Hadaa ya Mihimili ya Serikali

Samahani, naomba kuelezwa tafsiri ya DOLA?
 
Case study nzuri ni Kenya kwa ukanda huu wa Africa mashariki
 
Case study nzuri ni Kenya kwa ukanda huu wa Africa mashariki
Haswaaa, lakini nako tatizo lao Kiutawala liko wapi haswa? maana Ruto na Trump kama wanafanana vile! Je, ni support ya Wananchi, The Elites au inatoka kwenye mihimili yenyewe (Lobbyist na Rushwa)
 
Mkuu ahsante kwa mada fikirishi !
Naona swali limekuwa gumu kujibika kwa sababu Katiba yetu haisemi maneno hayo isipokuwa Ibara ya 4(1-3) inasema Shughuli zote za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na mihimili hiyo kwa pande mbili za Muungano.sehemy
Swali ni gumu kwasababu mfumohauel eweki. Katika mifumo ya utawala na serikali hatuna pa kusimama. Kwanza, Head wa government ni Head of State pia tukifuata presidential system kama USA.

Parliamentary system kuna Head of Gov anayeshughulikia mambo ya serikali tu ndani ya Bunge halafu kuna Head of State. Sasa Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge kama Parliamentary system inavyosema akiwa Head of Gov.

Wakati huo huo kuna ni Head of state kama presidential system inavyosema. Hapa ndipo tatizo linapoanzia

Mihimil imetamkwa kama ulivyonukuu kutoka Katiba kwa makusudi kabisa kutokana na mkanganyiko wa kati ya presidential system na Parliamentary system.

Tanzania, Rais ana nguvu za uendeshaji wa Mahakama na Bunge.
Nguvu hizo ni Budget! Rais anateua Katibu wa Bunge na Mawaziri. Rais anateua Majaji anavyoona

Mahakama na Bunge hazisimami kama ''pillar'' bali 'branch' za Serikali.
Yes nakubaliana nawe kuna tatizo la kimfumo linalonyima Bunge na Mahakama Uhuru. Unapochanganya na teuzi za Uchawa, tatizo ni kubwa

Mzee Warioba aliliona! bahati mbaya wakampiga stop! ili waendelee kutawala kwa kutokuwa na checks and balances. Matatizo tunayotaona sasa ni matokeo ya mfumo mbovu usio na checks and balance


 
Mimi najua sababu moja kubwa Tume ya Warioba walipo kosea ni kujadili maoni ya Wananchi kuhusiana na tuunde Serikali ngapi? Kana sikosei Warioba alimuuliza JK akamwambie go ahead knowing vyovyote itakavyokuwa, yeye atapigilia msumari hapo hapo..

Mtazamo wangu miye hili lisingekuwepo kabisa kwenye Rasimu ile, kwa sababu ni moja ya NGUZO kuu kabisa iloasisiwa na Wazee wetu toka 1922 hata kabla ya Mwalimu. Watu wengi hawaelewi kwamba African Association ilianzishwa kwanza Zanzibar na Dar es Salaam. AA ndiye babu mzazi wa Afro shiraz na TANU walomzaa hii CCM.

Kihistoria hapo awali Ushirika wao (Bara na Visiwani) ulikuja kujengwa nguvu zaidi na Pan Africanism na wakafungua tawi Ukombozi Pan-African Freedom Movement of East and Central Africa (PAFMECSA). mapinduzi.ya Zanzibar hayakuwa ya ghafla au sijui Okello laaa, Yalipangwa kutokea IF.

Kama sikosei swala la Serikali 3, ndilo lilomweka Marehemu Abdul Jumbe kifungo cha nje maisha Kigamboni na kumpelekea Mzee wetu Malecela balaa wakati ule Afro Shiraz ilijaa wana Mapinduzi wa African Association ya Zanzibar ambao hata Salim A Salim walimkataa kuwa rais wa JMT kwa imani yao kwamba hoja ya serikali 3 ni hoja ya wafuasi wa Hizbu na lengo lao ni kutengua Umoja wa Bara na Visiwani ulosababisha Mapinduzi ya 1964. Rasimu nzima ikapigwa vita.

Tuliposimama leo hii, tumekalia kuti kavu. Muungano upo matatani japokuwa Viongozi wote wa mihimili yote wameapa kuitetea na Kuilinda Katiba! Na katika vitu vyote vilopewa kipaumbele zaidi ndani ya Utaifa wetu ni MUUNGANO.

