Hadidhi yamenikuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hadidhi yamenikuta

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Yona F. Maro, Oct 1, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Siku hiyo ya jumatano

  Nimelala zangu kitandani , nasikiliza love and dedication ni kipindi kimoja kinarudhwa na radio moja maarufu jijini dar es salaam , kama kawaid nikawa nasikia watu wakituma salamu zao kwa wapenzi wao na kadhalika .

  Nikavutiwa sana siku hiyo , kuna dada mmoja alipiga simu , akaambiwa achague nyimbo , akachagua nyimbo moja inaitwa sacrifice kutoka kwa elton john , yule mtangazaji hakujua kwanini msichana yule amechagua nyimbo ile , yule mtangazaji pia hajui maana ya nyimbo ile .

  Mimi kusikia nyimbo ile , kausingizi kalinianza ikabidi niamke zangu , nikaanza kutafuta line za simu kwa mtangazaji huyo nimpigie , kwakuwa yule dada alichagua sacrifice , najua sacrifice ni nyimbo ya mapenzi yaliyovunjika ( broken heart love song ) , mie nikataka nitume nyimbo ingine zaidi ya hiyo scrifice kumpa moyo dada yule nikafikiria nyimbo nyingi sana za mahaba ninazo jua .

  Nikafikiri labda nimtumie YOUR BEAUTIFUL ya James Blunt au HEAVEN SENT ME YOU ya john mountgomery , na zingine nyingi lakini zote hizi nikajua hazitamtosheleza kwa sababu kwanza ni pop halafu zinaibwa kwa sauti laini zaidi kwa hisia kali , wasikilizaji wengi wanaweza kufikiri namtaka msichana yule .

  Nikapata jibu zuri zaidi katika list yangu ya nyimbo za mahaba nikapata nyimbo moja inaitwa IF I EVER NEEDED YOU nyimbo hii imeimbwa na julio igelesius , mara nyingi ukiongelea nyimbo laini za kilatini au spanish basi julio igelesius ni babalao kabisa kwanza sauti yake m mashairi yake , madoido yake na kadhalika .

  Saa ikafika nikapiga simu ikapokelewa , nikaongea na mtangazaji ,yule dada jina lake ni Judy , nikamwomba mtangazaji nitaje namba zangu za simu judy anitafute , na mwisho kabisa nikataja baadhi ya mashairi ya nyimbo ile ( if I ever needed you I need you now ) mtangazaji akacheka sana , nyimbo hii kwa bahati mbaya haikwepo basi nikamwomba apige nyimbo inaitwa WONDERFULL TONIGHT ya Eric Clapton .

  Dakika kadhaa baadaye baada ya nyimbo hiyo kupigwa nilipata simu kama 3 hivi kutoka kwa suzy , akiniuliza maswali kadhaa kuhusu mimi , niko wapi na ninafanya nini usiku huo , nilimweleza kila kitu , suzy alistajabu sana , hakuamini , ikaniambia anakuja nyumbani kwetu kunifanyia supprise , mie nikamngoja kwa moyo mkunjufu , ila nilijua kasheshe la kuingia getini manake kwetu kuanzia saa 2 usiku hakuna mtu kukanyaga .

  Baada ya dakika 45 hivi suzy huyo akaingizana saa hiyo ilikuwa ni saa 3 usiku , ilibidi apaki gari yake nje , nilimweleza mlinzi afunge mbwa ili suzy aingie ndani , mie nikatoka zangu nje nakumbuka nilivaa kaputula fupi sana bila shati na viatu , nikatoka kwenda kumpokea suzy akiingia ndani .

  Yaani nilichanganyikiwa sana , sikuamini kilichokuwa kinaendelea mimi nilifanya jokes tu suzy akachukulia ni ukweli namtaka , nilitaka kumpa moyo lakini sikutaka tufike mbali namna hii kama yeye alivyokuwa anafikiria .

  Haya tukaendelea

  Nikamkaribisha sebuleni , tukaanza story akaanza kunielezea kuhusu maisha yake , ametoka wapi na kadhalika , kumbe yeye ni mwenyeji wa nchi ya kenya , alikuja tanzania kwa mwezi mmoja kwa sababu ya masomo kuhusu mazingira , na yeye ni mwanafunzi , nikamuuliza na hilo gari hapo nje umekodisha au ?

