briophyta plantae
Member
- Feb 18, 2017
- 63
- 62
Kwa hatua ambayo imefikiwa na jiji letu la arusha ni muhimu kubadilishia aina ya usafiri. Daladala tunazotumia ni ndogo na zinabeba idadi ndogo ya watu kwa wakati mmoja jambo linalopelekea usafiri huu kuwa na kero za hapa na pale. Naona ni wasaa wa kuanza kutumia basi kubwa zaidi kama coaster angalao. Ukuaji wa jiji na miundombinu uende sambamba na usafiri wa umma ulio bora zaidi.