumba ya mzee Katobe, na walishindwa kuelewa yeye, mke wake na mtoto wao walikwenda wapi.


Je nini kitaendelea?
Je Nancy na mama yake wataweza kutoka kisiwani humo?
 
SEHEMU YA 22
Baada ya kuzama ziwani Nancy na mama yake wanajikuta katika kisiwa cha Galu kilichoko katikati ya ziwa Tanganyika, safari yao kuelekea Kongo kumtafuta mzee Mwinyimkuu aliyemlisha Nancy yamini inaonekana kufikia mwisho!
Wapo mikononi mwa wazee wawili, mzee Kiwembe na babu Ayoub. Wazee hao walifika kisiwani hapo miaka mingi iliyopita baada ya kupata ajali majini, wameishia hapo peke yao bila mwanamke! Hivyo kuja kwa Nancy na mama yake kunaonekana kuwa baraka, wanawageuza wake zao.
Mzee Kiwembe alimchagua mama Nancy, pamoja na kutaarifiwa juu ya kiapo ambacho msichana huyo alikula babu Ayoub anaamua kumwingilia Kimwili! Hapohapo Nancy anashikwa na wendawazimu na kuwa mwehu kamili.
Mama yake anasikitika lakini anakosa la kufanya sababu wao ni kama mateka baadaye anaamua kuukubali ukweli na kuendelea kuishi na mzee Kiwembe kama mumewe! Muda mfupi baadaye anakuwa mjamzito, hali inayomchanganya na kumfanya ashindwe kuelewa nini angemwambia mume wake mzee Katobe kama angeondoka kisiwani na kurejea Bagamoyo!
Hali ya mtoto wake ni mbaya, Nancy anazidi kukonda! Wendawazimu unamfanya agome kula chakula, ni mtu mwenye vurugu nyingi jambo linalosababisha afungwe kamba kwenye nguzo kubwa iliyokuwepo kibandani kwa babu Ayoub.
Mama Nancy hakuwa na uhakika kama siku moja angeondoka kisiwani hapo na mtoto wake na hakuwa tayari kushuhudia Nancy akifa! Kila siku aliwalilia mzee Kiwembe na babu Ayoub wamchukue Nancy kwenda Kigoma kwa matibabu zaidi.

SONGA NAYO

Kila siku iliyokuja na kupita mama Nancy alifikiria ni kwa namna gani angeweza kuondoka kisiwani na kufika Kigoma akiwa na mtoto wake, uwezekano ulizidi kupungua kadri siku zilivyozidi kusonga mbele, wakati huohuo hali ya Nancy ilizidi kudhoofika siku hadi siku!
Pamoja na kuwa mjamzito mwanamke huyo hakuogopa kwenda kwa mume wake, alimpenda mzee Katobe na aliamini kama angekutana naye na kumpa maelezo juu ya kilichotokea hakika angemwelewa na kukubali kumsamehe! Mimba hakikuwa kikwazo cha yeye kuondoka, tatizo lilikuwa usafiri na ni kwa namna gani angeweza kumpandisha Nancy katika mtumbwi hata kama angeamua kuondoka na kimtumbwi kidogo cha wazee wale usiku wakiwa wamelala.
“Mtoto mwenyewe wamemharibu akili, nikimsogelea anataka kunipiga! Hataki hata kuniona, sijui wamemfanyia kitu gani mpaka kunisahau mimi mama yake!” Aliwaza mama Nancy.
Mama Nancy alionekana kugota kabisa kimawazo, alikosa mpango au mbinu za kumwondoa kisiwani lakini kila siku akili yake ilifanya kazi! Hakuwa tayari kuona mtoto wake anakata roho wakiwa kisiwani, alikuwa tayari kufia mbele kwa mbele akitafuta usalama wa maisha yao wote wawili.
Miezi ilizidi kukatika taratibu hatimaye mama Nancy akajifungua mtoto wa kiume, mzee kiwembe alimwita mtoto huyo Magurumchumvi, jina la babu yake aliyewahi kuwa mganga maarufu wilayani Kasulu mkoani Kigoma! Pamoja na kumzaa mtoto huyo nje ya ndoa yake, bado mama Nancy alimpenda mtoto huyo, hata siku moja hakuwahi kumwita kwa jina la Magurumchumvi, alimwita David akimfananisha na Daudi wa Biblia aliyempiga na kumuua mtu mwenye nguvu, Goliath.
Hakuna siku iliyopita bila yeye kupanga mkakati wa kuondoka, ilikuwa ni lazima atoroke tena akiwa na watoto wake wote wawili, asingemwacha Nancy kisiwani vinginevyo alikuwa tayari kufa pamoja naye kisiwani Galu! Bado manyanyaso yaliendelea kila siku aliingiliwa na mzee kiwembe na alimsikia Nancy akilia usiku mzima babu Ayoub akimfanyia ukatili bila kujali alikuwa mwendawazimu.
Mtoto akiwa na miezi minne tu alianza kuhisi dalili ya mimba nyingine, kichefuchefu na kutapika asubuhi kwake kulimaanisha ujauzito! Ilikuwa ni kama utani lakini miezi mitatu baadaye mtoto David akiwa na umri wa miezi saba mimba ilionekana wazi, mzee kiwembe hakusikitishwa na hilo kwake ilikuwa furaha kupata watoto wawili katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu! Alijiona shujaa aliyekuwa akifidia muda aliopoteza kisiwani, hilo lilimfanya babu ayoub naye azidishe kasi ya kumwingilia Nancy akitafuta mtoto bila kujali mtu aliyemfanyia kitendo hicho alikuwa mgonjwa na mwendawazimu.
“Najitahidi sana lakini wa kwangu hapati mimba!”
“Pole sana, mimi sasa hivi naelekea kupata wawili!”
“Nimeona!”
“Ongeza juhudi!”
“SItachoka mpaka mtoto apatikane, vinginevyo atafia kwenye kamba!”
Waliongea wazee hao mama Nancy akisikia, aliumia sana moyoni mwake lakini wao hawakujali! Hawakuwachukulia Nancy na mama yake kama binadamu wa kawaida bali watumwa ambao kazi yao ilikuwa ni kuwaridhisha kingono. Kitu kimoja kilimsumbua mama Nancy kichwani mwake, mtumbwi! Alihitaji chombo cha kumsafirishia yeye na watoto wake, ni hapo ndipo alipofikia kuanza kuchonga au kutengeneza kitu chochote cha kuelea majini ambacho angetumia kukatisha ziwa Tanganyika akipiga kasia.
Aliliona wazo hilo la kufaa kabisa, hapakuwa na njia nyingine ya kujiokoa zaidi ya kupata mtumbwi, ni hapo ndipo alipoanza kila siku mzee Kiwembe na babu Ayoub wakiwa ziwani, alikwenda msituni na kukata miti ya Mikule! Iliokuwa kama boya ndani, ilifanana sana na Milingoti ya katani lakini yenyewe ikiwa na unene wa kama nguzo ya umeme, ilikuwa rahisi kuangusha kwa sababu iliota sehemu zenye majimaji!