  Ohh yes ndio , alinijibu nje kuna derefa ananisubiri haki

  Mhh okey sawa hakuna thida , sasa muda huu uliokuja hapa home huogopi chochote suzy ?

  La hapana siogopi !

  Haaa , huogopi kivipi kwahiyo wewe unajua sana huku dar es salaam kuliko sisi si ndio ?

  La si hivyoo , nimekuamini tu uliponipa namba zako

  Wow hiyo tamu kweli , kwahiyo ulukuwa unamipango gani usiku wa leo ? je kesho kuna sehemu yoyote unayotakiwa kuwahi ?

  We weee Yona unavituko sana , sasa unaniuliza kuhusu mipango wakati hata hatujuani ? na wewe unaniamini mimi kwanini ?” aliniuliza “

  Ahaha ( kicheko ) tukitoka hapa ntatoka na mlinzi mmoja si unaona kuna walinzi 4 kule juu na hapa chini ? kwahiyo wa huku chini mmoja tutaenda nae kama tutaenda popote pale kutokea hapa .

  Jamani Yona kumbe wewe ni muoga hivyo ?

  Mhh sio muoga bana ila huu ni usiku sana , na mimi ni mwanafunzi bora nikitoka niwe na mtu wa kutulinda si ndio ? unaonaje sweetie ?

  Uwiiiiii Yona yaani umeshaanza kuniita sweetie ? nani kakupa mamlaka hayo huogopi ?

  Tehe eehe , usijali natania bana , sasa unaelekea wapi ?

  Naelekea katika Hotel , unapenda twende wote ? Pls twende napenda ukanipe campani kwa hotel yetu kule mjini .

  Duh hapo nilitoka zangu nikapanda ngazi kwenda gorofa ya juu kumpa taarifa dada yangu kwamba natoka kidogo kuna mgeni na ntachelewa kurudi kwahiyo asinishangae nikichelewa au asiniulizie .
  Kwetu tupo kama 18 hivi lakini kila siku baba anauliza fulani yuko wapi tena wakati wa kuamka yeye huwa yuko mlangoni kuangalia nani kaamka nani anaumwa nani hajaenda shule .

  Kwangu hii haikuwa tatizo , nilimwambia dada yangu aniletee uniform shuleni , lakini kukawa na kitendawili kingine , shule pia ni ya baba , na skull bus zote za baba , je nikiuliziwa kwenye skull bus kama nipo au sipo ? na pale getini bila uniform hakuna kuingia hakuna sehemu ya kubadili nguo .

  Mengi yamenikuta lakini hili lilikuwa ni kiboko , sasa sijui nitumie njia zipi zingine na kulaghai nifanikiwe , basi nilipotoka nilienda kuchukuwa na uniform zangu na viatu , huyooo nikaingia kwenye gari ya suzy vuuuuuuum mpaka katika hotel yake pale kati kati ya jiji .

  Tukaingia chumbani kwake , baadaye nilienda kuoga yeye nikamwacha pale chumbani , lakini sikufunga mlango wote kwa ujumla , mlango ulikuwa wazi kidogo , nikasikia kelele za ajabu ajabu kwa mbali na harufu nzuri sana za perfume , well nikajiuliza yaani huyu mrembo anajipaka perfume saa hizi wakati hata hajaoga ? kunani ?

  Nikatoka bafuni ghafla nikaangalie kinachoendelea , sikukuta mtu na hiyo perfume iliisha na zile kelele siku zisikia tena , nikajua ni njee pale kwahiyo nilipuuza , nakajua ni jirani yangu labda ndio anajipodoa aende kudance kule chini ukumbini , nikarudi bafuni kwa spidi ya ajabu kuendelea na mambo ya kujisafisha .


  Nikafunga maji nikaanza kusikia tena kelele zile zile na perfume lakini saa hizi ni perfume ya aina nyingine , nikahisi leo nimepatikana mbona kelele kama hizi zijawahi kuzisikia ? kunanini humu leo ? halafu hata hotel hii sijawahi kufika inawezekana ndio style za hotel hii kulala usiku au ndio vituko vya uswahilini vimeanza ? yaani siamini mamboz yanayoendelea mazee .

