Hadidh

Strongmind

Member
Jun 22, 2016
37
29
HADITHI YA NYUMBA YA DHAHABU

Kulikuwa na binti mdogo aliyeishi kwenye nyumba ndogo tena katika maisha duni. Nyumba hiyo ilikuwa imejengwa juu ya mlima ambapo binti huyo alikuwa na uwezo wa kuiona nyumba moja ndogo iliyokuwa nzuri huko bondeni, nyumba hiyo ilikuwa inaonekana yenye rangi ya dhahabu.

Nyumba yenye madirisha ya dhahabu iliyopo bondeni ilimpendeza sana kwa jinsi ilivyokuwa inang’aa kiasi cha kwamba binti huyo alikuwa na ndoto kuwa akishakuwa mkubwa na kuruhusiwa kutoka nje basi ataenda kutembea kwenye nyumba hiyo ili afurahishe moyo wake mbali na nyumba ya kawaida kama ya kwao.

Japokuwa aliwapenda sana wazazi na familia yake, alitamani siku zote apate kuhamia kwenye nyumba ile ya dhahabu na kila siku aliwaza uzuri wa kuishi kwenye nyumba ile.

Basi siku ya siku binti yule alifikia umri ambao alipata ujuzi na kujiamini vya kutosha kuweza kuruhusiwa kutoka nje ya nyumba yao, alimuomba mama yake kama anaweza kutoka nje na kwenda kutembea na kushangaa nje ya uzio wa nyumba yao huko bondeni. Baada ya kumuomba sana mama yake alimkubalia kutoka nje kwa kumsisitizia kuwa asiende mbali sana na nyumba yao.

Ilikuwa siku nzuri na yule binti alijua fika wapi anaelekea baada ya kutoka nje; bondeni kwenye ile yule yenye madirisha ya dhahabu, akatembea lakini akaona anachelewa hivyo akaanza kukimbia hadi akafika kwenye geti la ile nyumba yenye madirisha ya dhahabu bondeni.

Alifungua geti na kuifuata njia iliyoelekea kwenye nyumba ile akafika na kisha akaingia ndani ya nyumba. Binti yule alikata tamaa baada ya kukuta madirisha yale kuwa matupu na machafu, aliuona ule mwanga wa dhahabu uliong’arisha nyumba hiyo ukiwa unatokea juu ya mlima na alipotazama vizuri ilikuwa ni nyumba yao.

Kumbe nyumba yao ndio ilikuwa ya dhahabu jua lilipopiga nyumba yao mwanga ulifika hadi kwenye ile nyumba ndogo bondeni na kuing’arisha.

Umejifunza nini?
 
Back
Top Bottom