Alikata miti mingi na kuikata katika vipande vya kama futi sita na kwa kutumia kamba za magome ya miti alianza kuvifunga vipande hivyo pamoja na kufanya kitu kama sakafu ya miti, haikuwa kazi ndogo! Aliifanya taratibu na kila siku alipopata nafasi, alitumia miezi miwili kukamilisha kutengeneza kitu alichokuwa akihitaji ingawa hakuwa na uhakika kama kingeweza kuelea na hatimaye kumvusha kwenda upande wa pili, alikuwa amechoka kuishi kisiwani akishuhudia mwanae akiteseka.
Alikiita kitu alichokitengeneza jina la pantoni na kukisukuma hadi majini akitaka kuona kama kingeelea, hivi ndivyo ilivyokuwa! Kwa macho yake alikiona kikielea majini, alipanda juu yake kuona kama kingezama lakini bado kilielea na hakikuonekana kuelemewa na uzito. Moyo wake ukaanza kurejewa na matumaini ya kuondoka kisiwani hapo, aliporudi nyumbani siku hiyo fikra zake zote zilikuwa ni lini angeondoka! Kila siku haikupatikana kwani babu ayoub alipoondoka kwenda ziwani kuvua aliacha mlango umefungwa.
Angetaka kuondoka peke yake bila Nancy ingekuwa rahisi lakini hakuwa tayari kumwacha mtoto wake hilo ndilo lilimfanya aendelee kukaa kisiwani mpaka akajifungua mtoto wa pili! Huyo alikuwa ni wa kike na mzee Kiwembe alimeita kwa jina la Mategelesi, jina la bibi yake ambaye alikuwa kuwa mganga wa kienyeji hata siku moja mama Nancy hakumwita mtoto wake kwa jina hilo, alimwita Catherine na alimpenda ingawa alizaliwa nje ya ndoa.
Tayari alikuwa na watoto watatu na wote alitaka kuondoka nao kwenda Kigoma au Kongo, alichotaka ni kufika nchi kavu! Huko angeelewa kitu cha kufanya ili hatimaye arejee Dar es Salaam na baadaye Bagamoyo hakuogopa kurudi kwa mzee Katobe na watoto, Mpaka wakati huo hakuelewa ni kwanini akiwa na mumewe hakuwahi kupata ujauzito zaidi ya ule wa Nancy lakini akiwa na mzee Kiwembe alikuwa akipata mimba mfululizo.
“Nitaondoka! Siku yoyote nitakayopata nafasi ya kumwondoa Nancy katika kibanda hicho ndio siku nitakayoondoka hapa kisiwani, itatokea tu! Kosa moja magoli mia kwa sasa wacha nijifanye mnyonge!”Aliwaza mama Nancy.
****
“Siwezi kuoa! Siwezi, tena wazo hili lisinijie tena kichwani mwangu, kama ni kufa kwa huzuni acha nife! Ningemzika mke wangu na kuliona kaburi lake hapo ndio ningefikiria kuoa! Siamini kama kama Nancy na mwanangu kweli wamekufa! Wanaweza kuwa mahali fulani wanaishi au wamekwama, nikaoa halafu siku moja mke wangu akarudi! Nitafanya nini mimi? Nitamwambia nini mke wangu? Haiwezekani nampenda sana mama Nancy na siamini kama kweli yeye na mwanangu wamekufa!” Aliwaza mzee Katobe.
Maisha yake yalikuwa ya huzuni mno, watu waliomfahamu walimwonea huruma! Aliishi peke yake bila hata mfanyakazi, alikonda kwa mawazo.
Marafiki zake wengi walimshauri aoe lakini hakukubali! Hisia kuwa siku moja mke pamoja na mtoto wake wangerudi zilimsumbua kichwani, alivumilia hadi mwaka ukapita na kuahidi kuendelea kuishi peke yake hadi mwisho wa maisha yake labda mke wake atokee.
Kwa Danny ilikuwa tofauti, alipoingia chuoni mara ya kwanza baada ya kutoka Kigoma kumtafuta Nancy na mama yake alikuwa mtu mwenye huzuni sana, mara nyingi alionekana kutokwa na machozi! Hakuamini maisha yake yangekuwa sawa tena, watu wengi waliomfahamu Nancy walihuzunishwa sana na habari za kifo chake lakini kwa wasichana waliomtamani Danny siku zote hali ilikuwa tofauti, baadhi yao walifurahia na kuona hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee kumpata mwanaume waliyempenda ambaye siku zote alijifanya mgumu.
Mmoja wa wasichana hao alikuwa ni Agness alisoma darasa moja na Danny lakini sababu ya kurudia mwaka Agness alijikuta yupo mbele yake, aliwahi kuwa rafiki mkubwa wa Nancy, lakini pia alimpenda Danny tangu mwanzo hakutaka kuliingilia penzi lao.
Alijifanya kumwonea huruma Danny, muda wote akiwa pembeni yake na kumfariji, lakini hilo halikuwa lengo lake, muda wote alitafuta kuwa naye karibu ili hatimaye aweze kumwingiza katika mtego wa kuwa mpenzi wake! Alichofahamu yeye ni kwamba, kumnasa mwanamume au mwanamke mwenye huzuni kimapenzi kilikuwa kitendo rahisi kuliko kumeza tonge la ugali.
Danny hakuweza kuitafsiri hali hiyo mapema, kila alichofanyiwa na Agness alikiona chema, walisoma pamoja, alipikiwa chakula, alinyooshewa nguo na hata kufuliwa nguo zake! Mambo yaliharibika zaidi Agness alipoomba kuwa anamchua mwili Danny, hilo pia Danny hakulitafsiri kwa upana wake akawa amekubali akifikiri ni huduma ya kawaida hatimaye akajikuta amenaswa kabisa, maisha bila Agness yakaanza kuonekana magumu, alionekana tiba ya huzuni yake.
Penzi lilianza taratibu kati yao, Agness akawa anaingia taratibu na kuzipa tundu lililoachwa na Nancy! Kidonda kikiaanza kupona moyoni, penzi likakomaa mpaka danny kuamua kumtambulisha Agness kwa mzee Katobe aliyemchukulia kama baba yake, bado hakuwa na mawasiliano na wazazi wake.
Mzee katobe hakuwa na kipingamizi, asingeweza kumzuia Danny asiwe na mpenzi au kuoa wakati hakuwa na uhakika mkubwa kama siku moja mwanae angerudi.