Maadam tumekalia kuti kavu, tunapitia mitihani kama Wa South hawaamini kama walisaidiwa kuupata Uhuru wao. Generation hii ni Chako chako Changu Changu, njaa kali Na viongozi wengi wanavunja miiko yote waziwazi kuwajaza Wananchi CHUKI na HOFU. Leo tunashughulikiana wenyewe badala ya kutafuta suluhu ya matatizo yetu Kitaifa, tunaanza kugawana Kuti.
 
Mimi najua sababu moja kubwa Tume ya Warioba walipo kosea ni kujadili maoni ya Wananchi kuhusiana na tuunde Serikali ngapi? Kana sikosei
Tume ya Warioba iliundwa kuchukua maoni ya Wananchi. Kumbuka wenye Nchi si viongozi ni Wananchi. Nyerere aliwahi kuonya, msipuuze maoni ya Wananchi hata kidogo. Maoni ya Wananchi ndio nguzo ya Muungano.
Hadi Tume inaundwa ilishapita miaka 40 na viongozi waliona tatizo na kubaini hali si ''sustainable''
Hakuna Tume yoyote iliyoundwa ikaja na proposal tofauti na Warioba. In Fact miaka 20 baada ya Tume ya Nyalali kusema, maoni yale yale yalirudiwa na Tume ya Warioba, Wananchi wanasema
Warioba alimuuliza JK akamwambie go ahead knowing vyovyote itakavyokuwa, yeye atapigilia msumari hapo hapo..
JK alikumbuna na tatizo la Muungano. Katika watu waliodhoofisha ni yeye kwasababu hakutaka kuwa mkweli bali kuwapendeza Wazanzibar! Tatizo sasa ni kubwa kuliko alipokuwa kiongozi
Mtazamo wangu miye hili lisingekuwepo kabisa kwenye Rasimu ile, kwa sababu ni moja ya NGUZO kuu kabisa iloasisiwa na Wazee wetu toka 1922 hata kabla ya Mwalimu
Huwezi kufunika kidonda na taulo ukasema unatibu. Dawa ya kidonda ni kukifunua na kusafisha
Miaka 60 na ushee leo Muungano ni dhaifu kuliko wakati wowote. Uwezekano wa Muungano kuvunjika ni mkubwa kuliko kuimarika hasa zama hizi za ''zamu' yetu.
Well, je, Jumbe, SAS n.k. kuwekewa vikwazo kume solve tatizo?
Hapana! Kwa miaka mingi Watanganyika hawakuwahi kuwa na tatizo na muungano. Tatizo limeanza baada ya Uzanzibar kuwa mkubwa kuliko Utanzania. Watanganyika wanajiuliza kipi hasa wanachonufaika nacho katika muungano walioubeba wenyewe?

Kama umepita mitandaoni leo kuna Mtanganyika analalamika kwamba Leseni yake ya udereva haitambuliwi Zanzibar. Trafiki anayeikataa analipwa na Wizara ya mambo ya ndani inayogharamiwa na Tanganyika. Leseni ya Tanganyika inakubalika Uganda, Kenya, Malawi, Zambia! Vipi ikataliwe Zanzibar
Ujinga kama huu unawafanya watu wajiulize, huu muungano ni wa kitu gani! na Watanganyika wananufaika na nini, na watakosa nini ikiwa haupo!
 
Hoja ya msingi hapa ni kujiuliza Serikali ambayo ina Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Inaongozwa na nani?
Nadhani Jamhuri (Republic) ndiyo yenye mamlaka ya kuiweka Serikali madarakani. Jamhuri ndio yenye serikali

Kituko ni kwamba katika Presidential system Rais (executive branch) hawezi kuvunja Bunge kama ilivyo USA. Tanzania Rais ni sehemu ya Bunge na ana uwezo wa kulivunja Bunge kama ilivyo kwa Parliamentary system ambayo Waziri Mkuu ana uwezo wa kuvunja Bunge.