  Nikatoka bafuni kwa wasi wasi sana , nilishaanza kuhisi mambo mengine yanaendelea tena makubwa tu , nikabadili nguo na kuanza kumtafuta yule dada suzy , kila sehemu simwoni , ghafla mikono ya moto ikashika mabega yangu , nilijisikia mahaba ya ajabu sana , mikono hiyo ikashuka mpaka katika mbavu zangu kisha mpaka chini ya miguu yangu .

  Akanipiga ngwala nikadondokea kitandani , kulala , sikuamini jinsi nilivyodondoka kiurahisi namna ile mpaka kitandani , nilianza kunyanyika kidogo kidogo mpaka nikasimama tena sakafuni ndio nikageuka kumbe ni suzy aliyenifanyia kisa hicho cha ajabu ajabu .

  Kumwangalia sasa nikataka kumfanya vile vile , nikamshika kiuno chake , kesha hips zake , nikarudi tena katika kiuno nikahisi kama kuna hirizi kwa kiuno chake sikumuuliza hiyo ni nini lakini nikaanza kuifuatilia hirizi ile mpaka nijui ilipoelekea nikaanza kuleta mikono yangu mbele kuzungusha kiuno chake mpaka katika kitovu .

  Nikafuatilia ile kama kwa mikono yangu kwenda mpaka chini nikaanza kuhisi kama nashika manyoya ya mnyama kama ngombe hivi au mbuvi , hapo nguvu zote za kunyanyuka sina , nikaendelea kwenda chini tu , hapo nilikuwa nimefunga macho nikafikiri labda amevaa sox za ngozi babake .

  Ghafla nikafungua macho yangu , kumbe nilizokuwa nashika ni miguu ya ngombe , tena ngombe huyo alinipiga teke nikarushwa kama hatua 3 toka pale nilipokuwa nilidondokea katika makabati mule ndani , alinipiga tehe la kifuani .

  Nikanyanyuka tena kuangalia yule nani akageuka panya , kisha akageuka nyoka tena cobra , nyoka akaasimama akanitolea mimacho yake , akajaza mapafu yake na sumu yake akaanza kunifuata ili anigonge na kuningata nife kabisa .

  Kwa sababu nilikuwa na mafunzo kidogo jinsi ya kujilinda na vitu au maaduwi , nilianza kutumia ushujaa wangu , nilipigwa teke na ngombe yule , sasa sikuwa na nguvu za kusimama , nakangoja huyu nyoka akija karibu nikapate kichwa chake mpaka mwisho au nikikamate kichwa chake halafu nimtupe nje .

  Huyooo nyoka akaja kwa kasi sana akarusha mate yake nikajikinga mate hayakuniingia machoni mwangu , alipofika karibu tena akabadilika safari hii akawa beberu kubwa akanipiga pembe , moja katika mguu wa kushoto , akarudi tena nyumba ili anipige pembe ingine , wakati anakuja nikarukia kitandani kwahiyo akagonga kabati .

  Zile pembe zake zilinasa katika kabati akashindwa kutoka pale , nikawa kitandani sina nguvu sasa kifua kimepigwa na mguu wa kushoto siwezi kukimbia sina pumzi ya kutosha , nikajikokota kidogo kidogo huku mbuzi akihangaika kutoka pale katika kabati

  Ghafla akageuka kuwa nyoka tena akanifuata kwa spidi ya ajabu , akanirukia ili anigonge , hapo niliruka pia upande mwingine , akagonga katika mbao moja hivi meno yake yalinasa mbao ile mpaka nguvu zikamwishia .

  Nikaenda pale , nilishika kichwa chake nikamchomoa toka katika ile mbao nikamrusha dirishani , nilikuwa niko ghorofa ya 5 , nilishuhudia akidondoka , niliona akigeuka kuwa beberu tena , kisha akageuka kuwa nyoka kisha akageuka kuwa binadamu mwanamke mrembo ndio nikasikia kelele zake akilalamika mama nakufaaaa

  Kisha nikasikia kishondo chini boom yaani amedondokea juu ya gari moja .


  Hakika yalinikutana

  Hadithi hii ni ya kutunga haina ukweli wowote ndani yake .
   
Loading...