“Agness! Kuna kila dalili kuwa ninakupenda na ninafikiria kukufanya mke wangu baadaye! Lakini kuna kitu kimoja kinachonisumbua!”Danny alimwambia Agness wakiwa wamekaa wawili chumbani mwao, waliishi kama mke na mume ingawa walikuwa wanafunzi.
“Kitu gani Danny?”
“Nakumbuka nimewahi kukueleza habari za Nancy!”
“Ndio!”
“Kifo cha Nancy kilitokea lakini sikuwahi kuiona maiti yake, kuna wakati huwa nahisi anaweza kuwa anaishi mahali fulani na mimi ninampenda itakuwaje akirudi!”
“Kwani unafikiri anaweza kurudi?”
“Kwa sababu sikuiona maiti wala kaburi lake!”
“Akirudi basi mimi nitawaacha muendelee!”
“Kweli?”
“Ndio!”
“Ahidi!”
“Naahidi!”
“Mh!”Aliguna Danny.
“Kwanini unaguna?”
“Haiwezi kuwa rahisi kiasi hicho!”
“Huo ndio ukweli siwezi kuwatenganisha watu wanaopenda, unampenda Nancy kuliko mimi eh?” Agness aliuliza.
“Unajua....!”Danny hakuwa na jibu la swali hilo lakini ukweli uliokuwa moyoni mwake ulikuwa ni sehemu ya swali alilouliza Agness.
“Najua nini? Inabidi unithibitishie Danny!”
“Nakupenda Agness, tatizo ni hilo tu!” Nancy akirudi nitalazimika kuwa naye, hapo naomba nieleweke.
“Utanioa?”
“Wakati wowote ukitaka lakini uelewe kuwa Nancy akirudi....!”
“Hilo halina tatizo kwangu! Watu wakienda ahera huwa hawarudi, angekuwa hai lazima angeshajitokeza!”Agness alisema.
“Unataka tufunge ndoa lini?” Mzee katobe yupo tayari kusimamia ndoa yangu.
“Hata mwezi ujao!”
****
Penzi lilizidi kupamba moto, Danny alionekana kupata faraja! Hakulia tena kama ilivyokuwa zamani, kila siku zilivyozidi kwenda ndivyo penzi kati yake Agness lilivyozidi kukua na kufanya mipango ya ndoa ipelekwe kwa kasi ya sauti! Kila mtu alitaka kuwa na mwenzake milele na kifupi kila mtu aliamini walifaa kuwa mke na mume!
Walikuwa kivutio kila walikokwenda, wakitembea mkono kwa mkono bwana mbele na bibi nyuma kiasi cha wanafunzi wenzao kuwabadilisha jina kuwaita kumbikumbi!
Kila siku najaribu kufikiria siku ya ndoa yetu nashindwa kuelewa itakuwaje! Bila shaka itakuwa miongoni mwa harusi kubwa hapa jijini Dar es Salaam maana wanachanga isivyo kawaida na mzee Katobe amedhamiria kuonyesha mfano anataka kuwaonyesha watu kuwa bado yupo katika chati si unajua kuna watu walianza kusema eti amechoka, sasa ameamua kuonyesha uwezo wake kwenye harusi yetu!”
“Ndiyo!”
“Basi itakuwa bomba! Hata baba na mama yangu wamepania kweli ila waliniuliza swali moja!”
“Swali gani darling?”
“Juu ya wazazi wako! Eti ni kwanini usimalize tofauti iliyopo ili harusi yetu ipate baraka zote?”
“Mzee Katobe analishughulikia jambo hili, mambo yanakwenda vizuri kuna uwezekano baba na mama wakaja hapa nchini wakati wa harusi!”
Haya ndiyo yalikuwa maongezi kati ya Danny na Agness kila siku waliyokutana, walikuwa na njaa na hamu kubwa ya harusi ili waweze kuishi pamoja!
Kwa Agness aliona ndoa ndio kitu pekee alichoamini kingemfunga Danny hata kama siku moja Nancy angerudi kutoka katika wafu, aliuteka moyo wa Danny kisawasawa na kumsahaulisha kabisa kama duniani aliweza kuishi na mtu aliyeitwa Nancy, hakumpa nafasi ya kumfikiria.
Karibu kila mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikuwa na taarifa juu ya harusi hiyo, wengi walichanga na kumpongeza Agness kwa kumpata mvulana mgumu kupatikana kuliko mwingine yeyote chuoni. Danny hakuwa mwanaume wa kujirahisisha kwa wanawake! Alijiheshimu lakini wakati yeye aliwatesa waliomtamani naye pia aliteswa na mwanamke aliyeitwa Nancy! Historia hiyo haikuwa rahisi kufutika kichwani mwake.
Mgogoro kati yake na wazazi wake ulimalizika, wazazi wakaja nchini kuonana naye, Danny akapiga magoti na kuwaomba wazazi wake msamaha! Wakashikana mikono na kumaliza tofauti zao.
Hawakuwa na tatizo juu ya mipango ya harusi hasa walipomwona mkamwana wao, Agness aliwavutia sana, hasa mama yake Danny! Alifurahishwa na kila kitu alichokuwa Agness kuanzia maumbile hadi kuongea kwake.
“This is the girl fit to be your wife my dear son!”(Mwanangu mpendwa huyu ndiye mwanamke anayefaa kuwa mke wako!)
“I know mom!”(Nafahamu mama!)
“So you have decided to get married?(Kwa hiyo umeamua kuoa?
“Yes mom!”(Ndio mama)
“You have to remember one thing!”(Ukumbuke kitu kimoja!)
“Nini mama?”
“Never start something you can’t finish!”(Kamwe usianzishe kitu ambacho huwezi kukimaliza!”)Alishauri mama yake Danny katika maongezi yao yakiyofanyika faragha nyumbani kwa mzee Katobe huko Bagamoyo,walishamkubali mzee huyo kama sehemu ya familia yao.
“I agree, but thre is one thing!”(Nakubali, lakini kuna kimoja!)
“What is it?”(Nini hicho!)
“I’m not sure of Nancy’s death!”(Sina uhakika juu ya kifo cha Nancy)
Danny alimwambia mama yake na baadae kutumia karibu masaa mawili kueleza kila kitu kati na msichana huyo na jinsi yeye na mzee Katobe walivyohangaika kumtafuta Nancy na mama yake, alipofika mwisho wa maelezo hayo hapakuwa na neno jingine kutoka kwa wazazi wake zaidi ya kumuhakikishia kuwa si Nancy wala mama yake walikuwa hai na kutaka ndoa yake ifungwe haraka iwezekanavyo.
“Mzee Katobe mmepanga ndoa hii ifungwe lini?”
“Kwa ninavyofahamu kila kitu kinakwenda sawa na tulikuwa tunawasubiri nyinyi tu!”
“Inawezekana kufunga mwezi ujao?”
“Ni wangapi kweli?”Mzee Katobe aliuliza.