Rejea hotuba ya Nyerere kwa Taifa alipozungumzia suala la Wabunge kupinga Bajeti ! Nyerere alisema ''kama hamtaki kupitisha Bajeti nina uwezo wa kulivunja Bunge, turudi kwa Wananchi na nina uhakika wa kurudi''
Wabunge wakanywea
Huwezi kuwa na Bunge huru ikiwa rais na mawaziri wake ni sehemu ya Bunge
Huwa najiuliza hivi ni kwanini Katibu wa Bunge anateuliwa na Rais? I mean kwamba Bunge haliwezi kuajiri au!
, na huwezi kuwa na Mahakama huru ikiwa majaji wa Mahakama ni wateule wa rais. Huu ni muundo nadhani wa Kiingereza ambao Serikali yao Kifalme yenye mihimili mitatu chini ya Ufalme huo.
Hapa kuna kituko kingine. Tume ya uajiri ya Mahakama huteua majina ya ''Majaji watarajiwa wengi''. Rais huweka majina katika data base na kitokea nafasi anachagua kutoka humo. Hii maana yake ni kuwavutia ''Watarajiwa ' kwamba wakimfurahisha Mhe. majina yao yatateuliwa. Majaji waliopo katika data base hiyo wana kazi moja tu '' UCHAWA''.
 
Niseme Ukweli:-
Wakati Pascal Mayalla anamuuliza Magufuli swali gumu kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari, mimi nilikuwa nimeshakaa pembeni JF kwa sababu JPM alikuwa mtu wangu , sikupenda ubishani ulokuwa ukiendelea hapa.

Niliandika hoja zangu FB zaidi na hata nilijibu hoja ya Mayala kule FB kwa kuzingatia Mamlaka alokuwa nayo Magufuli japo watu wengi hawakuelewa kuwa muundo wa Serikali yetu ndio unampa mamlaka hayo.

Isitoshe katika sakata lile rais ana Mamlaka ya kutunga Sheria ndani ya mhimili wake (Executive Order au Presidential decree) kupunguza matumizi holela ya fedha ndani ya Serikali.

Na mpaka leo naamini Magufuli alihujumiwa sana wakati akiwa madarakani kutokana na misimamo yake. Kwangu miye Magufuli alikuwa Kiongozi mwenye Vision, IQ ya juu kabisa na mwenye kuthamini UTU wa Watanzania.

Naandika haya nikijua MADONGO yanakuja lakini imani yangu ilikuwa ipo kabisa mpaka kesho, na katokea Polepole kuniwekea MHURI wa Kiimani kuwa Hisia na Fikra zangu zilikuwa on the right track.

Matatizo yoote ya Kiutawala tulokuwa nayo yanatokana na MUUNDO wa Mihimili yetu. Ndio unampa Kiongozi Udikteta (kuwa Baba au Mama wa Taifa) sisi sote tuko chini yake. Ndio ulojenga Machawa wakitegemea sauti zao zitawapandisha katika utumishi na matumaini ya nafasi za juu kwenye ajira n.k.

Mabadiriko lazima yaanzie hapa kuhakikisha vyombo na taasisi zote zinazotakiwa kuwa HURU hazipati maelekezo kutoka Juu. Hatuwezi kuwa na Check and Balance kwa mwendo huu. Tunahitaji Mabadiriko sasa.

Leo hii Kiongozi yeyote hawezi kumgomea Rais pale anapoona Sheria imepindishwa ama Katiba imekiukwa - Utatumbuliwa.

Kupata Viongozi kama Mzee Warioba alomgomea Nyerere na Nyerere akajishusha kidogo sii rahisi kabisa nyakati hizi. Wajibu wa Mihimili ni KATIBA na Katiba ndio Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bila Katiba hatuna JMT. Leo hii Katiba inapuuzwa, inabagazwa kiasi inaitwa ni Kitabu, hakika ni kwa sababu ya Muundo wa Serikali (Dola).
 
Hili ni swali kwa wahenga wa jukwaa hili la Siasa. Naomba pia ufafanuzi wake.

Ni Sura au Ibara gani ya Katiba ya JMT inayosema hivi: -

Serikali ina Mihimili mitatu.
1. Bunge -Parliament
2. Mahakama - Judicial
3. Serikali - Executive
Zamani ndio ilikuwa hivyo ila saizi, president ndo kila kitu.
 
Hili ni swali kwa wahenga wa jukwaa hili la Siasa. Naomba pia ufafanuzi wake.

Ni Sura au Ibara gani ya Katiba ya JMT inayosema hivi: -

Serikali ina Mihimili mitatu.
1. Bunge -Parliament
2. Mahakama - Judicial
3. Serikali - Executive
Ina maana tuna muhimili mmoja tu, hiyo mingine ni vivuli vya muhimili mkuu.
 