“Wa nne!”
“Tarehe ngapi?”
“Katikati ya mwezi baada ya Kwaresma,mfano tarehe kumi na saba mnaionaje?”
“Mimi sina matatizo labda mtoto!”
“Mimi na mwenzangu tunasubiri kauli yenu!”Aliongea Danny kwa sauti ya chini, moyoni mwake kulikuwa na furaha ambayo hakuwahi kuipata maishani, hakutegemea hata kidogo mambo yangekwenda kama yalivyokuwa yakiserereka, ndoa yake Agness ilikuwa hatua chache kutoka dakika hiyo! Kichwani mwake alianza kujiona akiwa baba wa familia, yeye na mke wake wakipenda na baadaye wanapata watoto ambao hakuelewa sura zao zingekuwa nzuri kiasi gani kama wangefanana na wazazi wao.
“Sisi tuna likizo ya mwezi mzima, tunaweza kubaki hapa mpaka harusi itakapofungwa! Tunakuomba mzee Katobe uendelee na mipango kama kawaida sisi tutasaidia kila utakapokwama, nafikiria tuna pesa ya kutosha.

Je Danny na Agnes wataweza kufunga ndoa?
Je mama Nancy ataweza kutoroka kisiwani na mtoto wake?
 
SEHEMU YA 23
“Sitaki lazima niondoke hawezi kumtesa mtoto wangu kiasi hiki, kila siku anamwingilia pamoja na kwamba ameshamsababishia uwendawazimu, huu ni unyama lazima nitoroke na nitaondoka kwa boya langu hilo hilo hata kama nitakufa mbele ya safari! Ni bora nikifa majini kuliko kuendelea kuteseka kiasi hiki!”
Hayo ndiyo yalikuwa mawazo ya mama Nancy karibu kila siku iliyokuja na kupita, hakukoma kutengeza boya lake mpaka aliporidhika limekaa vizuri zaidi na akabaki kusubiri siku ambayo angeweza kutoroka na watoto wake wote watatu lakini haikupatikana, siku zikazidi kusonga na mateso yakazidi kuongezeka.
Hali ya Nancy ilizidi kuwa mbaya, hakuweza tena kuongea chochote! Alishinda amelala asubuhi mpaka jioni, chakula acholishwa alikitapika na kuzidi kudhoofika zaidi, dalili kwamba angefia kisiwani zilizidi kuonekana wazi. Ni hapo ndipo mama Nancy alipoamua kuondoka mara moja bila kujali jambo lolote ambalo lingetokeza mbele ya safari, hofu yake kubwa ilikuwa ni mawimbi ziwani! Hakuwa na uhakika angeweza kufika upande wa pili lakini aliamua kujaribu.
Hakuelewa ilikuwa ni Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi ama Jumapili kwa sababu hapakuwa na kitu cha kumkumbusha! Nyakati za jioni mzee Kiwembe na babu Ayubu wakiwa ziwani kwa shughuli zao za uvuvi, alivunja mlango wa kibanda cha babu Ayubu na kuanza kakata kamba zilizomfunga mtoto wake kwenye nguzo, mikono ilikuwa imeharibiwa na vidonda vilivyotoa harufu vilivyosababishwa na msuguano kati ya kamba na mwili.
“Naondoka nikafie mbele kwa mbele!”Alisema mama Nancy akimbeba mtoto wake kutoka chini na kumweka begani na kuanza kukimbia naye kwenda upande wa pili wa kisiwa kulikokuwa na boya alilotengeneza.Alikuwa amedhamilia kuondoka hata kama angekufa mbele ya safari.
Alimlaza Nancy haraka juu ya boya hilo, hakuwa na uwezo hata wa kujigeuza akachukua kamba za magome ya miti na kumfunga kwenye boya akipitisha kamba tumboni, alikuwa amekonda mno mtu asingeweza kuamini kuwa yule alikuwa Nancy.
“Nikifika salama baba yake hataamini!”Aliwaza akikimbia tena kurudi kwenye kibanda cha mzee Kiwembe ambako aliwachukua watoto wake wawili na kuanza kukimbia nao kwenda ufukweni, alifanya kila kitu haraka ili mzee Kiwembe na babu Ayubu wasirudi na kumkuta katika pilika hizo, aliamini kuwa kifo ndiyo kingekuwa adhabu yake kwani mzee Kiwembe asingekubali mtu aondoke na watoto wake aliowapenda.
Baada ya kuwa yeye na watoto wake wamekaa vizuri juu ya boya lililotengenezwa kwa miti na lenye uwezo wa kuelea! Alirudi tena kwenye kibanda cha mzee Kiwembe na kuchukua samaki waliokaushwa ili wamsaidie yeye na watoto wake kama chakula njiani, akiwa na uhakika kila kitu kilikuwa sawa, kwa ushujaa kabisa alisukuma boya hadi majini na yeye kukaa juu yake.
Hakumsahau Mungu kwani aliamini bila muujiza asingeweza kufika upande wa pili, hapohapo alifumba macho na kuanza kusali sala ya baba yetu uliye mbinguni’akimuomba Mungu amnususru yeye na watoto wake! Alijisikia kama anamjaribu Mungu, kwani kifo kilionekana kuwa mbele yao na yeye alikuwa akifuata.
Alipofumbua macho tayari alikuwa akilia machozi, akanyoosha mkono wake na kuchukua kasia lilikuwa pembeni! Tayari safari ilikuwa imeiva, uzoefu wa kupiga kasia aliupata kutoka kwa mzee Kiwembe aliamini ungemsaidia kufika upande wa pili ambako hakuelewa kungekuwa Kigoma au Kongo na ingechukua siku ngapi, hakuwa na matumaini ya kuwa mzima katika muda wa siku tatu au nne lakini hiyo haikumvunja moyo.
Alianza kupiga kasia akiyakata maji taratibu alielewa wazi ilikuwa ni lazima awe mvumilivu kwani safari yake ilikuwa ndefu! Masaa manne baadae tayari giza lilishaingia, watoto wake wawili walikuwa wakilia kwa sababu ya baridi lakini Nancy alikuwa kimya kabisa kama aliyekuwa kwenye usingizi mzito! Aliwabembeleza huku akiendelea kupiga kasia kwenda mbele zaidi.
Hali ilikuwa ya giza kila upande, mama Nancy hakuweza hata kutambua ni upande gani alikuwa akielekea, alichoshukuru Mungu hali ya ziwa ilikuwa shwari kupita kiasi jambo lilimfanya kusonga kwake mbele kuwa rahisi zaidi, kwa mara moja hakukitambua lakini alipoangalia vizuri ingawa ilikuwa gizani aliweza kuona kitambaa cheupe na kuelewa kilichokuwa mbele yake lilikuwa jahazi likija kwa kasi kubwa.
Alijaribu kupiga kelele akiomba msaada lakini hakuna aliyemsikia, jahazi lilizidi kumsogelea na kuligonga boya lake! Yeye na watoto wake wakamwagwa majini, alijaribu kuwashika Catherine na David waliokuwa karibu naye na kuanza kuogelea nao akijaribu kutafuta boya ili awaokoe bila mafanikio.
“Nancy!Nancy!Nancy!”Aliita lakini hakuitikiwa na wala kumwona Nancy mahali popote kwa hali aliyokuwa nayo alikuwa na uhakika mwanawe amekufa maji, kwa mara ya pili alikuwa katika hatari za kuzama maji! Kumbukumbu za tukio la awali zilizopelekea yeye na Nancy kujikuta mokononi mwa mzee Kiwembe na babu Ayubu zilimwijia kichwani, alitamani kuokolewa lakini si na wazee hao wawili.
Alizidi kuogelea akimtafuta Nancy lakini hakuonekana, machozi yakamtoka na kumezwa na maji.
*****
Familia za pande zote mbili zilikubaliana juu ya ndoa kufungwa tarehe kumi na saba mwezi wa nne! Danny na Agness walifurahi kupita kiasi, mipango iliendelea kama ilivyopangwa na walibaki wakisubiri siku iliyokuwa umbali kama wa wiki tatu mbele yao kwa hamu kubwa.
Hatimaye siku ya siku ikafika, mamia ya watu wakakusanyika kanisa la Romani Katoliki Mantep huko Bagamoyo, wengi wao wakiwa wanafunzi wa chuo kikuu na watu mbalimbali maarufu jijini Dar es Salaam waliosafiri hadi Bagamoyo kushuhudia ndoa hiyo.
Kila kitu katika harusi hiyo kilifanyika kwa juhudi za mzee Katobe wazazi wa Danny hawakuamini! Ilikuwa ni zaidi ya hata undugu, mapenzi ya mzee Katobe kwa mtoto wao hayakuwa ya kawaida.
Kwa Danny na Agness ilikuwa ni siku ya ndoto yao kutimia! Mioyo yao ilijaa furaha, hapakuwa na kipingamizi tena na kilichokuwa mbele yao wakati huo ni familia, mafanikio na watoto! Ingawa mara chache Danny alikumbushia msimamo wake juu ya Nancy hapakuwa na matumaini tena kuwa msichana huyo angekuwa hai. Walisimama mbele ya Padri, meno yao yakiwa nje kwa tabasamu.
“Danny! Je umekubali kumpokea Agness awe mke wako? Katika shida, raha, magonjwa na kifo?” Padri aliuliza.
****
Wakati akihangaika kuogelea na watoto wake mara alishtukia kuona wanaume watatu wakitokea na kumnyang’anya watoto na mwingine aliyekuwa hajiwezi, alishtuka akifiri tayari alikuwa ameingia mikononi mwa mzee Kiwembe na babu Ayubu! Lakini alipowaangalia vizuri watu hao aligundua walikuwa ni vijana, jahazi alikuonekana kusimama lilikuwa limetia nanga.
“Waleteni! Waleteni!” Sauti nyingine ilisikika kutoa juu ya jahazi na hapo hapo zilianza kutupwa kamba watoto wote walianza kufungwa mmoja baada ya mwingine. Hata Nancy alikuwepo! Yeye ndiye akawa wa mwisho, alikuta vijana hao wakihangaika kumkamua Nancy maji tumboni, mmoja wao alimshika alimshika mkono na kwenda kumlaza pembeni.
“Pumzika!’
“Watoto wangu?”
“Wapo wanashughulikiwa!”
“Watapona?”
“Wawili tuna uhakika, lakini mmoja wao hali yake inasikitisha, amekunywa maji mengi! Hata hivyo bado wanamkamua!”
Baadaye alipopata nguvu alinyanyuka na kusonga mahali walipokuwa watoto, Nancy alikuwa bado taabani ingawa maji yalishaisha tumboni mwake! Alilala chini na kuanza kumpulizia pumzi mdomoni kama huduma ya kwanza hatimaye akaanza kuhema vizuri na matumaini yakarejea tena.
Aliwaeleza vijana hao kila kitu juu ya kilichomkuta katika ziwa Tanganyika, walimhurumia na kuamua kumsaidia! Alishukuru Mungu aliposikia walikuwa safarini kuelekea Kigoma, hali ya Nancy ilikuwa mbaya lakini bado alipumua na moyo wake ulikuwa ukidunda vizuri. Mama Nancy alipiga magoti chini na kubusu ardhi, hakuamini kama alikuwa huru tena.
“Sijui jinsi ya kuwashukuru! Mmeokoa maisha yangu na watoto wangu!” Alisema mama Nancy.
“Usijalia! Acha kwanza tuwapeleke hospitali!”
Hilo ndilo lilifanyika,mama Nancy na watoto wake wakapelekwa hospitali ya mkoa wa Kigoma ambako walilazwa na kuanza kupewa matibabu, Nancy alilazwa wodi ya wagonjwa mahututi na alifanyiwa vipimo aligundulika kuwa na Malaria sugu pamoja na homa ya matumbo.
Alianzishiwa matibabu, katika muda wa siku mbili akarejewa na nguvu zake kama kawaida lakini wendawazimu ukarudi pale pale! Hilo halikumsikitisha mama yake ili mradi mwanawe alikuwa hai, wasamalia waliwanunulia nguo nzuri na mpango wa usafiri kurejea Dar es salaam baadaye ulifanywa.

Je nini kitaendelea?
Je Nancy na mama yake wataweza kurudi Dar salama?
Je harusi itaweza kufungwa?
 
SEHEMU YA 24
Walishuka Bagamoyo saa tisa za alasiri siku ya Jumamosi tarehe kumi na saba mwezi wa nne, watu waliowaona waliwakimbia, hakuna aliyetaka kuongea nao wakiamini walikuwa ni misukule! Hali walizokuwa nazo zilitisha, isitoshe kila mtu wakati huo aliamini walikuwa ni marehemu.
Walinyoosha hadi nyumbani kwao na kukuta nyumba ikiwa imefungwa na hapakuwa na mtu yoyote, majirani jasiri waliwafuata wakitaka kufahamu kama kweli walikuwa ni wao! Mama Nancy alisimulia kila kitu kilichotokea, watu waliangua kilio na wao hawakumficha juu ya kilichokuwa kinaendelea kanisani. Bila kuchelewa gari lilikodishwa, mama Nancy na watoto wake wakapakiwa ndani na safari ya kwenda kanisani ikaanza! Lengo ikiwa ni kuzuia harusi ya Danny na Agness kwa sababu Nancy alikuwa amepatikana.