Nyerere aliwahi kutuasa juu ya Katiba hii ya mwaka 1977 lakini wengi hawakumuelewa.
Alituasa lakini hakuibadilisha sababu ilimnufaisha na aliacha makusudi kubadilisha Ili kukilinda chama chake cha Ccm.

Absolute power corrupts Absolutely...
 
Alituasa lakini hakuibadilisha sababu ilimnufaisha na aliacha makusudi kubadilisha Ili kukilinda chama chake cha Ccm.

Absolute power corrupts Absolutely...
Nyerere sio alotakiwa kubadilisha muundo wa Serikali ya JMT kwa sababu mageuzi yalikuja baada ya yeye kung'atuka. Badala ya Makamu wa rais kuendelea kuwa ndiye rais wa Zanzibar tukawa na rais wa Zanzibar, Zanzibar wakaandika Katiba yao kinzani na Katiba ya JMT. Ukazaliwa upya sisi Wazanzibar na wale Watanganyika!

Miiko na Maadili ya viongozi ikafutwa bila mfumo wa kudhibiti na kuwajibisha viongozi watakao kiuka Katiba. Ujio wa Vyama vingi ukazaa fitna na Uadui ambayo inatutesa mpaka leo.

Hatua zote hizi hazikuzingatia muundo wa Serikali kwa sababu huo ndio ulikuwa wakati wa Viongozi kutoka katika Umaskini na kujitajirisha. Kulizaa Ubwana viongozi kuitwa Waheshimiwa. Misingi ya Uongozi ikageuzwa kutoka Ujamaa kuhudumia Wananchi ukawa Biashara.

Matokeo yake huduma muhimu kama Maji, Afya na makazi viligeuzwa kuwa biashara na mpaka leo hii ni biashara kubwa ambayo tumeshindwa kuondokana na Ujinga, maradhi na Umaskini. Umimi umetamalaki kiasi kwamba sasa hivi tunaanza kujinasibisha na Dini, Kabila, Asili na Ukanda.

Naamini kabisa haya yote yametokana na marekebisho mengi ya Katiba ya Mwaka 1977 yalofanyika yalikuwa kwa faida ya Watawala badala ya kubadilisha mfumo wa Uongozi.

Na kama sikosei baada ya Mwalimu kunga'atuka, hotuba zake nyingi alizozitoa na zenye mvuto mpaka mpaka leo ni zile alozungumza wakati huo.
 
Mkuu kumpunguzia Rais madaraka ni kuondoa mambo yasiyomhitaji. Kwa mfano, Rais anabaki na madaraka ya mambo ya Kitaifa, Wizara ya Ulinzi, Mambo ya Nje, Fedha, Wizara ya mambo ya ndani na taasisi zake.

Mengine kama Elimu, utamaduni, Kilimo, ushirika, maliasili n.k. yatashughulikiwa na serikali washirika
Unapaswa kuelewa dhana yakumpunguzi madaraka inakwenda sambamba na uundwaji wa serikali 3
Katika mfumo wa sasa haiwezekani kwasababu yasiyomhusu hayana pa kupelekwa

Sioni tatizo kwasababu hata sasa hivi tuna serikali 3. Ukiacha Wizara ya fedha, ulinzi , mambo ya ndani mengine yanayojadiliwa Dodoma ni ya Tanganyika yamevalishwa koti la Tanzania ili ku accomodate Wazanzibar.
Wabunge wa Zanzibar pale Dodoma wanapswa kukaa wiki 2 tu kwasababu 97% hayahusu

Kwasababu mambo yanayojadiliwa hayahusu ndio maana hoja zao huwa vituko kama yale ya YUDA.
Hawana kazi! wanapokea posho na mishahara tu.

Waziri Mkuu pale Bungeni anasimamia mambo ya Tanganyika, Zanzibar wana serikali na Bunge lao
Waziri Mkuu hana mamlaka na mambo ya Zanzibar

Tayari tuna serikali 3 ingawa tunajidanganya ni 2. Wananchi wanataka kurasimisha serikali 3 ili ya Tanganyika iwe wazi na iwe na mipango yake.

 
Tayari tuna serikali 3 ingawa tunajidanganya ni 2. Wananchi wanataka kurasimisha serikali 3 ili ya Tanganyika iwe wazi na iwe na mipango yake.
Naona zipo serikali mbili (Tanganyika na Zanzibar), ila hiyo serikali ya Tanganyika ndio imevikwa koti la muungano.

Naamini Ccm wanataka huu mfumo ubakie kama ulivyo maana umekaa zaidi kichama kuliko kitaifa.

JokaKuu zitto junior
 
Hapana hapo siafiki mabadiliko haya na nadhani swala hili nimewahi kulizungumzia hapa wakati ule wa tume ya Katiba, kuhusiana na Mamlaka ya rais kupunguzwa.

Haihitaji kumpunguzia rais madaraka yake bali tupungu
ze mamlaka kwa kuunda mgawanyo wa mamlaka wa Serikali zetu kwa mujibu wa Katiba (Separation of Power) lengo haswa ni kudhibiti viongozi.

Unapoyaondoa madaraka ya rais na kuyapeleka kwenye Serikali zake ina maana unazaa marais wengine madikteta kwenye hizo Serikali ikiwa Bunge na Mahakama hazipo Huru. Kwanza tuvipe vyombo hivi meno badala ya kuendelea kulalamika.

Halafu, kuhusu Serikali 3, hiyo pia mimi siafiki kabisa kwa sababu ya GHARAMA ya kuendesha Serikali 3. Kumbuka kila Jimbo litatoa Wabunge wawili wa bunge la Muungano na Bunge la Serikali (State). Kama leo Bara ina Wabunge 314 basi tutakuwa na Wabunge 628 ambao wote watapokea Mishahara, posho na sijui magari ya thamani maana watu wenyewe ndio sisi hakuna Mbunge atakaye kubali kupokea sijui mil. 5 kwa mwezi.

Pili, watu wanadhani unapoondoa madaraka ya rais ndio njia sahihi lakini hawaelewi kwamba hata Marekani Federal Government bado ina wizara zote ndani yake isipokuwa mamlaka ya Sheria na uendeshaji ndio upo chini ya States. Kama Waikikwama kifedha ama any other emergency wanaomba msaada Serikali Kuu.

Kwa mfano, Nenda tazama Elimu na Afya utazikuta wizara hizo zipo Federal. Bila shaka unamkumbuka Dr. Fauci wakati wa Covid 19 huyu alikuwa Federal. Kwa hiyo tunakuwa na wizara nyingi upande wa Janhuri na upande wa nchi. Itazame vizuri Serikali ya Zanzibar leo ni mfano upo mbele yetu lakini hatuuoni.

Kwa hiyo, huwezi kumuondolea rais madaraka ya upande wa Elimu na Afya wakati rais anagombea kufuta Ujinga na Maradhi, anagombea kufuta rushwa na mikataba mibovu! Kutakuwa hakuna sababu kabisa ya Kumchagua rais Tanzania ikiwa hana madaraka hayo.

Nitaendelea kufafanua ikibidi.

Maasalaam
 
Na
naunga mkono hoja
 
Mbona warioba alipropose wabunge 75 nchi nzima. 50 bara, 25 zanzibar. Hakutokuwa na viti maalum.

Ikumbukwe kwa sasa zanzibar wana baraza la wawakilishi ila bado linapeleka wabunge dodoma. So kwa zanzibar dual system ni sawq ila ikija Tanganyika ndio issue ya gharama inatajwa!!
 
Kwa kuongezea, sehemu pekee inayotakiwa kudhibitiwa katika madaraka ya rais (Executive) ni teuzi zake zote lazima zifanyiwe Usaili iwe Mawaziri, Majaji, Mkuu wa Polisi, Majeshi, Usalama na hata Tume ya Uchaguzi na CAG wote lazima wawe na sifa za kushika madaraka hayo.

Tukiwa na Baraza Wazee Bungeni walokunywa maji ya Uhuru, wenye Hekima na Busara wawakilishi both Bara na Viziwani. Hapatakuwa na ujinga unaonendelea
 
Haswaaa, lakini nako tatizo lao Kiutawala liko wapi haswa? maana Ruto na Trump kama wanafanana vile! Je, ni support ya Wananchi, The Elites au inatoka kwenye mihimili yenyewe (Lobbyist na Rushwa)
Mahakama ipo huru katiba yao imeweka mpaka namna ya kupata funds za mahakama...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…