Gari liliegeshwa mbele ya kanisa, Nancy akionekana mwendawazimu kabisa na mama yake akiwa amechoka, walisaidiwa kushuka na kisha kuongozwa kuingia kanisani! Watu wote walipowaona walianza kupiga kelele wakikimbia kwenda nje, kilikuwa ni kitu cha kutisha! Maneno misukule yalisikika kila upande ndani ya kanisa.
Mama Nancy na watoto wake wakiongozwa na majirani hawakujua kilichokuwa kikiendelea! Walizidi kusonga mbele kwenda Altareni ambako pia watu walionekana kushutushwa na kilichokuwa kimetokea.
“Nini?”Padri aliuliza.
Watu walioaminika kufa maji katika ziwa Tanganyika wanaibuka kutoka Kisiwa cha Galu walikokuwa wamefichwa, ni mama Nancy, mke wa mzee Katobe pomoja na Nancy, binti wa familia hii ambaye pia ni kipenzi wa kijana aitwaye Danny.
Danny na mzee Katobe waliwatafuta sana watu hawa bila mafanikio, hatimaye kukata tamaa na kulazima kuendelea na maisha yao! Tayari Danny ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alishakutana na msichana mwingine aitwaye Agness huyu pia ni mwanafunzi chuo kikuu na leo hii wapo ndani ya kanisa wakifungishwa ndoa.
Ndoa hii imewezekana tu kwa sababu Danny anaamini Nancy ni marehemu ingawa hakuiona maiti yake, vinginevyo asingemwoa Agness na jambo hili alishaliweka wazi kwake kuwa akitokea Nancy akarejea basi atalazimika kumwacha Agness na kuwa naye.
Leo hii wakiwa ndani ya kanisa baada ya padri kumuuliza tu Danny kama alikuwa tayari kumwoa Agness kelele zinasikika nyuma yao, wanageuka na kukuta watu wanakimbia huku na kule wakipiga kelele na kusema “Misukule imeingia kanisani”
Danny na watu wengine walioko madhabahuni pamoja na padri wanapigwa na butwaa kuwaona wanawake wawili, mmoja akiwa mwendawazimu kamili wanaingia kanisani wakiwa wameongozana na watoto wawili na kundi kubwa la watu.

Je, nini kitatokea ndani ya kanisa?
Ndoa itafungwa?

SONGA NAYO

Padri, wazazi wa Dany nao walishindwa kuvumilia na kujikuta wakikimbia kutoka madhabahuni kwa woga, picha ya watu waliokuwa wakija mbele yao hasa wawili kati ya wote, mmoja akiwa amebeba watoto wawili walionekana kuwa wagonjwa iliwashtua.
Watu watatu tu walibaki mbele ya madhabahu, Danny, Agness na mzee Katobe wakiangalia picha iliyokuwa ikiendelea kwa mshangao, hakuna mtu kati yao akina nani walikuwa wakitembea kuelekea mahali walipokuwa wamesimama.
Walifika na kusimama na mama Nancy kuweka watoto wote chini kisha kumsogelea mzee Katobe aliyekuwa wima bila kuelewa nini kilikuwa kikiendelea, hali ya mama Nancy ilishaharibika hakuwa mwanamke yuleyule ambaye mzee katobe alimwona mara ya mwisho! Alikuwa na nywele ndefu sana zilizojisokota pia rangi yake ya ngozi ilikuwa nyeusi kuliko alivyoondoka.
“Katobe!” Alimwita mume wake.
“Ndiyo! wewe nani?”
“Niangalie vizuri usoni utanitambua!”
Mzee Katobe alikaza macho yake na kuyaelekeza usoni kwa mwanamke aliyesimama mbele yake, picha ilimwijia na kugundua alikuwa mke wake lakini badala ya kusimama kumsogelea alianza kukimbia kwenda nje ya kanisa, hakuwa tayari kuamini kuwa yule alikuwa mke wake kweli.
“Tafadhali rudi! Mimi ni mkeo, usiogope nitakueleza kila kitu!”
“Mzee Katobe rudi usikilize, sisi ndio tumemleta huyu si msukule ni mkeo halisi amerudi!”mmoja wa majirani wa mzee Katobe alisema huku akimkimbia hadi kumfikia na kumshika mkono kisha kuanza kurudi naye hadi madhabahuni ambako alimkuta mke wake akiwa amesimama mahali alipomwacha machozi yakimtoka, aliyakaza tena macho yake kumwangalia na kwa unyonge huku akiogopa alimsogelea.
Shughuli ya harusi ilishakoma kabisa ingawa baadhi ya watu waliokimbia nje walianza kuingia tena kanisani, hata padri na wazazi wa Danny walianza kujisogeza.
“Ni wewe?”Mzee Katobe alimuuliza.
“Ndiyo, kwanini huamini?” Mama Nancy aliuliza.
“Ulikufa maji!”
“Si kufa! Nilikuwa hai mahali fulani nikipata mateso!”Aliongea mama Nancy akilia.
“Kweli?”
“Nilikuwa kisiwani Galu!”
“Wapi?”
“Katika ziwa Tanganyika!”
“Haiwezekani! Tulivitembelea visiwa vyote tukikutafuta wewe na mwanangu Nancy! Kwanza yuko wapi? Nikimwona yeye naweza kuamini maneno yako!”
“Yule pale! Alijibu mama Nancy akisonta kidogo kuelekeza mahali alipokaa Nancy akiwa ameinamisha kichwa chake nywele zake ndefu na chafu zilizojisokota ziliufunika uso wake, mwili wake ulikuwa umekonda mno isingewezekana kwa mzee Katobe kuamini kuwa binti yake mrembo ndiye amekuwa mwendawazimu aliyekuwa amekaa chini mbele yake.
“Unanidanganya huyo sio Nancy, namfahamu vizuri mwanangu! Alikuwa na afya njema na sura ya kuvutia hawezi kuwa huyo mwendawazimu!”
“Tafadhali nakusihi usogee na umfunue hizo nywele!’
Tayari watu walishazunguka madhabahu wakishangaa kilichokuwa kikiendelea, haikuwa harusi tena huzuni kama za msiba zilitawala ndani ya kanisa, watu waliokuwa na furaha walikuwa wamebadilika na kuwa wanyonge kupita kiasi. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Danny pia, hakuamini mambo aliyokuwa akiyaona.
Mzee Katobe alitembea taratibu hadi mahali alipokuwa amekaa Nancy na kuchuchumaa kisha kukinyanyua kichwa cha binti aliyedaiwa kuwa wake ingawa yeye alimwona mwendawazimu! Macho yake yalithibitisha kuwa alichoambiwa kilikuwa ni kweli! hakuyaamuru machozi yake yatoke bali alishtukia mashavu yake yakilowa.
“Kweli ni mwanangu! Nini kiliwapata? Sogea karibu yangu mke wangu, tupige magoti tumwombe Mungu na kumshukuru kwa kuwarudisha salama!” Aliongea kwa huzuni mzee katobe na mama Nancy alisogea na kufanya kama alivyoelezwa, wote wakaanza kusali wakiwa wamemkumbatia Nancy. Kila mmoja wao alikuwa akilia kwa uchungu, hakika ilikuwa siku ya huzuni kuliko siku nyingine zote maishani mwao.
“Siamini!”
“Kwanini!”
“Kama kweli mmerudi, kila mtu alielewa mlishakufa!”
“Hapana tulikuwa hai katika mateso makubwa!”
“Na hawa watoto ni wa nani?”
Mama Nancy aliangua kilio, hakuwa na maneno ya kutosha kuwaelezea vizuri watoto aliowazaa na mzee Kiwembe bila ridhaa yake, hakutegemea kupewa msamaha wa aina yoyote ingawa siku zote alijiona si mwenye hatia na aliwapenda sana watoto wake.
“Nakuuliza hawa watoto ni wa nani?”
“Nitakueleza baadaye lakini naomba uniahidi msamaha!”Aliongea mama Nancy kwa huzuni kubwa huku akijifuta machozi.
Danny alikuwa amesimama pembeni, mwili wake ukiwa umepigwa na ganzi! Maongezi yote yaliyofanyika kati ya mzee Katobe na mkewe aliyasikia vizuri na hata uso wa Nancy uliponyanyuliwa aliuona na kumtambua!
Kitu kama sinema kiliendelea kichwani mwake na kujikuta akirudishwa moja kwa moja hadi chuo kikuu siku aliyokutana kwa mara ya kwanza na Nancy na kumpenda, bado ubongo wake uliukumbuka uzuri wa Nancy bila kutegemea yeye pia alijikuta akitokwa na machozi ya uchungu.
Alijikuta akitamani kumsogelea Nancy lakini hakuweza kufanya hivyo, mkono wake wa kushoto ulikuwa umekamatwa vizuri na Agness aliyeonakana kukerwa na kilichokuwa kikiendelea.
“Niachie!”
“Uende wapi?”
“Nataka nikamsalimie Nancy!”
“Huyo mwendawazimu?”
“Sijali yukoje, lakini nataka kumsalimia!”
“Hakuna!” Agness alikataa.
“Unakumbuka maneno niliyoongea na wewe kabla hatujaingia katika mapenzi yetu?”
“Maneno gani?”
“Usijifanye kusahau! Nilikueleza kabisa kuwa kama siku moja Nancy angerudi, lazima ingelazimika kuwa naye! Na sasa amerejea kwanini unanizuia kwenda kumsalimia?
“Lazima uelewe kitu kimoja Danny!”
“Kitu gani?”
“Tumekuja hapa kufunga ndoa!”
“Imekwishafungwa?”
“Bado lakini muda ndio huu!”
Tayari padri alishafika madhabahuni na kuwaomba watu waketi kwenye viti ili aendelee na shughuli iliyowakusanya ndani ya kansia, hakuelewa kabisa kilichokuwa kikiendelea kati ya mzee katobe na wanawake wachafu waliokuwemo ndani ya kanisa.
“Mzee Katobe!” Mzee katobe! naomba usogee hapa tuongee kidogo! Padri aliita na mzee katobe alijiondoa mikononi mwa mkewe aliyekuwa bado wamekumbatiana na kuanza kutembea kuelekea madhabahuni ambako aliungana na padri pamoja na wazazi wa Danny kwenda pembeni kuteta, hakuficha kitu katika maelezo yake! KIla kitu kiliwekwa bayana juu ya mke na mtoto wake walioaminika kufa maji!
“Kwa hiyo wamerudi?”
“Ndiyo! yaani siamini siku zote nilijua familia yangu ilishatangulia ahera!’
“Sasa tuendelee kufungisha ndoa au? Unataka uwapeleke nyumbani kwanza maana wakiwa hapa kanisa haliwezi kutulia!”
“Mtu wa muhimu sana katika ndoa hii hivi sasa ni Danny yeye ndiye mwenye uamuzi!” Aliongea mzee katobe bila padri kuelewa nini ilikuwa maana yake.
“Kwani kuna nini?”
“Kuna jambo kati ya yule binti yangu na bwana harusi mtarajiwa!”
“Jambo gani?” Padri aliuliza.
“Mnahitaji kuongea naye mwenyewe!”
Wakati hayo yakiendelea madhabahuni Danny alikuwa bado ameng’ang’aniwa mkono wake na Agness kiasi cha kushindwa kujiondoa na kwenda kumsalimia Nancy! Pamoja na kuwa mwendawazimu bado mapenzi yake kwa msichana huyo yalikuwa palepale hakuwa na taarifa ni nini kilichomfanya msichana huyo aliyewahi kuwa mrembo kufikia hali iliyokuwa nayo.
“Danny! Hebu sogea hapa kidogo!”Padri aliita.
“Amening’ang’ania hataki kuniachia!”
“Nani?”
“Huyu Agness!”
Ilibidi wazazi pamoja na padri wasogee hadi mahali waliposimama Danny na Agness wakiwa wameng’ang’aniana na kuanza kumuuliza Danny maswali juu ya kama shughuli ya ndoa ilikuwa inaendelea toka ilipoishia au la! Danny hakujibu kitu chochote, alibaki kimya huku macho yake yakiwa yamemwangalia Nancy aliyekuwa amejikunja chini, alionekana kutoelewa hata kitu kimoja kilichoendelea.
“Danny Padri anakuuliza!”
“Baba! Sipendi kuwaudhi nyinyi wala mtu yeyote, nafikiri niliwahi kuwaeleza vizuri juu ya msichana aliyekaa pale chini, anaitwa Nancy, nilimpenda na ndiye niliyetaka awe mke wangu lakini bahati mbaya akapotea na nikaamini alikufa! Kumbe yupo hai na kama amerudi sioni tatizo kuwa naye tena, ili mradi amefika mapema kabla sijavaa pete ya ndoa!”
“Kwahiyo ina maana hutaki kumwoa tena Agness?”
“Hilo ndilo jibu na hata yeye anaelewa, niliwahi kumweleza huko nyuma kuwa kama Nancy angerudi ingelazimu mimi na yeye tuachane!”
“Haweizekani wala usijidanganye, unapoteza muda wako Danny! Huwezi kuniacha dakika za mwisho kiasi hiki, aibu hii nitaificha wapi?”
“Hata mimi nakuunga mkono binti, mwanangu hawezi kuoa au kuishi na mwanamke mwendawazimu! Itakuwa ni aibu kubwa mno!” Mama yake Danny aliongea.
“Hata mimi nipo upande wa mke wangu!” Baba yake Danny aliongeza, mzee katobe alikuwa kimya muda wote wala hakufungua mdomo wake, macho yake yalikuwa yameelekezwa kwa watoto waliokuja na mama Nancy, mzee huyo alionekana kuwa mwenye maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
Danny alibaki kimya akiwashangaa wazazi wake kwa uamuzi waliotaka kuufikia, alijikuta njia panda! Hakupenda kuonekana mtoto asiyekuwa na nidhamu lakini pia alitaka apewe uhuru wa kuchagua akiamini kabisa maisha yake ya baadaye yalikuwa yake peke yake na hivyo alihitaji mwanamke ambaye angeiridhisha roho yake na kumletea furaha hata kama angekuwa mwendawazimu.
Alimpenda Nancy na alitaka kuwa naye, huyo ndiye alikuwa chaguo lake si Agness aliyekuja katika kipindi cha upweke, hakumchukia kwa lolote kwani alimsaidia sana kuutuliza moyo wake lakini kwa sababu Nancy alikuwa amerejea ilikuwa ni lazima amwache na kwenda kwa chaguo lake.
Alitumia nguvu nyingi na kujiondoa mikononi mwa Agness kisha kukimbia mpaka mahali alipokuwa amekaa Nancy, akakinyanyua kichwa chake na kumbusu usoni! Watu wote ndani ya kanisa walishangaa lakini kuna wengine walipiga makofi na kushangilia.
Akiwa bado katika hali hiyo bila kujua nini kilikuwa kikifuata, alishtukia kiti cha kanisani kikitua kichwani kwa Nancy! Damu zikaruka, alikuwa Agness akitetemeka kwa hasira, machozi yakimtoka kwa wingi. Nancy hakulia wala hakulalamika alichofanya ni kulala chali sakafuni!
“Agness umefanya nini tena?” Danny alipiga kelele.
Kulikuwa na dalili zote kuwa ndoa ilishashindikana, Nancy alikuwa amelala chini akivuja damu na Danny alikuwa akimfokkea Agness kwa kitendo huku watu wengine akiwemo mzee Katobe pamoja na majirani wakimbeba Nancy kumpeleka nje ya kanisa ambako alipakiwa garini na safari ya hospitali ikaanza.
****
Mama Nancy alibaki kanisani akiwa na watoto wake Catherine na David mikononi mwake, akishuhudia ugomvi mkubwa uliokuwa ukiendelea kati ya Danny na Agness kelele zilizidi kupanda ndani ya kanisa hata padri alijaribu kuwanyamazisha watu haikuwezekana! Ilikuwa ni aibu kwa Agness na wazazi wake, alifunika uso wake akilia.
“Danny”Padri alimwita.
“Naam Padri.”
“Msimamo wako ni upi?”
“Kuhusu nini Padri?”
“Kuhusu ndoa.”
Haiwekani tena hata kama Nancy ni mwendawazimu na nilimwambia Agnes jambo hili toka awali kwa kuwa amerudi akiwa hai ni lazima niwe naye!
“Kwa hiyo hakuna ndoa tena?”
“Kweli kabisa!”
Danny aliongea kwa kujiamini, hakuwaogopa hata wazazi wake, alikuwa amedhamilia kufanya alichokitamka! Ulikuwa ni uamuzi wake kuchagua amuoe nani hata kama baba na mama yake walitaka amuoe Agness lakini yeye alimpenda Nancy na alitaka awe nae maishani.
“Danny umemuona lakini huyo Nancy alivyo?”
“Ndio mama”
“Kwa hiyo utakuwa nae hivyo!”
“ Kweli kabisa”
“K wa nini usimuoe Agness kwa sababu mmeshafikia hatua nzuri?”
“Haiwezekani mama, nakuheshimu sana sana lakini kwa jambo hili naomba uniachie mwenyewe niamue!”Alijibu Danny akimuangalia Agness aliyekuwa pembeni akimwaga machozi, hakuwa na kitu kingine cha kusubiri kanisani alitaka kuelewa ni kitu gani kmimempata Nancy huko alikokuwa amepelekwa,bila hata kuuliza alikuwa na uhakika asilimia kubwa kuwa Nancy alipelekwa hospitali ingawa hakuelewa hospitali gani.
Alitoka akikimbia kwa kasi nje na kuingia ndani ya gari lililokodishwa kwa ajili yake na bibi harusi na kumwamuru dereva aliondoe haraka iwezekanavyo kuwafuata watu waliondoka na gari la mwanzo wazo la harusi tayari lishafutika hakuna alichokiwaza wakatim huo zaidi ya Nancy.
‘’Unafikiri wameelekea hospitali gani?”Aliuliza.
“Hakuna hospitali nyingine wanayoweza kuwa wamekwenda zaidi ya hospitali ya Wilaya”
“Twende huku huko basi”
Dereva aliondoa gari kwa mwendo uliotakiwa na Danny, akibadilisha gia hadi namba nne ingawa walipita katika njia yenye mabonde mengi, dakika na tano baadaye walifika hospitali na kuegesha gari lao. Danny akashuka na kukimbia hadi mapokezi akiwa ndani ya suti yake ya nyeusi. Alipowauliza wafanyakazi wa mapokezi kama walikuwa wamepokea mgonjwa aliyejeruhiwa kichwani, walionyesha mshangao na hatimaye baada ya kusoma ndani ya daftari la wagonjwa walimwambia hapakuwa na mgonjwa wa aina hiyo aliyepokelewa.
“Kwa hiyo yuko wapi?Kuna hospitali gani nyingine kubwa hapa Bagamoyo?
“Nendeni mkajaribu kumwangalia hospitali ya kanisa la Mennonite, ni mpya umejengwa hivi karibuni watu wengi wanakimbilia huko sababu hapa hatuna dawa!.
“Ahsante!”Alijibu Danny na kurudi tena mbio zile zile hadi kwenye gari,alipompa dereva taarifa mara moja alionekana kuielew hospitali hiyo na wakaondoka wakipandisha mlima hadi mahali hospitali ya Mennonite ilipokuwa,kabla hata ya kufika waliliona gari lililopambwa vizuri likiwa nje wakawa na uhakika hapo ndipo Nancy alipopelekwa.
Walishuka na kuingia ndani ambako walimkuta mzee Katobe pamoja na watu wengine wawili wakisubiri,Danny alianza kwa kuomba msamaha kwa yote yaliyotokea kisha akaketi pamoja nao kusubiri mgonjwa arudi kutoa katika chumba cha upasuaji alipokuwa amekwenda kushonwa!
“Vipi huko kanisani?”Mzee Katobe aliuliza.
“Ndoa imeshindikana!”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu ya Nancy!”
“Lakini ni kwa nini usingemuoa Agness? Si umemuona mwanangu alivyo?”
“Hapana baba!Nampenda sana Nancy nipo tayari kuwa naye katika hali hiyo hiyo aliyonayo wakati nikimtafutia tiba mpaka apone kwani hakuna kisichowezekana!”

Je nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom